Songwe: TANROADS Waahidi kukamilisha miradi ya Maendeleo kwa Wakati

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi katika kijiji cha Ruanda wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe baada ya kukagua ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Ruanda – Nyimbili – Hasamba – Izyola – Itumba yenye urefu wa Kilomita 76.69.

"Tunamuahidi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na viongozi wakuu akiwemo Waziri Mkuu, Makamu wa Rais, viongozi wa Mkoa na Chama kwamba sisi kama TANROADS tumejipanga kuhakikisha kuwa miradi yote ambayo tunayo, wakandarasi wote wanakuwa site na tunawasimamia kwa ukaribu na kwa uadilifu"

Mhandisi Suleiman Bishanga
Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania TANROADS mkoa wa Songwe


Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa ametembelea na kukagua barabara inayojengwa kwa kiwango lami Ruanda-Nyimbili- Idiwili -Itumba
iliyopo Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.

Waziri Mkuu amekagua barabara hiyo leo Ijumaa Novemba 24 ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani Songwe ambapo jana aliweka jiwe la msingi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe na kufanya ziara wilayani Ileje.

Waziri Mkuu ambaye aliwasili mkoani Songwe Jumatano anafanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Ileje na Wilaya ya Mbozi ikiwa ni mwendelezo wa ziara aliyoifanya mwezi Februari katika Halmashauri za Wilaya ya Songwe, Momba na Mji Tunduma.

Akikakua Barabara hiyo Mheshimiwa Waziri Mkuu huyo amesema kuwa barabara hiyo itakuwa ni chachu ya maendeleo katika wilaya ya Mbozi na Mkoa wa Songwe kwa ujumla kutokana na barabara hiyo kuwa ni niia ya mkato kuelekea nchi ya Malawi, ambapo pia itarahisisha ufanyaji wa biashara usafirishaji wa mazao ya kilimo
IMG_20231124_180925_168.jpg
IMG_20231124_180928_406.jpg
IMG_20231124_180930_901.jpg
IMG_20231124_180935_870.jpg
 
Back
Top Bottom