Sophia Simba akejeli kampeni ya TAMWA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sophia Simba akejeli kampeni ya TAMWA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Nov 20, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  19th November 2009


  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Sophia Simba.  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Sophia Simba, amedai kuwa baadhi ya vyama vya upinzani vimekuwa vikitumia baadhi ya vyombo vya habari au taasisi zisizo za kiserikali kama vile Tamwa na tangazo lao la 'Sidanganyiki' ili kukichafua chama hicho na serikali yake ili kionekane hakijafanya kitu.
  Alitoa kauli hiyo juzi mjini hapa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza Kuu la UWT na mafunzo kwa viongozi na wajumbe wa baraza hilo.
  Simba ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), alidai kuwa baadhi ya vyama vya upinzani vinapokea fedha kutoka nje kwa lengo hilo.
  Alitolea mfano tangazo linalotolewa katika vyombo vya habari na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) la 'Sidanganyiki' kwamba linatangazwa kwa ufadhili wa fedha nyingi kutoka nje.
  Hata hivyo, hakueleza uhusiano uliopo kati ya Tamwa na vyama vya upinzani.
  Tamwa imekuwa ikitumia tangazo hilo kama kampeni ya kuwalinda watoto wa kike dhidi ya vishawishi vya ngono. Kadhalika ilitumia tangazo kama hilo kuwahamasisha Watanzania kuwa macho kwa kuchagua
  Waziri huyo wa Utawala Bora alihoji kuwa wapinzani wanaotaka kukiangusha chama chake kwa kupeleka vijisenti siku zote walikuwa wapi.
  “Wapinzani hawana cha kuonyesha, wamefanya nini ila CCM wana uwezo wa kuonyesha wamefanya nini katika utekelezaji wa ilani yetu ya chama,” alisema Sophia, ambaye hivi karibuni anadaiwa kutoa kauli za matusi wakati wabunge wa CCM walipokutana na Kamati ya Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, kueleza kiini cha mpasuko ndani ya Bunge.
  “Kipindi cha nyuma hapakuwepo shule nyingi na zilizokuwepo zilikuwa mbali lakini sasa zipo nyingi mpaka wanafunzi wanajazana kwenye magari,” alisema na kuwataka wanawake wa chama tawala kuwa mstari wa mbele kujibu mapigo ya wapinzani.
  Alisema kuwa wanawake hao wawajibu wapinzani kwa kuonyesha ilani ya uchaguzi ya CCM kuwa imetekelezwa. Aidha, Sophia Simba alimtetea Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, kuwa anafanyakazi kwa juhudi licha ya kuwepo maneno maneno ya wivu dhidi yake.
  “Kikao cha UWT kinampongeza kwa kazi nzuri, wale wanaomsema vibaya washindwe na walegee,” alisema Waziri Sophia.  CHANZO: NIPASHE


  0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni
   
 2. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Hiyo picha Mhe, Sophia amependeza, katoka bombaaaaa!!
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo kudanganyika ndio mwendo?
  Nilidhani angewaunga mkono TAMWA KATIKA KUWALINDA WATOTO WASIRUBUNIWE ILI WAENDELEE KUJAZA HIZO SHULE!
  SITAKI KUAMINI KUWA HIKI NDICHO HUYU FORMER WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO AMEKISEMA!
   
 4. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  She looks like a bloodsucking vampire, with some of the blood still on her lips.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,698
  Trophy Points: 280
  Huyu mama kama alivyo boss wake ni mzigo mkubwa kwa Watanzania, lakini ndiyo hivyo tena hakuna wa kumshikisha adabu kwa kuropoka kwake.
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Labda awadanganye watoto, maana yake nini kujidai kuwa watoto wanakwenda shule wakati hata shuleni kwenye Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam anataka waje na madawati yao? watoto ambao karibu wote wanaishia shule ya msingi, wanaofaulu hata hawafiki asilimia 50.

  Is she serious kusema Makamba anafanya kazi nzuri? ipi? kazi ipi hiyo unayoweza kuwambia mtu na akili zake timamu kuwa ni kazi nzuri? Chama kina msukosuko na kinaelekea kupasuka.
   
 7. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Watu kwa kuponda hamjambo!!!!
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Nov 20, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Her complexion is getting more lighter!!! Chemistry or Physics in action?

  Nasikia Tanzania siku hizi hata makalio yanaweza kukuzwa kuwa wowowo.

  Huyu mama Simba ni bure kabisa kama tulivyo watanzania wengi; ni reflection yetu wenyewe. Kwa hiyo tusikimbie kivuli chetu.
   
 9. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Uchungu wa mwana aujuaye mzazi hasa mama.Pengine yeye hana watoto ambao wanaweza danganywa na fataki!
   
 10. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  haya mambo mara nyingine huwa yanachanganya sana! Pengine sisi wadanganyika hatujui tunachostahili...hiki ndicho nakiona kwa dada huyu. Fedha za wafadhili zikitumika kumlinda mtoto wa kike asidanganyike inakuwa taabu kwa vipi tena? Soffy anapaswa kuacha kukimbia kivuli chake...Hivi rafiki yako akikwambia hapo kwenye jino lako kuna mchicha umenasa hebu utoe utamjia juu? Kwani si ulikula mwenyewe anakusaidia tu kuhakikisha unakuwa safi! Any way tunavuna tulichopanda.
   
 11. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Mtoto wake wa kike alishaharibiwa siku nyingi amekuwa timing bomb.....sitaki kwenda ndani zaidi kwenye familia yake.....ila hajui analosema...tumuache tu..muda wake ukifika tutamshitaki kwa kiburi na ufedhuli wake.....anatumwa huyu na ujinga wake huwahapimi....yeye analichukua ka kuropoka
   
 12. k

  kweche New Member

  #12
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 29, 2008
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba wasomaji muelewe. Kwa uelewa wangu ni kuwa tangazo la SIDANGANYIKI linalomhusu yule binti mwanafunzi limetolewa na Haki Elimu. kama nimekosea mtanisahihisha. lakini hiyo siyo tatizo.

  kwa mtazamo wangu ni kuwa huyu SOFIA SIMBA tangazo analolilalamikia ni lile ambalo lilitawala sana kwenye TV wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa ambalo lilikuwa linawatahadhalisha wananchi kutochagua viongozi wapenda rushwa na wanaotoa ahadi hewa. nadhani tangazo hilo la TAMWA ndilo kiini cha hoja ya simba. Lakini wasomaji lazima muelewe kuwa huyu SOFIA SIMBA ni kibaraka na msemaji wa MAFISADI. si mnajua wao wenyewe walijaribu kusema wakashindwa. sasa wameamua kumtumia huyu mama. cha kushangaza ni kuwa yeye kwa kuwa ni waziri wa utawala bora anawakatisha tamaa TAMWA kwa kuwazushia mambo mengi eti wamepewa pesa na wafadhili kuichafua serikali. mie nafikiri angewaunga mkono badala ya kuwakatisha tamaa.

  simba atambue kuwa hata hao TAMWA ni wananchi wazalendo na wanaitakia mema Tanzania. wengi wamo wanafanya kazi kwenye vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali. asifikirie kuwa ni yeye tu mwenye uchungu na nchi hii. yeye ameikuta Tanzania ikiwa na neema tele ambazo wengi wamezipigania. ni bora akaamua kukaa kimya kuliko kuropoka.

  watanzania, kuendelea kujadili kuhusu Sofia Simba ni kupoteza muda. kama wengi walivyosema huyu mama ni vyema akapimwa hata uwezo wake wa kufikiri. kwani licha ya kupewa wizara nyeti yenye wasomi tele lakini anapotoka. nadhani anafuata mkondo wa baba yake ambaye hasikilizi ushauri wa wataalam wake.

  Rais mstaafu BENJAMIN MKAPA hivi karibuni amenukuliwa akisema, "huwezi kuwazuia watu kusikia bali unaweza kujizuia kusema". mie namshauri simba kuwa ikiwa anaitakia nchi hii mema ni vyema akajizuia kusema kuliko kuwachanganya wananchi
   
 13. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Sasa hapo nani ni FATAKI.
   
 14. k

  kweche New Member

  #14
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 29, 2008
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo fataki ni viongozi wa CCM ambao wanataka kuwarubuni wananchi ili wawape kura huku wakijua kuwa watawageuka baada ya kuchaguliwa na hawajafanya chochote kwa awamu iliyopita. si unajua fataki anavyokuja na lugha laini ili apate anachokihitaji. mara ooooooooo nitakununulia gari, simu ya mkononi au nitakulipia karo ya shule. kuhusu tangazo la tamwa hata hivyo limetahadhalisha wananchi na wanasiasa mafataki bila kujali wametokea chama gani. ufataki tunaousema ni ule wa kisiasa na si wa mapenzi au ngono.
   
 15. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #15
  Nov 20, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sofia sofia mbona unatuvua nguo wanawake wenzio? Huoni aibu kila siku kuongea pumba hadharani? si ukae kimya tu hakuna atayejua kama wewe mtupu? ona kina migiro na tibaijuka walivyotubeba! NAMKUMBUKA HATA BIBI TITI MOHAMEDI! mmmh lakini wewe ! kweli unaonyesha taswira mpya ya kiongozi mwanamke wa tanzania. Ona umepewa majukumu kubwa kuliko uwezo wako! kwa kweli unatuangusha sana ...nami nahofia madudu unayoyafanya kama hayaathiri taswira ya uongozi ya wanawake nchini ukiwa kama mwenyekiti wa UWT. Yaani wee sofia wee NAJUUUUUUTA KUKUFAHAMU!  NANYI MTAIFAHAMU HIYO KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Nov 20, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  mimi nadhani anajivua mwenyewe
   
 17. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #17
  Nov 20, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Sofia Simba
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Nov 20, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Akili ni nywele na kila mtu ana zake mama simba za kwako ndo hizo
   
 19. M

  Mundu JF-Expert Member

  #19
  Nov 20, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hivi mahakama ya kimataifa ya makosa ya kiuhalifu haihusiki na watu wanaotoa kauli zinazokera wananchi kama za sofia simba?
   
 20. W

  WildCard JF-Expert Member

  #20
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mama SS anafaa kumrithi YM atakapostaafu( kufa?). Yeye ndie anayeelewa JK anataka asikie nini kutoka kwa wasaidizi wake.
   
Loading...