Songea, Ruvuma: Watu 71 wanusurika kifo kwa kunywa togwa kwenye sherehe

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
Watu 71 wa kijiji cha Liula wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, wamenusurika kifo baada ya kunywa kinywaji aina togwa kinachodhaniwa kuwa na sumu wakiwa kwenye moja ya sherehe ya kidini maarufu kama sadaka.

Mkuu wa wilaya ya Songea, Bw.Pololeti Kamando Mgema amepiga marufuku matumizi ya togwa kwenye sherehe zote wilayani humo kutokana na matukio hayo kujirudia rudia.

Nao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Liula Songea waliokumbwa na kasumba hiyo wamesema baada yakunywa kinywaji hicho hali ilianza kubadilika kwa kuanza kuarisha na kutapika.

Chanzo: ITV
 
Kwa Songea kinywaji cha togwa ni kinywaji muhimu mno kwenye matukio yanayo wakutanisha watu Kama vile harusi,jando nk,wakati huu Songea ina ingia kwenye joto togwa huwa linauzwa pembezoni mwa barabara unakuta imewekwa kwenye chupa za soda na kizibo kimewekwa!

Ndugu dc kupiga marufuku hiyo kinywaji angalia wasije kuku adhibu Wana Songea!!
 
mkuu waliwafanya nini watu wa liula au mambo yetu ya lupatu yale

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mkuu Kuna jamaa yetu alifiwa tukaenda kuzika,,,tukafika salama tukazima gari. Tulivyomaliza shughuli ya mazishi washa gari tuondoke likawaka ile kukanyaga moto tuondoke gari wapi inapiga tu lesi.
Mkuu hatukitoka mpaka siku ya pili, lupatu ya pale nakumbuka mpaka leo Liula.
 
Mkuu Kuna jamaa yetu alifiwa tukaenda kuzika,,,tukafika salama tukazima gari. Tulivyomaliza shughuli ya mazishi washa gari tuondoke likawaka ile kukanyaga moto tuondoke gari wapi inapiga tu lesi.
Mkuu hatukitoka mpaka siku ya pili, lupatu ya pale nakumbuka mpaka leo Liula.
Duh ama kweli uchawi upo wazee wa liula kwani walikosewa nin au waliamua kuwatia hasara iyo noma sana huwa nasikia tu ayo mambo lakin bado hayajanikuta mkuu ila sio powa kabisa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Yaan ww ni mjinga kabisa unawezaje kuwaita wenzio primitive

wenzangu wakina nani? usinifananishe na wajinga wenzio ambao mna tamaa za kijinga na mapombe yenu ya kienyeji ambayo ukinywa unaharisha kama bata. ujue ni jambo la aibu kama wangekufa na sababu ni togwa eti. yani tamaa na undondocha wao, na hao wote ukiuliza hamna ata aliyekaribia kumaliza la saba. hawana maarifa vichwani ni watupu mno. wangekufa kama kuku wenye kideri. kaa humo bush lawyer.
 
Back
Top Bottom