Songombingo ya urithi wa mirathi: Somo limesomeka

Songombingo ya urithi wa mirathi: Somo limesomeka

Mtu anapokufa bila kuacha wosia, mali zake zinatakiwa kurithiwa na warithi halali chini ya msimamizi wa mirathi.

Wafuatao ndio warithi halali
  1. Mke, wake halali wa marehemu.
  2. Watoto halali wa marehemu
  3. Watoto wanaotambuliwa kifamilia
  4. Wazazi wa marehemu
  5. Ndugu wa kuzaliwa tumbo moja kwa baba mmoja
Wafuatao sio warithi halali
  1. Babu na Bibi
  2. Wajomba na mashangazi
  3. Vimada
  4. Watoto wa nje wasio julikana
  5. Watoto wa mama mmoja baba tofauti
  6. Watoto wa kufikia
  7. Ndugu wengine wowote ni ndugu tuu na sio warithi halali.
Marehemu anaweza kuacha wosio mtu mwingine yoyote kuwa mrithi wake, ila marehemu anapoacha wasio wa kutowarithisha warithi halali, then mrithi halali yoyote anaweza kufungua shauri mahakamani kupinga wosia wa marehemu.

Kwa bahati nzuri sana, mabilioneo hao wote wawili uliowataja, waliacha wosia.
Migogoro mikubwa ya urithi huanzia kwa nani awe msimamizi wa mirathi!.

P
Bill gate karithisha watoto wake 10% ya Mali sake zingine zitarithiwa na jamii 90%.Hii ina maana mali si kitu cha maana sana.
 
Kuna mzee mmoja kule Tanga kafanya hivi kwa watoto wake,
Viwanja kakata na kila mtu kapewa na hati kabisa,
Mzee bado yupo hai
Kuna wengine ukiwarithisha kabla hujafa wanakutanguliza ili watumbue Mali.Mali ni janga kama majanga mengine
 
Hata kwa marehemu masikini ni hayo hayo wakishidwa kugombania mali kwasababu huna watagomvania Maiti izikwe wapi? nanani wahusike kwenye sadaka nk.....kiufupi jamii yetu nimatatizo sana katika kila jambo
...Hivi imeishawahi kutokea kwenye Msiba ndugu wakagombania watoto wa Marehemu kila ndugu akiwataka yeye? Ama ni kugombania mali tu?
 
Mzee Msuya sio maskini Mkuu!ni Mfanyabiashara wa Madini wa zamani sana na hata huyo Marehemu alianza kufanya biashara za baba yake
Hapana Erasto alifanya biashara tofauti na za Baba yake
alikuwa na migodi mitatu miwili ni ya Baba yake na mmoja ni wake na mpaka leo Babu anasimamia (migodi hiyo haitoi kitu cha kuwa bilonea)
Mali kapata kutokana na wizi wa mawe kutoka Kampuni la Tanzanite One kwa kuuziwa na wanaApollo (hawa ni wezi au waokotaji wa mawe) na ndio chanzo cha mali zake Mkewe akiona umafia wa kudhulumiwa vijana hao, na siye yeye bali na wenzake kina Chusa, Mredii, Sharif na wengine waliiokuwa wakilangua kwa wahindi (mfano Leo umeteuliwa kuwa waziri au Mkuu wa Mkoa ukubwani tu na una mke ndio tuseme ukifa aje Baba kwa vile tu alikusomesha kwa Ng'ombe zake?)
Mkuu jitahidi usi judge watu kwa kuangalia tu,Familia yao Msuya sio wachovu ila ukiangalia wanachopambania ni mali za mtoto wao kuchukuliwa na kaka wa mke wa Marehemu (Wajomba) na ukizingatia huyo mke ana tuhuma za kumuua mtoto wao mwingine;Vaa viatu vyao yaani Mtu anayetuhumiwa kutuma watu kuua mtoto wako anawapa mali za wajukuu zako kaka zake
Mirathi imeelezewa vizuri na Pascal Mayalla , Babu, Bibi na Mashangazi wajomba hawahusiki na mirathi
je angekufa Mke ingekuwaje
Fuatilia Hukumu ya Mke wa Bilionea Msuya kwanini imeshindikana mpaka leo na alishaachiwa Huru akakamatwa tena licha kukiri kuua nipe hiyo hukumu (Atanyongwa, Maisha au kala miaka)
Mambo ua Bilionea Msuya ni Kizungumkuti sana acheni Mirathi iende km Sheria Watoto halali na Mke warithi hao wengine wakatafute yao (biashara ile leo haipo tena Tanzanite imekufa hakuna ujanja ujanja tena ndio maana wanarudi kwa wajukuu) na km ilikuwa na damu ya wanaapollo au Binadamu itapukutika yote
Kesi ilikuwa Julai 2019 PressReader.com - Journaux du Monde Entier PressReader.com - Journaux du Monde Entier
 
Kipindi chake mtume Muhammad (pbuh) baadhi ya wasio waislam hasa wayahudi na wakristo (walianza kuitwa hivyo kule Antiokia) walimwomba awahukumie baadhi ya mambo yao. Mpaka Allah akashusha aya kwamba wao si ni wanajivunia Taurati, kiko wapi leo!

Sasa kwenye maswala ya hukumu kama hizi za mirathi Qur'an imesolve mikanganyiko yote, kwani Qur'an ni kwa ajili ya watu na mambo yao, na bishara njema kwa watakaoiamini.

Mirathi imehukumiwa hiviiii....


النساء (11) An-Nisaa

Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu: Fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili. Na ikiwa wanawake zaidi ya wawili, basi watapata thuluthi mbili za alicho kiacha maiti. Lakini akiwa mtoto mwanamke ni mmoja, basi fungu lake ni nusu. Na wazazi wake wawili, kila mmoja wao apate sudusi ya alicho kiacha, ikiwa anaye mtoto. Akiwa hana mtoto, na wazazi wake wawili wamekuwa ndio warithi wake, basi mama yake atapata thuluthi moja. Na akiwa anao ndugu, basi mama yake atapata sudusi. Haya ni baada ya kutolewa alicho usia au kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu, nyinyi hamjui ni nani baina yao aliye karibia zaidi kwenu kwa manufaa. Hiyo ni Sharia iliyo toka kwa Mwenyezi Mungu. Bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima.

النساء (12) An-Nisaa

Na fungu lenu ni nusu walicho acha wake zenu ikiwa hawana mtoto. Wakiwa na mtoto basi fungu lenu ni robo ya walicho acha, baada ya wasia waliyo usia au kulipa deni. Na wake zenu watapata robo mlicho kiacha, ikiwa hamna mtoto. Mkiwa mna mtoto basi sehemu yao ni thumni ya mlicho kiacha, baada ya wasia mlio usia au kulipa deni. Na ikiwa mwanamume au mwanamke anaye rithiwa hana mtoto wala wazazi, lakini anaye ndugu mume au ndugu mke, basi kila mmoja katika hawa atapata sudusi. Na wakiwa zaidi kuliko hivyo basi watashirikiana katika thuluthi, baada ya wasia ulio usiwa au kulipa deni, pasio kuleta dhara. Huu ndio wasia ulio toka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mpole.
 
Kuna wengine ukiwarithisha kabla hujafa wanakutanguliza ili watumbue Mali.Mali ni janga kama majanga mengine
kuna sehemu maalum za kuweka Mirathi kwani ipo Kisheria km umeshindwa kuwatamkia bayana, na Mali zote hazigawiwi mpaka Mke au Mama wa Marehemu naye aondoke Duniani ndio wagawane. Kilichopo ni kuwa mirathi mtaikuta kwa Wakili fulani au Mahakama ya Mwanzo fulani, Na huwa inasomwa siku ya Matanga au kupeana siku 90Haya mambo yapo Kisheria kabisa hata km hayakuandikwa, Familia na wanandugu wanatakiwa kuteua Msimamizi wa Mirathi hata kama sio Ndugu na akishindwa anaweza kupingwa au kuwekwa mwingine. N a kwa Msuya ndiyo ilikuwa hivyo, baadaye Msahangazi wakaenda Mahakamani Kumipnga Mke wa Erasto Mahakama ikakataa ombi la kumtoa Mke, ndipo mauaji yakatokea, km alimpa Kaka yake Power of Attonery Mbazi ni sahihi, ndio maana ukoo unapinga wakdhan Mbazi ndiye Mrithi wakati sio, sasa atakuwa Kabidhi wasihi chini ya Mkuu wa wilaya najua watapinga tu
kuna kizungumkuti hapo ukichuma janga utachuma na ....
 
Yap ni uchungu wa kuuawa mtoto wao wa kike na kuona wanachohisi ni sababu ya huyo mtoto kuuawa (mali za Erasto) kikifanikiwa,bahati nzuri na mtoto mkubwa wa Erasto ame side na upande wa mama,ila wasiojua historia toka mwanzo wanaona ni uchu wa familia ya Msuya na hawajui hata utajiri wa Erasto umetokana na kufanya biashara za baba yake mwanzoni
Kama familia ya mzee Msuya ingekuwa na uchu wa mali wasingempitisha mke kuwa msimamizi wa mirathi kabla ya kupata kesi ya mauaji. Kuna kitu kipo nyuma ya pazia ndio kinasababisha yote haya
 
Inasemekana watoto walikuwa upande wa mama yao sana, hawakuonyesha balance ya upendo
Siku zote watoto wa kiume wapo upande mmoja na mama zao, ila dogo anatakiwa kucheza kwa akili sana, asipoangalia atapotea kwa umaskini au nae kuuawa endapo mama atapatikana na hatia na kuhukumiwa
 
Dawa ya mirathi SI kuandika wosia Wala Nini Cha kufanya milikisha Mali watu Wakiwa hai mfano nyumba gawia Watoto na wape title deeds zenye majina yao kabisa.

Kama ni.kampuni Hawa hisa kila Moja ajue ana hisa ngapi na kila Moja kwenye fomu ya hisa ajaze warithi wake wa hisa zake akifa Nani kwenye fomu

Siku akikatika mtu yeyote anakuta watu Wana title deeds zao hakuna Cha shangaxi sijui mjomba kuingiza pua Yake popote sababu kila mtu anacho chake hahitaji kikao Cha mirathi Wala Nini wakizika tu maisha yanaendelea.Ambaye alikuwa Kazi Yake kukodolea macho mirathi anaambulia mikono mitupu labda achukue nguo.za marehemu
Kama ukigawa kabla ya kufa unakuwa huna unachomiliki kihalali, let's say hisa, huwezi gawa zote na ww ukabaki huna kitu, na uwezo toa % kubwa kwa watu ww ukabaki na chache, unaweza zungukwa na mtu akaenda ku complain mahakamani kudai dividends coz ana own company legally. Ishu ya msuya alifanya vuzuri kabisa aligawa 40% kwa wazazi na 60% kwa mke na watoto na ndio maana hakukuwa na mgogoro be4. Tatizo lilianza baada ya mke kupata kesi ya mauaji na ndugu wa mke kuanza kuhusika kusimamia mali za Msuya wakidhani ni za dada yao wakati wazazi pamoja na mtoto tena ana umri wa miaka 18 wa marehemu msuya wapo.
 
Kuna mzee mmoja kule Tanga kafanya hivi kwa watoto wake,
Viwanja kakata na kila mtu kapewa na hati kabisa,
Mzee bado yupo hai
Hicho kiwanja alichojenga nyumba anayoishi nacho kashagawa? Hicho nacho unajua kuwa kinaweza kuwa chanzo cha ugomvi? Mwanadamu akishaingiwa na tamaa atataka apate kikubwa kuzidi wengine. Cha muhimu kuwajengea mazingira watoto wetu kama wata weza kufikia umri wa utu uzima kutokuwa tegemezi na kutokuwa na fikra kuwa mali za baba ni zao.
 
Ambapo ukiangalia kwa jicho pana tatizo kubwa hapa ni umaskini tu
Hao wazazi wangekuwa vizuri wanajiweza nao wasingehangaika na hizo mali za mtoto wao. Sasa mwanao naye ana watoto, je watoto hao (wajukuu) watabaki na nini kama wazazi mnataka mchukue mali za mwanenu?
Kwenye hii Case ya Msuya bora Mali zibaki kwa Baba yake Msuya maana hata Mtoto wa Msuya atazirithi tena kutoka kwa Babu yake kuliko Mali hizo kwenda kwa Wajomba maana kwa Mjomba siku zote hakuna urithi!!
 
Kitakachofuatia hapo ni vita vya angani,baada ya vita vya ardhini kuisha.
Ni kweli vidonda vya rohoni matibabu yake yanahitaji muda asee na pengine hata muda unaweza usitibu tunatofautiana na vinavohusisha mauaji ndo balaa kabisa!
 
Yule kijana mkubwa wa kiume wa Marehemu alisema Bibi yao alisugua tumbo na kusema kuwa kafuta kitovu alichotokea baba yao na kutowatambua hao wajukuu. Na huyu bibi hakukataa kabisa yule kijana aliposema hili! Sasa wanaposema wao hawataki Mali Bali wanaogopa mama na ndugu wa mwanamke hawatowapa watotovhaki yao Mimi siwaelewi bado!
Na hapo ndipo kuna ugomvi,Kwa nini watoto wasisimamiwe na Babu au Bibi upande wa baba ambao wapo hai na at least wana haki na hizo mali
 
Na k

Na kibaya naona wasimamizi wa mirathi wanajipaga temporary ownership au wengine hujimilikisha kabisa!
Yaani kibongobongo tumejiaminisha kuwa msimamizi wa mirathi ndiyo mmiliki mpya wa mali za marehemu. Anazifanya vile anavyotaka bila kujali maslahi ya wanufaika au mawazo ya marehemu juu ya mali zake kama angelikuwa hai.
 
Yap ni uchungu wa kuuawa mtoto wao wa kike na kuona wanachohisi ni sababu ya huyo mtoto kuuawa (mali za Erasto) kikifanikiwa,bahati nzuri na mtoto mkubwa wa Erasto ame side na upande wa mama,ila wasiojua historia toka mwanzo wanaona ni uchu wa familia ya Msuya na hawajui hata utajiri wa Erasto umetokana na kufanya biashara za baba yake mwanzoni
Nimekuelewa sana Mkuu.
 
Back
Top Bottom