SONGWE: Jeshi la Polisi linamshikilia tapeli, Jeriko Musukuma anayetengeneza fedha bandia akidai ni za Freemason

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Jeshi la Polisi Mkoani Songwe, linamshikilia mtu mmoja ambaye amekuwa akijihusisha na matukio mbalimbali ikiwemo, ujambazi, utapeli kwa kutumia nembo za freemason, akiwa na silaha aina ya Air Gun pamoja na risasi 135.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi Mathias Nyange amesema, mtuhumiwa huyo aliyejulikana kwa jina la Jerico Chifunda Msukuma, ni mkazi Nazareti Mjini Tunduma.

Mbali na kukutwa na vitu hivyo pia amekutwa na vitambulisho vinavyoonesha uraia wa nchi mbili Tanzania na Zambia ambapo anadaiwa kufanya matukio ya uhalifu kisha kukimbilia nchini Zambia.

Vitu vingine ambavyo amekutwa navyo Msukuma ni pamoja na jeneza dogo, pingu, pasi inayotumika kutapeli watu kupata fedha, mashine ya kunakilisha noti bandia, na karatasi zinazolingana ukubwa na noti ya shilingi 10,000.
 
Tukiwa na tafakuri pana mtu Kama huyu humpeleki jela bali chuo cha mafunzo ya ujuzi wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Picha tafadhali....asijekuwa ni shemeji yetu..tukajua dada kaolewa na mpambanaji...kumbe kaolewa na jizi
 
Back
Top Bottom