Nimekuwa ni kama sielewi Dunia inavyoenda, mawazo mengi mabaya yanazunguka kichwani mwangu na sijui nitaweza vipi kuiepuka hali hii ambayo inazidi kuweka mizizi na nashindwa kuimudu.
Haya yalianza miaka miwili iliyopita ambapo kwenye familia yetu tulipoipoteza nguzo muhimu, nguzo Baba. Aliondoka na kutuachia wagonjwa wawili ambao wakati wa uwepo wake alipambana kuhakikisha wapo salama. Mdogo wangu alikuwa na kichwa kikubwa na kilijaa maji mara kwa mara, pia alimuacha Mama ambae alikuwa na maradhi makubwa kidogo ambayo yalihitaji pesa nyingi sana kukabiliana nayo. Baada ya msiba huo Wadai wakajitokeza na kuchukua asilimia kubwa ya mali zilizoachwa na ni kweli, kwa sababu ya uhitaji wa pesa wakati huo alijikuta akiingia kwenye madeni makubwa.
Mzigo nikaubeba na ikawa ni mimi na wagonjwa na familia yangu ya mke na watoto wawili. Nilipambana kadri ya uwezo wangu, nikaingia kweny moja ya bank na kukopa kwa dhamana ya kazi, mzigo bado ukawa mgumu kuubeba lakini sikukata tamaa hadi pale ambapo kila njia ikawa haiwezi kunitoa na hapo ndipo kichwa kikajaa mawazo mengi ambayo sasa yamenifikisha kwenu waungwana.
Nikiwa bado kwenye mtanziko wa kifedha, mdogo wangu aliyekuwa mgonjwa aliaga Dunia mwaka Jana mwezi wa nane, likawa tatizo lingine kwa Mama ambae alianza kupata nafuu, alirudi kuugua upya Kwa sababu mdogo wangu alikuwa ni kipenzi chake angalau kuliko sisi wengine.
Mwaka huohuo mwanzoni mwa mwezi wa kumi na mbili binafsi nikaguswa moyo wangu, mwanangu wa miaka sita alifariki kwa homa ya siku mbili, hapo tatizo likaongezeka zaidi Kwa sababu nikawa na kazi ya kumliwaza mke wangu, mama yangu nae akiwa mikononi mwangu.
Nikiwa bado sijapona vizuri maumivu ya wapendwa wangu, mwezi huu tareh 20 nikapoteza tena mwanangu wa mwisho wa miaka minne. Hakika hapa nilipo kila wazo baya naona sahihi... Huku Mama mgonjwa, sasa ni mke wangu nae hayupo Sawa, anazimia kila mara. Nimejibeba kijasiri Sana lakini naona kama akili imeganda hivi.
Nahitaji ushauri wenu wa hali na mali nijue najiondoaje kwenye hali hii.... Mwenye kuweza kunipigia namba yangu ni 0785256311.
Mungu awabariki