Songas to buy Dowans generators?

Phillemon Mikael,
Mkuu sijakuelewa hapo unaposema akisema mpinzani tunaleta siasa una maana gani?.. Songas hawawezi kununua mitambo hiyo na kutuuzia sisi bila kuwepo mkataba unaohusiana manunuzi hayo..Na kama itatokea hivyo ni mbinu zimetumika, sasa kama wewe una taarifa kamili kwamba serikali imekubali kununua umeme zaidi toka songas tufahamishe..
Na kama una maana Zitto ndiye unamtumia hapa kuwa ni Mpinzani basi huyo Zitto sii mpinzani kwani Mpinzani ni yule anayepinga kubebeshwa mzigo kama huu!..Upinzani hauwezi kubeba mzigo wa CCM na kuuendesha kama mbinu zao ki CCM, hapana mkuu wangu changes ni kama Obama amekataa kuyaweka majeshi Iraq hata kama tayari yapo Iraq..Yanaondoka kinyume cha matakwa ya Republican!..
Ebu nikuulize hao kina Zitto mbona magari yao hawanunui kwa Charle Mtawale (mitumba) pale Kinondoni isipokuwa yanaagizwa toka nje ikiwa swala hapa ni kuwepo kwa magari tayari nchini?
Acheni siasa zenu wakuu.. hatuwezi kudanganyika kirahisi hivyo! Zitto alichemsha, aliteleza na kuangukia ktk shimo la taka, kasimama na kujikung'uta lakini kama bado anazengea zengea ktk tope hizo mkuu wangu tutamkuta huko shimoni...I strongly Oppose any deal with Dowans... kwani hawa sii watengenezaji wa mitambo hii ni kanyanga tu..
Yule mjinga mwingine Lipumba kaleta habari za mitambo mipya ati zinaweza kuwa feki.. uliona wapi hiyo mkuu wangu kama sio siasa..GE au Watsila wanaweza kweli kutuuzia mitambo feki! Hivi kuna mtu anaweza kunionyesha gari hata moja ambalo ni Feki?..Hiyo feki kivipi sijui maanake hata sielewi!
 
Naona Mr. Mkandara bado yuke kule kule kwenye siasa za kijamaa. Hapa tunazungumzia a business proposition. Hizo sentiments zenu za kisiasa hazina nafasi hapa. Tena mkisema songas ni wazungu ndio kabisaa.
 
Tk,
Mkuu wangu nitarudia maneno yangu ya kila siku.. kwamba mimi naishi nchi ya Kibepari.. nafikiri, nakula na kulala kama Bepari hivyo hizi habari za Ujamaa na siasa zinatoka wapi?..Uliambiwa wapi kuwa Business proposition haipo ktk Ujamaa au siasa!..vipi mkuu wangu mbona hatupo ukurasa mmoja.
Haya wewe nambie hiyo Songas inaendeshwa na kina nani maanake kusema ni ya nani haina maana yoyote kuhusiana na hoja yangu..labda soma maelezo haya kisha nambie wewe hiyo management ya Songas inayoongoza na kina nani ktk kutoa maamuzi ya kununua mitambo kama hii ya Dowans..

The main project sponsor was AES Sirroco of the USA, a large electricity company operating worldwide. The other sponsor is Pan African Energy, formerly Ocelot International, a gas development company, with operations in several African countries. Project investors are AES, Pan African Energy, TANESCO, TPDC, CDC, TDFL, EIB and World Bank, the later two through the Government of Tanzania. Project costs are estimated at US$ 350 million. The project will be implemented by SONGAS, a local joint venture company formed by Globeleq, TANESCO, TPDC and CDC. Ocelot, now Pan African Energy will operate the gas field on behalf of Globeleq.
 
Hii ni hujuma ya wazi wazi,hawa watu walishindwa kununua mitambo mipya kwa makusudi kabisa. Sasa hivi wanapitia songas ili waiumize serikali kuwalipa capacity charge.

Mimi nauliza gharama tunazolipa kwa ajili ya kapacity charge nchi hii tusingeongeza mzigo mwingine zaidi ya kununua mitambo mipya tuliona uhakika nayo kwa kuwa itazalisha umeme bila matatizo.

Serikali yetu ipo wapi hapa? Hizi capacity charges mpaka lini? Na je tutakuwa tunasolve matatizo kwa kushtukiza hadi lini? Toka mwaka jana hili suala linapigiwa kelele lakini wala hakuna mpango wa madhubuti uliowekwa wa kulikabili zaidi ya kutaka kununua mitambo ya dowans.

Naamini hata hiyo ya dowans ilitika ikiwa mipya na ilitengenezwa, Je ya kwetu inashindikana nini? Hii ni hujuma iliyoandaliwa muda mrefu.

Naamini hatuwezi kusolve matatizo pindi yanapotokea au kukaribia kutokea,bali ni kwa kuweka misingi madhubuti ili kuyakabili kabla hata ya kuonyesha dalili za kutokea.Na hii itayuletea maendeleo katika taifa letu.
 
Audax,
Mkuu wangu ebu tazama hizo millioni zilipitishwa toka Dec 2007, leo hii sijasikia umeme kuongezeka hata kata moja acha mbali kuwa Tanesco au serikali ilikuwa na uwezo, muda na kila sababu ya kujiandaa kununua mitambo mipya badala ya hiyo ya Dowans, lakini ndio hivyo.. sasa Tujiulize hizo Usd 111.5 millioni zimekwenda wapi (mwaka na ushee sasa hivi) maanake hatujaona kilichofanyika au ndio bado wataalam toka nje wanafanya uchunguzi wa kina..
 
Soko la kuuza umeme bongo lipo tena ni la uhakika.

I think na mimi niingie kwenye mchakato wa kununua hiyo mitambo ya Dowans endapo Songas watashindwa.

Je, nikinunua hiyo mitambo hamtatumia umeme utakaozalishwa na mitambo hiyo?
 
Soko la kuuza umeme bongo lipo tena ni la uhakika.

I think na mimi niingie kwenye mchakato wa kununua hiyo mitambo ya Dowans endapo Songas watashindwa.

Je, nikinunua hiyo mitambo hamtatumia umeme utazalishwa na mitambo hiyo?

- Ndugu yangu unanichana sana mbavu, huwa sikosi kusoma michango yako, keep it up!

William.
 
Naona Mr. Mkandara bado yuke kule kule kwenye siasa za kijamaa. Hapa tunazungumzia a business proposition. Hizo sentiments zenu za kisiasa hazina nafasi hapa. Tena mkisema songas ni wazungu ndio kabisaa.

Mjamaa Mkandara, anayeishi kwa mapebari Canada kwi kwi kwi!!!

Ningelikuwa mimi yule waziri mkuu wa Australia ningemwambia Mkandara kama wewe mjamaa, nenda North Korea basi! kwi kwi kwi!!!
 
Ahsante sana kwa kashfa yako. Sisi umetufikiria hivyo, sijui wewe nawe ukichunguzwa utakutwa kwenye kundi gani. Ni Mlalahoi kweli au umejaa kishenzi, isipokuwa tu malalamiko yako kwa hao mafisadi ni washindani wako wa kishughuli tu (kama kulangua viwanja!!). Conflic of interest???

Kama nafasi inakuruhusu,fuatilia posts zangu tangu ya kwanza hadi hii nayoandika,then utafahamu pasipo hsaka wapi nasimamia.Pengine uko sahihi kuhusu hiyo dhana ya conflict of interest,na INTEREST YENYEWE NI TAIFA LA TANZANIA.Mafisadi na vibaraka wao wanataka kutuletea ngonjera za soko huria,kifo cha ujamaa,etc kuhalalisha wizi,ujambazi,ubazazi,ubadhirifu,unyama,etc wao...kimsingi wanataka kutumia kila nyenzo waliyonayo ili waendelee KUIMONG'ONYOA TANZANIA.Kwa upande mwingine kuna sie tunaofahamu tumezaliwa familia za aina gani,marafiki zetu mitaani wanaishi vipi,mama na dada zetu wanajifungua vipi kwenye zahanati zisizo na huduma,watoto na wadogo zetu wanasomaje kwenye shule za kukaa chini huku mwalimu akiwaza madai yake ya mshahara,mabomba yasiyotoa maji,nk nk......kwa kifupi,TUNALILIA HAKI YA KUISHI KAMA TUKO NDANI YA NCHI YETU (na ndio,tuko ndani ya nchi yetu).

Mafisadi ni wabinafsi kwa vile wanatanguliza mbele maslahi yao badala ya yale ya taifa na watanzania wenzao kwa ujumla.Unaweza kusema hilo ndio soko huria,faida mbele.Kuna tofauti kati ya kusaka faida kwa njia halali na ujambazi.Na linapokuja suala la kuhujumu maslahi ya nchi basi hata hao vinara wa soko huria eg US,UK,etc hawana huruma na majambazi (muulize Madoff na ponzi scheme lake).

Katiba inakuruhusu kuamini unachotaka ikiwa ni pamoja na kuona hakuna ubaya kwa kilemba cha soko huria kutumiwa na majambazi kama njia ya mkato ya kutuibia.Sina ugomvi na soko huria kama mfumo (japo siamini kuwa mfumo huo ndio mkombozi wa dunia) ila ugomvi wangu ni namna mafisadi wanavyoutumia mfumo huo kutuibia.In the same manner,sina ugomvi na mtizamo wako lakini najiskia uchungu kuona kuna watanzania wenzetu wanaendelea kuwapa free pass mafisadi kwa porojo zilezile kama za Dr Idris Rashid kwamba tusiponunua mitambo ya Dowans taifa litaingia kizani.In your case,eti akina sie bado tunadhani nchi iko kwenye mfumo wa kijamaa.Kwani Ben Madoff huko US au Fred The Shred wa HBOS hapa UK wanapobanwa na mamlaka za jamii hizi za kibepari inamaanisha US au UK zimeamua kufuata ujamaa?
 
Songas:Hatununui Dowans
Jackson Odoyo

KAMPUNI ya kuzalisha umeme wa gesi ya Songas Limited imesema haina mpango wa kununua mitambo iliyotumika ya kampuni ya Dowans Tanzania Limited (DTL), kwa haina uwezo wa kutumiwa kibiashara.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya vyombo vya habari kuripoti kuwa Songas, inayomilikiwa kwa pamoja na mashirika matatu ya serikali na mawili ya nje, ina mpango wa kununua mitambo hiyo baada ya serikali kughairi kuinunua kutokana na shinikizo la Bunge.

Akizungumza na Mwananchi jana ofisini kwake, mkurugenzi mtendaji wa Songas, Christopher Ford alisema kampuni yake ina mitambo imara na yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha kwa ajili ya kuliuzia Shirika la Umeme (Tanesco).

"Sikiliza bwana mwandishi, taarifa hizo (za kununua mitambo ya Dowans) si za kweli hata sisi tulizisikia katika vyombo vya habari," alisema mkurugenzi wa Songas ambayo wamiliki wake ni pamoja na Globeleg ya Uingereza, ambayo ina hisa nyingi, taasisi ya kifedha ya FMO ya Uholanzi, Tanesco, Taasisi ya kifedha kwa Maendeleo (TDFL) na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC).

"Ukweli ni kwamba Songas haiwezi kununua mitambo ya Dowans kwa sababu tuna mitambo yetu yenye uwezo mkubwa, na iliyo imara kuliko hiyo ya Dowans.

"Hata kama tukihitaji kununua mitambo ya kuzalisha umeme, bado hatuwezi kununua mitambo iliyokwishatumika kwa sababu hiyo si sera ya Songas.

"Unafahamu kazi ya kuzalisha umeme ni ngumu na inahitajika kuwa na vifaa imara na vyenye uwezo mkubwa, hivyo itakuwa jambo la kushangaza tukiingia kwenye mchakato wa kununua mitambo hiyo yenye mgogoro mkubwa hapa nchini.

"Pili Songas ni kampuni inayoaminika na yeye uwezo mkubwa kifedha, hivyo itakuwa jambo la kushangaza tukijiingiza kwenye mgogoro wa kununua mitambo ya Dowans."

Taarifa kwamba Songas inataka kununua mitambo ya Dowans ilizua hisia kuwa serikali inataka kutumia njia nyingine kutekeleza azma yake ya kuinunua mitambo hiyo kutokana na mashirika yake matatu kuwa na hisa kwenye kampuni hiyo inayozalisha umeme kutokana na gesi.

Awali mpango huo wa kununua mitambo ya Songas ulikwama baada ya Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge kueleza kuwa kufanya hivyo ingekuwa ni kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma inayokataza serikali kununua vitu vilivyotumika.

Lakini serikali ikakimbizia mpango huo kwenye Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, lakini Bunge likasimama imara kupinga utekelezwa wa azma hiyo.

Mkurugenzi wa Tanesco, Dk Idris Rashid hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo.
 
KAMPUNI ya kuzalisha umeme wa gesi ya Songas Limited imesema haina mpango wa kununua mitambo iliyotumika ya kampuni ya Dowans Tanzania Limited (DTL), kwa haina uwezo wa kutumiwa kibiashara.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya vyombo vya habari kuripoti kuwa Songas, inayomilikiwa kwa pamoja na mashirika matatu ya serikali na mawili ya nje, ina mpango wa kununua mitambo hiyo baada ya serikali kughairi kuinunua kutokana na shinikizo la Bunge.

Akizungumza na Mwananchi jana ofisini kwake, mkurugenzi mtendaji wa Songas, Christopher Ford alisema kampuni yake ina mitambo imara na yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha kwa ajili ya kuliuzia Shirika la Umeme (Tanesco).

"Sikiliza bwana mwandishi, taarifa hizo (za kununua mitambo ya Dowans) si za kweli hata sisi tulizisikia katika vyombo vya habari," alisema mkurugenzi wa Songas ambayo wamiliki wake ni pamoja na Globeleg ya Uingereza, ambayo ina hisa nyingi, taasisi ya kifedha ya FMO ya Uholanzi, Tanesco, Taasisi ya kifedha kwa Maendeleo (TDFL) na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC).

"Ukweli ni kwamba Songas haiwezi kununua mitambo ya Dowans kwa sababu tuna mitambo yetu yenye uwezo mkubwa, na iliyo imara kuliko hiyo ya Dowans.

"Hata kama tukihitaji kununua mitambo ya kuzalisha umeme, bado hatuwezi kununua mitambo iliyokwishatumika kwa sababu hiyo si sera ya Songas.

"Unafahamu kazi ya kuzalisha umeme ni ngumu na inahitajika kuwa na vifaa imara na vyenye uwezo mkubwa, hivyo itakuwa jambo la kushangaza tukiingia kwenye mchakato wa kununua mitambo hiyo yenye mgogoro mkubwa hapa nchini.

"Pili Songas ni kampuni inayoaminika na yeye uwezo mkubwa kifedha, hivyo itakuwa jambo la kushangaza tukijiingiza kwenye mgogoro wa kununua mitambo ya Dowans."

Taarifa kwamba Songas inataka kununua mitambo ya Dowans ilizua hisia kuwa serikali inataka kutumia njia nyingine kutekeleza azma yake ya kuinunua mitambo hiyo kutokana na mashirika yake matatu kuwa na hisa kwenye kampuni hiyo inayozalisha umeme kutokana na gesi.

Awali mpango huo wa kununua mitambo ya Dowans ulikwama baada ya Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge kueleza kuwa kufanya hivyo ingekuwa ni kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma inayokataza serikali kununua vitu vilivyotumika.

Lakini serikali ikakimbizia mpango huo kwenye Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, lakini Bunge likasimama imara kupinga utekelezwa wa azma hiyo.
Mkurugenzi wa Tanesco, Dk Idris Rashid hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo.
Source:Mwananchi
Hawa watalia na mitambo yao iliyochoka sijui watamuuzia nani? labda watuuzie kwa sent moja kama Jaguar/Land rover walivyouziwa TATA
 
Last edited:
"Hata kama tukihitaji kununua mitambo ya kuzalisha umeme, bado hatuwezi kununua mitambo iliyokwishatumika kwa sababu hiyo si sera ya Songas.

"Unafahamu kazi ya kuzalisha umeme ni ngumu na inahitajika kuwa na vifaa imara na vyenye uwezo mkubwa, hivyo itakuwa jambo la kushangaza tukiingia kwenye mchakato wa kununua mitambo hiyo yenye mgogoro mkubwa hapa nchini.

"Pili Songas ni kampuni inayoaminika na yeye uwezo mkubwa kifedha, hivyo itakuwa jambo la kushangaza tukijiingiza kwenye mgogoro wa kununua mitambo ya Dowans."
Tunawashukuru Songas kwa kutuondolea kiwingu.
 
Duh!!!
Inaonekana wazi kuwa jitihada za kuuzwa hiyo mitambo kukwama, lakini bado nina shaka kuwa huenda wahusika watafanya tu njia zingine kutimiza azma yao.
Ila kwa kweli wananchi sasa wameanza japo kwa mbaaaali kukomaaa na kukataaa hoja na mipango inanukia nukia ufisadi. Inshaaaala tutafika.
MUNGU IBARIKI TZ
 
Nadhani sasa watetezi wa mitambo ya dowans wataelimika kwa nini watu walikuwa wanapinga uhujumu uliotaka kufanywa na akina ngeleja, idrisa rashid na mdogo wao zito. Watu walikuwa wakipinga wanaambiwa wanaingiza siasa tuambiwe basi kuwa songas nao wameingiza siasa.
 
Dawakali,
Mkuu hizi ni tetesi tu Songas inaongozwa na wazungu na nakuhakikishia hawawezi kununua mitambo ya Dowans kwa sababu ambazo sisi tumezitaja, Haiwezekani! hawaihitaji mitambo hiyo isipokuwa sisi ndio tunalazimisha..ni swala la logic tu kwa mfanya biashara..
Na kama mnafikiria yatakuwa basi tusubiri ukweli unless Tanesco wenyewe wananunua kwa kutumia hadithi ya kwamba Songas wamenunua..

You were right to the point jamaa wamechomoa kwa kusema kama waliokuwa wakipinga kuwa hawawezi kununua mitumba. sasa tunasubiri tk na mtanzania washabiki vipofu wa dowans sijui watakuja na longolongo gani
 
Cpt Hadock,

You are missing the point here, binafsi sishabikii Dowans wala sina maslahi yoyote na Dowans, ninachosema tutumie sababu za kiuchumi kuamua kama tunataka kununua au la na wala sio sababu za kisiasa. Kama hakuna sababu za kiuchumi, basi hakuna haja ya kununua, hiyo ndio point yangu tokea mwanzoni. Kitu ambacho mimi napinga ni hii sababu ya kwamba tusinunue kwasababu Dowans watafaidika, kwa mimi ningeangalia je taifa litafaidika?

Kama Songas wametumia sababu za kiuchumi kutoa uamuzi wao mimi niko happy nao. Pia wao wamesema hawana tatizo na uzalishaji wa umeme. Kama wameogopa kuwa PR dissaster pia nitawaelewa maana ni hatari kwa private investor kuwa kwenye vita na wananchi, PR inakataza unless kuwe na maslahi makubwa sana kwenye hilo jambo.

Kwa Tanesco matatizo yao ni kuingiza siasa badala ya kutafuta solution. Miezi inaenda hakuna kinachofanyika na hapo ndipo kwenye tatizo. Tutaendelea kubishana hapa lakini tatizo liko pale pale na uzalishaji TZ unaenda chini shauri ya matatizo ya umeme.

Tanesco wameshaamua hawanunui hiyo mitambo, sawa, lakini pia inatakiwa pia watuletee solution nyingine haraka.
 
Kama investors wa Kiwira wamekimbia kwasababu ya politics, nita washangaa sana Songas kujiingiza katika mzigo very risky kama huu wakununua mitambo ya Dowans ambayo politically ni very sensitive nchini. Sidhani kama Songas watataka kujiiniza kwenye situation just for 100Mw and jeopardise investments zao. Kwahio this deal does not make sense
Tulisha waeleza in business terms kwanini Songas aiwezi kununua mitambo ya Dowans, watu wakasema tunaongea siasa. Lakini as presumed, Songas wamerudi na jibu hilo hilo.
 
Last edited:
Cpt Hadock,

You are missing the point here, binafsi sishabikii Dowans wala sina maslahi yoyote na Dowans, ninachosema tutumie sababu za kiuchumi kuamua kama tunataka kununua au la na wala sio sababu za kisiasa. Kama hakuna sababu za kiuchumi, basi hakuna haja ya kununua, hiyo ndio point yangu tokea mwanzoni. Kitu ambacho mimi napinga ni hii sababu ya kwamba tusinunue kwasababu Dowans watafaidika, kwa mimi ningeangalia je taifa litafaidika?

Kama Songas wametumia sababu za kiuchumi kutoa uamuzi wao mimi niko happy nao. Pia wao wamesema hawana tatizo na uzalishaji wa umeme. Kama wameogopa kuwa PR dissaster pia nitawaelewa maana ni hatari kwa private investor kuwa kwenye vita na wananchi, PR inakataza unless kuwe na maslahi makubwa sana kwenye hilo jambo.

Kwa Tanesco matatizo yao ni kuingiza siasa badala ya kutafuta solution. Miezi inaenda hakuna kinachofanyika na hapo ndipo kwenye tatizo. Tutaendelea kubishana hapa lakini tatizo liko pale pale na uzalishaji TZ unaenda chini shauri ya matatizo ya umeme.

Tanesco wameshaamua hawanunui hiyo mitambo, sawa, lakini pia inatakiwa pia watuletee solution nyingine haraka.

Mtanzania,
Labda ni kweli huwatetei dowans lakini mimi napata shida sana kuamini hivyo. Huo uchumi unaousema sijakufahamu una maanisha upi. Lakini hata kama ni uchumi kinachotakiwa ni suluhisho kudumu siyo miaka nenda rudi dharula tu. Richmond ilivyokuja tuliambiwa dharula, hadi dharula ikaisha bila richmond kuzalisha umeme na huo uchumi tukambiwa unakua.
Mnaposema tanesco wanaleta siasa hapo ndipo mnapokosea wanacholeta ni UFISADI na kwa sababu hawawezi kuiba hivihivi tu ndio maana maneno mengi ya kuhalalisha ujambazi huu. Wengine mnasema uchumi tanesco wanasema ni suala la kitaalamu almradi ni mkorogo tu kama wa mafuta ya transfoma.
Songas hawawezi kuogopa wananchi labda wangekuwa wananchi wa nchi za wajomba lakini siyo wadanganyika kwani serikali si iko pamoja nao. BA system si walituuzia rada. Na kupinga si kwa sababu tunaogopa dowans watapa faida la hasha tunachopinga ni kuibiwa mara ya pili na juu ya yote tusitatue matatizo yetu. Kinachotakiwa ni mitambo mipya inunuliwe itachukua miezi sita, mwaka au hata miaka miwili tutasubiri. Mbona tangu richmond iingie karibu tunaingia mwaka wa tatu? NI ufisadi tu na si kingine chochote. Songas wameshtuka kwani hata mmliki hajulikani sasa watafanya biashara na na nan? Nyie mnaosema tununue tuambieni tutafanya biashara na nani.
 
Back
Top Bottom