...Songea Wanaokota Mabunda Ya Noti...Wahi Utajirike!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
16,202
Reaction score
8,788
Kwenye taarifa ya TBC1 jana , kulikuwa na habari za kimiujiza kutoka huko Songea, ambapo kuna mahali pamegundulika kuwa na kisima au chanzo cha pesa cha kipekee, na watu wengi wa rika mbalimbali wamehamia hapo na wanajiokotea noti za denomination mbalimbali(shs 500/=,1000/=, 2000/= 5,000/= na 10,000!

Akiripoti tukio hilo la ajabu, mwakilishi wa TBC1 Songea, Gerishon Msigwa aliwasili eneo la tukio, ambapo alihojiana na umati wa watu waliokuwa hapo wakisuburi neema hiyo ya bure, na wengi walikiri kuokota mabunda ya noti, wengine laki moja, wengine 20,000, wengine 5000 na kadhalika, na kwamba ni siku kadha sasa tangu miujiza hiyo ilipoanza kutendeka eneo hilo! ....mwanajamvi ushawahi kubahatika hivi maishani?

Mimi nimejaribu kufikiria juu ya hili suala, nahisi ni aina fulani ya ushirikina, ambapo baadaye utakuja leta madhara kwa baadhi ya watu, hasa wanaozimiliki baada ya kuokotwa!

Ama kweli Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Bombambili huko Songea!
 
Hi! na mie nimejiunga kwenye jukwaa hili la weledi. bilashaka na mie nitatoa mchangu wangu na kupata nafasi ya kuelimika zaidi.
Siku njema wapendwa!
 
Sasas broda/sisto, kuna jukwaa limeandikwa..UTAMBULISHO!..Nenda huko ukajitambulishe kwanza, hapa ulipokuja si mahala pake...Lakini karibu sana, ndo ugeni wenyewe huu,na mababu walisema .."Mgeni siku ya kwanza mpe mchele na panza, mtilie kifuuni umkaribishe!!
 
Mimi nimejaribu kufikiria juu ya hili suala, nahisi ni aina fulani ya ushirikina, ambapo baadaye utakuja leta madhara kwa baadhi ya watu, hasa wanaozimiliki baada ya kuokotwa!

Ama kweli Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Bombambili huko Songea!

kweli tuna matatizo makubwa zaidi ndugu yangu..
 
hahahaha
za kishirikina huwa haziko hivi, wacha waziokote tu
 
Kwenye taarifa ya TBC1 jana , kulikuwa na habari za kimiujiza kutoka huko Songea, ambapo kuna mahali pamegundulika kuwa na kisima au chanzo cha pesa cha kipekee, na watu wengi wa rika mbalimbali wamehamia hapo na wanajiokotea noti za denomination mbalimbali(shs 500/=,1000/=, 2000/= 5,000/= na 10,000!

Akiripoti tukio hilo la ajabu, mwakilishi wa TBC1 Songea, Gerishon Msigwa aliwasili eneo la tukio, ambapo alihojiana na umati wa watu waliokuwa hapo wakisuburi neema hiyo ya bure, na wengi walikiri kuokota mabunda ya noti, wengine laki moja, wengine 20,000, wengine 5000 na kadhalika, na kwamba ni siku kadha sasa tangu miujiza hiyo ilipoanza kutendeka eneo hilo! ....mwanajamvi ushawahi kubahatika hivi maishani?

Mimi nimejaribu kufikiria juu ya hili suala, nahisi ni aina fulani ya ushirikina, ambapo baadaye utakuja leta madhara kwa baadhi ya watu, hasa wanaozimiliki baada ya kuokotwa!

Ama kweli Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Bombambili huko Songea!

PJ kwa hiyo wakiziona waziaje ?
Ngoja niende eneo hilo kwa maombi maalum
 
Huyo muandishi wa habari alitakiwa kupiga picha hayo mabunda ya hela na yeye pia angeokota yake hili kuwahakikishia watazamaji wake.au ndio kakuta watu wanasubiri round nyingine zitoke? Tanzania tutakuwa tunabahati sana ,yani baada kupewa madini na kushindwa kuyatumia kukomboa maisha yetu sasa tunapewa second chance na safari hii tunamwagiwa pesa kabisa moja kwa moja loooool.
 
kweli tuna matatizo makubwa zaidi ndugu yangu..

Mzee mwenye nyumba, Hizo ni dalili za kukithiri kwa umasikini, kukata tamaa na kukinai maisha, Haiingii akilini ni kwa vp unaweza kwenda kusubiri pesa zidondoke?
 
Kwenye taarifa ya TBC1 jana , kulikuwa na habari za kimiujiza kutoka huko Songea, ambapo kuna mahali pamegundulika kuwa na kisima au chanzo cha pesa cha kipekee, na watu wengi wa rika mbalimbali wamehamia hapo na wanajiokotea noti za denomination mbalimbali(shs 500/=,1000/=, 2000/= 5,000/= na 10,000!

Akiripoti tukio hilo la ajabu, mwakilishi wa TBC1 Songea, Gerishon Msigwa aliwasili eneo la tukio, ambapo alihojiana na umati wa watu waliokuwa hapo wakisuburi neema hiyo ya bure, na wengi walikiri kuokota mabunda ya noti, wengine laki moja, wengine 20,000, wengine 5000 na kadhalika, na kwamba ni siku kadha sasa tangu miujiza hiyo ilipoanza kutendeka eneo hilo! ....mwanajamvi ushawahi kubahatika hivi maishani?

Mimi nimejaribu kufikiria juu ya hili suala, nahisi ni aina fulani ya ushirikina, ambapo baadaye utakuja leta madhara kwa baadhi ya watu, hasa wanaozimiliki baada ya kuokotwa!

Ama kweli Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Bombambili huko Songea!

wakwetu twende tuwahi huko, tusije baki sie tu....ngoja nikate tiketi...hivi ni meli ya saa ngapi tunaondoka nayo?
 
Meli ya mchana saa 9 hadi Dar, then pale tunachukua KISWELE hadi eneo la tukio...Kumbuka kubeba viroba vya kutosha!
 
wakwetu twende tuwahi huko, tusije baki sie tu....ngoja nikate tiketi...hivi ni meli ya saa ngapi tunaondoka nayo?

Utamgoja wakwenu PJ mpaka mwaka kesho,ndio meli ya kwenda Songea itakapokuja sijui kama mtazikuta hizo noti zinawangoja; Shukuru Kawambwa kaua wizara ya miundombinu meli zote zimehalibika!!
 
Zina tofauti gani na fedha bandia?
Isije ikawa watu wanatupa fedha bandia baada ya kushindwa kuzibadilisha na halali
 
Muda si mrefu utasikia waziri kaingia mkataba na kampuni la nje waje wachimbe na kuzisafisha hizo fedha.
 
wakwetu twende tuwahi huko, tusije baki sie tu....ngoja nikate tiketi...hivi ni meli ya saa ngapi tunaondoka nayo?

Watanzania twapenda sana vya ubwete....t-shirt za bure, msosi wa bure, vyakula vya bure.. Aibu tupu!!
 
Ukiwa masikini na mwenye njaa unaweza kuambiwa na ukaamini jambo lolote hata lile ambalo liko dhahiri ni uongo kama hili.
 
Hizi zitakuwa zilifichwa na majambazi/wezi baada ya kuibiwa au ni wale watu wasiojua maana ya benki wamefariki na kuziacha chini ya ardhi.
 
Hahaha Jamani Bibi KALEMBWANI karudi nini? maana miaka ya 80' kuna bibi mmoja alikuwa mganga wa kienyeji maeneo ya ifakara huko akiitwa KALEMBWANI lkn alisifika sana Songea kwa uganga wake machachari hahahaha
 
Nakumbuka usemi huu kwa Tanzania yenye neema yawezekana....makao makuu ya benki kuu yahamie hapo. Wtz tunavimbwanga kweli kweli duuh !!!!!
 
Back
Top Bottom