bhikola
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,132
- 1,668
Habari ndugu zangu, jamaa na marafiki katika familia hii pana ya JF
Wadau, katika siku za hivi karibuni kumetokea mirathi mbili ambazo zimeleta funzo kubwa kwa jamii yetu, hasa yenye familia pana (extended family). Siyo vizuri kuwajadili au kuwataja marehemu (wapumzike kwa amani), lakini tuna kitu cha kujifunza kutoka kwa Mzee Mengi na bilionea Msuya (Mungu awarehemu)
Swali kubwa ninalojiuliza: Ni nani hasa anastahili kurithi mali za marehemu?
1. Wazazi (kama wapo) ambao wamekulea na kuhangaika na wewe, wamepambana kibongobongo walau miaka 25 mpaka 30 kukufikisha kuweza kujitegemea. Kisha umepambana, na ukiwa na miaka 40/45 umefariki. Je, wanastahili kupata chochote?
2. Una mke/wake zako. Tuseme umeishi naye miaka 10/15. Mmeshirikiana kinachowezekana mmevumiliana na hayo yote mliyoyapata. Then umerest in peace. Anastahili kupata nini? Je, ni sahihi kusema achukue vyotevyote vilivyopo pasipo kujali ndugu wengine? - extended family
3. Una watoto: iwe wakubwa au bado wadogo. Wanastahili kupata nini?
4. Mashemeji
5. Kaka na dada zako kutoka katika tumbo/familia yako
6. Mashangazi, wajomba, babu na bibi, wakwe n.k
Kiukweli, kuna vile vitu vinaendelea huku duniani unaweza waza uache kutafuta mpunga wala kuweka vitega uchumi hasa ukiwaza songombingo utakaloacha siku ukiondoka na kuiacha duniani.
Imagine, watu wanapelekana mahakamani, wengine wameuana (mke wa Erasto kamuua - inasemekana - wifi yake), nyumba haikaliki, magali hayaendesheki, biashara zimefungwa why?
Jamani tutafakari pamoja