Sorry madam (Destination of my enemies)

vinneboy

JF-Expert Member
Aug 12, 2015
478
436
NINGEPENDA KUKUSHUKURU MPENZI MSOMAJI, ULIYE KUWA NAMI KATIKA SIMULIZI YA KWANZA YA SORRY MDAM.

KARIBU TENA KWENYE SIMULIZI HII MPYA YA SORRY MDAMA (Destination of my
Enemies).

MUNGU ATUONGOZE KUANZA MWANZO HADI MWISHO WA KISA HICHI CHA KUSISIMUA.

KARIBU.

Televishen pamoja na Tv zote nchini Tanzania, zipo hewani, kuweza kuyanyakua mazungumzo ya moja kwa moja ya Raisi Praygod Makuya, kwenye uteuzi wa mawaziri wapya, hii ni kutokana na waziri mkuu kuweza kujiudhulu, kwa kusumbuliwa na matatizo ya kiafya yaliyo mchukua kipindi kirefu kukaa nje ya ofisi pasipo uwepo wake. Kama
kanuni na taratibu za nchi ya Tanzania, inamlazimu raisi kuweza kufanya hivyo punde tu
waziri mkuu anapokuwa ameachia kiti hicho kinacho tamaniwa na kila kiongozi aliyopo
serikalini.

Raisi akaanza kutaja majina ya mawaziri wapya watakao chukua nafasi za mawaziri walio punguzwa kwenye wizara mbalimbali. Masikio ya wananchi wengi wa Tanzania, ni kwenye wizara ya ulinzi, ambayo katika siku za hivi karibuni imetokea kuyumba, hadi wananchi kuanza kupoteza imani na serikali yao pamoja na jeshi zima la polisi. Majina kadhalika ya mawaziri wapya na wazamani walio badilishwa wizara ya kaendelea kutajwa, ikafikia kwenye wizara ya ulinzi ulinzi, hapa raisi akanyamaza kidogo na kumeza fumba la mate huku akizikodolea kamera zilizopo mita chache kutoka katika sehemu aliyo simama.

“Katika wizara ya ulinzi, nimeweza kufanya mabadiliko makubwa sana, ambayo ninaamini yatakwenda kufurahiwa na wananchi walio wengi. Kwa maana katika kipindi changu cha utawala nimeweza kupokea malalamiko mengi sana kuhusiana na uhalifu katika jamii inayo tuzunguka.” “Wizara hii nimeweza kuweka watu hodari, wanao weza kuhakikisha wanafuta hofu yote iliyo jengeka katika mioyo mingi ya wananchi”

“Basi hapa waziri wa wizara hii, anaitwa Eddy Godwin, makamu wake atakuwa Bernad Ngoswe” Wananchi wengi wakabaki wakiwa wameshangazwa na jina hilo kwani, hawajawahi kulisikia kwenye serikali tangu raisi Praygod kuingia madarakani.

“Hivi huyo Eddy Godwin ni nani?” Mchaga mmoja alisikika akiwauliza wezake walio kusanyika katika duka lake la kuuza tv, redio na vitu vingine vya majumbani, lililopo maeneo ya Kariakoo.

“Hata mimi simfahamu” “Hawa watakuwa wanagawiana, kwanini wasimpe yule….yule nani….” “Chande?” “Hapana yule, ambaye wamekwenda kumtupia kwenye kilimo”
“Ahaaaa Masele” “Ehee huyo huyo, yule jamaa anaonekana yupo fiti sana” “Yaani wee acha. Ila baadaye si wanaapishwa, tutakuja kumcheki huyo jamaa mwenyewe” “Etieee” “Naye asije akatuletea ufala kama huyu mwenzie aliye pita Haki ya Mungu, naye tutamuombeamabaya” “Hahaaa maswawe punguza munkari bwana” “Sio
munkarti chalii yangu, yaani waziri akiwa ovyo hata hawa watendaji wake huku chini wote wanakuwa mambumbu, hembu nenda pale sentral kaseme unatatizo uone kama hawata taka rushwa”.

Nazungumzo ya watu mbalimbali katika mitaa tofauti ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam, yalikuwa ni kuhusiana na huyo waziri mpya waliyemsikia jina lake likitajwa. Wengi wao hawakuonyesha imani yoyote kwa waziri huyo, wanaamini naye atafanya madudu kama aliyo yafanya waziri aliye pita, kwa kuweza kuwapa polisi, uhuru ulio ptiliza, hadi inafikia hatua kwamba wananchi wa maisha ya chini wananyimwa haki zao za msingi, na wenye pesa ndio waliweza kupata haki zao na kuwakandamiza wale wasio kuwa nacho.
***

“Mume wangu utaweza, au ndio majukumu mazito uliyo kabidhiwa?” Phidaya alimuulimuuliza mumewe, huku akimfunga tai vizuri kwenda kwenye sherehe ya wao kuapishwa inayo fanyikia kwenye viwanja vya ikulu muda wa jioni ya siku hii,waliyo tangazwa kama mawaziri wapya.

“Mungu ni mwema nitaweza tu” “Eddy mume wangu usije ukaenda ukaboronga
huko ikawa ni mamatizo, mengine. Napenda tuishi kwa amani” “Baby wewe ndio mtu wa kunipa mimi moyo, ila si mtu wa kunikatisha tamaa”.

“Sio kama nakukatisha tamaa mume wangu, kumbuka kwamba tumepitia shida nyingi sana, hadi leo tumepata hii amani, ninaona kwamba tutaipoteza amani hii” “Never, nitahakikisha amani ya familia yangu kwanza, haiyumbi kisha nitahakikisha imani ya wananchi wangu, pia inapatikana” “Sawa mume wangu mimi ninakuombea kila laheri, ila usisahau kwamba ninakupenda sana Eddy wangu, kupota maelezo” “Nakupenda pia mke wangu” Taratibu Phidaya akambusu mume wake mdomoni, akamuweka vizuri koti la suti aliyo ivaa.

Wakatoka nje ya chumba chao na kuanza kushusha ngazi za gorofani hadi wakafika sebleni, walipo wakuta Shamsa na Junio wakitazama tv.

“Badilisheni chaneli muda si mrefu mutaniona nikiwa nimetokelezea kwenye kideo, nitaringaje” Eddy alizungumza huku akizunguka zunguka na kuwafanya watoto wake wote kucheka. “Mungu wangu…!! Hapa hawajapata waziri” Phidaya alizungumza huku akicheka kicheko, kilicho mfanya hadi machozi ya furaha kumwagika.

“Weee, waziri wameupata, yaani varangati nitakalo kwenda kulianzisha ni kama shehe aliye lishwa nguruwe pasipo kujua, sasa akagundua, hiyo movie yake nitawaadisia nikirudi” “Hembu nenda huko muda ujue unakwenda, ngoja uvuliwe huo uwaziri wako uone kama utazunguka zunguka tena” “Nani anivue, subutuu nitampiga ngumii moja tuu,
hadi aimbe haleluya”.

“Dady usisahaku kuniletea zawadi?” “Mwanangu, huko ikulu kuna zawadi gani” “Eddy
nenda bwana unachelewa, weee jizungushe zungushe kama tiara” Eddy akambusu mke wake, akafungua mlango na kutoka nje na kumkuta dereva wa gari la serikali akiwa anamsubiria kwa ajili ya kumpeleka ikulu kwenye sherehe hiyo.

“Shikamoo muheshimiwa?” Eddy hakuitikia salamu hiyo zaidi ya kuingia ndani ya gari na dereva huyo naye akaingia ndani ya gari, akawasha gari taratibu wakatoka kwenye geti kubwa la jumbu hili la Eddy alilo linunua siku chache baada ya kutoka katika mapumziko ya harusi yao yeye na mke wake Phidaya.

“Samahani ndugu yangu” “Bila samahani muheshimiwa?” “Wewe una miaka mingapi?” “Arobaini na tano” “Sasa mbona umenisalimia, wakati mimi bado kijana mdogo hata miaka thelethini bado sijainusa” “Ahaa ujajua shida hizi mdogo wangu, ndio zinazo
pelekea haya yote kutokea” “Ahaaa basi, kuanzi leo nitakuwa ninakusalimia
mimi, hata kama mim ni bosi wako. Naanza kwa kusema Shikamooo bwana nani…….”
“Selema Mbogo” “Ahaa itikia basi salamu yangu, au hutaki” “Marahabaa. Unajua pale nilivyo ona hujaitikia salamu yangu nikahisi kwamba ni mtu
ambaye hupendi mazoea na mtu, kumbe ni mcheshi kiasi hichi” “Kaka Mbogo, yaani mimi ni mcheshi sana, huwa sipendi kumkera mtu, hata kama nina kitu chochote kwenye maisha yangu”.

Mazungumzo yao yaliendelea hadi wakafika ikulu, wakaruhusiwa kupita na kuingia, dereva akasimamisha gari kwenye maegesho yaliyopo hapo ikulu. Eddy akashuka na kupokelewa na wadada walio wekwa kwa kazi hiyo ya kuwapokea wageni wanao wasili kwenye viwanja hivyo, na moja kwa moja akapelekwa hadi kwenye viti maalumu walivyo andaliwa mawaziri wanao apishwa kwenye sherehe hizo. Karibia vyombo vyote vya habari nchini Tanzania, wakawa wameweka kambi ikulu, ili kuweza kurusha matangazo hayo yanayo ruka moja kwa moja kutokea ikulu. Karibia viongozi waliopo ndani ya serikali macho yao mara kadhaa wakawa wanayatupia kwa Eddy,ambaye anaonekana ni kijana mdogo kupita viongozi wengine wote waliopo katika viwanja hivi.

“Huyu si yule kijana wa waziri mkuu?” Mzee mmoja alimuuliza mwenzake huku wakiwa
wememkodolea mimacho Eddy “Ndio huyu” “Si alikufa, au emefufuka?” “Mimi wala sijui mwenzangu, ila mama yake si yupo tutamuuliza kimetokea nini” “Ila huyu kijana wala sithani kama anastahili kuwa kiongozi kwenye wizara ya ulinzi” “Watakuwa wamepeana peana tu” Maneno yote waliyo kuwa wanazungumza wazee haya Eddy aliyasikia vizuri,
ikabidi awageukie na kuwatazama, nao wakajikausha na kujifacha kama si wao walio kuwa wakizungumza maneno kama hayo, mbaya zadi ni miongoni mwa mawaziri walio pigwa chini kwenye wizara walizo kuwa waklizitumikia kiuvivu uvivu.

Eddy akatabasama na kuwakonyeza kisha akageukia mbele. “Huyu mtoto mpumbavu kweli, anaonekana ana dharau sana” “Anatukonyeza sisi, tumekuwa mademu zake” “Ngoja tutamuonyesha, anadhani hii serikali ni rahisi kama anavyo fikiria na akili zake za asubuhi” Eddy alibaki kucheka, kwani maneno wanayo yazungumza wazee hao yanaonekana ni maneno ya wakosaji kwani walipewa nafasi na wakashindwa kuzitumia katika muda muafaka.

Haikuchukua muda, raisi akaanza kazi ya kuwapisha mawaziri wake wapya ambao aliwateua majira ya asubuhi na kuwatangazia taifa kwa kupitia vyombo vya habari. Ikafikia zamu ya jia la Eddy kuitwa, Akanyanyuka na kujiweka vizuri, kwa mwendo wa kujiaminai akatembea hadi akafika mbele, alipo simaa raisi pamoja na majaji.

Akakabithiwa biblia kama misingi ya viapo vinavyo tumiwa kwenye kipindi hichi cha kuapishwa na kama ni dini ya uislam, wanatuma msaafu na kama huna dini basi unanyoosha mkono wako bila kushika chochote.

“Mimi Eddy Godwin, ninaapa kwamba nitaitumikia katiba ya nchi hii, kwa kuilinda na kuitunza. Ehee Mungu nisaidie” Watu wakapiga makofi, hadi raisi mwenye akaonekana kupiga makofi kuashiria kumkubali kijana huyu mdogo aliye mkabidhi majukumu yaliyo washindwa wazee walio dumu kwenye serikali kwa miaka mingi sana. Eddy akapeana
mikono na muheshimiwa raisi pamoja na majaji walio kuwepo katika eneo la hapo mbele kisha akarudi kuketi kwenye kiti chake.

***
Msunyo mkali ukasikika ukitokea kwenye kundi la watu walio jikusanya kwenye mgaha huu maarufu ulipo katika jiji la Nairobi, hadi watu walio kuwemo ndani ya mgahawa huu wakageuza shingo zao kumtazama mtu huyo aliye achia msunyo mmoja mkali. Wengi wao hawakushangaa sana kuona sura ya mtu huyo anaye onekana ni wamakamo kiasi,
wanaamini watu wakisha fikisha umri kama huo mara nyingi huwa na matatizo ya akili, na
wanafanyaga mambo ambayo mara nyingi yanapaswa kuweza kufanywa na watoto wadogo.

Kila mmoja akaendelea na shuhuli yiliyo mpeleka hapo, huku baadhi yao wakiyapeleka macho yao kwenye tv. Inayo onyesha majirani zao nchi ya Tanzania wakiwaapisha mawaziri wao.

“Eddy nilazima nikuue kwa mikono yangu mwenyewe, hata kama umepewa uwaziri ni lazima nikuue tuu” Mzee Godwin alizungumza huku akiachia msunyo mwengine ulio wafanya watu wote kumgeukia na kumshangaa, baadhi yao wakaanza kuzungumza
maneno ya chini chini, wakimuhusisha na imani za kishirikina.

ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 2 YA SIMUHILI HII.

SORRY MADAM(1)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188.
 
RRY MADAM(3)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storyzaeddy.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
“Yule mshenzi amepewa uwaziri wa ulinzi
Tanzania?”
“Mungu wangu………ana sifa gani za yeye kuwa
waziri?”
“Ndio hivyo. Yaani laiti ningejua huyu mchenzi
ningemuua tangu tukiwa ndani ya ndege ninaamini
kwamba tusinge kuwa tunazungumza
mazungumuzo ya kumuuhusu huyu kibwengo
mtu” “Kwa nini usimuue?” “Mazingira
hayakuruhusu, alipelekea kunipa shida ya
kutafutwa hapo bendeni kwa hayati Mzee Madiba”
“Ulitokaje tokaje ndani ya ndege?” Swali la Madam
Mery likamfanya Mzee Godwin kurudisha
kumbukumbu zake nyuma kwa haraka hadi siku
aliyo toka kupambana na Eddy ndani ya ndege na
taratibu akaanza kusimulia.
ENDELEA
“Nilipo onekanana sura yangu, iliniazimu mimi
kuondoka na kuachana na Edddy kwani endepo
ningeendelea kupambana naye ningeingia
mikononi mwa askari na ingekuwa ni swala
jengine.”
“Nilijichanganya katikati ya askari ambao walikuwa
wakikagua watu basi, nikafanikiwa kutoka pasipo
wao kugundua kwamba mimi ndio niliye kuwa
nimesababisha maafa hayo” “Sasa uliingiaje ndani
ya ndege?”
“Ahaa, nilimtumia njia ya kujificha kwenye mizigo,
baada ya kumuona Eddy akiwa anahangaikia usafiri
wa kuja nchini Tanzania” “Aiseee una hatari kweli
kweli wewe” “Weee acha tu, sasa lengo na thumuni
la kukuita hapa ninahitaji kuweza kumpoteza Eddy
mara moja kwenye huu uso wa dunia. Ila tahadhari
ni moja, dogo amekuwa waziri, tena waziri wa
ulinzi” “Kama nilishindwa kumuua kipindi akiwa
mtu wa kawaida, basi ujue kazi ya kumuangamiza
yeye ni kubwa sana” Madam Mery akashusha
pumzi nyingi huku akimtazama Mzee Godwin
anaye onekana kuwa na mawazo mengi kichwani
mwake. Mzee Gowin kabla hajaendelea
kuzungumza ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu
yake, taratibu akaanza kuusoma, na tabasamu
pana likajijenga usoni mwake ikiwa ni ishara ya
furaha
***
Kukamatwa kwa mchungaji Mandingo na Madam
Glory watu maarufu katika nchi ya Tanzania
kukaana kuwashangaza wananchi wengi, vyombo
vingi vya habari vilidai kwamba watu hao
wamekamatwa na waziri mpya wa ulinzi. Waandishi
wengi walifunga foleni kwenye jengo la waziri wa
ulinzi wakihitaji kufanya mkotano na waziri huyo
ambaye hadi sasa hivi hawamuelewi nini ni maana
ya kuwakamata watumishi hao wenye kumsaidia
kila mwenye shida mbele ya macho yao
“Muhesimiwa, muheshimiwaa” Waandishi baadhi
walimuuita Eddy alipo kuwa akishuka kwenye gari
lake.
“Ni kwa nini umeamua kuwakamata watumishi wa
bwana Mchungaji Mandingo na Madam Grory?”
Muandishi mmoja wa gazeti la Habari Sasa
alimuuliza waziri Eddy Godwin
“Siwezi kuzungumza lolote kwa sasa, ila huo ni
mwanzo tu waujibikaji wangu, ila kazi inaendelea”
Eddy alijibu na kuomba kupishwa kukiwahi kikao
cha wakuu wa jeshi la polisi ambao tayari
wamesha wasili kwenye ukumbi wa mikutano
tangu saa mbili asubuhi. Eddy hakuwa na haja ya
kwenda ofisisni kwake moja kwa moja akaelekea
katika ukumbi wa mkutano, Akawakuta wakuu wote
wa jeshi la polisi, kutoka mikoani mwote wakiwa
wanamngojea.
“Wakubwa zangu shikamoni” Waziri Eddy
alisalimia kwani watu wote waliomo ndani ya ofisi
yake wamempita umri mkubwa sana na wengine ni
sawa na baba zake. Kila mmoja akaitikia salamu
hiyo
“Samahani kwa kuchelewa kuweza kuwahi kwenye
kikao, ila hakuna kilicho haribika.” “Lengo la
kuwaita hapa ninahitaji kujadiliana nanyi,
kuhusiana na watendaji wenu katika mikoa yenu.”
“Napenda kujua ni nini kilicho pungua kwenye
idara yenu kuanzia madai munayo idaia serikali ili
yaweze kulipwa haraka iwezekanavyo” Eddy
alizungumza na kuwatazama wakuu wote walio fika
kwenye kikao hichi. Mmoja akanyoosha kidole na
kuzungumza.
“Mkuu hapo kinacho tusumbua kwanza ni ufinyu
wa mishahara kwa vijana wetu, mishahara
kupungua na mazingira mabaya ya nyumba
wanazo ishi kambini. Magari ni machakavu,
piklikipi za doria ni chache kwahiyo inapelekea
vitendo vingi vya uhalifu kufanyika katika nchi
yetu”
“Asante nitalishuhulikia, mwengine” “Muheshimiwa
sisi tunahitaji sihasa isiingizwe kwenye majeshi
kama hawa wezako walio pita kwa maana
walikuwa wakituletea siaaa kwenye kazi zetu na
kujikuta vijana wetu wakishindwa kufanya kazi kwa
amani, jambo linalo pelekea uhalifu kuzidi
kuongezeka” “Asante baba yangu, ngoja niwatoe
hofu kwenye hili. Mimi si mwana siasa na wala
sina chama ila ninanchi. Labda nitoe rai moja
kwenu. Musidanganyike na mwanasiasa yoyote.
Yoyote ambaye ataingia kwenye jeshi la polisi,
kama muhalifu hakikisheni munamuua na si
kumuacha hai” Wazo la waziri Eddy Godwin
likawafanya wakuu wengi wa jeshi kushangaa
kwani hawakutegemea kupata wazo kama hilo
kwenye kikao hicho.
“Muheshimiwa kumbuka kwamba sisi ni jeshi la
polisi kazi yetu ni kulinda wananchi na mali zao.
Sasa unapo sema tuwaue inakuwa ni kazi kidogo
kwetu huoni kwamba tutakuwa na sifa mbaya?”
“Samahani baba yangu kwa majibu haya nitakayo
kupa, ila kiukweli hadi sasa hivi nyinyi muna sifa
mbaya mbaya mbaya zaidi ya shetani na ubaya
wake. Wahalifu wengi tupo nao huku juu serikalini.
Wanawatumikisha vijana wadogo wanakamatwa na
kufungwa, ila muzizi ipo inaendelea kuzalisha
matatizo mengine mengi kwenye ngi hii. Sasa hii
ni amri wala sio ombi, na lolote litakalo fanyika
basi mimi nitakuwa muwajibikaji katika kuyajibu
hayo ICC” Baadhi ya wakuu wa polisi wakapiga
makofi kwa ujasiri anao uonyesha kijana mdogo
mwenye mamlaka makubwa kwenye nchi hii.
“Tumekuelewa muheshimiwa” “Asanteni kwa
kunielelewa, ila wapeni tahathari vijana wenu.
Nitakuwa nikizunguka zunguka kwenye kila mkoa
na vituo vyote kisiri pasipo wao kujua, endapo
nitaumdua kuna ubadhilifu wowote kwa wananchi
basi, kijana huyo au hao watawajibika katika hilo.
Asanteni kwa muda wenu”
***
“Mbona unatabasamu?” Madam Mery alimuuliza
mzee Godwin
“Kijana wangu, niliye potezana naye muda yupo
hai” “Ni nani?” “John” “John yupi?”
“Yule aliye kua mwanafunzi wako” Furaha ya mzee
Godwin na Madam Mery ikazidi kuongezeka kwani
mtu waliye kuwa wanamtegemea kwenye mipango
yao wamepata ujumbe wake kwa njia ya simu.
“Sasa yupo wapi?” “Yeye mwenyewe hakuniambia
kwamba yupo wapi ila atanijulisha kwamba yupo
wapi” “Sawa”
“Ila itabidi kuunda kikosi chenye nguvu na safari
hii, Eddy nilazima afee” Mzee Godwin alizungumza
huku akiachia tabasamu pana usoni mwake,
macho yake akiwa amemtazama Madam Mery.
***
“Mume wangu huoni kama unalo lifanya ni jambo
la hatari kuwakamata hao watumishi wa Mungu”
Phidaya alizungumza kwa saut ya unyonge huku
akimuandalia mumewe chakula cha usiku
“Haiwezi kuwa hivyo mke wangu, na wale si watu
wa Mungu kama munavyo dhani nyinyi ni waovu
sana”
“Wamefanya nini watu wa watu?” “Wale ndio wanao
jihusisha na mauaji ya walemavu wa ngozi na
kuingiza madawa ya kulevya nchini” “Wewe
umejuaje?” “Wao wenyewe wanadai hilo, ila
uchunguzi unaendelea kufanyika mambo yakiwa
sawa nitakujulisha” “Mmmm ila kua makini mke
wangu nisinge penda kuona unarudi kwenye
matatizo kama ilivyo kua awali”
Phidaya alizungumza huku akimsogelea mume
wake na kumkumbatia mumewe anaye onekana
kutawaliwa na mawazo mengi baada ya kazi
ngumu,
“Shamsa yupo wapi?” “Yupo ndani amelala”
“Nenda kamuite. Ninamazungumza naye kido”
Phidaya akanondoka na kupandisha ngazi za
gorofani na kwenda chumbani kwa Shamsa,
akamkuta Shamsa akiwa anasoma kitabu cha My
Mommy’s friend.
“Bado hujamaliza kusoma kitabu chako?” “Ahaaa
bado hichi kitabu kimenichanganya” “Kwani
amekiandika nani?” “Jamaa mmoja anaitwa
Eddazaria Gershom Msulwa”
“Haya weka pause baba yako anakuhitaji yupo
chini, huko anakula” Shamsa akaongozana na
Phidaya hadi alipo Eddy, wakamkuta akiendelea
kula taratibu huku mawazo mengi yakiendelea
kukitawala kichwa chake
“Vipi umefanya kazi ile nilioyokuagiza?” Eddy
alizungumza kwa sauti iliyo jaa uchovu mwingi.
“Kazi ipi baba?”
“Ile ya kutafuta chuo cha udaktari?” “Ndio baba, ila
bado hadi sasa hivi sijapata chuo kizuri” “Basi
kesho nitaulizia ofisini, je india si unaweza kwenda
kusoma?” “Ndio baba”
“Poa, basi wewe jiandae muda wowote nikipata
chuo ukusanye virago ukasome” “Sawa baba”
Shamsa akaondoka akiwa na furaha sana moyoni
mwake kwani ni moja ya ndoto zake kuja kuwa
daktari bingwa wa magonjwa ya wamama na
watoto.
Eddy akamaliza kula na kuingia ndani kwake na
kujitupa kitandani, usingizi mzito ukampitia.
***
Siku zikazidi kukatika huku hofu kubwa ikaanza
kutawala katika vikundi vya majambazi ambao
mara nyingi waliweza kuyafanya matukio yao kwa
kujiamini sana, wakiamni kwamba wapo baadhi ya
wakuu wa serikali wanaweza kuwatetea, pale
wanapo kamatwa. Mfano ukaanza kwa majambazi
walio teka gari la abiria katika mkoa wa Kagera,
Kwa bahati mbaya au nzuri, gari ya polisi iliweza
kufika katika eneo la tukioa ambapo wakafanikiwa
kuwatia nguvuni majambazi wanne. Kutokana na
agizo la waziri wa ulinzi Eddy Godwin, majambazi
wote walipigwa risasi za kichwa mbele ya abiria
walio kuwa wametekwa, ikiashiria kwamba jeshi la
polisi lilianza kufanya kazi yake kama ilivyo paswa
kufanya.
Taratibu wananchi wakaanza kurudisha imani zao
katika jeshi la polisi, huku wakianza kumsifu
kichini chini waziri wa ulinzi ambaye kwa mara ya
kwanza walihisi atakua ni mbabaishaji kwao.
Utendaji kazi wa waziri mpya bwana Eddy Godwin,
ukaanza kuzua mtafaruku kwenye bunge, huku
baadhh ya wabunge wali,subiri kwa hamu, mbunge
huyo kwenye kipindi cha maswali na majibu,
ambacho kimeanza leo,
“Mke wangu, leo nipo kikaangioni naomba
uniombee” Eddy alizungumza kwa kupitia simu
akiwa ndani ya chumba cha hoteli aliyo fikizia mjini
Dodoma
“Upunguze hasira kwa maana ninavyo kujua wewe,
unaweza kumng’oa mtu meno”
Phidaya alizungumza kwa sauti ya ipole iliyo jaa
usingizi mzito kwani ni alfajiri na mapema aliweza
kuanshwa na mlio wa simu iliyo pigwa na
mimewe.
“Siwezi mke wangu, unajua tangu nimepewa haya
madaraka nimejikuta nikiwa mstaarabu sana”
“Sawa mume wangu, mimi nakutakia kila la heri
katika hilo” “Asante mke wangu”
“Alafu nilikua nimesahau kukukumbusha, Shamsa
leo anaondoka na ndege ya saa tisa alasiri kwenda
India” “Ahaaa, hata mimi nilikua nimesha jisahau.
Lakini si kila kitu mumesha kikamilisha?” “Ndio”
“Junio bado yupo kwa bibi yake?” “Ndio, jana
nimekwenda kumchukua kakataa kata kata yaani
sijui nitaishije peke yangu kwenye hili jumba”
“Usijali mke wangu, nikipata nafasi nitachomoka
mara moja kuja kukuona, Au unweza kwenda
kukaa kwa mama kama unaogopa”
“Sawa mume wangu, nakupenda sana”
“Nami pia ninakupenda” Phidaya akambusu Eddy
kama mazoea waliyo yajenga kwenye mahusiano
yao, pale wanapo kua wakiwasiliana kwa simu,
mmoja wao anaweza kuanza kumbusu mwenzake,
Eddy taratibu akanyanyuka kitandani, akaingia
bafuni na kuoga kisha akarudi chumbani,
akafungua kabati alilo weka suti yake ya kuvaa siku
hiyo, akaivaa taratibu hadi akamaliza. Akaweka kila
kitu chake sawa. Kisha akampigia simu mzee
Selemani Mbogo, ajitayarishe kwa safari ya
kuelekea bungeni/
“Mimi mbona nipo tayari, mwanangu ninakusubiria
wewe tu” “Sawa ninakuja baba yangu”
Eddu a;ipo hakikisha kila kitu amekiweka sawa,
akatoka chumbani kwake na moja kwa moja
akaelekea mapokezi ambapo akakutana na askari
anaye mlinda, na wote kwa pamoja wakeelekea
kwenye gari. Haikuchukua dakika nyingi wakawa
wamefika bungeni, tayari waandishi wa habari wa
mashirika mbalimbali wakamvamia kumuhoji
maswali mawili matatu.
“Una lipi la kuwaambia wananchi juu ya ulinzi wao
na mali zao?” Muandishi wa gazeti la FURAHA LEO,
aliuliza
“Ulinzi unaendelea kuhimarika kikubwa
ninawaambia wasiwe na mashaka na jeshi zima.
Asanteni ninawahi ndani”
Eddy kwa msaada wa askari anaye mlinda
akaondoka mikononi mwa waandishi wa habari na
kufanikiwa kuingia ndani, ya bunge moja kwa moja
akelekea kwenye kiti chake kilichopo karibu sana
na sehemu ya kujibia maswali atakayo ulizwa na
wabunge wezake pamoja na mawaziri. Kama ilivyo
kawaida ya wabunge kusimama pale anapo ingia
spika wa bunge, akafika kwenye kiti chake ambapo,
akasoma sala ya kuliombea taifa kwa ujumla
pamoja na bunge tukufu, kisha shughulii za
kibunge zikaanza.
Macho na masikio ya wananchi wengie
waliyaelekeza kwenye, televishion pamoja na redio
zao kuweza kusikia kitakacho jibiwa na waziri huyu
mpya ambaye utendaji wake wa kazi ni tofauti sana
na mawaziri wengine ambao, wamepita kwenye
sekta yake ya ulinzi. Waziri Eddy Godwin akaanza
kusoma taarifa fupi kuhusiana na wizara yake
tangu aweze kuachiwa madaraka na waziri aliye
pita.
“Muheshimiwa spika, wizara yangu ya ulinzi, hadi
sasa hivi utendaji wake umekua ni mzuri japo
bado tunaendelea kufanyia kazi baadhi ya maeneo
ikiwemo, kuendelea kuwalipa watumishi wa jeshi la
polisi madai ya mishaara yao ambayo, hadi
ninaingia madarakani, walikua wakiidai serikali
kiasi cha shilingi bilioni kumi na nusu.” “Pesa hizo
hadi leo nimeweza kukabidhiwa shilingi bilioni
mbili tu, huku nikiambiwa kuweza kusubiri mwaka
wa serikali uweze kufika jambo ambalo inaonyesha
kuna ukiritimba unao endelea ndani ya serikali
hususani kwenye sekta ya fedha, Labda niseme
kitu kimoja kwenye serikali yangu tukufu. Sinto
mfumbia macho kiongozi yoyote awe ni raisi au
nani, endapo nitabaini kwamba anahusika kula ela
ya uma na kuwapa shida watendaji wadogo, basi
nitahakikisha sheria inachukua mkondo, Asanteni”
Risala ndogo ya waziri Eddy Godwin, ikawastua
baadhi wa viongozi, kwani tayari wamesha anza
kuziona cheche za kijana huyo ambaye ni waziri
aliye chaguliwa na muheshimiwa raisi bwana
Praygod Makuya.
“Nakaribisha maswali na majibu”
Spika wa bunge akatoa nafasi kwa mbunge wa viti
maalumu kuweza kuuliza maswali yake kwa waziri
wa ulinzi bwana Eddy Godwin.
“Muheshimiwa spika swali langu la kwanza kwa
huyu waziri mpya, Je anasifa za kuingia humu
bungeni na kukabidhiwa wizara hiyo. Pili mbona
kama amerithishwa kutoka kwa waziri mkuu aliye
pita, tatu umri wake ni miaka mingapi? Asante
muheshimiwa naibu spika”
Macho ya Eddy yakamtizama mama huyo aliye
zungumza kwa asauti kali akionyesha dhahiri
amejenga chuki dhidi yake,
“Laiti ningekua si waziri, ningekushushia matusi
hadi ujisikie vizuri”
Eddy alijikuta akiropoka pasipo kuzima kinasa
sauti chake(maiki), Jambo lililo wafanya watu
wengi kushangaza na hiyo kauli.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 4 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM(4)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storyzaeddy.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Spika wa bunge akatoa nafasi kwa mbunge wa viti
maalumu kuweza kuuliza maswali yake kwa waziri
wa ulinzi bwana Eddy Godwin.
“Muheshimiwa spika swali langu la kwanza kwa
huyu waziri mpya, Je anasifa za kuingia humu
bungeni na kukabidhiwa wizara hiyo. Pili mbona
kama amerithishwa kutoka kwa waziri mkuu aliye
pita, tatu umri wake ni miaka mingapi? Asante
muheshimiwa naibu spika”
Macho ya Eddy yakamtizama mama huyo aliye
zungumza kwa asauti kali akionyesha dhahiri
amejenga chuki dhidi yake,
“Laiti ningekua si waziri, ningekushushia matusi
hadi ujisikie vizuri”
Eddy alijikuta akiropoka pasipo kuzima kinasa
sauti chake(maiki), Jambo lililo wafanya watu
wengi kushangaza na hiyo kauli.
ENDELEA
Eddy akajikuta akimtazama mama huyo kwa hasira
kali kwani maswali aliyo yauliza hayakuwa na tija
yoyote kwake, isitoshe swali lililo mkera zaidi ni
lile la kuambiwa kwamba ameridhishwa uongozi
huo kutoka kwa mama yake ambaye alikuwa ni
waziri mkuu wa Tanzania. Kamera zaote za
vyombo vya habari vilivyo kua ndani ya bunge,
vikamuelekea Eddy, huku baadhi ya makamera
man, wakiivuta sura ya Eddy akiwa amekasirika,
gafla hali ya Eddy ikabadilika na kuachia tabasamu
pana, lililo mfanya mke wake Phidaya kushusha
pumzi kubwa kwani anamuelewa vizuri sana mume
wake akiwa amekasirika.
“Nianze kukujibu hivi, Moja sina sifa ya kuongoza
wizara hii, kwasababu mimi sio mwama siasa ila
nina uwezo wa kuiongoza kwa sababa ninajua nini
ninafanya.”
“Mbili umri wangu haukuhusu, kwani kwa uzee
wako wewe mama, ila unaonekana una akili ndogo
kama mtoto wa chekechea.”
“Tatu, sijaridhi uongozi, ila raisi wangu mtukufu
ndio ameniteua kuchukua hii nafasi baada ya
wanasiasa wezako kushindwa, Asante”
Majibu ya Eddy yakepelekea wabunge baadhi
kupiga makofi kwenye meza zao ikiashiria kwamba
wamependezwa na majibu yake huku baadhi yao
wakionekana kukasirishwa na majibu hayo ya
kebehi kutoka kwa kijana mdoho huyo.
“Muhesimiwa muongozoo”
Mbunge mmoja alizungumza pasipo kuruhusiwa
na spika wa bunge, ikamlazimu spika wa bunge
kumruhusu mbunge huyo.
“Muheshimiwa spika, katika kifungu cha maadili
mwaka 1979 namba 11, kina sema hivi ninanukuu.
Si ruhusa kwa mbunge yoyote au waziri kutoa
lugha ya kudharau mwengine, akitokea mmoja
wapo akakiuka hilo basi inampasa aweze kuomba
radhi. Mwisho wa kunukuu. Tunamuomba waziri
wa ulinzi kuweza kuomba Radhi kwa kumdharau
mbunge wa viti maalumu kwa kumlinganisha akili
zake kama mtoto wa chekechea.”
Mbunge huyo akakaa kwenye kiyi chake na
kuwafanya wanao muunga mkono katika hilo
kuweza kupiga madawati yao na kuifanya sauti ya
madawati yao kuizidi sauti ya walio muunga Eddy
kwa majibu yake.
“Waziri wa ulinzi, unatakiwa kuomba Radhi kwa
lugha hiyo”
Spika wa bunge alizungumza huku akimtazama
Waziri Eddy Godwin katika sehemu aliyo simama.
“Mungu wangu…..!!! Kwa bahati mbaya
mumekosea sana kutamka swala la mimi kuomba
radhi, ninasema hivi siwezi kuomba radhi kwa
mshenzi mmoja ambaye yeye na wezake humu
ndani wanajihusisha na uuzaji wa madawa ya
kulevya, ufisadi na mambo mengine. Hembu ngoja
niwaambie kitu kimoja mimi sio mwana siasa na
hakuna ambaye anaweza kunifanya chochote
kutokana ninasimama kwenye sheria ya kuwatetea
wananchi na walala hoi ambao maisha yao
yanazidi kua magumu kutokana na wajinga
wachache kama huyo mama na huyo mwehu
mwengine aliye nitaka mimi kuomba radhi,
musahau juu ya hilo swala na wale wote ambao
wanajijua wana mijidudu yao wanaifanya huko nje
wajiweke tayari kwani vita imeanza, nitamkamata
mmoja baada ya mwengine. Asanteni”
Ukumbi mzima wa bunge ukatawaliwa kwa fujo za
maneno, ya baadhi ya wabunge ambao walihisi
wametukanwa na kijana huyu mdogo, huku
wengine wakionekana kushangilia kwa ujasiri
ambao ameuchukua kijana huyo ambaye ni mpya
kuingia kwenye bunge hili tena akiwa na cheo cha
waziri wa ulinzi.
“Jamani waheshimiwa wabunge ninaomba mutulie”
Spika wa bunge akawa na kazi ya ziada kuweza
kuwanyamazisha wabunge hao kutulia, Eddy
hakubanduka kwenye sehemu aliyo simama,
macho yake yakawa na kazi ya kuwatazama
wabunge walio nyanyuka akiwemo aliye muhitaji
aweze kuomba radhi, akionekana akiwa na jazba
kubwa sana akitamani kushuka kwenda
kumtandika Eddy pale alipo kwani anamfananisha
na mwanaye wa mwisho kabisa. Spika wa bunge
akafanikiwa kutuliza ghasia hizo zilizo zuka gafla
bungeni.
Wananchi walio sehemu mbali mbali, wakajikuta
mioyo yao ikizidi kumpenda waziri Eddy ambaye
anaonekana kuwa yupo tofauti sana na viongozi
wengine
“Aisee chalaa wangu, tungepata mawaziri kumi
kama hawa, ninaimani nchi ingenyookoa hii”
Alisikika mchaga mmoja akiropoka katikati ya
walevi ambao, wanaendelea kuburudika na unywaji
wa pombe ya mbege mapema hii na asubuhi.
“Tunaendelea na maswali”
“Asante sana muheshimiwa spika, kwanza
ningependa kumpongeza muheshimiwa Eddy kwa
majibu yake, kusema kweli ni viongozi wachache
ambao wanaujasiri wa kujibu kama alivyo jibu
bwana Eddy. Kusema kweli muheshimiwa Eddy
wewe kaza buti achana nao hawa walanguzi wa
mali za uma, langu ni hilo kaka”
Mbunge mwengine ambaye anaonekana ni kijana,
alijitoa muhanga kumsifia Eddy ambaye kwa muda
mchache umaarufu wake, ukazidi kuongezeka
kwenye mitandoa mingi ya kijamii, huku picha zake
zikiwekwa kwenye mitandao kama facebook,
twitter, jamii forams, whatsapp na kadhalika, huku
kukiwa na maandishi kwenye picha yeki yanayo
sema. (“UNAAKILI NDOGO KAMA MTOTO WA
CHEKECHEA)
Amani ikazidi kutoweka kwa baadhi ya viongozi
ambao, wanamambo ambayo ni kinyume na
maadili ya kazi zao. Kila mmoja akaanza kutuma
ujumbe wa simu kwa watu wanao shirikiana nao
ambao si viongozi wakiwaomba waweze kua
makini kwani hali ya kazi zao hizo ipo hatarini.
{MUHESHIMIWA USIWE NA SHAKA HIZO NI NGUVU
ZA SODA}
Meseji moja ikaingia kwenye simu ya mbunge
mmoja ambaye alikua akiendelea kusikiliza majibu
na maswali ambayo anaendelea kuyatoa waziri
Eddy Godwin. Msisimko wa bunge ukazidi
kuongezeka, kwa wananchi ambao mara kwa mara
walisikika wakimzungumzia Eddy ambaye
anaendelea kuwapasha baadhi ya wabunge.
“Natoa agizo kwa jeshi la polisi kuanzia kesho,
wahakikishe kwamba baa zote zinaanza kufanya
kazi kuanzia saa tisa jioni, watakao kiuka agizo
hatua za kisherika zichukuliwe, Asanteni”
Eddy akamalizia kwa kutoa agizo na kuwafanya
wabunge wanao muunga mkono kumpigia makofia
ya kumpongeza huku wanao mchukia wakikaa
kimya. Bunge likahairishwa hadi jioni na wabunge
wote wakapata muda wa kwenda kupumzika.
Waandishi wa habari wakajiandaa kwa kuweza
kumuhoji maswali waziri Eddy huku swali lao
kubwa wakihitaji kumjua ni nani anaye jihusisha na
mtandao wa madawa ya kulevya,
“Bado mapema sana, ila watakua hadharani hivi
karibuni, naombeni nikapumzike nijiandae kwa
kikao kijacho”
Eddy akaondoka na kuingia ndani ya gari lake.
Wakarudi hotelini walipo fikizia moja kwa moja
akaelekea chumbani kwake huku akiwa na askari
anaye mlinda, baada ya kuufungua mlango akaingia
askari wake na kukikagua chumba kisha
akamruhusu Eddy na yeye kuingia ndani ya
chumba hicho kisha askari huyo akatoka nje. Eddy
akajiputa kitandani huku akionekana akiwa
amechoka sana kwa shuhuli nzima ya kujibu
maswali ambayo mengine hayakumuhusu yeye ila
kutokana yupo kwenye wizara hiyo ilimpasa
kuweza kuyajibu kikamilifu.
“Hii kazi kweli ngumu mmmmmm”
Alizungumza huku akiwa amejilaza kitandani, akiwa
anaendelea kujizungusha zungusha kitandani, ili
kuupumzisha mwili wake, simu yake ikaita akaitoa
mfukoni, na kukuta namba ngeni ikiwa inaita,
akaipokea na kuiweka sikioni taraibu.
“Habari”
Eddy alinza kumsalimia mtu huyo aliye mpigia
simu hiyo.
“Hahahahaa, Eddyyyyyyy. Wewe pia ni jasiri kama
mama yako si ndio?”
Sauti ya mzee Godwin ilisikika upende wa pili wa
simu jambo lililo mstua sana Eddy kwani
hakutegemea kusikia sauti ya baba yake huyo
ambaye ni adui yake nambari moja
“Naamini kwamba, utakua unajiuliza namba yako
nimeitoa wapi, ila usijali ni swali dogo sana hilo, na
jibu lake namba yako amenipa mwanangu…..”
“Mwanao nani?”
Eddy aliuliza kwa sauti ya ukali, iliyo mfanya mzee
Godwin kuangua kicheko cha dharau
***
Kazi ambayo walianza kuifanya Mzee Godwin na
Madam Mery ni kuweza kuchunguza ni wapi anapo
ishi Eddy, ikawalazimu kufunga safari hadi nchini
Tanzania wakitumia basi wakitokea Nairobi nchini
Kenya, ambapo walipitia mpaka wa horohoro
uliopo Tanga, moja kwa moja wakafika Tanga
mjini, ambapo kwa kutumia basi wakaweza kufika
jijini Dar es Salaam, wakachukua chumba katika
holel ya HOLDAY INN, na taratibu wakaanza
kufanya upepelezi wa kugundua ni wapi anapo ishi
Eddy.
Haikuwa ni kazi ngumu sana kwao kuweza
kupatambua anapo ishi Eddy, hii ni kutokana na
jina lake kuzungumza sana midomoni mwa watu
wali wengie wakiukosoa uteuzi wa raisi bawa
Praygod Makuya juu ya kiongozi huyu Eddy. Siku
walio weza kupafahamu nyumbani kwa Eddy ni
siku ambayo Eddy, yupo bungeni kwenye kipindi
maalimu cha maswali na majibu, dereva taksi
mmoja aliweza kuwapeleka nyumbani kwa Eddy
bwana Godwin na Madam Mery.
“Nyinyi ni kina nani?”
Askari anaye linda geti la Eddy alimuuliza Mzee
Godwin kimashaka, kwani sura ya mzee Godwin,
inaendana sana na sura ya bosi wake Eddy
“Hivi ukinitazama unahisi mimi ni nani kwa Eddy?”
Mzee Godwin, alijibu kwa mtindo wa kuuliza swali
kwa askari huyo, aliye bakia akimtazama Mzee
Godwin, kwa umakini. Taratibu akajikuta akifungua
geti na kuwakaribisha mzee Godwin na Madam
Mery. Pasipo kuwakagua kwa kifaa maalumu
ambacho hukitumia kumkagua kila aingiaye ndani
ya jumba hilo la kifahari.
“Wenyewe wapo?”
“Yupo tu mama, twende niwapeleke”
Askari huyo alizungumza huku akitangulia kwenda
sehemu alipo kaa Phidaya, kwenye moya ya
kibanda cha kupumzikia chenye Tv kubwa,
akiendelea kufwatilia bunge hilo, akimshuhudia
mumuwe jinsi anavyo jibu maswali kwa kujiamini.
Hatua chache mbeleni, Mzee Godwin akatoa
bastola yake pasipo askari kugundua lolote, kwa
nguvu akapiga askari kichwani kwa kutumia kitako
cha bunduki na kumfanya aanguke chini mzima
mzima na kuzimi.
“Mbona hivi….!!?”
Madam Mery alilishangaa tukio hilo la mzee
Godwin, kumfanyia askari huyo.
“Najua nini nafanya”
Kutokana walisha kiona kibanda alicho kaa
Phidaya, ambaye akili na mawazo yake yote
ameyepeleka kwenye bunge hilo, hakulishuhudia
tukio la askari wao kupigwa. Mzee Godwin na
Madam Mery wakafika sehemu alipo kaa Phidaya.
“Habari”
Madam Mety alianza kumsalimia Phidaya na
kumfanya astuke, baada ya kumuona mzee Godwin
akikaa kwenye kiti cha karibu yake, huku mkononi
mwake akiwa ameshika bastola.
“Mwanangu amejitahidi sana, ameoa
shombeshombe”
Mzee Godwin alizungumza huku akizishika nywele
ndefu za Phidaya na kuzisogeza puani mwake na
kuzinusa
“Mmmmmm, zinanukia marashi mazuri sana”
Mzee Godwin aliendelea kuzungumza kwa sauti ya
kebehi, iliyo zidi kumuogopesha Phidaya ambaye
hakujua afanye nini kwa wakati huo, na laiti ange
dhubutu kunyanyua kinywa chake, labda ungekua
ndio mwisho wa maisha yake.
“Bunge limeisha, badilisha chaneli”
Mzee Godwin alizungumza huku akimpa rimoti
Phidaya, ambaye mwili mzima unamtetemeka kwa
woga. Madam Mery muda wote akawa na kazi ya
kumdhaminisha Phidaya kuanzia chini hadi juu,
huku akiwa haamini kwamba Eddy, ameweza
kumiliki mwanamke mwenye vigezo vyote kuanzia
chini hadi juu.
“Nipe namba ya mumeo”
“Eehee”
“Nipe namba ya mumeo, hujanisikia?”
Phidaya kwa uwoga akaichukua simu yake aliyo
kua ameiweka pembeni ya glasi iliyo jaa juisi ya
embe, vyote kwa pamoja vikiwa juu ya meza ya
kioo iliyopo ndani ya kibanda hicho. Kwa
kutetemeka Phidaya akaitafuta namba ya simu ya
mumewe na kumuonyesha Mzee Godwin, ambaye
taratibu akainadika kwenye simu yake na kuipiga
namba hiyo.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 5 YA SIMUHILI HII.
 
RRY MADAM(5)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storyzaeddy.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
“Nipe namba ya mumeo”
“Eehee”
“Nipe namba ya mumeo, hujanisikia?”
Phidaya kwa uwoga akaichukua simi yake aliyo
kua ameiweka pembeni ya glasi iliyo jaa juisi ya
embe, vyote kwa pamoja vikiwa juu ya meza ya
kioo iliyopo ndani ya kibanda hicho. Kwa
kutetemeka Phidaya akaitafuta namba ya simu ya
mumewe na kumuonyesha Mzee Godwin, ambaye
taratibu akainadika kwenye simu yake na kuipiga
namba hiyo.
ENDELEA
“Mwanangu Phidaya”
Mzee Godwin alijibu kwa kujiamni, jambo lililo zidi
kumchanganya Eddy ambaye mapigo ya moyo
yakaanza kumuenda mbio, kwani uhasama wake
na Mzee Godwin ni mkubwa kupita kiasi.
“Nakuomba usifanye chochote kwa mke wangu,
nakuomba baba yangu”
“Mmmm leo ndio unajua kwamba mimi ni baba
yako?”
Mzee Godwin aliendelea kuzungumza kwa dharau
jambo lililo zidi kumpagawisha Eddy, kwani umbali
kutoka Dododma hadi Dar es Salaam, unachukua
muda mwingi sana kuweza kufika mbaya zaidi
bado anakipengele cha kumalizia bungeni kuweza
kujibu maswali atakayo ulizwa kama waziri wa
ulinzi, ambaye amechukua majukumu ya
kusimamia sekta zote za jeshi kuanzia polisi hadi
jeshhi la kujenga taifa, na wizara ya mambo ya
ndani ikatolewa katika usimamizi wa jeshi la polisi
na kubaki ikiendelea kusimamia mabo mengi na si
jeshi la polisi, ambalo lilihamishiwa kwenye wizara
ya ulinzi moja kwa moja
“Leo, mke wangu atanipikia chakula kizuriii,
kwahiyo usiwe na wasiwasi wowote, wewe endelea
kupiga kazi”
Baada ya kuzungumza hivyo mzee Godwin akakata
simu, na kuizima kabiasa kisha akamtazama
Phidaya ambaye bado anaendelea kutetemeka
mwili wake wote kwa woga mwingi ulio mtawala.
Madam Mery akatoa kitambaa cheupe kilicho
kunywa vizuri ambacho walikipulizia madawa ya
kulevya kisha akamkabidhi mzee Godwin.
Mzee Godwin akamsogelea Phidaya sehemu alipo
na kumziba na kitambaa hicho puani mwake,
Phidaya akajitahidi kushindana nguvu na mkono
wa mzee Godwin ulio mziba puani ila akajikuta
akishindwa, huku nguvu zikianza kumuishia
taratibu taratibu hadi akalala fofofo.
Mzee Godwin akambeba Phidaya begani na kuingia
naye ndani, ambapo wakamlaza kwenye moja ya
sofa kubwa walilo likuta hapo sebleni, kisha
akaanza kuingia chumba kimoja baada ya kingine
kuweza kutafuta funguo ya gari walizo zikuta
zimewekwa sehemu maalu za maegesho. Madam
Mery yeye akawa na kazi ya kuchungulia
madirishani ili kuweza kuona nje kama kuna mtu
anaingia aweze kumstua mzee Godwin ambaye
anaendelea kuwajibika na utafutaji wa funguo hizo.
Mngurumo wa gari, ukisimama nje, ukamstua
Madama Mery aliye kuwa ameketi kwenye sofa, kila
mara akitazama tazama saa yake ya mkononi,
akihesabu muda jinsi unavyo kwenda. Akasimama
kwa haraka na kwenda kuchungulia dirishani,
akamuona mtoto mdogo wa kiume akishuka
kwenye gari hilo aina ya BMW Z8, huku akiwa
ameongozana na mtu anaye onekana kama ni
dereva. Kwa jinsi mototo huyo anavyo fanana na
Eddy moja kwa moja Madam Mery akagundua
kwamba huyo ni mtoto wa Eddy. Kwa haraka
Madam Mery akapandisha ngazi za kuelekea
gorofani, ambapo ndipo alipo Mzee Godwin. Kwa
bahati nzuri akakutana na Mzee Godwin akitoka
kwenye moja ya chumba akitaka kuelekea kwenye
chumba kingine.
“Vipi?”
“Kuna watu wanakuja”
Madam Mery alizungumza huku akihema kwani,
alizipandisha ngazi hizo zipatzo thelathini kwa
kukimbia
“Kina nani?”
Mzee Godwin alizungumza huku akitembea
kuelekea sehemu ambapo ataweza kuiona seble
vizuri. Mzee Godwin akamshuhudia mjukuu wake
Junio akiingia huku nyuma akiwa ameongozana na
dereva wa gari aliye mleta. Junio akamkimbilia
mama yake aliye lala kwenye sofa na kumrukia
kwa lengo la kumstua, ila hakufanikiwa kumstua
mama yeka kwani hakuweza kustuka wala
kutikisika, jambo lililo mpa wasiwasi mwingi Junio
na kumfanya anze kulengwa lengwa namachozi.
***
Eddy akajaribu kuipiga tena namba ya Mzee
Godwin iliyo toka kumpigia muda mchache ulio
pita ila haikupatiokana, wasiwasi mwingi ukazidi
kumsumbua Eddy, akajaribu kupiga kwa mara ya
pili ila hali ikawa ni ile ile ya kuto kupatikana kwa
namba hiyo. Akajaribu kuipiga namba ya mke
wake, ikaita pasipo kupokelewa.
“Mungu wangu?”
Eddy alizungumza huku akizunguka zunguka ndani
ya chumba huku jasho jingi likimwagika mwilini
mwake, na kujikuta akifungua vifungo vyote vya
shati lake. Eddy akafungua mlango na kuanza
kutembea kwenye kordo ndefu, ya hoteli aliyo
fikizia akielekea sehemu ya mapokezi, kabla
hajafika akakutana na askari wake anaye mlinda
“Vipi muheshimiwa”
“Nahitaji kwenda, Dar sasa hivi”
Eddy alizungumza kwa haraka huku akizidi kupiga
hatua kuelekea nje ya hotel hiyo kwenda kwenye
maegesho ya magari.
“Unakwenda kufanya nini muheshimiwa?”
“Mke wangu ametekwa, fanya hivi mpigie simu
naibu waziri, mkabidhi mafaili yangu yote na
kipindi cha pili yeye ndio atajibu maswali sawa”
“Sawa mkuu”
Eddy akafika kwenye gari lake, na kumkuta dereva
akiwa amejilaza.
“Shuka nipishe niendeshe”
Eddy alizungumza na kumfanya dereva wake
kustuka kutoka usingizini
“Mmmmm”
“Hujanisikia au, nimekuambia kwamba zunguka
upende wapili wa gari, tunahitaji kwenda Dar es
Salaam sasa hivi”
“Muheshimiwa ni jukumu langu mimi
kukuendesha”
“Wewe mzee, mimi ni nani yako? Nimekuambia
nipishe”
Eddy alizungumza kwa hasira na kumfanya mzee
Selemani Mbogo, kutii amri ya bosi wake,
akashuka kwa haraka na kuzunguka upende wapili
wa gari, askari akataka kuingia kwenye gari ila
Eddy akamzuia
“Wewe baki, hakikisha document zangu zote
unampa naibu waziri sawa?”
“Sawa mkuu”
“Naomba bastola yako”
Hapo askari akasita kidogo kuichomoa bastola
yake aliyo ichomeka kiunoni mwake, kwa ishara
Waziri Eddy akamuomba amkabidhi bastola hiyo,
taratibu askari huyo akaichomoa na kumpa bosi
wake. Eddy akaipokea na kuifunga mlango wa gari,
akaliwasha, akakanyaga mafuta pamoja na breki na
kuzifanya tairi za gari hilo kuserereka, na kutoa
moshi mwingi, kisha akaachia breki na kulifanya
gari hilo kuchoka kwa kasi, na kuwafanya watu
wlaiopo katika eneo la hoteli kushangaa.
Kwa bahati nzuri, waziri Eddy akafanikiwa
kuliingiza gari hilo barabarani, pasipo kuligonga
sehemu yoyote. Akawasha taa zote za gari,
akishiria kwamba anaomba nafasi kwa kila gari
lililopo mbele yake, Safari ikaanza ya kuelekea Dar
es Salaam, huku kila muda waziri Eddy akizidi
kuongeza mwendo wa gari hilo la serikali aina ya
Landcruser VX X8. Maombi ya Mzee Selemani
Mbogo, yakwa ni kumuomba Mungu wasiweze
kupata ajali kwani, mwendo anao tembelea bosi
wake ni mkali sana na endapo itatokea tatizo
kidogo inaweza kuwa ni ajlali kubwa, itakayo
waponda ponda hadi mifupa yao.
Macho ya Mzee Selemani Mbogo aliye kaa siti ya
pembeni, mwa Eddy, alishuhudia mlolongo wa gari
zipatazo sita zikiwa zimeongozana huku kati ya
hizo magari matatu yakiwa ni malori yenye trela,
mawili, mawili. Eddy hakujali kwamba wapo kwenye
kilima, alicho kifanya yeye ni kuanza kupita gari
moja baada ya jengine,huku mshale wa spidi mita
ukielekea kwenye spidi miambili na ishiri.
Kitendo cha kumaliza kilima hicho mabasi mawili
yanayo tokea Dar es Salaam, kwenda Dodoma,
yakawa yanakuja kwa kasi upande ambao wamuiba
ili kuweza kuyapita magari haya ambayo Eddy
alihisi kwamba yanakwenda kwa mwendo mdogo,
japo nayo pia yapo kwenye mwendo kasi.
Mzee Selemani Mbogo, akajikuta akiyafumba
macho yake, kwani ni mida chache zimebakia
kutoka pale walipo na kukutana na mabasi hayo
ambayo nayo yapo kwenye mwendo kasi. Alicho
kifanya Eddy ni kuzidi kuipeleka gari yake, upande
wa kulia, na kutoka kabisa nje ya barabara na
kuingia kwenye barabara ya vumbi,na kuyafanya
mabasi hayo yapite kwa kasi huku madereva wake
wakipiga honi zao. Yalipo pita magari hayo,
akairudisha gari yake ndani ya barabara ya lami,
na kuendelea kutembea kwa kasi ile ile, iliyo
wafanya maderava wa magari walio pitwa
kuishangaa gari hiyo ya serikali ambayo namba
zake zionaonyesha ni gari ya waziri wa ulinzi.
“Mmmmmm”
Dereva mmoja wa roli aliguna, huku akiishuhudia
gari hiyo, ikipandisha kilima kingine hadi
wanashusha ikawa imepotea kwenye uwepo wa
macho yao.
“Mzee wewe ni muoga sana eheee?”
Eddy alimuuliza mzee Selemani Mbogo, baada ya
kumtazama na kumkuta amefumba macho yake
pasipo kuyafungua.
“Eheee….!!”
Mzee Mbogo akakosa jibu zaidi ya kuendelea
kushangaa wala hakujua ni jinsi gari, Eddy aliweza
kuyakwepa mabasi hayo ambayo walikuwa
wagongane nayo uso kwa uso. Kwa mwendo kasi
wa gari,alio utumia Eddy, hadi wanafika Morogoro
mjini, walitumia masaa mawili na nusu, kuingia
kwenye ardhi ya mkoa huo.
Eddy akapunguza mwendo wa gari, kuepuka
kugonga baadhi ya wandesha pikipiki waliopo
Morogoro mjini, alipo pata nafasi ya kukikiacha
kiplefti cha Morogoro mjini, kasi ya gari lake
ikaongezeka, tena ikwa ni rahisi sana kwake
kutokana barabara hiyo imenyooka sana, na
magari yanayokwenda kwenye barabara hiyo mengi
yanakwenda kwa kasi
“Nipe lisaa, nitakua nimesha ikanyaga mbezi, na
kama hakuna foleni huu mchana hdi lisaa na nusu
nitakua nyumbani”
Eddy alimuambia Mzee Mbogo na kumfanya abaki
ameduwaa, pasipo kujibu kitu chochote kile.
***
“Mama, mama mamaaaa”
Junio alimuita mama yake huku anamtingisha, ila
mama yake hakustuka kabisa na kumfanya Junio
kuanza kulengwa lengwa na machozi.
“Ka Devi mama amekufaaa”
Junio alimuambia dereva wa bibi yake, kwa haraka
Devi akamsogelea Phidaya na kumuwekea kiganja
cha mkono kwenye kifua chake, mapigo ya moyo
akayasikia yakifanya kazi kwa mbali sana, jambo
lililo anza kumstua Devi mwenye. Devi akachukua
simu yake na kumpigia bosi wake mama Eddy.
“Tunafanyaje sasa?”
Madam Mery aliuliza huku mwili ukimtetemeka,
“Tuwaue wote wawli”
Mzee Godwin alizungumza huku akiikoki bastola
yeka.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 6 YA SIMUHILI HII.
 
ORRY MADAM(6)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogsport.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
“Ka Devi mama amekufaaa”
Junio alimuambia dereva wa bibi yake, kwa haraka
Devi akamsogelea Phidaya na kumuwekea kiganja
cha mkono kwenye kifua chake, mapigo ya moyo
akayasikia yakifanya kazi kwa mbali sana, jambo
lililo anza kumstua Devi mwenye. Devi akachukua
simu yake na kumpigia bosi wake mama Eddy.
“Tunafanyaje sasa?”
Madam Mery aliuliza huku mwili ukimtetemeka,
“Tuwaue wote wawli”
Mzee Godwin alizungumza huku akiikoki bastola
yeka.
ENDELEA
“Godwin……!!!”
“Nini?”
“Usiwaue, kwani hawana hatia yoyote”
Madam Mery alizungumza kwa sauti iliyo jaa upole
kwani hakuamini kama Godwina atachukua uamuzi
huo haswa kwa Junio ambaye fika amefanana naye
sana, ikiashiria kwamba hiyo ni damu yao, japo ni
Eddy ni mtoto wa mdogo pacha wake.
“Ndio mama, tumefika nyumbani hapa tumekuta
mama anamatatizo”
Devi alizungumza kupitia simu, huku akizunguka
zunguka zunguka sebleni
‘Mpeleke hospitalini’
Sauti ya bibi Junio, ilisikika kwenye simu ya Devi,
akizungumza huku akiwa na wasiwasi mwingi
“Sawa muheshimiwa”
Devi akakata simu na kuiweka mfukoni, kisha
akarudi kwenye sofa alilo lala Phidaya, akaikunya
mikono ya shati lake refu jeupe, kisha
akamnyanyua Phidaya aliye mzito kiasi,
“Junio fungua mlango”
Devi alizungumza na kumfanya Junio akimbilie
mlanoni na kuufungua mlango wa sebleni,
wakatoka nje, Junio akakimbia kwenye gari na
kufungua mlango wa gari, siti za nyumba. Devi
akamuingiza Phidaya ndnai ya gari kisha wao
wakaingia ndani ya gari na kuondoka kwa kasi
pasipo kugundua kwamba ndani ya jumba hilo
kulikuwa na watu ambao wamesababisha Phidaya
kuwa katika hali kama hiyo.
“Umeona sasa”
Mzee Godwin alizungumza kwa sauti ya ulali
akimfokea Madam Mery, aliye mshukuru Mungu
kwa upande mmoja, kwani hakuhitaji kuona damu
ya mtoto mdogo kama Junio ikimwagika mbele ya
macho yake.
“Lakini hilo sio lengo letu lililo sababisha sisi kufika
hapa”
“Wewe mwanamke utaniyumbisha kwenye mipango
yangu”
Mzee Godwin akafyatua risasi mbili, zilizlo tua
kifuani mwa Madam Mery na kumuangusha chini
huku akitoa ukelele wa maumivu huku akiwa
haamini kwa kile alicho kifanya mpenzi wake huyo
“G..ood..win kweli unaniu…a”
“Kufa pumbavu wewe”
Mzee Godwin alizungumza kwa hasira huku
akifungua kiwambo cha kuzuia sauti cha bastola
yake, amabyo kulisaidi kuzuia sauti ya risasi mbili
alizo mtandika madam Mery zisisikike nje. Mzee
Godwin akashuka kwenye ngazi haraka na kutoka
nje, akapiga hatua za kasi hadi nje ya geti ambalo
lipo wazi. Akatizama pande zote za barabara iliyo
tulia hakuona gari lolote, jambo lililo zidi
kumchukiza.
“Shiiiitii”
Mzee Godwin alizungumza huku akiwa amechukia
sana, akapita mtu wa bodaboda ya pikipiki,
akamsimamisha na kumuomba aelekee barabara
aliyo hisi, gari alilo pakizwa Phidaya ndipo lilipo
kwenda
***
Kweli ndani ya masaa mawili, Eddy akaingiza gari
lake kwenye geti lake alilo likuta wazi, Wasiwasi
mwingi ukamuingia, akashuka ndnai ya gari huku
akiwa na bastola aliyo pewa asakri wake. Mzee
Selemani Mbogo naye akashuka kwenye gari huku
akimfwata Eddy kwa nyuma, wakafika kwenye
mlango wakuingilia ndani, tararibu Eddy
akausukuma mlango, huku kidole chake kimoja
kikiwa kwenye traiga tayari kwa kufyatu risasi kwa
yoyote atakaye jaribu kumfanyia shambulizi lolote.
Akachungulia ndani, ambapo kidogo kagiza
kametawala,
“Muheshimiwa”
Mzee Mbogo aliita kwa sauti cha chini, huku
akimuonyesha Eddy damu zinazo churuzika
kwenye ngazi zikitokea juu gorofani. Eddy kwa
hatua za haraka akaanza kutembea kuelekea
kwenye ngazi hizo, wasiwasi mwingi, ukamjaa
mwili mwake huku akiamini damu hiyo ni yamke
wake Phidaya. Akapandishia ngazi kwa haraka
hadi juu kabisa. Hakuamini macho yake baada ya
kumkuta Madam Mery akiwa amalala kwenye
sakafu, huku damu zikiendelea kumwagika kifuani
mwake taratibu,
“Huyu bado yupo hai”
Mzee Selemani Mbogo alizungumza baada ya
kuishika damu ya madam Mery inayotoka kwenye
kifua chake na kukuta bado niyamoto. Eddy
akatembea kwa haraka kuelekea kwenye chumba
cha Junio lilicho kua wazi, akaingia na kukuta
pakiwa pamachanguliwa vibaya.
Akatoka na kuiongia chumba cha Shamsa na
kukuta nacho kikiwa kimevurugwa mno, pia
hapakuwa na dalili yoyote ya kuwa na mtu
“Phidaya, Phidaya”
Eddy aliita kwa sauti ya juu huku akieeleka kwenye
chumba chao, akafungua na kukuta kikiwa
kimepangwa vizuri na hapakuwa na mtu aliye
pakanyaga humo ndani. Akarudi sehemu alipo
Madam Merya na kukuta mzee selemani Mbogo,
akimpa huduma ya kwanza Madam Mery
Eddy akaitoa simu yake mfukoni na kukuta ikiwa
imezima, akaiwasha na kukuta ikiwa imepungukiwa
na chaji, Mfululizo wa meseji zikaingia kwenye
simya yeka, huku nyingi zikiwa ni zamama yake.
(MKEO YUPO OCEA ROAD HOSPITAL, FANYA UFIKE
HARAKA)
Eddy kuisoma meseji hiyo, kidogo ikampa nguvu
hata ya kusaidia na mzee Selemani Mbogo
kumbeba Madam Mery ambaye hadi sasa hivi
maisha yake, yapo hatarini kupotea kwani ni damu
nyingi zimemtoka mwilini mwake.
“Endesha”
Eddy alimuambia Mzee Selemani, huku yeye
akipanda siti ya nyuma walipo mlaza Madam Mery,
huku kicha cha Madam Mery akikiweka mapajani
mwake, na kiganya cha mkono wake wakulia
akikiweka kwenye kifua cha madam Mery ili damu
isiendelee kumwagika. Wakaondoka na kwenda
hadi Hospitali ya Ocean Road, ambapo, wakaomba
masaada kwa manesi, ambao wakampakiza Madam
Mery kwenye kitanda cha kusukuma na matairi.
Moja kwa moja wakamkimbizi Madam Mery
kwenye chumba cha upasuaji, ili kuweza kutoa
risasi
“Eddy Eddy”
Eddy akageuka nyuma na kukutana na mama yake
akiwa amejifunga kitenge kiunoni mwake, huku
akijifuta kwa jasho
“Mama vipi, mke wangu yupo wapi?”
“Yupo chumba cha wagonjwa mahututi, hali yake
sio nzuri kabisa”
Eddy akaondoka na mama yake huku wakiwa
wameongoza, wakitembea kwa kasi kwenye kordo
ya hospitali hiyo kutazama hali ya mke wake.
“Chumba hichi”
Mama yake alizungumza huku akiusukuma mlango
wa chumba hicho, na kuingia ndani. Akamkuta
Junio akiwa pembeni ya kitanda, huku akiwa analia
sana. Phidaya kwa wakati huo aliwekewa mashine
za kumsaidia kupumu, huku pembei kukiwa na
mashine za kuhesabu mapigi ya moyo wake
unavyo dunda kwa kila dakika. Junio akamkimbila
baba yake na kumkumbatia huku akimwagika na
machozi mengi.
“Dady, mama anakufaaaa”
Junio alizungumza huku machozi yakimwagika,
jambo lililo zidi kumtia uchungu Eddy
“Noo, tumuombee mama, hawezi kufariki”
Eddy alizungumza kwa kujikaza tu, ili kumfariji
mwane na asiyaruhusu machozi yake kutoka
mbele ya mwanae huyo
“Dokta yupo wapi?”
“Nilikuwa naye ofisini kwake, pale nilikuwa
ninatoka ofisini kwake, ndio nikakuona”
“Anasemaje?”
“Hajanipa jibu la kuelekewa”
“Baki na mtoto”
Eddy akafungua mlango na kutoka ndani ya
chumba hichi alicho lazwa mke wake. Moja kwa
moja akaongoza hadi kwenye ofisi ya dokta, aliye
elekezwa na mama yake ndio aliye muhudumia
mke wake baada ya kufikishwa hapo hospitalini.
“Karibu muheshimiwa”
Daktari huyo mwenye asili ya kihindi alishtuka
mara baada ya kumuona Eddy ameingia ndani ya
ofisi yake huku sura yake ikiwa imepoteza furaha.
“Mke wangu amepatwa na nini?”
“Kaa basi chini muheshimiwa Waziri”
Eddy akamtazama daktari huyo kwa mamcho
makali yaliyo jaa uchungu, kisha akaka kwenye kiti
alicho omba kukaa na dokta huyo.
“Mke wangu anatatizo gani?”
“Tumemfanyia uchunguzi mke wangu na kugundua
kwamba, amevuta sumu kali sana ambayo laiti
kama angechelewa kuletwa hospitalini basi,
angefarki. Tumemuwekea tripu za maji, ili kuweza
kuisafisha sumu hiyo ambayo inakimbilia kuua
kiumbe kilichopo tumboni”
“Do…do…do…kta ii…iiinamaana mke wangu…. Ni
mjamzito”
“Ndio, na kiumbe endapo kitavuta sumu hiyo basi
kitaweza kutoka kabla ya siku zake”
***
Katika pita pita zake, huku akijilaumu moyoni
mwake ni kwanini hajafanikisha adhima ya kumuua
mke wa mwanae, kwasababu ya Madam Mery aliye
mzubaisha hadi mwanamke huyo akachukuliwa.
Pikipiki iliyo mpakiza ya bodaboda aliye mkodisha
tangu asubuhi, ikaisha mafuta mbele ya hospitali
ya Ocean Road
“Ohhh samahani mzee wangu pikipiki kidogo
imekata mafuta”
“Wewe kijana mbona mzembe sana, utaendeshaje
pikipiki hadi inakuzimikia kwa mafuta”
Mzee Godwin alizungumza kwa sauti ya kufoka
sana
“Samahani sana mzee wangu”
“Pumbuvu sana wewe kijana”
Mzee Godwin alizunumza huku akizunguka
zunguka, kwa bahati nzuri macho yake
yakamshuhudia mke wake Mama Eddy akitoka nje
ya hospitali hiyo, huku simu yake ikiwa sikioni
akionekana anazungumza natu
“Unanidai shilling ngap?”
Mzee Godwin alizungumza huku akitoa pochi yake
mfukoni, huku macho yake yote yakiwa kwa mama
Eddy.
“Elfu hamsini”
Akachomoa noti tano za elfu kumi kumi,
nakumkabidhi dereva bodaboda pasipo
kumtazama, kisha akaanza kupiga hatua kuelekea
alipo Mama Eddy, huku taratibu hasira kali dhidi ya
mke wake huyu ikiongezeka na kujikuta
akiichomoa bastola yake tayari kwa kumpiga risasi.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 7 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM(7)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storyzaeddy.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
“Unanidai shilling ngap?”
Mzee Godwin alizungumza huku akitoa pochi yake
mfukoni, huku macho yake yote yakiwa kwa mama
Eddy.
“Elfu hamsini”
Akachomoa noti tano za elfu kumi kumi,
nakumkabidhi dereva bodaboda pasipo
kumtazama, kisha akaanza kupiga hatua kuelekea
alipo Mama Eddy, huku taratibu hasira kali dhidi ya
mke wake huyu ikiongezeka na kujikuta
akiichomoa bastola yake tayari kwa kumpiga risasi.
ENDELEA
Mama Eddy baada ya kuzungumza na simu,
akaingia ndani ya hospitali na kumfanya Mzee
Godwin kusimama kwenye moja ta gari lililo
egeshwa kwenye maeneo haya huku macho yake
akimsindikiza mke wake huyo, ambaye
alimshuhudia akizungumza na Eddy kisha
wakaondoka
“Eddy Eddy Eddy”
Mzee Godwin alizungumza huku akiwa
amekasirika, tukio kubwa linalo muuliza kichani
mwake ni pale anapovuta picha jinsi pacha
mwenzake alivyo kuwa akifanya mapenzi na mke
wake huyo, jambo linalomfanya kuzidi kumchukia
Eddy
“Nitakuua kwa mkono wangu mimi mwenyewe”
Mzee Godwin alizungumza huku akiwashuhudia
Eddy na mama yake wakitoka tena nje ya hospitali
huku wakiwa na Junio, aliye bebwa mikononi mwa
Eddy akionekana kupitiwa na usingizi. Gari la
mama Eddy likafika sehemu walipo simama huku
kukiwa na dereva ndani yake.
“Nitakuja basi asubuhi, kumuona mgonjwa. Ngoja
nikamlaze huyu chekbud wako”
“Sawa mama, usisahau kuja na chakula”
“Sawa nitakiandaa mimi mwenyewe”
Mama Eddy akaingia siti ya nyuma alipo lazwa
Junio aliye jichokea kwa usingizi.
“Mama kumbuka hajala huyo akifika ale”
Eddy alizungumza huku gari la mama yake
likiondoka taratibu, Eddy akalisindikiza kwa macho
gari hilo hadi linatoka kwenye geti, Macho ya Eddy
yakashuhudia mtu akiwa amejibanza kwenye moja
ya gari huku akionekana kama anachunguza kitu
fulani, kutokana na mwanga hafifu ya eneo la
maegesho hakuweza kumuona sura yake.
Eddy akataka kwenda ndani ila roho yake ikasita
kabisa na kujikuta akianza kupiga hatua za taratibu
kwenda sehemu lilipo gari hilo. Mzee Godwin
akatabasamu, alipo kua anamuona Eddy akija
katika eneo alipo jificha yeye. Akaishika bastola
yake huku akimsubiria kwa hamu kubwa, Eddy
afike ili amuulie mbali
Gafla simu ya Eddy ikaita na kumfanya asimame
na kuitoa mfukoni mwake, na kukuta ni namba ya
spika wa bunge, akaitazama kwa sekunde kadhaa,
kisha akaipokea
“Ndio kiongozi habari”
Eddy akuzungumza huku akitazama pembeni
upande ambapo hayupo mtu aliye hitaji kumuona
ni nani na kwanini anajificha
“Salama vipi, mbona umekimbia bila taarifa?”
“Kuna matatizo yakifamilia ilinibidi niwahi
kuyatatua”
“Kwema lakini?”
“Hapana si kwema kiongozi, kwani mke wangu
alivamiwa na majambazi na kumuwekea sumu, pia
nikakuta mwili mwengine wa rafiki wa karibu ukiwa
ndani ya nyumba yangu, naye akiwa amepigwa
risasi”
“Aisee, basi mimi nilijua kwamba umekimbia
maswali”
“Hapana kiongozi”
“Pole sana, vipi polisi umewataarifu?”
“Bado, ila hili swala nitalimaliza kimya kimya”
“Basi kama ni hivyo, ila nikusifie kwa vidonge
vyako vya leo, Umeniburudisha japo nilikuwa
ninajikaza”
“Ni moja ya kazi yangu”
“Basi endelea na majukumu ukiwa saswa
utaniambia”
“Sawa kiongozi”
Eddy akakata simu na kuzunguka sehemu alipo
hisi kuna mtu, ila hakukuta mtu yoyote aliyepo
kwenye eneo hilo. Kumbe kitendo cha Eddy
kuzungumza na simu, ikawa ni nafasi kubwa sana
kwa Mzee Godwin kutembea kwa hatua za haraka
na kuingia kwenye jembo moja la kuhifadhia nguo,
ikiwemo mashuka, neti, na mavazi ya kidaktari
“Kumbe huyu mwanamke hajafaa, nilazima
nimuue”
Mzee Godwin alizungumza baada ya kumsikia
Eddy akidai kwamba Madam Mery hajafa. Mzee
Godwin akavaa moja ya koti la kidaktari akachukua
na kipimo cha kupimia mapigo ya moyo, kisha
kwa haraka akaanza kupita wodi moja baada ya
nyingine ya wagonjwa mahututi
Halikuwa ni jambo la kustukiwa mara moja
kwamba yeye sio dokta, hii nikutokana na wingi wa
wafanya kazi katika hospitali hii, huku wengine
wakiwa wameingia zamu ya usiku wakiwapokeza
wezao walio fanya kazi kutwa nzima. Eddy akapiga
namba za Mzee Seleman aliye kuwa akisimamia
ufanyiwaji wa oparesheni wa Madam Mery kutolewa
risasi
“Ndio bosi”
“Hali ya mgonjwa inaendeleaje?”
Eddy alizungumza huku akiingia ndani, kuelekea
kwenye chumba alicho lazwa mke wake
“Bado madaktari wanaendelea kuzitoa risasi, nipo
kwa nje hapa ninachungulia kwenye kioo cha
mlangi
“Sawa hakikisha haumruhusu mtu kuwa karibu ya
mgonjwa zaidi ya madaktari, au nikuongezee
nguvu ya ziada?”
“Hapana”
“Sawa fanya hivyo”
Eddy baada ya kumaliza kuzungumza na mzee
Selemani Mbogo, simu yake ikazima chaji kabisa
na kujikuta akiidumbukiza mfukoni mwake. Eddy
akafika kwenye chumba alicholazwa Phidaya,
akaingia na kukaa pembeni ya kitanda cha mke
wake na kuanza kumtazama usoni mwake, na
kuanza kufikiria ni kitu gani ambacho anaweza
kumfanya Mzee Godwin pale atakapo mtia
mikononi
“Sasa huyu mzee amevuka mipaka kwa sasa,
nitamuua kimya kimya”
Eddy alizungumza kwa sauti ya chini kabisa huku
akiendelea kumtaza mke wake kwa macho ya
masikitiko. Taratibu akamshika mkono mke wake
ambao haujachomwa sindano ya dripu, taratibu
akaubusu kisha akakanyanyuka na kuanza kupiga
hatua taratibu za kuelelea kwenye mlango
Mzee Godwin akajaribu kupitia kila wodi ya
wagonjwa mahututi ila hakufanikiwa kumuona
Madam Mery, ambaye kwa wakatii huu yupo katika
chumba cha upasuliwaji. Akajikuta akiwa
amesimama nje ya moja ya chumba huku macho
yake yakitazama sehemu anapo tokea upande wa
kushoto kwenye kordo ndefu sana, huku akiendelea
kujiuliza ni wapi alipo Madam Mery ambaye
anaweza kufichua mipango yake ambayo
ameipanga. Simu yake ikaita kutazama akakauta ni
namba ambayo anawasiliana nayo sana.
“Bosi kuna watu nimewapata”
Sauti hiyo ya kiume inayo kwaruza kwaruza
kwenye simu, ilisikika vizuri masikioni mwa mzee
Godwim
“Wapo wangapi?”
“Wanne, na inavyo onekanani ni watu wenye
uchungu sana na kazi, ila ni wanawake”
“Wanawake, hivi mwanamke kweli tunaweza
kufanya naye kazi?”
Mzee Godwin alizungumza huku akipiga hatua
kusogea pembeni kidogo mwa chumba hicho
kilicho
“Bosi niamini hakuna litakalo haribika, kila kitu
nimekiweka kwenye mpango sawia”
“Basi fanya hivyo nahitaji kuonana na hao watu”
“Inabidi uje huku nilipo, si unajua afya yangu
ilivyo”
“Sawa, nitawasiliana nawe”
Eddy akafungua mlango na kutoa nje chumba
chake, hakumtazama daktari aliye mpa mgongo
huku akioenekana akiminya minya simu yake. Eddy
akaelekea upande wa kulia ambapo kuna duka la
hospitali, nia yake kubwa ni kwenda kununu maji.
Mzee Godwin alipo geuka na kumtazama mtu aliye
toka kwenye chumba hicho, akamshuhudia Eddy
akizidi kutokomea kwenye kordo hiyo ndefu
akielekea upande wa kulia.
Mzee Godwin akageuka na kukitazama chumbu
hichi, akagundua ni chumba nacho cha wagonjwa
mahututi, akatazama pande zote mbili za kordo,
hakuona mtu anaye mfwatilia, akashika kitasa cha
mlango na kuingia ndani ya chumba hicho. Mzee
Godwin hakutegemea kumkuta mkwe wake akiwa
kwenye kitanda kilicho zungukwa na mitambo ya
kumsaidia kuhema, huku akionekana kuwa ni mfu
mtarajiwa.
“Waooooooo”
Mzee Godwin alizungumza huku akipiga hatua
akielekea kwenye kitanda alicho lala Phidaya, kama
kawaida yake akaanza kumchezea nywele zake
ambazo ni ndefu. Taratibu akaichomoa bastola
yeke na kukikaza vizuri kiwambo cha kuzuia sauti
na kuisogeza taratibu kwenye paji la uso wa
Phidaya, aliye lala fofofo bila hata kujitambua,
Kabla hajafanya chochote, macho ya Mzee Godwin
yakatua kwenye kifua cha Phidaya, akazishuhudia
chuchu za Phidaya zilizo tengeneza bonde zuri
katikati, taratibu akajikuta akiupeleka mkono wake
wa kushoto kifua cha Phidaya na kuuingiza kwenye
nguo aliyo ivaa, na kuanza kushika chuchu zake
taratibu huku akiziminya minya kwa hisia kali
sana.
Mwili wa Mzee Godwin ukaanza kusisimka, na
kujikuta bastola yake akiiweka pembeni ya kitanda,
kisha kwa mkono yake miwili akaanza kufungua
vifungo vya shati la Phidaya na kuziacha chuchu
zake waze wazi, taratibu akapiga magoti chini, na
kuanza kunyonyoa moja baada ya nyingine, huku
kichwa chake kikiwa kimesahau ni kitu gani anacho
kifanya na kitamletea madhara gani
Eddy akafika kwenye duka la hospitali ambapo,
akatoa pesa na kununua maji makubwa ya baridi
pamoja na biskuti. Akamuomba muhudumu wa
duka kukaa na chenchi hiyo, kwani asubuhi atarudi
kununua baadhi ya mahitaji kama dawa ya mswali
na mswaki wenyewe. Akaanza kutembea kwa
mwendo wa kawaida akirudi kwenye chumba
alichopo mke wake kwani hakuhitaji kukaa mbali
sana na mke wake, laiti angejuwa wala asinge
dhubutu kuendelea kutembea kwa mwendo huo
Mzee Godwin akazidi kunogewa na kujikuta
akiuingiza mkono wake mmoja kwenye suruali
yake na kuanza kuchezea uume wake, huku akitoa
miguno ya raha. Eddy akazidi kuukaribia mlango
wa chumba alicho lazwa mke wake, huku akiwa
hajui hili wale lile. Mzee Godwin naye akazidi
kuzinyonyo chuchu za Phidaya, kiasi kwamba hadi
zikaanza kubadilika rangi na kuweka uwekundu
fulani
Eddy akafika mlangoni kabla hajashika kitasa
akamuona Mzee Seleman akija kwa kasi, huku
anakimbia akimfwata yeye ikamlazimu kusimama
na kumsubiria amsikilize ni kitu gani anahitaji
kuambiwa.
“Muheshimiwa, muheshimiwa”
Mzee Selemani aliita huku akiwa anahema kama
amekimbizwa na mbwa wakali sana walio simama
na kumuacha aende zake
“Vipi?”
“Mgonjwa mgonjwa anakuita anataka kuzungumza
na wewe”
Mzee Selemani Mbogo alizungumza huku akihema
sana, hadi akawa anarudia baadhi ya maneno
anayo yazungumza.
“Basi ngoja niweke vitu ndani, twende pamoja”
“Muheshimiwa wewe twende kwani hali yake ni
mbaya, anasema kuna siri anahitaji kukuambia
wewe”
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 8 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (8)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
“Muheshimiwa, muheshimiwa”
Mzee Selemani aliita huku akiwa anahema kama
amekimbizwa na mbwa wakali sana walio simama
na kumuacha aende zake
“Vipi?”
“Mgonjwa mgonjwa anakuita anataka kuzungumza
na wewe”
Mzee Selemani Mbogo alizungumza huku akihema
sana, hadi akawa anarudia baadhi ya maneno
anayo yazungumza.
“Basi ngoja niweke vitu ndani, twende pamoja”
“Muheshimiwa wewe twende kwani hali yake ni
mbaya, anasema kuna siri anahitaji kukuambia
wewe”
ENDELEA
“Mmmmm”
Eddy akaguna na kuanza kupiga hatua kuelekea
kwenye alipo lazwa Madam Mery. Mzee Godwin
akamtoa Phidaya mashine ya kumsaidia kupumua,
na kuanza kumnyonya mdomo wake, kwa papara
na hamu ya kumuingilia kimwili mkwewe kwa
bahati mbaya akatingisha meza iliyo jirani na
kitanda, na kulifanya jagi la kioo lililo kuwa mezani
hapo kuanguka chini na kupasuka.
Gafla Eddy akasimama, baada ya kusikia mlio wa
kitu cha kioo kikipasuka kikitokea kwnye chumba
alicholazwa Phidaya. Eddy akageuka na kutazama
nyuma kuangalia mlango wa chumba hicho ulipo
mbali kidogo kutoka katika sehemu walipo
simama.
‘Nenda kamuone Madam Mery’
‘Nenda katazame kuna nini kwenye chumba cha
mke wako’
Ni sauti mbili zilizo kua zikiendelea kubishana
kwenye akili ya Eddy.
“Muheshimiwa twende”
Mzee Selemani Mbogo alimsisitizia waziri Eddy
waendelea na safari hiyo ambayo ni muhimu sana
kwao kuweza kwenda. Taratibu Eddy akataka
kupiga hatua kuelekea anapo seme Mzee Mbogo,
ila akajikuta mzito sana kuendelea na safari hiyo,
kwa hatua za haraka haraka zilizo changanyika kila
alipo zipiga, zikamfanya Eddy aweze kukimbia
kuelekea kilipo chumba alicho lazwa mke wake
Phidaya.
Mzee Godwin alilitazama jagi lililo pasuka, na
kulipotezea, akaushusha mdomo wake kwa mara
nyingine kwenye chuchu za Phidaya. Zilizo kaa
vizuri kana kwamba binti mdogo anaye anza
kuvunja ungo na huwezi kuamni kwamba anamtoto
wa miaka mitano. Pumzi nzito za kimahaba
zikazidi kumtoka mzee Godwin na kujikuta
akiushusha mkono wake mmoja hadi sehemu za
siri za Phidaya. Ugumu alio ukuta ni skintait aliyo
ivaa Phidaya pamoja na chupi, vilivyo mfanya
mzee Godwin, kujikuta akiulazimisha mkono wake
kuingia kwenye nguo hizo za ndani.
Gafla mlango ukafunguliwa na kujibamiza, macho
ya Mzee Godwin yakatua kwenye sura ya Eddy
aliye yatumbua macho yake, huku akionekena
kutetemeka kwa hasira kali, aliyo nayo. Kufumba
na kufumbua mzee Godwin akajikuta akiona nyota
nyota kwenye macho yake, hii ni baada ya Eddy
kukimbia kwa kasi hadi sehemu alipo piga magoti
na kumtandika ngumi nzito ya uso, iliyo
muangusha chini, kabla hata Mzee Godwin
hajafanya chochote, kutafuta ni wapi alipo iweka
bastola yake akastukia akinyanyuliwa na
kutandikwa kichwa kikali cha pua kilicho zidi
kuifanya pua yake kumwagika na damu nyini na
kuzidi kumchanganya Mzee Godwin. Eddy hakujua
nguvu alizo nazo zilitokea wapi kwani, alimshika
mzee Godwin na kumuweka begani mwake na
kunyanyua kuu kisha akambwaga chini mithili watu
wanao pigana myereka.
Mzee Selemani Mbogo akaingia ndani ya chumba
alicho ingia bosi wake na kumkuta akiwa
anamshindilia ngumi mwanaume ambaye alisha
wahi kipindi cha nyuma, akiwa ni mkuu wa jeshi la
ulinzi JWTZ.
“Muheshimiwa muheshimiwa”
Mzee Mbogo aliita huku akijitahidi kumshika Eddy
mabegani na kumnyanyua ili asiendelee
kumkandamiza ngumi mzee huyo. Haikuwa kazi
rahisi kwa mzee Selemani Mbogo, kwani misuli
iliyo kaza ya Eddy ilimpa ugumu wa kuweza
kuendelea kumuamua asiendelee kumshambulia
mzee huyo.
“Hhaaahahaaa”
Mzee Godwin alicheka kila konde alilo pigwa na
mwanaye, Eddy akazidi kuendelea kufanya
mashambulizi kwa mzee Godwin, ila gafla mambo
yakabadilika kwani Mzee Godwin aliweza kuidaka
ngumi ya Eddy iliyo kuwa ikielekea kumpiga
kwenye uso wake. Mzee Mbogo ikabidi atoke kasi
kwenda kuomba msaada kwa askari wanao linda
kwenye hospitali hii. Mzee Godwin, akamzungusha
Eddy aliye kuwa amemkalia kwenye tumbo lake,
akambwaga chini na yeye akawa juu, akashusha
makonde mawili ya nguvu yaliyo tua kwenye
mikono ya Eddy aliye kinga kichwa chake kisiweze
kupigwa na makonde hayo mazito. Eddy
akajitutumua na kujaribu kumrudisha chini Mzee
Godwin ila hakuweza kwani aliweza kuzidiwa
nguvu na baba yake huyo, aliye jazia kwa misuli
na nimkakamavu kutokana na kazi yake ya jeshi
aliyo kuwa akiifanya kwa takribani miaka thelethini
na tano, kabla hajapotea kwa kuhofia kukamatwa
baada ya kusadikika yeye ndiye aliye mteka mke
wake ambaye alikuwa ndio waziri mkuu.
Mzee Godwin akamnyanyua Eddy na kumrushia
kwenye kitanda alicho lala Phidaya asiye jielewa,
Eddy akajitahidi kwa uwezo wake wote asitue
kwenye mwili wa mke wake na kujikuta akiangukia
upande wapili wakitanda na kuangukia bega. Mzee
Godwin akaichukua bastola yeka kabla
hajamfyatulia risasi Eddy askari wawili wakaingia
ndani ya chumba hichi, askari wakaonekana
kustushwa na kukutana na mdomo mdogo wa
bastola ukiwa umewaelekea wao.
Eddy akajaribu kunyanyuka ili kuitoa bastola yake
aliyo ichomeka nyuma kwenye mkanda wake, ila
maumivu ya bega la mkono wakulia yakamfanya
ashindwe kufanya hivyo, akajaribu kuupeleka
mkono wakulia ukakubali kufika sehemu alipo
ichomeka bastola yake, ila kwabahati mbaya
hakuikutwa na hakujua ni wapi ilipo angukia. Kwa
aishara Mzee Godwin, akawaamrisha askari hao
kusogea mlangoni nao wakatii kutokana hawakuwa
na silaha yoyote, wao walihisi ni ugomvi mdogo
wakuwatenganisha watu walio ambiwa
wanagombana.
Kitanda kikaanza kutingishika, Eddy alipo mtazama
mke wake akamkuta akiwa anarusha rusha miguu
kama mtu anaye elekea kukata roho, Eddy akataka
kunyanyuka ila kwa ishara mzee Godwin
akamuamrisha akae chini la sivyo atamfumua
ubongo, Mzee Godwin akaufikia mlango huku
akiendelea kujifuta damu zinazo mtoka puani
mwake na mkono mmoja akiwa amewaelekezea
bastola yake Eddy na askari walio jipendekeza
kuingilia ugomvi usio wahusu.
Mlango ukafunguliwa na Mzee Selemani Mbogo
akaingia huku akiwa anahema akiamimini kwamba
ugomvi umetatuliwa na askari hao. Mzee Mbogo
akastukia akivutwa ndani nakusukumizwa kwenye
sakafu na kuangukia uso wake alipo geukuka
kuangalia ni nani aliye fanya hivyo akakutana
akitazamana na bastola.
“Eddy nikihitaji kuua nitakuua kwa mkono wangu
ila si kwakutumia risasi, weka hilo akilini”
Mzee Godwin alizungumza kwa dharau huku
akiachia tabasamu pana, kisha akafungua mlango
na kutoka nje
“Kamkamateni yuleee”
Eddy alizungumza huku akijinyanyua na kumzuia
mke wake kwa mkono mmoja ili asianguke
kitandani kwani tayari alisha anza kusoge
pembezoni mwa kitanda.
“Muheshimiwa anabastola yule”
Askari mmoja alizungumza sentensi iliyo mchukiza
Eddy akajaribu kurusha kofi kwa mkono wake wa
kulia ila akashindwa kwa maumivu makali
“Kuanzia leo huna kazi”
Asakri huyo baada ya kusikia hivyo wakatoka kasi
kumfwatilia Mzee Godwin sehemu alipo kwenda.
“Na wewe unashangaa nini nenda kawaite
madaktari”
Eddy alimfokea mzee Mbogo na kumfanya naye
atoke kasi ndani ya chumba nakuelekea kwenye
mapokezi kuomba msaada kwa manesi walio kaa
kwenye sehemu hiyo.
“Mke wangu usife”
Eddy alizungumza huku akiendelea kujitahidi
kumtuliza Phidaya ambaye kwa sasa alianza
kumwagikwa na povu mdomoni mwake. Manesi
watatu wakingia ndani ya chumba wakiwa
wameongozana na mzee Mbogo ambaye jasho
linamwagika na kuhema juu.
“Mungu wangu…..!!”
Nesi mmoja alizungumza baada ya kuona kifaa
kiliicho kuwa kikimsaidia Phidaya kupumulia kikiwa
kinaning’inia kwenye mtungi wa gesi. Kwa haraka
akakichukua na kumfuta povu linalo toka mdomoni
mwake na kumvalisha, hewa ilivyo anza kuingia
mapafuni mwake taratibu ikaanza kumtuliza
Phidaya kurusha rusha miguu yake na baada ya
muda akaanza kurudi katika hali yakawaida japo
fahamu zake bado hazijamrudia
“Kaka kwani imekuaje hadi mgonjwa akawa katika
hali hii?”
Nesi aliye muwekea Phidaya kifaa cha kupumulia
kwenye pua yake alizungumza huku akimshika
bega la kushoto Eddy aliye ikunja sura yake kwa
maumivu makali
“Hembu nione”
Nesi huyo alizungumza kwa kujiamini huku
akihitaji kuliona bega la Eddy.
“Linauma”
Kwa uzoefu alio kua nao nesi Maria akagundua
kwamba bega la Eddy halijavunjika zaidi ya
kutenguka. Akamshika shika Eddy ambaye kila
alipo shikwa alijihisi maumivu makali kwenye bega
lake hilo, gafla nesi Maria akaliminya kwa nguvu
bega la Eddy na kumfanya atoae ukelele mkubwa
kwani nitukio ambalo hakulitegemea kulipa kutoka
kwa nesi Maria aliye onekani kuwa na umri kati ya
miaka arobaini hadi arobaini na tano. Ukelele wa
Eddy ukapenya kwa haraka kwenye masikio ya
Phidaya na kujikuta akiyafumbua macho yake,
akiwa kama mtu aliye toka kwenye njozi nzito
yakutisha.
“Pole ehee”
Nesi Maria alizungumza huku akiendelea kumgusa
gusa Eddy begani
“Muheshimiwa”
Mzee Selemani Mbogo aliita na kumfanya Eddy
kugeuka na kumtazama kwa ishara yakidole mzee
Mbogo akamuonyesha Eddy jinsi mke wake anavyo
endele kushangaa shangaa kwenye chumba alicho
kuwepo.
“Baby umeamka…..”
Eddy alizungumza kwa furaha huku akimtazama
mke wake akataka kujaribu kumtoa mashine ya
kupumulia ila Nesi Maria akamzuia asifanye hivyo
“Huyo bado hajarudi katika hali yake ya kawaida,
hapo bado akili yake inavuta kumbukumbu ni wapi
alipo na ukimtoa hiyo mashine anaweza kufariki”
Nesi Maria alizungumza na kumfanya Eddy
asimamishe zoezi lake la kutaka kukitoa kifaa
hicho kilicho funika mdomo pamoja na pua ya
Phidaya. Phidaya akaigeuza shingo yake na
kumtazama Eddy, akaachia tabasamu dogo kisha
akafumba macho yake na kuifanya mashine iliyopo
pembeni ya kitanda inayo hesabu mapigo ya moyo
kutoa mlio wa kupiga kelele, ndogo huku mistari
miwili myekundu ikikatiza kwa kasi, ikiashiria
mapigo ya moyo ya Phidaya yameacha kufanya
kazi
“Jamani nawaombeni mutupishe, nesi Lily nenda
kamuite dokta Khan”
Nesi Maria alizungumza huku akiheme, akiianza
kumkandamiza kandamiza kwa nguvu Phidaya
kifuani mwake, Wasiwasi mwingi ukazidi
kumtawala Eddy ambaye macho yake tote
amayetoa kwa mke wake ambaye ametulia tuli,
kwenye swala la kutoka nje hakuwa mmbishi zaidi
ya kutoka nje kuwaacha manesi waendelea kufanya
kazi yao. Hawakwenda mbali na chumba alichopo
Phidaya, wakawashuhudia daktari wa kuhindi akija
kwasi huku nyuma yake kukiwa na nesi aliye pewa
jukumu lakwenda kumuita. Wakaingia ndani ya
chumba na kuanza kumfanyia litakalo wezekana
Phidaya ili kuweza kuyaokoa maisha yake,
kwakutumia mashine za umeme zinazo stulia
mapigo ya moyo, wakaanza kufanya hivyo kwa
haraka,
“Again”(Tena)
Dokta Khan alimuamuru nesi Maria kuweza kurudia
kuyastua mapigo ya moyo ya Phidaya anaye
onekana kulala kuzidi kuwa katika hali mbaya
sana,
Wakiwa nje ya chumba alicho lazwa Phidaya, Eddy
hakuweza kutulia kila mara akawa na kazi ya
kuzunguka zunguka kwenye kordo ya hospitali
huku kila mara akijaribu kumuomba Mungu
kuweza kufanikisha mkewe kuweza kupona.
“Muheshimiwa tumemkosa”
Askari walio agizwa kwenda kumfwatilia Mzee
Godwin walikuja huku wakihema kana kwamba ni
kweli waliweza kumfwatilia ila ukweli ni kwamba
walipo toka ndani ya chumba cha walicho kuwepo
na kwenda nje ya geti, wakatazama kila upande na
kushauriana wakimbie kimbie, kama nusu saa ili
kuitoa miili yao jasho, ili wakirudi watoe ripoti ya
kwamba hawakufanikiwa kumuona mzee Godwin.
Eddy akawatazama kwa muda jinsi wanavyo hema
“Hamuna kazi, kuanzia sasa rudishni magwanda
kwenye vituo vyenu vya kazi”
Askari hao wakabaki wamemtumbulia mimacho
Eddy na mmoja akaanza kuangua kilio kikubwa
cha kujutia
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 9 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (9)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
“Muheshimiwa tumemkosa”
Askari walio agizwa kwenda kumfwatilia Mzee
Godwin walikuja huku wakihema kana kwamba ni
kweli waliweza kumfwatilia ila ukweli ni kwamba
walipo toka ndani ya chumba cha walicho kuwepo
na kwenda nje ya geti, wakatazama kila upande na
kushauriana wakimbie kimbie, kama nusu saa ili
kuitoa miili yao jasho, ili wakirudi watoe ripoti ya
kwamba hawakufanikiwa kumuona mzee Godwin.
Eddy akawatazama kwa muda jinsi wanavyo hema
“Hamuna kazi, kuanzia sasa rudishni magwanda
kwenye vituo vyenu vya kazi”
Askari hao wakabaki wamemtumbulia mimacho
Eddy na mmoja akaanza kuangua kilio kikubwa
cha kujutia
ENDELEA
“Muheshimiwa mimi kwetu ninategemewa, na mimi
itetezi change ni hii kazi”
Askari huyo alizungumza huku akiendelea kulia
kwa machozi, Eddy hakuhitaji kusikiliza kitu cha
aina yoyote zaidi ya kuwasisitiza wakalilie mbele
ya safari kwani hawana sifa ya kuwa maaskari.
Hali ya Phidaya ikaendelea kuwa tata huku daktari
na manesi wakindelea kuyastua mapigo ya moyo
yaweze kufanya kazi, ila haikuwa rahisi kama
wanavyo zoea kufanya kwa wagonjwa wengine
“Dokta vipi?”
Nesi Maria aliuliza huku akiwamgikwa na jasho
jingi kwani nimara nyingi wamejaribu kumstua
Phidaya ila juhudi zao hazikuzaa matunda
“Atakuwa amekufa nini?”
Doktar Khan alimuuliza nesi Maria kwa sauti ya
chini ili waziri Eddy aliyopo nje asiweze kusikia
kinacho endelea ndani ya chumba hicho
“Hata mimi pia nahisi hivyo kwani si kawaida”
“Sasa utamuambiaje huyo waziri hapo nje?”
“Nani niwaziri?”
Nesi Maria alizungumza kwani kwa kipindi chote
alicho kuwa anazungumza na Eddy hakujua
kwamba ni waziri
“Mungu wangu, mimi sijajua……!!!”
“Ohooo hapo sasa na wewe unaharibu, mimi
nimesikia watu hapo nje wakiangua vilio baada ya
kuambiwa hawana kazi”
“Mmmmm ehee Mungu sijui itakuwaje”
Wakiwa wakiendelea kujadilia, taratibu mashine
ikaanza kuonyesha vimishale viwili vya kijani
ikiashiria mapigo ya moyo ya Phidaya ayamesha
anza kudunda japo kwa utaratibu bali anaashiria
kwamba yu hai na si mfu kama wanavyo hisi
“Ohhh asante Mungu wewe baba wa majeshi,
hakuna lishindikanalo kwako”
Nesi Maria alisali kwani kupona kwa Phidaya ndio
kupona kwa kazi zao wanazo zitegemea maishani
mwao.
***
Upasuaji wa kutoa risasi zilizo kuwa kwenye kifua
cha Madam Mery, ukafanikiwa kwa kiasi kikubwa
na madaktari wakafanikiwa kuweza kuzitoa risasi
hizo kwa usalama kisha wakamshona vizuri
Madam Mery na kumpeleka kwenye chumba
maalumu cha wagonjwa mahututi. Kwa msaada wa
mashine akaendelea kupumua huku dripu la maji
na damu yakiendelea kufanya kazi ya kuongeza
maji na damu vilivyo pungua mwilini mwa Madam
Mery.
Usiku wa manane Madam Mery akaweza kufumbua
macho yake kwa mara ya pili, kwani mara ya
kwanza alikua wakiomba kuzungumza na Eddy,
pale alipo pata hofu kwamba anaweza kupotea
maisha yake muda wowote kuanzia pale
Akayazungusha macho yake kwenye kila kono ya
chumba, kwaufahanu wake unao fanya kazi vizuri
akagundua kwamba pale ni hospitali. Pameni ya
kitanda akaona kuna kifaa maalumu ambacho
ukikiminya nesi au daktari aliye karibu mtambo
huo wa kisasa unao weza kuwataarifu manesi na
madaktari kwamba mgonjwa wa chumba Fulani ana
hitaji msaada.
Hazikupita dakika tano mlango wa chumbani kwakr
ukafunguliwa na kuingia nesi mrefu kiasi aliye jazia
maungo yake ya nyuma
“Nikusaidie nini?”
Nesi huyo alizungumza kwa sauti ya upole huku
akimtazama Madam Mery.
“Eddy, Eddy waziri namuhitaji”
Madam Mery alizungumza, kutokana na uwepo wa
Eddy kwenye hospitali hii uliwafanya watu wengi
kuutambua uwepo wake. Hakuwa na kipingamizi
nesi huyo, aliye vaa kagauni kalisho ishia kenye
maagoti na kuyafanay makalio yake makubwa
kutingishika vibaya mno kila anapo tembea
Nesi akaongoza hadi sehemu alipo Eddy, nje ya
chumba, kwaheshima zote akasimama mbele ya
Eddy
“Muheshimiwa kuna mwana mama anakuhitaji
kwenye chumba cha wagonjwa mahuti”
Kabla Eddy hajamjibu neno lolote nesi huyo
mlango wa chumba alicho lazwa mke wake,
ukafunguliwa akatoka doktar Khan, akiwa na
tabasamu usoni mwake
“Dokta vipi mke wangu?”
Doktar Khan akashusha pumzi nyingi kisha
akaanza kuzungumza
“Tumejitahidi kadri ya uwezo na..”
“Mke wangu amekufa doktar?”
Eddy aliuliza kwa wasiwasi mwingi
“Hapana hajafa, tumeweza kuyaokoa masha yake,
ila kwa sasa atakuwa chini ya uangalizi wa manesi
watau, mutamuona kesho asubuhi kwa sasa
nitaomba mumuache apumzike”
“Sawa”
Eddy alijubu kwa unyonge huku akitamni
kuzungumza kitu kwa daktari huyo, ila akajikuta
akisahau ni kitu gani alihitaji kukizungumza.
Hapakuwa na jinsi yoyote ikambidi Eddy amuombe
Mzee Mboho kukaa nje ya chumba hicho hadi yeye
pale atakapo rejea, yeye akaongozana nesi aliye
kuja kumuita na kufikishwa kwenye chumba
alichopo Madam Mery
***
Mzee Godwin baada ya kutoka kwenye geti la
hospitali akakodi taksi iliyo mfikisha kwenye hoteli
aliyo kuwa amefikizia na Madam Mery, akaingia
bafuni na kunyoo ndevu zake zote alizo kuwa nazo
na kumfanya arudi kwenye sura ya ukijana japo ni
mzee, akakushanya nguo zake na kuziingiza ndani
ya begi alilo kuja nalo, akiamini anaweza kuifanya
kazi yake na kuimaliza ila hali tayari ilisha kuwa
mbaya kwani mwanae Eddy anamamlaka makubwa
serikalini na endapo atamtia nguvuni nilazima
atahukumiwa. Mzee Godwin akatoa kwenye
chumba cha hoteli na kuanza kutembea kwenye
kordo ndefu, hakuhitaji kutumi lifti kuhofia
kukamatwa kizembe pale lifti itakapo funguka na
kukumbana na kundi la askari. Akaanza kushuka
kwenye ngazi akitokea gorofa ya saba kushuka
chini, na kila mara akawa na kazi ya kuchungulia
chini kuona kama atakutana na mtu yoyote.
Mzee Godwin akafanikiwa kufika nje ya hoteli
pasipo kustukiwa akakodi taksi nyingine na
kumuomba dereva kumpeleka kwenye uwanja wa
ndege wa mwalimu Julias K.Nyerere ili aweze
kuondoka nchini Tanzania haraka iwezekanavyo na
kuelekea brazil alipo weka makazi yake ya
maficho.
Mzee Godwin akastushwa kukuta gari zipatazo sita
za polisi zikiwa zimefunga barabara ambayo
walihitaji kupita kuelekea uwanja wa ndege. Na
kundi hilo la askari wote walionekana kuwa na
silaha mikononi mwao na wawili wakiwa namatochi
makubwa yakiimulika taksi hiyo
***
Eddy akafungua mlango na kuingia ndani ya
chumba alicho lazwa Madam Mery na kumkuta
akiwa yupo macho. Taratibu Eddy akaka kwenye
kiti cha pembeni ya kiti cha Madam Mery, huku
akiwa na maswali mengi ni kwanini amemkuta
Madam Mery akiwa amepigwa risasi nyumbani
kwake na kama alikuja na mzee Godwin imekuwaje
wameanza kushirikiana na mzee huyo. Ila
kutokana Madam Mery ni mngonjwa hakuhitaji
kuuliza swali lolote zaidi ya kusubiria kitu kilicho
mfanya yeye kuitwa hapo
Madam Mery alipo mtazama Eddy, akajikuta
akimwagikwa na machozi, kila alivyo lia maumivu
kwa mbali akaanza kuyasikia kwani dawa ya
maumivu aliyo chomwa ndio ilikuwa ina kwenda
kuishia kupoma.
“Eddy kwanza nahitaji kukuambia kitu kitu
kitakacho tokea muda wowote, Godwin amepanga
kutegesha bumu kwenye uwanja wa ndege wataifa
na kuteka ndege ambayo, atataka kuitumia kwa
shuhuli zake binafsi”
Maneno ya Madam Mery yakamfanya Eddy kustuka
kwani hajafanikiwa kumtia mikononi mzee Godwin,
Eddy kwa haraka akaitoa simu yake mfukoni,
akajaribu kuiwasha akakuta imezima
“Mungu wangu”
Eddy alionekana kuchanganyikiwa, akajaribu mara
kadhaa kuiwasha simu yake ila haikukubali kuwaka,
kwa haraka akatoka nje ya chumba pasipo
kumuaga madama Mery kwa bahati nzuri
akakutana na nesi aliye kuwa amemuita
“Lete lete simu yako”
Eddy alizungumza na kumfanya nesi huyo kuanza
kujipapasa papasa ila akajikuta akishangaa
“Ahaa nimeicha kule mapokezi ninaichaji”
Alizungumza na kuanza kukimbi kuelekea
mapokezi, huku Eddy akifwata kwa nyuma. Kila
walio pishana naye alihisi kuna jambo linalo
endelea, wakafika kwenye chumba cha mapokezi,
nesi huyo akaingia ndani naichomo simu yake
kwenye chaji na kumkabidhi Eddy aliye onekean
kuchanganyikiwa.
“Unafunguaje hiii”
Eddy alizungumza baada ya kushindwa kufungua
mfuniko wa simu ili kuweza kubadilisha line za
simu na aweke yakwake. Nesi akamsaidia kufungu
simu hiyo, kisha akatoa line yake na kumpa Eddy,
akaweka line yake na kuchua batrii na kuiweka na
kuiwasha simu hiyo pasipo pasipo kuurudishia
mfuniko wa nyuma. Eddy kwa haraka akatafuta
namba ya mkuu wa polisi, kisha akaipiga. Ikaita
kwa muda na kupokelewa na sauti iliyo jaa
usingizi
“Haloo”
“Kuna tukio la ugaidi lanataka kutendeka muda
wowote kuanzia sasa, huku uwanja wa ndege wa
JK unatakla kulipuliwa”
Eddy alizungumza kwa haraka haraka huku
akihema
“Wewe nani kwani?”
Mkuu wa askari aliuliza
“Unataka kunijua mimi ni nani?”
“Ndio kwa maana wewe ugaidi Tanzania utokee
wapi, hembu acha upuuzi wako. Acha tulale sisi”
“Kabla hujakata simu, kuanzia sasa huna kazi
pumbavu wewe. Unazungumza na waziri wa Ulinzi
Eddy, Eddy Godwin”
“Muhe……”
Eddy akaakata simu na kutafuta simu ya makamu
msaidizi wa kamanda huyo wa kanda maalumu,
akaipiga namba hiyo hata sekunde tano hazikupita,
simu ikaokelewa
“Ndio muheshimiwa”
Kamanda huyo alizungumza kwa wasiwasi mwingi,
na kumuomba dereva wa gari anaye muendesha
kusimamisha pembeni
“Kuna tiukio la uwanja wa ndege kulipuliwa
hakikisheni munafunga barabara ya kwenda uwanja
wa taifa na gari zote munazisimamisha na
kuzikagua na mumkamate Godwin aliye kuwa
mkuu wa jeshi la ulinzi”
“Sawa mkuu nimekuelewa, kwanza nipo doria
muda huu na vijana”
“Fanya hivyo kuanzia sasa hivi unachukua nafasi
ya mkuu wako, nimefukuza kazi muda huu”
“Ohh asante sana muheshimiwa”
Eddy akakata simu, akakata simu na kumpigia
simu mkuu wa ulizi katika uwanja wa ndege wa
mwalimu Julius Nyerere, simu yake nayo
ikapokelewa ndani ya muda mchache
“Haloo”
“Panga vijana wako, waimarishe ulizi kunahatihati
ya uwanja wa ndege kulipuliwa kwa bomu”
“Haaaa…..!!!”
“Unashangaa nini?”
“Hapana nimekuelewa muheshimiwa”
Kilicho muokoa mkuu huyu kuto fukuzwa kazi ni
kuweza kuikumbuka sauti ya Eddy aliyo toka
kuisikia kwenye bunge mida ya saubuhi na wala
hakufahamu namba yeka waziri huyo ameitolea
wapi. Hakutaka makuu zaidi ya kupiga simu
kwenye sekta nzima za ulinzi uwanja wa ndege
kuwaamuru askari kudumisha ulinzi kwa anaye
ingia na kutoka na kila waliye mtilia mashaka
akamatwe kwa mahojiano
***
Dereva taksi akasimamisha taksi yake baada ya
kuona gari nyingi za polisi zikiwa mbele yake.
“Wanataka nini hawa”
Dereva taksi alijisemea mwenye akisubiria
kuungwa mkono na mteja wake Mzee Godwin aliye
kaa siti ya pembeni mwake. Mzee Godwin
alitambua kwamba anaye tafutwa ni yeye kwani
tayari mwanae amesha kuwa na mkono mrefu
serikalini wakuweza kufanya chochote ndani ya
dakika kikafanyika. Kila askari aliye kuwa doria
aliweza kusambaziwa picha ya mzee Godwin,
kwenye namba yake ya whatsapp na hata aliye
kuwa hayupo doria aliweza kutumia ujumbe wa
kumuamrisha kuweza kuingia kazini, usiku huo wa
saa tisa.
“Haya ndo matatizo ya hii kazi”
Askari mmoja alizungumza akiwa anajiandaa
kupata chakula cha kitandani kutoka kwa mke
wake
“Kuna nini?”
“Tumepigiwa simu ya upepo, inanibidi kuwasili
kituoni muda huu”
“Jamani mbona wanawatesa hivyo”
“Ahaa wee acha tu mke wangu, ngoja nijiandae
niende”
Askari wote waliopo ndani ya jiji la Dar esaalam
wakawa wapo macho kwa muda wausiku,
wakiendelea kufanya masako mkali kwa kila gari
waliyo kutana nayo kwenye barabara ikitembea
kwa muda huo, si wenye magari waliweza
kukumbana na kasheshe ya kukaguliwa, bali hata
pikipiki na watembea kwa miguu walio kuwa
wakiamka majira hayo kuwahi kwenye kazi zoa,
nao wakumbana na doria hiyo kali
“Shuka kwenye gari”
Mzee Godwin alizungumza kwa sauti nzito ya
kukoroma tofauti na suati aliyo kuwa
ameizungumza nayo kwa mara ya kwanza alipo
mkodi dereva huyo
“Mzee wangu vipi, gari si yangu hii bwana kama
vipi shuka wewe”
Mzee Godwin hakutaka mazungumzo mengi,
akachomo bastola yake kwenye soksi, mguu wa
kulia na kiumtandika risasi moja ya kichwa, dereva
taksi na kumuua hapo hapo. Alafungua mlango wa
dereva na kimsukumia nje, akakaa kwenye siti ya
gari nakuanza kulirudisha nyuma jambo lililo
wafanya askari kuanza kuishambulia taksi hiyo kwa
risasi. Mzee Godwin akafanikiwa kuigeuza taksi
hiyo kwa utaalamu mkubwa, na kugeukia inapo
toka, ubaya zaidi wapo kwenye daraja ambalo kwa
chini linapitisha maji ya mto
Risasi za polisi zikapiga kwenye matairi ya nyuma
na kuzifanya rimu za gari hilo kuanza kuserereka
kwenye lami na kuifanya gari hiyo kushindwa
kwenda kwa kasi na kuzidi kuyumba yumba. Mzee
Godwin akashududia gari nyingine za polisi zikija
mbele yake sehemu anapo elekea. Hakua na
uchaguzi wowote zaidi ya kugonga bomba za
daraja, zikavunjika na kuifanya gari kuanza
kushuka kwenye mto huyo wenye maji mengi chini
pamoja na mawe makubwa.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 10 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (10)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Risasi za polisi zikapiga kwenye matairi ya nyuma
na kuzifanya rimu za gari hilo kuanza kuserereka
kwenye lami na kuifanya gari hiyo kushindwa
kwenda kwa kasi na kuzidi kuyumba yumba. Mzee
Godwin akashududia gari nyingine za polisi zikija
mbele yake sehemu anapo elekea. Hakua na
uchaguzi wowote zaidi ya kugonga bomba za
daraja, zikavunjika na kuifanya gari kuanza
kushuka kwenye mto huyo wenye maji mengi chini
pamoja na mawe makubwa.
ENDELEA
Mzee Godwin akawahi kuufungua mlango wa gari
kabla halija fika chini, kisha akajirusha peke yake
na kuingia ndani ya maji. Askari wakafika sehemu
ambayo taksi hiyo imedumbukia na kuanza
kushambulia kwa risasi wakiamini mtu aliyopo
kwenye gari hilo ni lazima atakuwa hai.
Risasi zinazo ingia ndani ya maji ya mto huu,
hazikuweza kumpata mzee Godwin, ambaye
alizama ndani ya maji ambayo yanakwenda kwa
mwendo wa kasi, hii ni kutokana na maji hayo
kuwa mengi. Mazoezi ya kijeshi yakaweza
kumsaidia mzee Godwin kuwatoroka polisi ambao
waliendelea kumulika mulika katika sehemu
ambayo gari hilo limedumbukia.
Hadi yanajiri majira ya saa kumi na mbili asubuhi
hawakufanikiwa kumuona mzee Godwin, ila taksi
iliyo tumiwa na mzee huyo kutorokea ilibaki
sehemu ya tukio, huku mwili wa dereva taksi
ukichukuliwa na kupelekwa kwenye chumba cha
kuhifadia maiti hospitali ya taifa Muhimbili.
“Muhehimiwa tumemkosa”
“Endeleni kudumisha ulinzi kila sehemu, na
muhakikishe munamkamata, ninawapa masaa
ishirini na nne kuweza kulikamilisha hilo”
Eddy alizungumza na mkuu wa jeshi la polisi, kwa
njia ya simu huku akiwa amekaa pembeni ya
kitanda cha mke wake ambaye bado anaendelea
kupumulia mashine.
“Sawa muheshimiwa”
Eddy akakata simu, nakushusha pumzi nzito huku
akimfikiria mzee Godwin, ambaye ni amekoswa
koswa kuuawa na baba yake huyo ambaye hadi
sasa hivi hatambui ni nini chanzo cha mzee huyo
kugeuka na kuwa katili sana kwake wakati kipindi
cha nyuma alimpenda sana na kumfundisha
mambo mengi sana
Mama Eddy akaingia kwenye chumba, alichopo
Eddy na mkewe, akiwa ameongozana na Junio.
Eddy akamsalimia mama yake huyo ambaye
hakuonekana kuwa na furaha moyoni mwake.
“Mama mbona kama haupo sawa?”
Mama Eddy akashusha pumzi nyingi huku
akimtazama Eddy aliye nyanyuka na kumpisha
sehemu ambayo alikuwa amekaa.
“Jana kulitokea nini?”
Eddy akamtazama mwanaye kisha akamuomba
mama yake waweze kutoka nje, wazungumze
kwani asinge penda mazungumzo hayo Junio
aweze kuyasikia. Wakakaa kwenye viti vilivyopo nje
ya chumba alicho lazwa Phidaya.
“Jana hapa, Mzee Godwin alikuja, mimi nikiwa nipo
nje. Basi nikamkuta akimchezea chezea mke
wangu akitaka kumuingilia kimwili”
“Wewe hayo yanatokea ulikuwa wapi?”
“Mimi nilikwenda kununu maji”
“Ila Eddy, kama ni hili swala usinge lipeleka
kwenye vyombo vya sheria japo wewe kwa sasa
unahusika na sheria ila si vizuri”
“Sasa mama hapo unahisi mimi ningefanya nini?”
“Ungefanya hata kwa njia nyingine, yaa ni hvi
niniavyo zungumza, kila stesheni ya televishion
ukifungua ni Godwin Godwin, na waandishi
wengine wasivyo na aibu wanaongezea maneno
kwamba ni mume wa waziri mkuu mstafu. Kusema
kweli mimi sijisikii vizuri kwa hilo”
Bibi Junio alizungumza kwa sauti ya upole huku
akiwa ametizama chini, Eddy akabaki kimya kwani
hakujua ni kitu gani anaweza kukizungumza ili
mama yake aweze kumuelewa.
“Eddy ni bora hili swala ungelipeleka kama ulivyo
kuwa unalipeleka pale awali, hembu tazama sasa
hivi jinsi familia sasa hivi inavyo zalilika kwenye
vyombo vya habari”
Mama alizungumza na kutoa gazeti kwenye pochi
yake, gazeti hilo zimepambwa na maandishi meusi
yaliyo andikwa kwa herufi kubwa yakisomeka
(BABA JAMBAZI, MAMA WAZIRI MSTAAFU, MTOTO
STERING, NI BONGE LA MOVIE), chini ya maandishi
hayo kuna picha tatu, moja ikiwa ya mzee Godwin
akiwa amevalia mavazi yake ya jeshi, nyingine
ikiwa ya mama huku yakwangu ikiwa chini ya hizo
picha mbili.
“Hilo ni gazeti la leo, na kama waandishi wa habari
wakijua upo hapo watakuja kuleta fujo hapa wewe
fanya uende nyumbani kwako ukabadilishe hizo
nguo kisha ukafanye mambo mengine”
“Mama siwezi kuondoka na kumuacha mke wangu
hapa. Kwani lolote linaweza kujitokeza”
“Hata kama mama, ila tambua kwamba mkwe
wangu huko ndani hali yake ni mbaya, hivi
makelele ya hao waandishi yakihamia hapa
hospitalini, utamjua ni nani ni mbaya kwako aliye
tumwa kuja kumuua mke wako hapa”
Maneno ya bibi Junio yakamfanya Eddy kukaa
kimya huku akishusha pumzi nyingi.
“Nitakaa hapa na mke wangu hadi hali yake iwe
nzuri, omba ulinzi wa askari wa jeshi la polisi
wawili waje kulinda hapa la sivyo siwezi
kukubaliana wewe kuendelea kukaa hapa”
“Ila ma….”
“Hakuna cha mama, mimi nahitaji amani. Nahitaji
amani ya moyo wangu, nakupenda sana
mwanangu, nampenda mjukuu wangu, nampenda
mkwe wangu. Pia ninampenda sana Godwin
wangu”
Bibi Junio alizungumza huku machozi
yakimwagika, kwa uchungu mkubwa
“Mom what, are you seriously?”(Je upo makini?)
Eddy alishangaa kumsikia mama yake kwamba
bado anampenda mzee Godwin
***
Kwa bahati nzuri maji ya mto huo, yanaelekea
baharini, ikawa ni nafasi nyingine kwa mzee
Godwin kuweza kuingia kwenye bahari ya hidi,
akatazama kila sehemu, ila hapakuwa na uwepo
wowote wa mtu kwenye eneo hilo. Mzee Godwin
akatafuta sehemu iliyo tulia na kujitupa chini na
kulala, usingizi wa magamu gamu ulio
andamanana na njaa kali pamoja na hofu kubwa ya
kuweza kukamatwa na jeshi la polisi kwani tayari
amaanza kusakwa kila kona ya Tanzania.
Kijua cha machana kikaanza kupenya kwenye
macho ya Mzee Godwin ambaye aliye amejilaza
pembeni ya mti wa mkoko, akafumbua macho yake
na yaliyo jaa uchovu mwingi, taratibu akanyanyuka
huku akijikung’uta machanga ulio mjaa sehemu za
mgongoni na kichwani, hii ni kutokana na kujilaza
chali.
Kila sehemu aliyo tazama hakuona uwepo wa mtu
kufika katika eneo hilo. Taratibu akaanza kuelekea
upende wa kaskazini mwake, huku kila muda akiwa
makini sana kwa kutazama kama kuna mtu
anamfwatilia au laa.
Akafanikiwa kukuta kidao kidogo kwa mahesabu ya
haraka haraka wanaingia watu wapatao wawili,
huku ndani ya kidao hicho kilichopo pembezoni
mwa fukwe ya bahari kukiwa na makasia mawili,
Mzee Godwin hakuitaji kupoteza muda kabisa,
alicho kifanya ni kufungua kamba ya manila iliyo
kuwa imefungwa kwenye mti wa mkoko, kuelekea
kwenye kidau hicho, ili kisiweze kuchukuliwa na
maji kipindi yanapo ongezeka pembezoni mwa
fukwe hiyo. Akakisukuma hadi kwenye maji kisha
akavua, shati lake na kulifunga kichwani ili kuzuia
makali ya juu, linalo piga sama kwenye utosi wake.
Taratibu akaanza kupiga makasia huku akiwa
anaimani anapo elekea atapata msaada na kikubwa
zaidi, anahitaji kuondoka nchini Tanzania kabla
hajaingia kwenye mikono ya mwanaye Eddy.
Haikuwa kazi rahisi kwa mzee Godwin kuweza
kuendesha kidau hicho, hii ni kutokana na kuto
kuwa na uzoefu katika kuendesha chombo hicho
ambacho mara nyingi hutumiwa na wavuvi wadogo
wadogo.
Kila alivyo zidi kwenda ndivyo jinsi alivyozidi
kwenda katikati ya bahari, pande zote
amezungukwa na maji ambayo yametulia sana,
nguvu nyingi anazo zitumia, zikazidi kulitesa
tumbo lake ambalo lilianza kukoroma kwa njaa kali
iliyo anza kumpiga kisawasawa, kila alipo jaribu
kujipa moyo ndivyo hali ilivyo muwia ugumu
kwani, nguvu zilidi kumuishia, njaa nayo
haikucheza mbali, akaikuta akijinyoosha ndani ya
kimtumbwi hicho, huku akijaribu kuvuta pumnzi
nyingi, ili aweze kupata nguvu za kumuwezesha
kuendesha kimtumbwi hichi. Gafla kufumba na
kufumbua, mzee Godwin akajikuta akitupwa ndani
ya maji na kimtumbi kumfunika kwa juu, jambo
lililo anza kumchanganya, na kujikuta akianza
kupiga mafumba kadhaa ya maji kwenye kinywa
chake
***
“Mama huwezi kumpenda mtu jambazi, katili, gaidi
kama yu…..”
“Eddy Stop talking”(Eddy acha kuzungumza)
Bibi Junio alizungumza huku machozi yakimtoka,
akamtazama Eddy kwa muda, huku akionekana
kumvumilia mwanaye, na laiti angekuwa si waziri
angemtandika kibao cha shavu, ila akamstiri
kutokana na wauguzi wanao pita pita kwenye kordo
walipo kaa.
“Godwin is your blood dady”(Godwin ni baba yako
wa damu)
“It’s impossible”(Haiwezekani)
Eddy alijibu huku machozi yakimlenga lenga kwani
mtu aliye mpa mareso makali kipindi cha nyuma
leo hii amuambie kwamba ni baba yake wa damu
“Mama mbona siwaelewi”
“Huo ndio ukweli halisi mwanangu, wewe si mtoto
wa Godfrey, baba yako wewe ni Godwin. Am your
mother na natambua ni nani aliyenipa ujauzito
wako”
Eddy akajikuta akishusha pumzi huku macho
yakiwa yamemtoka kiasi kwamba akawa anajihisi
kuchanganyikiwa kwani si jambo rahisi kwani
anavyo tambua kwamba baba yake halisi ni
Godfrey
“Unataka kujua ukweli eheee?”
Mama Eddy alizungumza kwa uchungu mkubwa
huku wakitazama na mwanye, hadi baadhi ya
wauguzi wakaanza kuyatega masikio yao kuweza
kusikia ni kitu gani mama huyo anahitaji
kukizungumza kwa mwanaye huyo
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 11 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (11)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
“Mama mbona siwaelewi”
“Huo ndio ukweli halisi mwanangu, wewe si mtoto
wa Godfrey, baba yako wewe ni Godwin. Am your
mother na natambua ni nani aliyenipa ujauzito
wako”
Eddy akajikuta akishusha pumzi huku macho
yakiwa yamemtoka kiasi kwamba akawa anajihisi
kuchanganyikiwa kwani si jambo rahisi kwani
anavyo tambua kwamba baba yake halisi ni
Godfrey
“Unataka kujua ukweli eheee?”
Mama Eddy alizungumza kwa uchungu mkubwa
huku wakitazama na mwanye, hadi baadhi ya
wauguzi wakaanza kuyatega masikio yao kuweza
kusikia ni kitu gani mama huyo anahitaji
kukizungumza kwa mwanaye huyo
ENDELEA
“Mama”
Eddy alimuita mama yake kwa sauti ya chini,
akaupitisha mkono wake mmoja kwenye bega la
mama yake na kumkumbatia huku akiendelea
kusononeka
“Eddy natambua kwamba Godfrey alikuambia
mambo mengi kuhusiana na sisi, ila yote aliyo
zungumza kwako ni uongo mwanangu”
Mama Eddy aliendelea kuzungumza huku machozi
yakiendelea kumwagika, macho ya Eddy
yakazunguka kwenye eneo walilopo na kuwastua
wauguzi wa kike ambao mara kwa mara waliweza
kuwatazama. Eddy akamnyanyua mama yake na
kuongozana naye hadi lilipo gari lake na kuingia
ndani. Akafunga vioo vyote vya gari ili sauti isitoke
nje
“Mama nimesha kua sasa, nahitaji kujua ukweli wa
kila kitu kuhusiana na yupi ni baba yangu kati ya
Godwin na Godfrey?”
Mama Eddy akashusha pumzi nyingi, huku taratibu
akiipa nafasi akili yake kuweza kuvuta
kumbukumbu zake za nyuma.
**
Miaka arobaini na tano iliyo pita, nilikuwa ni binti
mzuri sana mwenye kuvutia machoni mwa wengi,
nilikuwa ninapendezeshwa na mama yangu, kila
asubuhi nilipo kuwa ninaamka. Kipindi hicho
nilikuwa ninami mitatu, jambo ambalo liliwafanya
wazazi wangu kwa kipindi kile kuweza kunianzisha
masomo ya chekechea. Ilikuwa ni furaha kubwa
kwangu mimi, kuweza kuanza shule mapema kiasi
hichi, ila nilijikuta ninakuwa kivutio kwa wanafunzi
wengine wakiwemo Godwin na Godfrey, ambao nao
pia walikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wa
chekechea niliyo kuwa ninasoma, Godwin na
Godfery walitokea kuwa marafiki zangu sana, hii
nikutokana na kufanana kwao. Kila mmoja alikuwa
na sifa zake za kipekee
Godwin yeye alikuwa ni mcheshi, mpenda michezo,
mteteaji. Alikuwa ananitetea kila pale nilipokuwa
ninaonelewa na baadhi ya wanafunzi wezetu
ambao walikuwa wakizivuta nywele zangu
nilizokuwa nimesukwa mabutu mabutu.
Ila Godfrey alikuwa ni mvivu darasani, alikuwa
hapendi michezo na mara nyingi alikuwa anapenda
kukaa na wasichana wengine, jambo lililo kuwa
likitukera mimi na Godwin. Tulibahatika kusoma
shule ya msingi pamoja, hadi tunafika sekondari
sote tukawa katika shule mmoja. Ila Godfrey
alikuwa bize na visichana wengine. Nilimpenda
sana Godfrey nikawa ninawivu naye japo
sikumueleza ukweli kwamba ninampenda sana na
kumuhitaji. Godwin alinipenda sana kiasi kwamba
sikuwa na jinsi zaidi ya kujikuta nikimpenda
Godwin.
Tulipo maliza kidato cha nne mimi nilibahatika
kwenda kusoma Uingereza, kutokana baba yangu
alikuwa na uwezo na pia alikuwa ni mwanasheria
mkuu wa kipindi hicho. Nilikaa Uingereza kwa
miaka nane. Kwakipindi chote sikuwa na
mawasiliano kati ya Godwin na Godfrey, ila nilikuja
kusikia kwamba baba yao alifariki kwa ugonjwa wa
sartani ya damu. Na sikuweza kujua ni wapi
walipo. Nilijitahidi kadri ya uwezo wangu
kuwatafuta ila sikuweza kupata mafanikio.
Nilipo anza kazi ya udaktari kwenye kitengo cha
upasuaji katika hospitali ya Muhimbili, ndipo kuna
siku kulitokea ajali ya basi, hapo ndipo nilipo weza
kumpata Godwin, akiwa ni miongoni mwa majeruhi
wa ajali hiyo. Godwin alikuwa mahututi, ilinilazimu
kumfanyia upasuji mimi na madaktari wezangu,
Alipo pata nafuu, mapenzi yetu yakafufuka upya.
Ndipo nilipo amua kuanza kuishi naye nikiwa katika
mapenzi mazito, ndipo alipo mleta Godfrey kuja
kuishi nasi pale nyumbani. Godwin kwa kipindi
hicho alikuwa nimwanajeshi, na alikuwa anakwenda
sana nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo mbalimbali.
Ninakumbuka alipangiwa safari ya kwenda
Pakistani, huko walipangiwa kwenda kukaa kwa
kipindi kisicho julikana.
Ulikuwa ni usiku wa fauraha na majonzi mimi na
Godwin, pale tulipo kuwa kitandani, kwani ilikuwa
ni muda mchache tangu tufunge ndoa yetu. Siku
hiyo ndio siku ambayo nilikuwa kwenye siku za
hatari kama mwanamke, aliye kamilika, niliweza
kuzipokea mbegu za Godwin, na kujua kabisa
zimekwenda kuingia kwenye mfuko wangu wa
uzazi. Asubuhi ya siku iliyo fwata tulimsindikiza
Godwin hadi kwenye uwanja wa ndege
“Gody, mlinde shemeji yako, najua ninapo kwenda
nipagumu sana, ila ningependa nirudi nimkute mke
wangu akiwa salama”
“Sawa ndugu, nitamlinda hakuna kitakacho mpata”
“Baby usilie, kila kitu kitakuwa sawa, pia moyo
kondo mbona ni siku chake tu nitarejea”
“Godwin si kweli, najua unapo kwenda si sehemu
salama”
“Noo baby nitarudi siku za si nyingi”
Godwin alinibusu mdomoni mwangu, kisha
akanyanyua begi lake kubwa alilokuwa amehifadhia
vitu vingi kisha taratibu akanikumbatia vya mwisho
mwisho kisha akaondoka na kwenda kuungana na
wanajeshi wengine, kwa macho yangu
nilimshuhudia akiingi kwenye ndege na kuondoka,
jambo lililo nipa uchungu mkubwa sana kwenye
maisha yangu
“Shem twende nyumbani”
Godfrey alinibembeleza kwa uchungu pale nilipo
ninalia nikimshuhudia mume wangu akiondoka
nchini na kuniacha mimi peke yangu. Kusema
kweli Godfrey alikuwa ni mzuri sana, na wakuvutia
kupita Godwin ambaye mafunzo ya jeshi yaliweza
kumkomaza kwa kipindi alicho kuwa akifanya hayo
mazoezi magumu
Tulirudi nyumbani, huku tukiwa katika hali ya
huzuni, hususani mimi ndio upweke ulinijaa sana
moyoni mwangu, moja kwa moja niliingia
chumbani kwangu kwa ajili ya kulala, ili nijitahidi
kuzoea mazingira ya upweke. Sikujua ni kwanini
nilikuwa na huzuni kubwa sana kwa kipindi hicho
tofauti sana na ilivyo kuwa akisafiri nchi za afrika.
Nilivua nguo zangu zote na kujitupa kitandani,
usingizi fofofo ulinipitia. Ila nilivyo kuwa katikati ya
usingizi, nilistukia kitu kikinipapasa kwenye
makalio yangu, nikastuka na kufumbua macho
yangu, hapo ndipo nilipo mkuta Godfrey akiwa
nyuma kitandani, akinipapasa na mikono yake.
Nilijitahidi kumuomba asifanye kitu chochote, ila
kwa ushawishi namaneno yake matamu aliweza
kunishawishi na kujikuta nikifanya naye mapenzi,
huku akiahidi kwamba itakuwa ni siri kubwa kati
yangu mimi na yeye.
Ila mapenzi yalizidi kukua siku hadi siku, hapo
ndipo nilipo kuja kuhisi kwamba ninaujauzito,
ambao ulianza kuniumiza kichwa changu. Ila
nikiwa katika kipindi hicho kwabahati nzuri
nilibahatika kupata mawasiliano na Godwin,
niliweza kumuelelea juu ya hali yangu kwamba
mimi ni mjamzito. Kusema ukweli Godwin
alishangilia na kuwa ni mtu mwenye furaha kusikia
kwamba mimi ni mjamzito. Na kwakipindi chote
alikuwa akiniambia kwamba anafanya mpango
aweze kupata japo likizo ya wiki moja ili aje
kuniona nikiwa katika hali yangu ya ujauzito
“Hiyo ni mimba yangu na si ya Godwin”
Godfrey alinitishi, kwamba ujauzito ni wakwangu,
na nikikataa kwamba si wakwake, atakuja kusema
ukweli kwa kaka yake, ambaye siku zote
walipendana sana na sikupenda siku hata moja
kuja kuwachonganisha Godwin na Godfrey.
Nilimueleza ukweli baba yangu, ambaye alisha
nifanyia mpango wa mimi kuingia serikalini na
kuwa kiongozi mkubwa. Baba yangu alichukizwa
na Godfrey kunifanyia hivyo, ndipo alipo anza
kusuka mpango wa kumuangamiza Godfrey, ili siri
isivuje nje kwamba nilikuwa na mahusiano naye.
Siku ninapata uchungu wa mimba yako Eddy,
Ndipo siku Godwin alipo fika nyumbani na kunikuta
katika hali hiyo, huku Gofrey alikuwa hayupo
nyumbani amekwenda kwenye mishe mishe zake.
Godwin hakubadili hata nguo zake za jeshi,
alinipeleka hospitalini ambapo ninashukuru Mungu
niliweza kubahatika kujifungua salama na kukupata
wewe.
Godwin alifurahi sana kwani wewe na yeye
mulifanana sana, hapakuwa na mtu ambaye
aliweza kutofautisha kufanana kwenu, Moyoni
nikapata amani kwamba mtoto amefanana na baba
yake.
Vitisho vya Godfrey vilizidi kupamba moto, hai
ikafikia hatua kwamba ikanilazimu kuanza kuufanya
mpango wa kuweza kumuu, ili siri ibaki kuwa pale
pale. Niliingia serikalini na kuwa mbunge wa viti
maalimu, Mwaka mmoja nikiwa kama mbunge wa
viti maalumu babu yako Mzee Eddy alifariki kwa
ajali ya gari akitokea kazini. Lilikuwa ni pigo kubwa
sana kwangu, kipindi hicho Godwin alikuwa
amerudi Pakistani kuendelea na kazi waliyo itiwa
kule.
Godfrey alinipa kitisho kwamba ataweka kila kitu
wazi kwenye mazishi ya kumuaga baba yangu,
hapo ndipo nilipo tumia nguvu ya ziada ya
kuwatuma watu ambao walimteka Godfrey na
kumtesa sana, Nilimpa nafasi ya moja, aweze
kuondoka nchini, la sivyo nitamuua kwa mkono
wangu mwenyewe, ili siri yangu ibaki pale pale.
Ulizidi kukua na kuwa ni mtoto mzuri, uliye weza
kupata marafiki wengi wakubwa, kwawatoto
ulikuwa ni kivutio kizuri machoni mwa wengi, ulipo
fikisha miaka mitatu uliweza kupata mkataba katika
kampuni moja ya waingereza inayo tengeneza
nguo za watoto, na walikutumia wewe kama njia ya
matangazo kwa kuzitangaza nguo zao. Baba yako
alipo rudi, hakuhitaji kusikia kwamba unaendelea
kufanya hivyo. Alijaribu kumtafuta pacha wake ili
kuweza kujua kwamba yupo wapi, ila hakufanikiwa,
kwani nilimuambia aliondoka kwa kipindi kirefu na
sikuweza kumpata.
Miaka mingi ilipita, hapo ndipo Godwin alipo kuja
kugundua kwamba mimi nilihusika katika mauji ya
mdogo wake, Na pia akahisi kwamba wewe si
mwanae ni damu ya mdogo wake, hapo ndipo
alipo anza kufanya visasi vya kutaka kukua wewe
na mimi kwani alijiapiza kwamba asinge hitaji
kuona mimi ninaendelea kuishi, wala wewe kuishi
kwani alihitaji akuue ili amsahau mdohgo wake
**
Mama Eddy alimaliza kuzungumza historia fupi
iliyo mfanya Eddy kumwagikwa na machozi, kwani
kosa hakuwa nalo Mzee Godwin, kuso kubwa lipo
kwa mama yake
“Eddy am sorry”(Eddy samahani)
Mama Eddy alizungumza huku akijaribu kumshika
mkono Eddy, ambaye aliusogeza pembeni kwani
hakuhitaji
“Mama you’re a killer”(Mama wewe ni muaji)
Eddy alizungumza kwa hasira huku akishuka
kwenye gari, kwa hasira na kumuacha mama yake
akiendelea kulia kwa uchungu.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 12 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (12)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Mama Eddy alimaliza kuzungumza historia fupi
iliyo mfanya Eddy kumwagikwa na machozi, kwani
kosa hakuwa nalo Mzee Godwin, kuso kubwa lipo
kwa mama yake
“Eddy am sorry”(Eddy samahani)
Mama Eddy alizungumza huku akijaribu kumshika
mkono Eddy, ambaye aliusogeza pembeni kwani
hakuhitaji
“Mama you’re a killer”(Mama wewe ni muaji)
Eddy alizungumza kwa hasira huku akishuka
kwenye gari, kwa hasira na kumuacha mama yake
akiendelea kulia kwa uchungu.
ENDELEA
Eddy akatoka na kutembea kwa hasira hadi nje ya
geti na kuvuka barabara na kutafuta sehemu iliyo
tulia na kukaa hapo, ili hasira iweze kumshuka,
hakuamini kwamba makosa ya mama yake
yamesababisaha matatizo makubwa makubwa
kwenye maisha yao.
Baadhi ya watu walio kuwa kwenye eneo hilo,
hawakusita kumtazama Eddy ambaye
wanamfahamu kama waziri wa ulinzi, hawakujuwa
ni kwani yupo pale kwa wakati huu.
***
Junio akiwa pembezoni mwa kitanda cha mama
yake, akijitahidi kumfanyia maombi kwa Mungu, ili
aweze kupona. Akahisi kukanyaga kitu kigumu
chini ya uvungu wa kitanda, akainama taratibu na
kuchungulia kuona ni kitu gani kilichopo chini ya
uvungu wa kitanda hicho. Akakuta bastola ikiwa
ipo chini ya kitanda alicho lalia mama yake.
Akaichukua na kuitazama vizuri, hakuwa mgeni
sana kuona silaha hiyo, kwani kwa mikiki mikiki
aliyo pitia kwenye maisha yake, milio ya risasi
kwake ilikuwa ni jambo la kawaida japo anaumri
mdogo sana. Akaitazama vizuri na kunyanyuka,
akiwa ameishika mlango wa chumba ukafunguliwa,
akaingia bibi yake akiwa na macho mekundu
akionekana kama ametoka kulia muda si mrefu
“Juniooo”
Mama Eddy aliita kwa sauti ya juu, huku aliyo
mfanya Junio kushangaa kwanini bibi yake
anamuita kwa sauti hiyo. Bibi yake akapiga hatua
hadi sehemu alipo simama na kumpokonya
bastola hiyo
“Umeitoa wapi hii?”
Mama Eddy alimuuliza kwa sauti ya ukali
“Hapo chini ya kitanda”
Junio alijibu kwa sauti ya uoga kwani hakuwahi
kumuona bibi yake akiwa katika hali ya kukasirika
kama hiyo, Mama Eddy alipo gundua, kuna hali ya
hofu kwa mjukuu yake kipenzi anaye mpenda
kuliko kitu chochote, taratibu akapiga magoti na
kumkumbatia mjuu kuu wake
“Nisamehe kwa kukufokea”
Mama Eddy alizungumza huku akiendelea kulia,
Junio hadi muda huu hakuelewa ni kitu gani
kinacho endelea kwa bibi yake
“Baba yupo wapi?”
Junio aluuliza kwa wasiwasi mwingi huku
akimtazama bibi yake
“Yupo nje ya geti”
“Anafanyaje?”
Mama Eddy hakujibu chochote zaidi ya kuangua
kilio kilicho changanyikana na uchungu mwingi.
Mama Eddy akaiokota bastola yake na kujiwekea
kichwani huku akimuachia mjukuu wake
“Bibi…..!!!”
Junio aliita huku machozi yakimwagika, kwani
anatambua kwamba bibi yake kuna kuti
kinamsumbua hadi anafikia hatua ya kutka kujiua
“Nenda kamuite baba”
Junio kwa kuchanganyikiwa akachomoka kwa
haraka na kuanza kukimbilia nje ya geti
***
Sifa za uzuri wa Shamsa, zikaanza kuenea katika
chuo kizima, huku vijana wakiume wanao jihisi wao
niwazuri hawakucheza mbali na Shamsa, ambaye
tangu afike chuoni hapo, alibahatika kupata rafiki
mmoja wa kike ambaye anaishi naye chumba
kimoja, uzuri wa rafiki yake huyo ni kwamba wapo
darasa moja, na rafiki yake anaifahamu vizuri lugha
ya kiswahili.
“Habari”
Suuti ya kiume ya kijana mmoja wa kihindi
ilimsalimia Shamsa, mara baada ya kukaa kwenye
kiti chake darasani, akageuka na kumtazama kijana
huyo ambaye anaonekana kuwa ni mgeni machoni
mwake na ndani ya darasa hilo. Uzuri zaidi kijana
huyo amemsehemsha kwa lugha ya kiswahili.
“Salama tu vipi?”
“Safi, naitwa Ajay Khan, wewe ni Shamsa?”
“Umelijuaje jina langu?”
“Chuo kizima umakuwa maarufu kwa uzuri wako?”
Ajay Khan alizungumza na kumfanya Sahmsa
kutabasamu, na ukitazama ni kweli, japo vijana
wengi kwenye chuo hicho cha udaktari wao ni
wahindi halisi, ila yeye kwa bahati nzuri aliweza
kuchanganyia na muafrika na kumfanya uzuri wake
uwe maradufu, huku vijana wengi wakimtamani
kimapenzi
“Asante”
“Sijui ninaweza kupata nafasi ya kuzungumza na
wewe?”
“Kwanza umejua vipi kiswahili?”
“Ahaaa mimi ninandugu, Tanzania, maeneo ya
Kariakoo pale kuna maduka ya baba zangu
wadogo na nimeishi Tanzania kwa miaka kama
mitano hivi”
“Ahaa kumbe unapajua Tanzania?”
Shamsa, alizidi kujisikia furaha kwa kumpata rafiki
mwengine anaye itambua lugha ya kiswahili, kabla
hajamjibu Ajay Khan, profesa akingia darasani kwa
ajili ya kuwafunidisha kushusiana na somo la
mifupa
“Tutazungumza baadae”
Ajay Khan alizungumza kwa sauti ya chini, huku
akifungua vitabu vyake na kumfanya Shamsa
aachie tabasamu pana lililo mfanya azidi
kuonekana kuwa yeye ni msichana nzuri na
wakuvutia sana. Baada ya kipindi hicho, kwisha,
Shamsa akaingiza vitabu vyake kwenye begi lake
la mgongoni na kutoka nje ya darasa, huku kila
mwanafunzi akiondoka zake, kwani ni muda wa
mapumziko
“Shamsa Shamsa”
Ajay Khan aliita kwa sauti ya juu, huku
akimkimbilia Shamsa. Shamsa akageuka na
kumtazama Ajay Khan
“Vipi?”
“Nahisi ulisahau kwamba tutazungumza baadae”
“Ohoo samahani, unajua masomo yanabana
ukitegemea kwamba wiki ijayo ni mtihani”
“Hakuna kitakacho haribika”
“Ehee niambie?”
“Napenda kukualika leo uje kwenye mechi yetu ya
Rugby”
“Wewe ni mchezaji pia?”
“Ndio si unaona misuli hii”
Ajay Khan, akatunisha misuli yake na kuifanya
ionekane vizuri, Shamsa akatabasamu
“Ni saa ngapi?”
“Saa kumi jioni”
“Basi nitajitahidi kuja, kwa maana mimi sio mpenzi
sana wa michezo hiyo”
“Mmm itabidi uipende tu”
“Sawa nitakuja”
Wakaachana kila mmoja akaelekea kwenye
mabweni yao, huku Ajay Khna, akianza kuamini
kwamba mpango wake wa kumpata mtoto mzuri
kama huyo unaanza kufanikiwa katika siku chache
zijazo. Muda wa mechi, Shamsa na rafiki yake,
Kajol Khapoor, wakeelekea kwenye uwaja ulipo
kwenye eneo la chuo, ambao unayumika kwa
mchezo wa rugby. Uwanja mzima umejaa
wanachuo na watu toka nje ya chuo, kwani ni
mechi inayo husisha timu ya chuo chao, pamoja
na timu moja ya club, iliyo kuja kuomba kuweza
kucheza timu hiyo ya chuo. Shamsa na Kajol
wakatafuta sehemu ambayo wanaweza kukaa na
kuona vizuri kiwanja hicho kwa juu, wakapata viti
viwili, na kukaa huku pembeni yao kukiwa na
wanachuo wengine walio valia sare za timu ya
chuo chao.
“Unajua ni sisi tu hatujavaa sare, na tumekaa
sehemu walipo vaa sare wezetu”
Shamsa alizungumza akionekana kuwa na
wasiwasi mkubwa
“Hakuna tatizo kwani wao si wanafunzi kama sisi”
“Mmm haya”
Wachezaji wakaanza kuingia uwanjani, huku
makofia yao wakiwa wameyashika mikononi,
macho ya Shamsa yakatua kwa Ajay Khan, aliye
miongoni mwa wachezaji hao. Akaitazama jezi ya
Ajay Khan, kwa nyuma imeandikwa jila AJAY, kwa
maandishi makubwa huku namba themanini, ikiwa
imeandikwa kwa maanshi makubwa.
Ajay Khan, kwa haraka akaanza kupitisha macho
yake kwenye majukwaa yaliyopo katika uwanja,
akijitahidi kutafuta Shamsa kama amweza kufika
kwenye kiwanja hichi. Kwa bahati nzuri akafanikiwa
kumuona kwenye mashabiki wa timu yao, huku
Shamsa na mwenzake wa pembeni wao wakio ndio
hawajavalia jezi za timu yao. Ajay Khnan kwa
ishara akambusu Shamsa kisha akavaa kofia lake
ambalo mchezo huo unawahitaji kuvaa hivyo ili
wasiweze kuumia vicha vyao, kwani ni mchazo
unao tumia nguvu sana.
“Amekubusu wewe yule kaka?”
“Hapana Kajol hajanibusu mimi”
“Mmmm haya mwaya”
Mchezo ukaanza, kwa kasi kubwa, huku Ajay Khan
akionekana kushambulia wapinzani wake, kwa kasi
alizo kuwa nazo ziliweza kuwafanya wezake
kumpatia mpira, kila mara walipo upata na Ajay
Khan, aliweza kuwapita kwa spidi wachezaji wa
timu pinzani na mpira kwenda kuuweka mwisho
wa mstari ambapo kwa mchezo huo hilo
linahesabika ni goli.
Uwanja mzima, ukawa unalitaja jina la Ajay, Ajay.
Kila mmoja alimshangilia na kila alipo ushika
mpira kila mmoja alitarajia kumuona Ajay akifika
kwenye mstari wa mwisho wa wapinzani wao na
kuuweka mpira chini na kuhesabu goli. Hali ya
Ajay kupanda kiumaarufu, ikapenya moyoni mwa
Shamsa na kujikuta akitamani Ajay awe ni mtu
wake wa karibu, isitoshe ni mtu ambaye
anaifahamu nchi aliyo tokea kwa sasa. Ajay
akajirusha juu kuunyaka mpira alio rushiwa na
mwenzake, Kwa bahati mbaya beki wa timu
pinzani kwa nguvu akamrukia na kwakutumia bega
lake akampiga tumboni na kuanguka naye chini, na
kumfanya Ajay Khan atulie kimya, jambo lililo
wafanya mashabiki wote pamoja na Shamsa kukaa
kimya na kukodoa macho yao kila mmoja akiamini
muanguko wa Ajay Khan umeleta matatizo
makubwa kwa Ajay
***
Junio akaanza kuangaza macho yake huku na huku
akiwa nje ya geti la hospitali, akimtafuta baba yake
ni sehemu gani ambapo yupo. Kwa hahati nzuri
akamuona akiwe amesimama kwenye moja ya
sehemu iliyopo upande wapili wa barabara
Eddy akiwa katika msongamano wa mawazo
akifikiria ni nini afanye, breki kali za gari zikamstua
na kumfanya ageuke kwa haraka na macho yake
kutazama barabarani, ambapo alimshuhudia
mwane Junio akiwa katikati ya barabara, huku gari
aina ya Verosa, ikiwa imemlanga Junio, aliye
shikwa na bumbuazi asijue ni nini afanye.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 13 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (13)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Junio akaanza kuangaza macho yake huku na huku
akiwa nje ya geti la hospitali, akimtafuta baba yake
ni sehemu gani ambapo yupo. Kwa hahati nzuri
akamuona akiwe amesimama kwenye moja ya
sehemu iliyopo upande wapili wa barabara
Eddy akiwa katika msongamano wa mawazo
akifikiria ni nini afanye, breki kali za gari zikamstua
na kumfanya ageuke kwa haraka na macho yake
kutazama barabarani, ambapo alimshuhudia
mwane Junio akiwa katikati ya barabara, huku gari
aina ya Verosa, ikiwa imemlanga Junio, aliye
shikwa na bumbuazi asijue ni nini afanye.
ENDELEA
“Junioooooooooo”
Eddy alipaza sauti kama mwenda wazimu kumstua
mwanae huyo wa kiume, ila haikuwa hivyo kwani
gari hiyo tayari ilishamfikia Junio karibu na
kumbamiza kwa nguvu, akarushwa juu futi kadhaa
kisha akaanguka chini kwenye lami, na kichwa
chake kikaanza kuvuja damu sehemu ya usogoni.
Mlio wa risasi, ukawastua watu wote walio ndani
ya hospitali hadi wale waliopo nje, na kuwafanya
kila mmoja kuweza kutafuta ustarabu wake kwa
kukimbia sehemu anayo ifahamu yeye kwani kila
mmoja alihisi sehemu hiyo si salama, kutokana na
fununu za kwamba Mzee Godwin alipanga kuweza
kufanya mashambulizi katika sehemu muhimu,
ikiwemo hospitalini.
Miguu ya Eddy ikachanganya kasi ya ajabu, hadi
katika sehemu alipo lala mwanaye aliye anza
kuzingirwa na wananchi walio fika kuweza kutoa
msaada kwa mwanae.
“Juniooo”
Eddy alizungumza huku akiwa katika mshangao
mkubwa, akimtazama mwanaye mwenye sura nzuri
akivujwa na damu puani pamoja na sehemu ya
nyuma ya kichwa ikiashiria kwamba mwanaye
ameweza kupasuka kichwa kwa nyuma,
Wanaume walio majasiri waliweza kunyanyua Junio
na haraka haraka, wakamuingiza ndani ya hospitali
kwani kwa mbali mapigo yake ya moyo bado
yanakwenda taratibu. Baadhi ya askari walio weza
kufika katika eneo la tukio wakamchukua waziri
Eddy na kumungiza ndani ya hospitali, kwani kwa
kipindi chote alikuwa amesimama kwenye kundi
lawatu akizitazama damu nyingi za mwanaye zilizo
kuwa zimetapakaa kwenye lami.
“Muheshimiwa yupo wapi?”
Mzee Selemani Mbogo alimuuliza daktari huku
akiwa anahema sana, na jasho jingi likiendelea
kumwagika kwani alicho kishuhudia katika chumba
alicho lazwa mke wake kinaogopesha sana.
“Aaa..a amepelekwa chumba cha mapumziko?”
“Nipeleke”
Mzee Selemani Mbogo akamshika mkono
muhudumu huyo hadi kwenye chumba alicho
pumzisha Eddy, akamkuta akiwa ametulia kimya
huku amejikunyata asijue ni kitu gani kilicho tokea
kwa wakati ule.
“Muheshimiwa muheshimiwa”
Mzee Mbogo alimuuita Eddy na kumfanya
amgeukie na kumtazama kwa muda huku macho
yake yakiwa mekundu huku machozi yakimwagika
kwa wingi. Mzee Mbogo akasimama kwa muda
huku akiwa na bumbuazi akiwa na maswali mengi
kwani yeye ndio mtu wa kwangu kuingia katika
chumba alicho lazwa mkewe baada ya mlio wa
risasi kusikika.
“Muheshimiwa kuna tatizo”
Mzee Mbogo alizungumza kwa sauti ya upole iliyo
jaa unyenyekevu wa hali ya juu, Eddy akaachia
tabasamu dogo huku machozi yakimwagika
“Nimeona, Junio ame…….”
Eddy hakuweza kumalizia sentensi yake, machozi
yakamtiririka kwa wingi mno. Mzee Mbogo akaki
akiwa ameduwaa, akashusha pumzi nyingi na
kumfwata Eddy kitandani alipo kaa na kumshika
bega la kushoto.
“Twende ukaone”
Mzee Mbogo akamshika mkono Eddy na kumvuta
mkono Eddy, ila Eddy akajikaza misuli yake
akiashiria kwamba hato weza kwenda mahala
popote. Mlango ukafunguliwa kwa pupa na kuingia
nesi mmoja akiwa anahema kwa nguvu
akioenekana ametoka kukimbia kwani jasho jingi
pia liliweza kimwagika.
“Muheshimiwa unaitwa chumba alicho la…laa lazwa
mkeo kuna tatizo”
Nesi huyo alizungumza huku akihema sana, Eddy
akamtumbulia macho nesi huyo, kichwani mwake
kukamjia picha ya mke wake kipenzi PHIDAYA.
Eddy bila hata kusukumwa na mzee Mbogo,
akakurupuka kitandani na kutoka nje ya chumba
huku akiwa katika kasi ya ajabu sana, akafanikiwa
kufika hadi sehemu ya nje ya chumba alicho lazwa
Phidaya, akakuta baadhi ya askari wa jeshi la polisi
wakiwa wamesimama kuimarisha ulinzi huku
manesi, wagonjwa na wanandugu walio kuja
kutembelea wagonjwa wao, wakiwa wamekusanyika
nje ya chumba cha mke wake, huku maaskari
wakijaribu kuwazuia kuwez kuona nini
kinaendeleka ndani ya chumba hicho. Kasi ya Eddy
ikapungua baada ya kukuta hali kama hiyo,
akajikuta taratibu akiaanza kutembea kwa mwendo
wa kawaidia, ila akiwa na hamu ya kuweza kufika
mlangoni mwa chumba hicho, ila tatizo kubwa
likawa kwenye miguu yake kwani ilijawa na uzito
wa gafla,
Kwa kijikongoja taratibu akaweza kufika kwenye
mlango ambapo ulifungwa, askari mmojaa
akagonnga mlango huo akiashiria kwamba walipo
ndani waweze kuufungua mlango huo, nafasi ya
mlango ulipo weza kufunguliwa, kwa msaada wa
askari huyo Eddy aliweza kuingizwa ndani
kujishuhudia kilicho tokea. Macho yakamtoka
Eddy, kizunguzungu kikali kikamkamata na kujikuta
akianguka chini, kabla hajafika sakafuni baadhi ya
watu wakamdaka na kumlaza chini taratibu.
(Nusu saa kabla)
Baada ya mjukuu wake kutoka, mama Eddy
akaitazama bastola aliyo kuwa ameishika Eddy
nakujikuta akishusha pumzi nyingi zilizo mfanya
kukigeuza kichwa chake kwa mkwe wake aliye lala
kitandani huku ajitambui, akaachia tabasamu pana
kisha taratibu akamsogelea Phidaya aliye lala
pasipo kijitambua, akaushusha uso wake taratibu
na kulibusu paji la uso la Phidaya, huku machozi
yakimwagika kwa wingi.
“Najua mwanangu anakupenda sana, si wewe tu
hata mwanaye anampenda”
Mama Eddy alizungumza huku machozi
yakiendelea kumwagika usoni mwake,
akajipangusa machozi yake kisha akarudia tena
kumbusu Phidaya kwenye paji la uso wake.
“Eddy nisamehe mwanangu, sihitaji mtoto wa watu
aweze kupata tabu kwa ajili yangu, kwani mimi
ndio mkosefu mkuu katika haya yote”
Mama Eddy akaiweka bastola yake pembeni na
kukitoa kifaa maalumu cha kumsaidia Phidaya
kupumua kisha kwa kutumia nguvu zake zote
akaanza kumkaba Phidaya shingoni, Phidaya
akaanza kurusha rusha miguu yake kuweza,
kuipigania roho yake isitoke kwa wakati huo ila
hakuwa na jinsi kwani yupo katika wakati wa kuto
kujitambua. Mama Eddy alipo jiridhisha kazi yake
imefanikiwa na Phidaya ametulia kimya,
akausokomeza mdomo wa bastola mdomoni
mwake na kumtazama Phidaya tena usoni na
kuachia tabasamu pana.
Mzee Mbogo akiwa halitambui hili wala lile akiwa
hatua chache kutoka ulipo mlango wa chumba
alicho lazwa mke wa Eddy, mlio mkubwa wa
bastola ukamshua, na kujikuta akiwa amesiama,
watu waliokuwa eneo la karibu wakaanza
kuchanguka pasipo yeye, ujasiri mkubwa ukamvaa
na kujikuta akikimbilia katika chumba hicho,
akausukuma mlango na kuingia ndani. Hakuamini
macho yake, akamkuta Mama Eddy akiwa
amejifumua kichwa chake kwa risasi na
kumuangukia Phidaya aliye kimya kitandani na
damu nyingi zikasambaa kwenye shuka lililo
mfunika Phidaya.
“Mungu wangu!!!”
Mzee Mbogo alizungumza huku akiwa ameuziba
mdomo wake kwa kiganja, akataka kupiga hatua
chache kuingia ndani ya chumba hicho ila miguu
ikashindwa kumsogeza ndani, ikabidi kugeuka na
kutazama nje.
Kwa kiwewe alicho kipata hakuweza hata kujua ni
wapi aendee, ni nini azungumze, hata manesi walio
kuwa wamejibanza kwenye kona mbalimbali kika
mmoja akijitahidi kuyaokoa maisha yake, wakaanza
kuchungulia na kumuona mzee huyo akiwa
anatetemeka nje ya mlango. Wakaendelea
kusikilizia kwa dakika kadhaa, kuona kama mtu
aliye fyatua hiyo risasi atatoka nje au laa. Hadi
walipo fika askari wawili wenye bunduki, ndipo
mzee Mbogo akarudiwa na kumbukumbu zake
kuweza kujitambua ni wapi alipi. Kila askari aliye
chungulia ndani ya chumba hicho, aliweza kutoka
nje kupata mwangaza wa mwanga wa nje, kwani
chumba hicho kimetapakaa damu nyingi sana.
“Eddy, EDDY”
Mzee Mbogo alizungumza na kuanza kukimbia
huku na huku kumtafuta Eddy ni wapi alipo,
haikuwa kazi rahisi kuweza kumpata Eddy, hadi
alipo weza kumsimamisha nesi mmoja na
kumuulizia bosi wake huyo ni wapi alipo.
***
Mstuko mkubwa ukampata Shamsa na kujikuta
furaha yote ikitoweka usoni mwake, haikuwa ni
mstuko kwa Ajay kuanguka chini na kuonekana
kama ameumiua sana, ila mstuko, ambao ulianza
kujenga hisia mbaya kichwani mwake. Picha ya
mdogo wake Junio ikamjia kichwani mwake, na
kujikuta moyo wake ukikumbwa na maumivu
makubwa sana kiasi kwamba akaanza kujihisi
mnyonge sana. Taratibu akaanza kuondoka
kwenye kundi kubwa la mashabiki walio fika
uwanjani, huku kwa mbali machozi yakianza
kumlenga lenga.
“Shamsa unakwenda wapi?”
Kajol alimuita Shamsa, aliye kuwa akitembea
pasipo kujua ni wapi anakwenda kwani kichwani
mwake alkijisikia vibaya sana.
Kajol akawahi kumshika mkono Shamsa na
kumsimamisha akilini mwake, Kajol akahisi ni
labada Ajay alivyo anguka vibaya uwanjani na
kutolewa na machela.
“Njoo ukae hapa”
Kajol kwa upendo mkubwa akamsogeza rafiki hadi
kwenye moja ya kiti na kumkalisha kisha na yeye
akavuta kiti kingeni cha plastik kilicho kuwa
pembeni na kumshika begani.
“Usijali Ajay atapona tu sawa wangu?”
Shamsa hakujibu kitu chochote, mapigo ya moyo
yakazidi kumuenda kasi kiasi kwamba akajikuta
jasho likianza kumwagika. Kitendo cha jasho
kumwagika Shamsa, kikamstua sana Kajol na
kuhisi kwamba rafiki yake ameshikwa na homa ya
gafla. Kajol akamuwekea mkono shamsa kwenye
shavu kutazama kama kuna kitu chochote kilicho
mpata, mwili mzima wa Shamsa ukawa unachemka
kwa joto kali sana.
“Mungu wangu, Shamsa unaumwa wewe!!”
Shamsa akatingisha kichwa kukataa kwamba
anaumwa, Kajol hakutaka kukubaliana na rafiki
yake huyo ikambidi amuage ukaombe msaada wa
madaktari waliopo ndani ya uwanja. Shamsa
akaitoa simu yake mfukoni na kuiwasha, ujumbe
wa njia ya whatsapp ukaingia huku kikiwa na
namba ngeni.
“Ni nani?”
Shamsa alijiuliza kabla ya kufungua ujumbe huo
wenye meseji kumi, huku meseji inayo onekana
kati ya kumi inamuuliza kwa herufi kubwa ‘WEWE
NDIO SHAMSA EDDY?’
Ikamlazimu Shamsa kuweza kuufungua ujumbe
huo na kukutana na mlolongo mkubwa wa picha
ambazo hazionekani vizuri hadi azifungue,
akafanya hivyo. Picha ya kwanza ikamstua na
kumfanya mapigo ya moyo kuzidi kumuenda kasi,
akajaribu kusimama ila nguvu za miguu
zikamuishia na kuanguka chini, akapoteza fahamu.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 14 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (14)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Shamsa alijiuliza kabla ya kufungua ujumbe huo
wenye meseji kumi, huku meseji inayo onekana
kati ya kumi inamuuliza kwa herufi kubwa ‘WEWE
NDIO SHAMSA EDDY?’
Ikamlazimu Shamsa kuweza kuufungua ujumbe
huo na kukutana na mlolongo mkubwa wa picha
ambazo hazionekani vizuri hadi azifungue,
akafanya hivyo. Picha ya kwanza ikamstua na
kumfanya mapigo ya moyo kuzidi kumuenda kasi,
akajaribu kusimama ila nguvu za miguu
zikamuishia na kuanguka chini, akapoteza fahamu
ENDELEA
Kajol anafika sehemu alipo muacha Shamsa akiwa
na madaktari wawili, wanamkuta Shamsa akiwa
chini huku mkononi mwake akiwa ameishika simu
yake. Kwa haraka madaktaari wanamuwahi na
kuanza kumpa huduma ya kwanza. Kajol
anaichukua simu ya Shamsa, anashindwa
kuifungua kutokana na namba za siri zilizopo
kwenye simu hiyo.
“Tunahitaji msaada wa gari lawagonjwa”
Daktari mmoja alizungumza na simu, ndani ya
dakika tano gari moja ya wagonjwa ikafika katiika
sehemu walipo. Wakamuingiza Shamsa ndani ya
gari na kumuwahisha hospitalini.
***
Mafumba ya maji aliyo kunywa mzee Godwin
yakazidi kuufanya mwili wake kuishiwa na nguvu
na kujikuta akiishiwa na pumzi na kupoteza
fahamu. Mwili wa mzee Godwin ukaanza kuelea juu
ya maji. Giza likazidi kuenea juu ya anga huku
kukiwa na hali kubwa ya mawingu ya mvua,
ikiashiria kwamba ni ni muda wowote mvua
inaweza kunyesha. Akiwa anaendelea kuelea juu ya
maji ya bahari, radi na upepo mkali vikaanza
kupiga baharini, vitone vidogo vidogo vya mvua
vikaanza kunyesha. Hali iliyo wafanya baadhi ya
wavuvi wadogo wadogo kuanza kuzitoa boti zao
kwenye bahari kwani hali ya hewa tayari imesha
anza kuchafuka na kuwa mbaya. Bwana Tukuyu,
akiwa na wasaidizi wake wanne, wakapita na boti
yao inayo tumia mashine mbili, karibu na ulipo
mwili wa mzee Godwin
“Jamani yule si mtu?”
Mzee huyo aliwauliza vijana wake, huku
akipunguza mwendo kasi wa boti yake hiyo
ambayo kwa siku ya leo amefanikiwa kuvua
samaki kiasi.
“Ndio mzee, alafu anaoenekana kama amezimia”
“Tukampe msaada”
Taratibu akaisogeza boti yake hadi sehemu alipo
lala mzee Godwin, vijana wake wawili ambao ni
mahiri sana katilka kuogelea wakajitosa ndani ya
maji kisha wakasaidiana na wezao walio ndani ya
boti, wakamuingiza mzee Godwin ndani ya boti
hiyo, jambo lililo mfanya mzee Tukuyu kustuka
kidogo, ila akajikaza vijana wake hao wasiweze
kustukia kitu chochote. Wakaanza kumminya mzee
Godwin tumboni ili kuweza kumtapisha maji aliyo
kunywa. Zoezi halikuwa gumu la kumtapisha mzee
Godwin, baada ya muda mzee Godwin fahamu zake
zikamrudia, na kukurupuka kwa haraka.
“Nipo wapi hapa?”
Mzee Godwin aliuliza huku alkiyafumbua huku
akitazama kila mtu aliye mzunguka
“Upo mikono salama”
Mzee Tukuyu alizunumza huku akimtazama Mzee
Godwin jinsi anavyo babaika, kijana mmoja
akamletea mzee Godwin kikombe cha kahawa ya
moto ili kuweza kumuweka sawa.
“Kunywa upate nguvu kidogo”
Mzee Tukuyu alizungumza huku akimtazama Mzee
Godwin aliye baki ameshika kikombe cha kahawa
huku akisita sita kuweza kukinywa.
Mzee Godwin akaanza kunywa taratibu kahawa
hiyo huku akiendelea kuvuta kumbukumbu ni kitu
gani kilicho weza kumtokea, kitu cha mwisho
alicho weza kukumbuka ni pale kidau chake kilivyo
weza kupinduliwa na mawimbo mazito. Hapakuwa
na mazungumzo yoyote hadi wakafika ufukweni
mwa bahari, Mzee Tukuyu akaondoka na Mzee
Godwin na kuelekea nyumbani kwake ambao ni
kwenye moja ya kijiji kijulikanacho Pande kilichopo
mkoani Tanga.
“Jisikie huru mzee mwenzangu, hapa ndio
nyumbani kwangu”
“Asante sana”
“Sijui unanikumbuka?”
Mzee Gowin akamtazama kwa muda mzee Tukuyu,
kisha kwa mbali akaanza kuhisi kwamba huyu mtu
anamfahamu.
“Ndugu yako Tukuyu hapa, unakumbuka kipindi
unaingia jeshini mimi ndio niliekupokea kipindi kile
ulikuwa bado kijana mdogo sana”
“Ahaaaaa, za masiku ndugu yangu?”
Mzee Godwin alizungumza huku akiwa na furaha
kubwa kwani anamkumbuka vizuri mzee Tukuyu, ni
moja ya mwanajeshi aliye mtangulia mwaka mmoja
katika kazi. Kipindi ambacho mzee Godwin
anajiunga na jeshi, Mzee Tukuyu alikuwa ni
miongoni mwa watu wake wakaribu sana, ila
walikuja kupotezana kipindi Mzee Godwin alipo
kwenda masoni nchini Cuba, baada ya kurudi Mzee
Godwin akapandishwa cheo na kuhamishwa katika
kambi waliyo kuwepo. Usiku mzima ukawa ni
usiku wa wao kukumbushana mambo mbalimbali
yaliyo weza kutokea kwenye ujana wao huku mzee
Godwin akimsimulia rafiki yake huyo mkasa mzima
wa maisha yake tangu walipo achana.
***
Shamsa baada ya kupaata nafuu, akakuta pembeni
yake kukiwa na mzee mefu mweusi pamoja na
rafiki yake Kajol.
“Vipi Shamsa?”
“Junio”
Ikawa ni sentesi ya kwanza ya Shamsa
kuzungumza, mzee huyo akamtuliza kwanza ili
aweze kuzungumza kilicho mleta hapo hospitalini
“Mimi ninaitawa Paul Lukanyangwa, ni balozi wa
Tanzania hapa nchini Tanzania, nimeagizwa nije
kukupa uangalizi kwa ajili ya kwenda nchini
Tanzania”
“Twenda hata sasa hivi?”
“Kwa sasa hivi ni ngumu hadi upate ruhusa ya
daktari”
“Kajol kamuuite dokta mwambie kwamba mimi
nipo salama tu”
Kajol akafanya kama rafiki yake alivyo mtaka,
baada ya muda akarejea akiwa na daktari ambaye
alianza kumchunguza na kugundua kwamba yupo
salama. Baada ya kurithika kwa vipimo daktari
akampa ruhusa Shamsa ya kuweza kutoka
hospitalini, wakaondoka na moja kwa moja
wakaeleka makao makuu ya ubalozi wa Tanzania.
“Nahitaji kwenda na rafiki yangu?”
“Ila tiketi ni moja iliyo andaliwa kwa ajili yako”
“Nahitaji kwenda na Kajol”
Shamsa alizungumza huku machozi yakimwagika,
Kajol akawa na kazi ya kumbembeleza rafiki yake
huyo aliye fiwa na mdogo wake. Utaraibu wa
kumkatia tiketi Kajol ukafanikiwa kufanyika, majira
ya saa nne usiku wakaondoka na ndege ya shirika
la India. Njia nzima Shamsa akwa anaomba
kuweza kufika salama ili kuweza kujua ni kitu gani
ambacho kinaendelea kwa Junio .
***
Siku mbili zikakatika pasipo Eddy kuweza
kuzinduka baada ya kupoteza fahamu, madaktari
na manesi wakawa na kazi ya kuweza kuyaokoa
maisha ya waziri Eddy aliye pata mstuko baada ya
kushuhudia mwili wa mama pamoja na mke wake
wakiwa wamefariki. Kilio kikazidi kuongezeka kwa
Shamsa ambaye muda wote hakuhitaji kukaa mbali
na Eddy, aliye mkuta hospitalini mara baada ya
kushuka kwenye ndege.
Shamsa akiwa amejilaza pembeni ya kitanda huku
akiwa amekaa kwenye kiti, akastushwa na kitu
kilicho mshika kwenye mkono wake alio uweka
kwenye kifua cha Eddy. Akafumbua macho yake
taratibu na kumkuta Eddy akiwa anachezesha
chezesha mkono wake ulio mshika.
“Eddy Eddy”
Shamsa aliita huku akimtazama Eddy usoni aliye
yafumba macho yake. Eddy akazidi kuutingisha
mkono wake, kama mtu anaye zidi kujitahidi
kutoka sehemu fulani, iliyo yahatari sana. Shamsa
akautoa mkono wake kwa nguvu kwenye kiganja
cha Eddy, akasimama haraka na katoka ndani ya
chumba na kwenda kumita daktari.
Madaktari wakaingia ndani ya chumba walipo
mlaza Eddy, wakamkuta hali yake ikiwa ni ileile ya
kurusha mkono wake mmoja.
“Baba anakufaa…….?”
Shamsa aliuliza huku machozi yakimwagika usoni
mwake
“Hapana, nesi mtoe binti nje”
Nesi mmoja akamshika mkono Shamsa na kutmoa
nje ya chumba hicho na kumkabidhi kwa askari
wanao endelea kulilinda eneo hilo. Madaktari
wakendelea kufanya juhudi zao zote za
kuhakikisha wanayaokoa maisha ya waziri Eddy,
ambaye mwili wake wote ulianza kutetemeka kwa
nguvu hadi kupelekea smashine ya kupumulia
waliyo muwekea puani kuweza kuanguka chini.
“Itabadi tumchome sindano ya usingizi”
Daktari mmoja alishauri
“Naona si nzuri kwani mishipa yake imekakamaa,
hii inaweza kupelekea umauti wake”
Ikawa ni kazi ya madaktari kuweza kuendelea
kuminyana na waziri Eddy, ili asiendelee kuruka
ruka katika kitanda hicho. Kilicho zidi kuwastua
zaidi ni jinsi ulimi wake alivyo utoa kwa nje huku
ukiambatana na mapovu mengi. Kila daktari
alijikuta akiwa amechanganyikiwa kwa hali ya
waziri Eddy, kila walicho jaribu kukifanya
hakikuweza kuleta matumaini yoyote kwa mgonjwa
wao.
***
Habari ya hali kuwa mbaya ya waziri Eddy,
ikamfikia Raisi Praygod Makuya, pamoja na mke
wake Rahab
“Inabidi twende hospitali mume wangu”
“Sawa, ila nina kikao kimoja hapa, au fanya hivi
wewe tangulia kisha mimi nitakuja”
“Sawa”
Raisi Praygod akatoka katika chumbani kwake na
kuelekea moja kwa moja kwenye ofisi yake,
ambapo amejiandaa kuweza kukutana na balozi wa
Ujerumani kuweza kujadiliana na mambo ya
kiuchumi. Rahaba hakuona haja ya kuendelea
kulala kitandani, akajiandaa haraka haraka, alipo
hakikisha kwamba yupo salama. Akatoka ndani ya
chumba
“Madam leo hupati kifungua kinywa?”
Mlinzi wake wa kike alimuuliza mara baada ya
kuona wanaelekea nje na si kwenye chumba cha
yeye kupata kifungua kinywa
“Hapana tunaelekea ocean road hospital”
“Sawa madam, gari zipo tayari”
“Samson yupo wapi?”
“Yupo na muheshimiwa anajukumu la kumlinda”
“Mmmmm sawa”
Rahab akaingia ndani ya gari lake, ambalo
hulitumia kama mke wa raisi. Taratibu wakatoka
ndani ya ikulu, safari ya kuelekea hospitalini alipo
lazwa waziri wa ulinzi ikaanza. Mawazo taratibu
yakaanza kutawala kichwani mwa Rahab, kila alivyo
jaribu kuvuta hisia zake juu ya Eddy, akaona jinsi
anavyo teseka.
“Mungu wangu”
Alijikuta akizungumza kwa sauti kubwa hadi mlinzi
wake akamgeukia na kumshangaa
“Kuna tatizo lolote Madam?”
“Hapana”
Wakafika hospitalini, moja kwa moja wakaelekea
katika ya wagonjwa mahututi alipo lazwa waziri
Eddy
“Madam heshima kwako”
Askari waliopo katika eneo hilo walimpa heshima
Rahab, naye akawasalimia, macho ya Rahab
yakamtazama sana Shamsa aliye kaa pembeni ya
chumba hicho, huku akimwagikwa na machozi
mengi. Taratibu akamsogelea Shamsa na
kuchuchumaa taratibu
“Binti nyamaza ehee”
Rahaba alizungumza kwa sauti ya upole, kwa
kutumia kitambaa chake alicho kishika akamfuta
Shamsa machozi yanayo mwagika. Shamsa kwa
uchungu na maumivu makali ndani ya moyo wake
akamkumbia Rahab kwa nguvu na kuendelea kulia
sana. Kila aliye weza kumuona Shamsa aliweza
kulengwa lengwa na machozi, kwani kulia kwake
kunaashiria kwamba ana hali ngumu sana ya
maumivu anayo kutana nayo kwenye maisha yake.
“Shiiii….. dady atapona sawa”
Rahab aliendelea kumbembeleza Shamsa, huku na
yeye machozi yakimwagika. Wakiwa
wamekumbatiana mlango ukafunguliwa, akatoka
daktari akiwa katika sura iliyo jaa majonzi mengi,
Rahaba baada ya kuligundua hilo kwa haraka
akasimama na kumtazama daktari huyo usoni.
“Madam…..”
Daktari huyo alijikuta akimuita Rahab, na kuishia
katikati mara baada ya kumtazama Shamsa aliye
simama pembeni yake. Daktari akabaki kimya
akiwa katika hali ya kunto kufahamu asememe nini
mbele ya mke wa raisi. Akaingiza mkono wake
kwenye mfuko wa koti, akatoa simu yake na
kuiwasha. Alipo hakikisha imewaka, akaingia
upande wa meseji na kuandika maneno mafupi
kisha akamkabidhi Rahab. Rahab kabla hata
hayaisoma akastukia akipokonywa simu na
Shamsa, hakuamini alicho kiona kimeandikwa
kwenye simu hiyo kwa herufi kubwa
(MUHESHIMIWA AMETUTOKA)
Taratibu Shamsa akaiachia simu hiyo, huku miguu
ikimlegea na kujikuta akianza kwenda chini, kabla
hajafika sakafuni Rahab, akamdaka.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 15 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (15)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Daktari huyo alijikuta akimuita Rahab, na kuishia
katikati mara baada ya kumtazama Shamsa aliye
simama pembeni yake. Daktari akabaki kimya
akiwa katika hali ya kunto kufahamu asememe nini
mbele ya mke wa raisi. Akaingiza mkono wake
kwenye mfuko wa koti, akatoa simu yake na
kuiwasha. Alipo hakikisha imewaka, akaingia
upande wa meseji na kuandika maneno mafupi
kisha akamkabidhi Rahab. Rahab kabla hata
hayaisoma akastukia akipokonywa simu na
Shamsa, hakuamini alicho kiona kimeandikwa
kwenye simu hiyo kwa herufi kubwa
(MUHESHIMIWA AMETUTOKA)
Taratibu Shamsa akaiachia simu hiyo, huku miguu
ikimlegea na kujikuta akianza kwenda chini, kabla
hajafika sakafuni Rahab, akamdaka.
ENDELEA
“Mpelekeni wodini”
Rahab aliwaamuru askari waliopo katika eneo hilo,
wakambeba Shamsa na kumpeleka kwenye moja
ya wodi kwa ajili ya kupumzishwa. Rahab akaingia
kwenye chumba alicho lazwa Eddy, akawakuta
madaktari wakiwa wamemfunika shuka,
Ukimya mwingi ukatawala ndani ya chumba hicho,
kila aliye kuweomo ndani ya chumba, huzuni
ilimtawala katika moyo wake.
‘EDDY, EDDY’
Rahab aliita kimoyo moyo, huku akiwa
ameyafumba macho yake.
‘EDDY EDYYY EDDYYY’
Rahab alizidi kuita kwa hisia kubwa pasipo mtu
yoyote kuweza kuhisi kitu chochote, jinsi alivyo
zidi kumuita Eddy, kuizuia roho yake isiweze
kwenda mbali na ulimwengu huu, ndivyo jinsi
nguvu za mwili wake zilivyo zidi kumuishia,
akazidi kumita hadi damu za pua zikaanza
kumtoka. Gafla Eddy akazinduka kutoka katika
usingizi wa kifo na kukaa kitako kitandani, jambo
lililo wastua madaktari wote, wengine nusura
wapige ukelele. Taratibu rahaba akaanguka chini,
akiwa amechoka kwani ni kwakiasi kikubwa
ametumia nguvu nyingi katika kumpigania Eddy.
“Madam Madam”
Nesi mmoja alimuwahi kumuita Rahab baada ya
kumkuta akiwa amekaa chini, huku damu za puani
zikiwa zinamwagika.
“Nipo sawa”
Rahab alizungumza huku taratibu akinyanyuka,
macho yake yote alimtazama Eddy, jinsi anavyo
endelea kuhema kitandani. Eddy akamtazama
Rahab, wote wakajikuta wakitabasamu kwa pamoja.
***
“Sasa ni nini mpango wako?”
Mzee Tukuyu alimuuliza Mzee Godwin baada ya
kumaliza kumsimulia historia nzima ya maisha
yake.
“Nahitaji kuchukua kiti cha madaraka katika hii
nchi?”
“Mmmmmm……. Sasa utajiunga na chama gani
cha siasa wakati tayari wewe ni muhalifu?”
“Si kwakutumia siasa, ila ni kwakutumia mtutu”
Bwana Tukuyu akastuka, akajikuta wasiwasi wake
ukistukiwa na Mzee Godwin.
“Sa…sa kwa nini unahitaji kulifanya hilo wakati
nchi yetu ni nchi ya amani?”
“Amani ni hapo zamani, ila nahitaji kulipiza kisasi
kwa wale wote walio weza kuniharibia maisha
yangu”
“Godwin kumbuka hilo swala unalo lifanya ni swala
moja la hatari sana?”
“Nafahamu, ila itabdidi niweze kulifanya hilo”
Ukimwa ukatawala kati yao, akili ya bwana Tukuyu
ikazidi kuwa na mashaka na rafiki yake huyo. Akili
yake ikamtuma kwenda kuweza kuita askari ambao
wataweza kumkamata Mzee Godwin, na
kumsalimisha katika mikono ya serikali, kwani
mpango wake utakwenda kusababisha mauti kwa
wananchi wengi wasio na hatia.
“Mbona upo kimya unawaza nini ndugu yangu?”
“Aahaa… haapana bwana”
Mzee Tukuyu, alitabasamu huku taratibu
akisimama kuingia ndani ya nyumba yake. Mzee
Godwin akamtazama Mzee Tukuyu, kisha na yeye
akasimama na kuingia ndani, akamkuta mzee
Tukuyu akivaa shati pamoja na suruali.
“Unakwenda wapi?”
“Na….naa kwenda hapo mbele”
Kubabaika kwa mzee Tukuyu tayari kulisha mpa
alama ya hatari mzee Godwin, aliye anza kuikunja
ngumi yake ya mkono wa kushoto taratibu. Gafla
Mzee Godwin akachomoa mkanda wa suruli ya
Mzee Tukuyu, alio kuwa amening’inia kwenye
suruali yake.
“Una……..”
Mzee Godwin akamuwahi Mzee Tukuyu kwa
kuuzungusha mkanda kwenye shingo ya mzee
huyo, bila hata ya huruma akamkaba Mzee Tukuyu
hadi akapoteza maisha yake
“Pumbavu sana”
Mzee Godwin alizungumza kwa dharau kubwa,
kisha akaupandisha kitandani mwili wa mzee
Tukuyu, akamfunika vizuri kwa shuka kama mtu
aliye lala fofofo.
“Tutaonana katika maisha yajayo”
Mzee Godwin alizungumza huku akiyafunika macho
ya mzee Tukuyu. Mzee Godwin akatoka nje ya
nyumba hiyo na kusimama kila kona, kabla
hajapiga hatua hata moyo ya kuondoka, akamuona
kijana mmoja akija katika eneo hilo.
“Shikamoo”
“Marahabaa, nikusaidie nini?”
“Nahitaji kumuona mzee, kwani huu ni muda wa
kwenda kutega nyavu?”
“Ahaaa mzee kidogo anajisikia vibaya, ila kama
huto jali ninaweza kuichukua nafasi yake”
Kutokana kijana ni miongoni mwa vijana walio
weza kumuokoa mzee Godwin jana usiku, na
kiongozi wao mzee Tukuyu, alikiri kwamba huyo ni
rafiki yake wa muda mrefu, basi hakuona ni tatizo
kuweza kuongozana na Mzee Godwin kuelekea
maeneo ya baharini.
“Mzee anasumbuliwa na nini?”
“Homa ilimshika asubuhi, nimemtafutia dawa
amemeza”
“Ahaaa, ila vipi na wewe hali yako?”
Kijana huyo mwenye umri si chini ya miaka ishirini
alionekana kuwa mchangamfu sana kwa Mzee
Godwin tofauti sana na jinsi mzee Godwin alivyo
weza kuhisi
“Mim naendelea vizuri. Unaitwa nani?”
“Mimi?, mimi naitwa Thomas, ila watu wengi hapa
kijijini wamenizoea kuniita TOM”
“Una jina zuri”
“Asante na wewe je?”
“Mimi niite babu tu”
“Babu nani?”
“Babu kama babu”
Mzee Godwin hakuhitaji maswali zaidi kutoka kwa
Tom, wakafika maeoneo ya fukwe za bahari,
wakakuta vijana wengine wawili wakiwasuribi
kwenye boti inayomilikiwa na mzee Tukuyu
“Mzee leo anauwa hatokuja”
Tom aliwaambia wezake huku akikunya suruali
yake kwa ajili ya kuingia ndani ya maji, hapakuwa
na aliye kuwa na swali lolote, zaidi ya kumshangaa
mzee Godwin, anaye ambatana nao. Wakawasha
boti na kuondoka.
“Tunaelekea mpaka wapi?”
Mzee Godwin aliwauliza, wakiwa tayari wamefika
mbali sana na kutoka nchi kavu
“Hapa tunakwenda mbali sana, katikati huko ya
kina, ndipo tunapo tegaga nyavu”
“Kwahiyo huwa munazama ndani ya maji?”
“Ndio, tunazama ndani kabisa, huwa tunatumia
hiyo mirija ya kuhemea kuzama ndani ya maji”
Maswali yote aliyajibu Tom, aliye onekana
kumpenda sana mzee Godwin, pasipo kufahamu
kwamba ni moja kati ya watu magaidi wanao
isumbua nchi ya Tanzania, na pia ni mtu aliye
waulia mzee wao waliye mtegemea sana.
Wakafika hadi sehemu ambayo wanazoea kutega
nyavu, ili kuweza kupata samaki wengi sana,
Vijana wawili wakajiandaa, Tom naye akataka
kujiandaa ila mzee Godwin akamzuia kwa ishara
na Tom akatii pasipo kuelewa ni kwa nini mzee
Godwin amemzuia. Vijana hao wawili wakipemba,
wakajitosa ndani ya maji, huku wakionekana kuwa
ni hodari katika zadi hiyo, wakaipokea nyuvu
waliyo shushiwa na Tom pamoja na mzee Godwin,
kisha wakazama nayo ndani ya maji.
“Watachukua muda gani hadi kutoka?”
“Zaidi ya dakika kumi na tano, kutokana hawa ni
wazoefu sana”
“Ahaaa sawa tuachane na hayo. Nyumbani unaishi
na nani?’
“Peke yangu?”
“Wazazi wako?”
“Wazazi wangu walisha fariki dunia siku nyingi
sana, nimelelewa na majirani zangu wema, hadi
leo nimekuwa hivi”
“Una umri gani?”
“Miaka ishirini na moja”
Nzee Godwin alitingisha kichwa huku akitabasamu.
Tom akasimama kwenye boti hiyo na kuangalia
magharibi kwake.
“Babu unauona huu usawa huu?”
“Ndio”
“Kuna siku mzee Tukuyu aliniambia kwamba kuna
msitu, kuna hazina yake ya thamani ameiweka,
hata siku nikifa basi nikaichukue”
Maneno ya Toma yakamstua mzee Godwin na
kujikuta na yeye akisimama, akatazama sehemu
ambayo Tom anamuonyesha.
“Ni hazina gani hiyo?”
“Yeye aliniambia zipo kwenye msitu, upande huu,
ila ni vitu vya thamani sana”
“Unaonaje tukaenda kuvitazama?”
“Sasa hivi!!!?”
“Ndio”
“Kuna wezetu humu hatuwezi kuwaacha”
“Hao ni mahodari wa kuogelea, tunakwenda mara
moja kisha tunarudi”
Tom akamuangalia usoni mzee Godwin, kutokana
ni mzee aliye weza kutambulishwa na babu aliye
mchukulia kama ni baba yake, basi akaamua
kuufwata ushauri wa mzee Godwin. Wakawasha
boti hiyo inayo kwenda kwa kasi kutokana
namshine zake mbili kuwa na uwezo mkubwa
sana. Ikawachukua zaidi ya lisaaa moja kuweza
kufika kwenye moja ya msitu mkubwa, ulipo
pembezoni mwa bahari. Wakashuka na kuiweka
boti pembeni, kutokana kagiza kilisha anza kuingia,
Tom akachukua tochi kubwa ambayo huwa
wanaitumiaga sana kwenye maswala ya kuwavuta
samaki kipindi wakivua nyakati za giza.
“Ila aliniambia kwamba msitu huu una wanyama na
wadudu wabaya sana”
“Kwani hapa ni wapi?”
“Huu msitu, upo maeneo ya mkoa wa pwani”
“Pwani…..!!”
“Ndio, ukizunguka kivile utakuta mji wa pwani”
Tom alimuelekeza mzee Godwin kwa njia ya
baharini. Wakaanza kuingia kwenye msitu huo,
huku ujasiri wa Tom ukizidi kumvutia mzee
Godwin.
“Mbona hatufiki, alikuambia ni wapi?”
“Mbele kidogo aliniambia kuna miti mitano mirefu
sana, kisha chini kuna handaki lenye mfuniko ulio
wekewa jiwe kubwa juu yake”
“Ahaa sawa”
Wakazidi kutembea zaidi ya lisaa zima jingnine
hadi wakafanikiwa kufika katika sehemu ambayo,
Tom alielekweza na Mzee Tukuyu na kila alicho
elekezwa alikikuta katika eneo hilo.
“Hapa ndipo penyewe”
Tom alizungumza huku akishangaa shangaa eneo
hilo, wakalisukuma jiwe hilo kubwa, ambapo kweli
kwa chini wakakuta mfuniko wa chuma. Kutokana
Mzee Godwin ananguvu nyingi, aliweza kuufungua
mfuniko huo ulio jaa kutu. Wakakuta ngazi nyingi
zilizo jengwa kwa saruji zikielekea chini.
“Lete tochi”
Mzee Godwin akachukua tochi, akatangulia mbele
huku Tom akifwata kwa nyuma. Wakaingia ndani
ambapo katika kumulika mulika mzee Godwin
aliweza kuona swichi ukutani. Akaiminya na taa za
ndani zote zikawaka
“Waooooo……!!!”
“Tom alishangaa sana, kwani hakuamini kama
eneo hilo ni kubwa kiasi hicho na linapendaza sana
kwa kiasi kikubwa. Wakakuta baadhi ya computer
zikiwa katika eneo hilo, inavyo onekana kama kuna
watu walikuwa wanaishi hapo kipindi cha nyuma.
Tom akaanza kukagua chumba kimoja baada ya
kingine, chumba cha kwanza aliweza kukuta
kitanda pamoja na nguo za kike.
“Babu kuna nguo za kike huku”
Alimuita Mzee Godwin, aliye mfwata na
kuzishuhudia nguo hizo, wakaingia kwa pamoja
kwenye chumba cha pili na kukuta nguo nyingine
za kike. Wakaingia chumba cha tatu wakakuta
nguo za kike pamoja na bastola, ikiwa kitandani,
Tom akaichukua
“Hii ni bunduki……!!!”
Aliitazama huku akiishangaa sana kwani alisha
zoae kuiona silaha hiyo kwenye filamu za kizungu
za mapambano.
“Ndio ni bastola, hembu ilete”
Akamkabidhi mzee Godwin, aliye itazama vizuri na
kugundua ipo sawa, na magazine yake ina risasi
za kutosha, japo inaoenekana zimesha tumiwa.
Wakaingia kwenye chumba cha nne, wakakuta
nguo nyingi za kike zikiwa zimemwagwa kitandani,
wakaingia chumba cha tano na kukuta mabegi
mawili walipo yafungua wakakuta simu moja ya
thamini sana. Samsung Galaxy note two, pamoja
na nguo za kike.
“Ina maana walio kuwa wakiishi humu ni
wanawake?”
Tom alimuuliza mzee Godwin huku akishangaa
“Ina wezekana”
“Sasa ni kina nani hao, hadi waishi kwenye hili
handaki?”
“Mmmm kusema kweli safahamu”
Wakatoka na kuelekea kwenye chumba cha sita,
hapo ndipo wakajikuta wamebaki wameduwaa,
kwani chumba hicho, kina mlango wa chumba
ambao kufunguliwa kwake kunahitaji kuingizwa
namba za siri, ili ufunguke.
“Njoo huku”
Mzee Godwin alizungumza, wakaelekea kwenye
meza yenye computer sita, akaziwasha zote, kwa
bahati nzuri ziliwaka. Akashusha pumzi kidogo
akisubiria zimalize kuwaka, ila kilicho mshangaza
zaidi, computer zote zilihitaji namba za siri ili
kuwaka.
“Eheee”
“Nini tene babu?”
“Zinahiutaji namba za siri”
“Sasa tunazijulia wapi?”
“Hembu lete hiyo simu”
Tom akamkabidhi mzee Godwin simu, akaiwasha
kwa bahati nzuri ikawaka pasipo tatizo la aina
yoyote, huku ikiwa imebakiwa na kiasi kidogo cha
chaji.
“Simu nzuri hiyo”
Tom alizungumza huku akitabasamu sana, mzee
Godwin akaingia upande wa picha kuangalia kama
ataweza kubahatika kuona sura ya mmiliki wa simu
hiyo. Kwa bahati nzuri wakakuta picha nyingi sana,
moja ikiwaonyesha wasichana watano waklwa
pamoja. Sura hizo hazikuwa ngeni sana kwa Mzee
Godwin, kwani alisha weza kuziona sehemu, huku
sura moja akiwa anaitambua vizuri sana, kwani ni
mke wa raisi Praygod, bi Rahab. Mzee Godwin
akajikuta akimeza mate, huku akiwa
ameyatumbulia macho kwenye picha hiyo, kwani
Rahab anamfahamu sifa yake, ni miongoni mwa
watu walio weza kuvuruga mipango yake yeye
pamoja na makamu wa raisi, mwaka mmoja na
nusu ulio pita.
***
Vurugu na ubabe zinazidi kutawala ndani ya
gereza la Pentagon, ila wasichana watatu wanazidi
kujijengea umaarufu kwa uwezo wao mkubwa
wakuweza kuwaparanganyua, maadui zao ambao
walijitia vihere here katika kujaribu kupambana
nao. Makundi ya wasichana wababe yalizidi
kuongezeka siku hadi siku, hadi ikafikia hatua
ulinzi katika gereza hilo kwa upande wa wanawake
ukaongezwa mara dufu, ili kuzuia fujo zinazo tokea
kila siku.
“Unakwenda wapi?”
Fetty alimuuliza Anna aliye simama gafla
“Nakwenda kuoga”
“Kuoga, mida hii?”
“Ndio”
“Kuwa makini si unajua tuna windwa humu ndani?”
“Usijali”
Anna akajifuta amjani majani kwenye nguo yake,
sehemu ya makalio, kisha taratibu akaondoka
katika eneo hilo la wafungwa kufanyia mazoezi.
Moja kwa moja akaelekea kwenye maeneo ya bafu,
kwa bahati mbaya akakuta kikundi cha wasichana
wengine wenye asili ya Marekani wakimpiga binti
mmoja wakizungu. Anaa akataka kupita, ila kila
alivyo muangalia binti huyo anavyo chezea kipigo,
roho ikamuuma, akatizama idadi yao wapo
wangapi, kwa haraka haraka akagundua wapo sita.
‘Ninawamudu’
Ana alizungumza kimoyo moyo, huku akipiga hatua
kwenda kwenye eneo hilo
“Heiii nyinyi muacheni huyo”
Anna alizungumza kwa lugha ya kimarekani, huku
akiwatazama wasichana hao walio simamisha zoezi
hilo na kumtazama vizuri.
“Wewe malaya unasemaje?”
Kiongozi wao alizungumza huku akichomoa kisu
chake na kuanza kupiga hatua kusonga mbele
akimfwata Anaa katika sehemu alipo simama.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 16 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (16)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Ana alizungumza kimoyo moyo, huku akipiga hatua
kwenda kwenye eneo hilo
“Heiii nyinyi muacheni huyo”
Anna alizungumza kwa lugha ya kimarekani, huku
akiwatazama wasichana hao walio simamisha zoezi
hilo na kumtazama vizuri.
“Wewe malaya unasemaje?”
Kiongozi wao alizungumza huku akichomoa kisu
chake na kuanza kupiga hatua kusonga mbele
akimfwata Anaa katika sehemu alipo simama.
ENDELEA
Kitendo cha mkuu wao, kumkaribia Anna, ikawa ni
kama kosa la jinahi kwake, kwani akakukutana na
teke zito la shingo, lililo muangusha chini, huku
kisu chake kikiangukia pembeni. Anaa baada ya
kufanya shambulizi hilo akajiweka sawa suruali
yake na kukunja ngumi tayari kwa kupambana.
Walipo muona kiongozi wao amelala chini,
kunyanyua anajishauri, hapakuwa na aliye weza
kufanya chochote zaidi ya kumnyanyua kiongozi
wao na kuondoka katika eneo hilo la sivyo nao
wanaweza kukumbana na dhahama aliyo ipata
kiongozi wao.
“Vipi umeumia?”
Anna alimuuliza binti huyo, anaye onekana kuwa
na mwili mdogo mdogo na nimnyonge sana
“Ndio”
Akamsaidia kumnyanya, akampeleka bafunia,
kwenda kumfuta damu zinazo mwagika mdomoni,
kwani kipigo alicho kutana nacho ni kikali sana.
“Asante dada”
Binti huyo alizungumza huku akimtazama Anna
machoni.
“Usijali”
“Unaitwa nani?”
Binti huyo alimuuliza Anna huku akiwa
ametabasamu.
“Jina langu kwa sasa si lamuhimu sana
kulifahamu”
Anna alizungumza huku akivua nguo zake,
akasimama kwenye bomba la mvua, taratibu
akaanza kuoga, muda wote binti huyo akiendelea
kumtazama Anna umbo lake zuri ila limejaa
mikwaruzo mingi sana ya mateso ambayo
anaonekana kuweza kuyapa miaka ya nyuma.
***
“Ni kina nani hawa wadada?”
Tom alimuuliza Mzee Godwin huku wakiendelea
kuwatazama Rahab na wezake kwenye picha katika
simu hiyo.
“Siwafahamu”
Mzee Godwin alizungumza huku akiendelea
kutazama tazama picha nyingine, akatoka upande
wa picha na kuingia upande wa mesiji ambapo
akakutana na meseji moja iliyo tumwa na doktar
William. Akaifungua na kukuta maelezo.
(Namba ya siri ya computer zote ni HHrJ93,
Namba ya siri ya chumba ni HHRj94)
Mzee Godwin akatabasamu, huku akiitazama
meseji hiyo, kwa haraka akaiingiza neno la siri
alilo lisoma, nayo computer hiyo ikafunguka.
“Bingoo”
Mzee Godwin alifuraha sana kwa kufanikiwa kwa
tukio hilo, akasimama na kwenda kwenye chumba
walicho shindwa kufungua, akaingiza namba za
chumba hicho, ambapo mlango wake ukafunguka.
Wote wawili wakabaki wakiwa wamesimama
wameduwaa, kitu wanacho kiona mbele yao.
Vibunda vingi vya pesa vilivyo pangiliwa vizuri
kwenye vimbao vidogo vilivyo jengewa ndani ya
chumba hicho, kilicho kaa kama duka dogo,
vikawafanya wote wasimama kwa muda kisha
Mzee Godwin akaanza kuingia ndani na
kuhakikisha kwamba ni pesa wanayo iona au yupo
kwenye ndoto. Vibunda vya pesa za kitanzania
pamoja na dola ya kimarekani, viliweza kuwatoa
ufahamu mzee Godwin na Tom, kwani
wanashangilia na kuruka ruka kama watoto
wadogo, muda mwingine wakajikuta
wakikumbatiana na kuruka ruka sana.
“Tumesha kuwa matajirii”
Mzee Godwin alizungumza huku akizidi
kumkumbatia Tom, kila mmoja akajikuta
akimwagikwa na machozi ya furaha. Kwa upande
mmoja wa ukuta wa chumba hicho wakakuta
mlango mdogo ulio rudishiwa, Tom akausukuma
ukafunguka. Wakakuta bunduki nyingi zikiwa
zimepangwa vizuri pamoja na risasi nyingi zilizopo
kwenye viboksi vingi.
“Mmmmmmmm…….!!!!”
Mzee Godwin akamsogeza Tom pembeni, kisha
akaingia ndani ya chumba hicho, akaanza kukagua
bunduki hizo, akagundua kwamba ni mali ya jeshi
la Tanzania, na inavyo oenekana ziliibiwa kwa usiri
mkubwa katika moja wapo ya kambi za jeshi. Hapa
ndipo mzee Godwin akaanza kupata picha ya
wasichana alio weza kuwaona kwenye picha.
“Inabidi tufanya mpango wa kuchukua kila kitu
tuondoke hapa”
“Sasa babu tutakwenda wapi?”
“Tutajua pa kwenda, ila unaweza kuendesha gari?”
“Hapana”
Mzee Godwin akawaza kitu kichwani mwake haraka
haraka, kisha akachukua vibunda viwili vya dola
laki moja moja. Akaingia kwenye moja ya chumba
alipo ona moja ya koti jeusi, akaona litamfaa,
akalivaa, kwa bahati nzuri akakuta moja ya kofia,
akaivaa vizuri
“Hapo ninaonekanaje?”
“Umependeza sana babu”
“Basi ninahitaji kwenda Dar er salaam mara moja,
ninakuomba uningojee hapa”
“Unakwenda kufanya nini?”
“Utaona ila usitoke katika hili eneo sawa”
“Sawa babu”
Mzee Godwin akarudi kwenye chumba akachuku
kibunda kingine cha noti za shilingi elfu kumikumi,
akahakikisha bastola yake inasila za kutosha,
akachukua moja ya magazine ya akiba iliyo jaa
risasi, kisha akaondoka na kumuacha Tom peke
yake ndani ya handaki hilo. Akainaza safari kwa
miguu, akifwata muelekeo wa barabara iliyo jaa
majani mengi, na inavyo onekana hapo awali
ilikuwa ikitumika. Hadi inatimu majira ya saa kumi
na moja alfajiri tayari, akawa amefika katika
barabara ya mkoani, inayo tokea Dar kuelekea
mikoa ya Tanga na Arusha. Kwa jinsi alivyo vaa si
rahisi kwa mtu kuweza kumgundua mara moja.
Akaanza kusimamisha magari yanayo pita, ila
mengi hayakuweza kusimama katika eneo hilo la
porini, kwa bahati nzuri akamsimamisha
muendesha pikipiki mmoja, aliye weza kusimama.
“Kijana unaelekea wapi?”
“Chalinze”
“ Bei gani hadi hapo?”
“Nitakufanyia elfu ishirini”
“Sawa”
Mzee Godwin hakuhitaji kupoteza muda kwani
anafahamu ni kitu gani ambacho anakwenda
kukifanya Dar es Salaam, isitoshe jeshi la polisi
linamtafuta kwa udi na uvumba. Safari
ikawachukua takribani masaa mawili kuweza kufika
Chalinze pasipo kuweza kustukiwa na askari polisi.
Akamlipa muendesha pikipiki huyo kiasi cha pesa
walicho kubaliana. Akapanda basi la Abood linalo
toka mkoani Morogoro kuelekea Dar es Salaam.
Akiwa ndani ya gari, pembeni yake kuna kijana
binti mmoja, ameshikika gazeti lililo pambwa kwa
kichwa cha habari kilicho mstua sana.
‘PIGO WAZIRI MKUU MSTAAFU, MJUKUU WAKE NA
MKWE WAKE WAFARIJI DUNIA HOSPITALINI’
Mzee Godwin akaitaza vizuri picha ya mke wake,
pamoja na mjukuu wake kipindi cha enzi za uwahi
wapo. Maandishi madogo ya chini ya kichwa cha
habari hicho yakazidi kumuogopesha Mzee
Godwin.
(Mauajiya mama na mke wa waziri Eddy
yamefanywa na mume wa waziri mkuu mstaafu
general mstaafu GODWIN)
Mzee Godwin akaishusha kofia yak chini kidogo ili
kuificha sura yake, hakuhitaji binti huyo aweze
kuiona sura yake. Wakafanikiwa kufika ubungo
majira ya saa nne asubuhi, Mzee Godwin akashuka
huku moyoni mwake akiwa na hasira kubwa
pamoja na huzuni, kwani hakujua ni kwanini kesi
ya mauji ya mke wake ameweze kusukumiwa yeye.
“Ila wamenirahisisia kazi”
Mzee Godwin alizungumza huku akitoka kwenye
geti kuu la stendi ya basi ubungo.
***
Mipango ya mazishi ikaanza kufanywa na serikali
ya jamuhuri wa muungano wa Tanzania. Huzuni
kubwa ikazidi kutanda kwa ndugu jamaaa na
marafiki ambao wanamfahamu waziri Eddy, hata
baadhi ya wananchi walio tokea kumpenda waziri
Eddy, wakajikuta wakiwa katika simanzi kubwa
kwani kiongozi huyo ni muda mchache tangu
aingie madarakani amekubwa na tukio ambalo
hatoweza kulisahau kwenye maisha yake.
Ulinzi mkali na madhubuti ukandelea kuimarishwa
nyumbani kwa waziri Eddy, ambaye tayari alisha
toka hospitalini pamoja na Shamsa. Viongozi
wengi wakiserikali, kutoka baadhi ya nchi wakazidi
kufurika katika jumba la Eddy, kuhuzuria msiba
huo, ulio chukukuliwa uzito, mkubwa na serikali,
huku ikitolewa amri ya kumtafuta Mzee Godwin
popote ndani na nje ya Tanzania.
Picha za mzee Godwin zikaendelea kusambazwa
kwenye kila eneo la nchi ya Tanzania, hadi mitaani
picha zake ziliweza kubandikwa, huku kukiwa na
zawadi nono kwa yule atakaye fanikisha
kukamatwa kwake.
Hasiri dhidi yam zee Godwin ikazidi kujijenga
moyoni mwa Eddy, safari hii akazidi kujiapiza
moyoni mwake ni lazima aweze kumuua mzee
Godwin kwa mikono yake yeye mwenyewe. Kila
alipo tazama picha ya Junio, Phidaya pamoja ya
mama yake, Eddy machozi yakazidi kumwagika.
“Muheshimiwa kuna mgeni amekuja kukuona”
Mfanya kazi mmoja alimnong’oneza Eddy sikioni,
akanyanyuka kwenye kiti alicho kikalia,
akaongozana na mfanya kazi huyo, wanao
shuhulikia maswala ya msiba kwa ujumla,
akampeleka ndani sebleni.
Eddy akamkuta Rahab akiwa amekaa kwenye sofa,
huku amevalia mavazi meusi pamoja na miwani
nyeusi.
Rahab alipo muona Eddy akanyanyuka na
kumkumbatia kwa nguvu. Eddy akashindwa
kuyazuia machozi yake na kujikuta akilia kama
mtoto mdogo.
“Naomba mutupishe”
Rahab aliwaambia walinzi wake, wakatoka nje na
kubaki wao wawili sebleni, wakakaa kwenye
masofa.
“Eddy pole kwa kila jambo, lililo teokea kwani ni
kazi ya mola haina makosa”
“Asante madam”
“Natambua ya kwamba una uchungu mkubwa sana
moyoni mwako kwani kuondokewa na mama, mke
pamoja na mtoto ni jambo ambalo ni zito sana.”
“Wewe ni mwanaume, miongoni mwa watu ambao
ninawaona watakuja kuwa ni watetezi wa taifa hili
mmoja wapo ni wewe”
“Kivipi sijakuelewa muheshimiwa”
Eddy alizungumza kwa sauti ya upole huku
akimatazama Rahab machoni mwake.
“Usijali utakuja kufahamu tu. Ila nimetangulia mimi
kufika hapa kutoa rambi rambi zangu, ila raisi
atakuja kesho, leo kidogo mambo yameingiliana”
“Sawa mama”
Kikaletwa kitabu cha kuandika rambi rambi za
wageni walio weza kuhudhuria katika eneo hilo,
Rahaba akaandika mchango wake kama mke wa
raisi.
***
Mzee Godwin moja kwa moja akaelekea kwenye
hospitali ya mhimbili, kuoanana na mmoja wa
marafiki zake ambao ni madaktari bingwa wa
kutengeneza sura bandia. Akajumuika na wananchi
wanao kwenda kuwaona ndugu zao, kuingia
kwenye geti la hospitali hiyo pasipo mtu kuweza
kumstukia. Moja kwa moja akaongoza kwenye
gorofa la maabara, akaanza kupandisha ngazi
taratibu kuelekea juu. Akiwa gorofa ya kwanza
kwenda gorofa ya pili, akakutana na askari wawili
wakishiuka chini, akaishusha kofia yake chini
kidogo, akapisha na askari hao wakimtazama.
“Ngoja kwanza”
Askari mmoja alizungumza baada ya kushuka
ngazi sita kwenda chini, akatoa picha iliyopo
mfukoni mwake.
“Ndio huyu tunaye mtafuta”
Askari mmoja alizungumza na kuanza kupandisha
kwenda ngazi za juu huku akikimbia, kwa bahati
nzuri akafanikiwa kumuona mzee Godwin
akitembea kwenye moja ya kordo.
“Simama polisii”
Askari huyo alizungumza huku bunduki yake akiwa
amemnyooshea mzee Godwin kwa nyuma.
ITAENDELEA
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 17 YA SIMUHILI HII.
 
Back
Top Bottom