Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Polisi mkoani Songwe inamshikilia Jelicko msukuma kwa tuhuma za kukutwa na silaha aina ya Airgun,risasi 135,jeneza dogo, pasi iliyotengenezwa ujerumani,vitambulisho vya Tanzania na Zambia pamoja na mabango yanayotangaza kuwa anaweza kuwafanya watu kuwa matajiri kwa kutumia imani ya Freemason .
Akithibitisha tukio hilo kamanda wa polisi mkoani songwe kamishna msaidizi wa polisi Mathias Nyange amesema mtuhumiwa huyo ni mkazi wa Mtaa wa Nazareth halmashauri ya Mji wa Tunduma na kwamba amekuwa akiishi katika eneo huru la mpaka wa Zambia na Tanzania kinyume cha sheria na hivyo amedaiwa kufanya matukio ya utapeli na kisha kukimbilia nchini Zambia.
Mbali na kukutwa na vitu hivyo Mtuhumiwa amekutwa na karatasi zinazolingana ukubwa na noti ya shilingi 10,000 pamoja na fedha ya Zambia (Kwacha) na mashine ya kurudufu noti za bandia.
Kamanda Nyange ameeleza kuwa uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.