The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,911
- 2,891
kwa nionavyo mimi mazingira ya uchaguzi wa burundi uliomuweka madarakani rais pier una muktadha unaofanana sana na kinachoendelea visiwani zanzibar burundi kulikua makundi mawili kundi moja lilikua tayari kwa lolote ikibidi kuvunja sheria ilimradi wanaingia madarakani ni kweli wakafanikiwa katika hiyo nia yao ovu lakini kinachoendelea burundi shen anakijua na ccm pia wanakijua lakini wanaendelea na taratibu za kuvunja katiba na sheria kama ilivyokua burundi huku wakijificha nyuma ya kivuli cha tume ya uchaguzi yaani zec aka jecha hivi kwa nini wanashndwa kufananisha haya matukio na kuchukua tahadhari mapema? labda ni kutokana na madhaifu haya ndio maana serikali yetu haikuwahi kumkemea nkurunziza kwa kukiuka makubaliano ya arusha!