Sophia Simba aifagilia CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sophia Simba aifagilia CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUKUTUKU, Feb 28, 2011.

 1. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mwenyekiti wa umoja wa wanawake ((UWT) bi Sophia Simba ameweka hadharani upungufu wa chama cha mapinduzi(CCM) na kukisifia chama cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa mfumo walionao wa kisasa unaovutia kizazi cha sasa na kupata umaarufu wa ghafla.
  Bi Simba ambaye ni Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto alisema hayo jana katika mkutano wa kwanza wa Baraza la UWT katika wilaya ya kinondoni akiwa kama mgeni rasmi ambapo mwenyeji wake alikuwa ni mwenyekiti wa UWT wa wilaya hiyo Bi Anna Makete.
  Bi Simba alisema kuwa katika kipindi kifupi kilichopita na sasa,CCM imepoteza umaarufu wake kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo mfumo wao wa sasa, kutoendana na kizazi kipya ambacho asilimia kubwa ni vijana,kuzidiwa na manano ya propaganda za vyama vya upinzani na kusababisha kushindwa kujibu mapigo na kuwa wanyonge,makundi ndani ya chama,ubinafsi pamoja vijana kukosa uwezesho wa ujasiriamali ndani ya chama.
  Alitaja sabubu nyingine kuwa ni mfumo uliotumika mwaka jana kuwapata wagombea katika nafasi mbalimbali za uongozi uliochangia kuwapoteza wana CCM pia wananchi kuchelewa kumtambua mgombea wao na mambo mengine madogo madogo.
  Akizungumzia umaarufu wa CHADEMA alisema umetokana na mfumo na sera walionayo sasa,DKt Willbrod Slaa kuibua suala la Richmond na Dowans bungeni na kutaka kuvunja mkataba ambao umesababisha nchi kushitakiwa na kutakiwa kulipa mabilioni ya fedha pamoja na njama za wafadhili wa chama hicho kutoka nje ya nchi kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kuking'oa CCM madarakani.
  Nyingine ni kupanda kwa gharama za maisha kutokana na sababu mbalimbali ambayo yanamgusa kila mtu alisema kwamba CHADEMA imetumia mwanya huo kufanya maandamano huku wakidai kwamba ni kutokana na CCM kuwepo madarakani.


  Bi Simba alisema kuwa kitendo cha CHADEMA kufanya maandamano jijini Mwanza juzi ni kutafuta umaarufu na si vinginevyo huku wakisingizia kupinga malipo ya Dowans na mgawo wa umeme.
  Alisema kuwa kilichokuwa kinazungumzwa na viongozi wa CHADEMA juzi kilikuwa tayari kimefikishwa mezani na kinafanyiwa kazi ikiwemo mazungumzo kati ya mmiliki wa Dowans na Serikali ili kuondoa suala la mgawo wa umeme pamoja na mkakati wa kushusha bei ya bidhaa muhimu kama sukari.
  Bi Sophia alisema hatua iliyofikia ya kutaka serikali ilipe shs bilioni 94 za Dowans inatokana na mipango ya Dkt.Slaa na wanasiasa wengine kutaka mkataba uvunjwe huku wakijua matatizo yatatokea(Chanzo cha habari:Majira 26/02/2011,pp 1&4).
  My take
  Naona sasa baadhi ya mawaziri wa JK wanaanza kukubali kuwa CHADEMA inatisha,CCM sasa inabidi wajipange upya vinginevyo watang'olewa madarakani.
   
 2. only83

  only83 JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Naaaaaaaaaaaaaaaaaammm hapo penyewe bado mkuu wao kukubali.......
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kwa huyu Bibi kusema hivyo si ajabu kabisa. alishawahi kukiri kwamba ndani ya CCM hakuna msafi, leo anaibuka na kuisifu CHADEMA, ingawa kuna mahali kajaribu kusafisha chama chake. Inawezekana kabisa asingekuwa na uhakika wa ulaji CCM angelikwisha hamia upinzani.. Labda afanye kazi ya kuwaelimisha wenzie wengine ili waanze kujenga chama.
  Good luck...
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Huyu mama alishapata mume?naona kwa sasa akili yake inaanza kufanya kazi labda haangaiki tena kutafuta mume.
  ILA INAWEZEKANA KASHAJUA JK anaondoka 2015 kwa hiyo anataka kuwa neutral ili upepo umbebe baada ya uchaguzi as it has been noted that JK's inner circle inachukiwa hata na CCM wenyewe
   
 5. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nafikiri imefika wakati CCM wajaribu kuambiana ukweli ili kutafuta mbinu za kukinusuru chama chao vinginevyo wataenda na maji,muda si mrefu!!
   
 6. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ipo siko JK naye ataikubali CHADEMA hadharani!!
   
 7. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mume wake ni Kitwana Kondo!!,ni mapepe yake tu ana mume tangu siku nyingi!!
   
 8. Panga la Yesu

  Panga la Yesu JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unapokiri tatizo ni sehemu ya Uponyaji,
  Mgonjwa wa Ukimwi lazima alikubali tatizo ili walau aweze ongeza maisha, Ni vema JK akalitambua hilo!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 9. Mvuni

  Mvuni JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Alisema kuwa kilichokuwa kinazungumzwa na viongozi wa CHADEMA juzi kilikuwa tayari kimefikishwa mezani na kinafanyiwa kazi ikiwemo mazungumzo kati ya mmiliki wa Dowans na Serikali ili kuondoa suala la mgawo wa umeme.

  Jamaaani, mbona Mhe. Dkt mkwere alisema kuwa mmiliki wa DOWANS hawamjui???!!! sasa huyu ambaye Simba anasema serikali inazungumza naye wawapi? Hivi wao somo la woga na aibu kwao ni wakwe zao? sasa ngoja waona ya Tunisia na Misri yakija kwa style ya aina yake. Kheri mama huyu kwa kuanza kuuona na kuuthibitisha ukweli wa nguvu ya CHADEMA.
   
 10. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Inaonekana mama sasa ameanza kujitambua polepole,nafikiri makada wengine wa CCM watafuata!!
   
 11. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  CHADEMA ikishinda na waho watahasi CCM na kuhamia CHADEMA kwa kutaka madaraka!
   
 12. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Phase four Government is full of contradictions,there is no sign of good governance!!
   
 13. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,869
  Likes Received: 2,814
  Trophy Points: 280
  Mjomba unatoka kule kwenye migomba mingi nini? Angalia hapo kwenye red!!!
   
 14. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  wao wataasi CCM upo hapo!
   
 15. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #15
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Si kwamba wote walio CCM ni wabaya!wengine watapokelewa na CHADEMA,lengo ni moja nchi yetu iendelee!
   
 16. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #16
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  It is alright,message was sent and delivery!no problem mkuu!!
   
 17. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #17
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  yaah ni kweli mzee mimi siwachukiii CCM wote mbona kuna vichwa pale vizuri tu na vinachapa mzigo vizuri man wala sina ugomvi na CCM ila nawaza juu ya wale ambao wanaongea sana na kuuponda upinzani kwamba si lolote na baadae Nguvu ya umma ikishachukua uongozi na wao sababu ya uroho wa madaraka na kuogopa kufungwa sababu ya kua wameharibu sana ili kujiepusha na mkono wa sheria si wanaweza kukimbilia huku nao!
   
 18. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #18
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,636
  Likes Received: 4,746
  Trophy Points: 280
  Hana lolote huyo PASHKUNA wa CCM
   
 19. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #19
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Samahanini nauliza kuhusu kushushwa kwa bei ya sukari mpaka Tsh 1700 je ni kweli na kama ni kweli mbona aijaanza kutekelezwa sababu raia hawajui nini kinachnendelea sababu ktk mikutano ya Dr Slaa nilisikia baada ya CDM kuanzisha maandamano bei za bidhaa muhimu zimeshuka.
   
 20. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #20
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hizi ni tambo za wanasiasa. Poleni sana CDM
   
Loading...