Maalim Seif: Mimi sina sababu ya kukutana na Dr. Shein na kutafuta suluhu na Prof. Lipumba

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,884
2,000

Asema adhabu ya msaliti ni kupigwa risasi.

Akanusha minong'ono inayosambaa mitaani kua, amekua akifanya Vikao na Dr. Shein.

Afafanua kauli yake ya miezi mitatu na kusistiza kwamba, Dr. Shein hafiki 2020.

Asema nyimbo ya Tanzania ya Viwanda imekosa mipango.

Leo tarehe 24/05/2018 akiwa Mkoani Mwanza, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na mshindi wa Uchaguzi wa 2015, Maalim Seif Sharif Hamad, alifanya mahojiano na Waandishi wa Habari wa vituo mbali mbali vya tv na redio.

Mahojiano hayo yaliyokuja kufatia Mualiko aliopewa Katibu Mkuu huyo na Muungano wa Clubs za Waandinshi wa Habari Tanzania (UTPC) wenye Makao Makuu yake Mjini Mwanza yalilenga kuzungumzia maswala mbali mbali ya kisiasa, kiuchumi na kijimii yanayoendelea nchini Tanzania.

Maalim Seif anaetambulika kwa sifa ya kupenda suluhu na umoja wa kitaifa, leo aliweka wazi mambo mbali mbali kupitia vyombo kadhaa vya habari nchini Tanzania ambapo pamoja na mambo mengine, Maalim Seif ameeleza wazi kua, hakuna suluhu kwake yeye na Prof. Lipumba.

Hayo yamejiri baada ya Waandishi wingi wa habari kushangazwa na muendeleo wa migogoro mbali mbali inayokikabili Chama cha Wananchi CUF, huku Maalim Seif akiwa mmoja wa Viongozi waliopasi vizuri katika somo la Sayansi ya siasa akishindwa kutafta suluhu ya kutatua migogoro hiyo na Prof. Lipumba.

Mmoja wa Waandishi wa habari hao ilimlazimu kuhoji ukubwa wa kosa la Prof. Lipumba linalomfanya Katibu Mkuu huyo ashindwe kumsamehe M'kiti huyo wa zamani wa Chama cha Wananchi CUF. Katika hoja yake, muandishi huyo alihoji kwa nini, licha ya Maalim Seif kupenda sana suluhu wameshindwa kutafta suluhu na Prof. Lipumba huku akihoji ukubwa wa kosa la Prof. Lipumba linalomfanya ashindwe kusamehewa licha ya kua, Wanasayansi wa siasa wanasema kua, katika siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu?

Maalim Seif katika majibu yake alibainisha kwamba, kosa kubwa alilolifanya Prof. Lipumba ni usaliti. Kwa mujibu wa Maalim Seif ni kwamba, Prof. Lipumba sio tu ameisaliti CUF bali kawasaliti Watanzania na kuwaacha katika kipindi kigumu (Kipindi cha Uchaguzi).

Maalim Seif alisema kwamba, hakuna kosa kubwa kama usaliti na kudai kua, hukumu ya msaliti ni kupigwa risasi huku akiongeza kwamba, hata yeye kama angekua na Serikali halafu mtu akafanya usaliti angempiga risasi.

Kutokana na uzito wa kosa hilo ambalo Maalim Seif alilieleza kua ndio kosa kubwa la Prof. Lipumba, Maalim Seif aliweka wazi kua, licha ya kua ni kweli yeye hupenda sana suluhu, lakini hakuna suluhu kwa Prof. Lipumba.

Akiendelea kufafanua migogoro inayokikabili Chama hicho, Maalim Seif alisema kua, migogoro yote iliyokikabili Chama cha Wananchi CUF tangu kuasisiwa kwake hadi sasa ni migogoro inayopandikizwa na Serikali huku akitolea mfano wa mgogoro wa mwazo wa Mzee Mapalala kwa kusema kua, Serikali ilipotaka kupandikiza mgogoro huo ili-forge barua ambayo ilionyesha Katibu Mkuu huyo (Maalim Seif) akizungumza na nchi za kiarabu na kuwaahidi kua, baada ya kupewa Uraisi wa Visiwa vya Zanzibar atawafukuza Wakristo wote walioko Zanzibar.

Barua hiyo ambayo kwa mujibu wa Maalim Seif ndio iliyozaa mgogoro wa mwanzo wa Mzee Mapalala ilipelekwa kwa Mzee Mapalala ambapo kwa mujibu wa Maalim Seif, Mzee Mapalala pasi na kufkiria, aliikubali barua hiyo na huo ukawa ndio mwanzo wa mgogoro huo wa kwanza kukikabili Chama cha Wananchi CUF. Kwa mujibu wa Maalim Seif, Mzee Mapalala baada ya kubebeshwa uzushi huo akaanza kuwakataza Viongozi wa Chama wasiende Tanzania Bara na akawa anawafukuza Viongozi bila ya kufata taratibu jambo lililopelekea Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kuchukua hatua.

Alipotakiwa kutoa ushahidi wa namna Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyopandikiza migogoro ndani ya Chama hicho, Maalim Seif alitoa vielelezo mbali mbali vya kisheria na kikatiba vinavyoonyesha namna ya Serikali inavyohusika katika kupandikiza Migogoro ndani ya Chama cha Wananchi CUF, kama vile, kukiukwa kwa taratibu za Uchaguzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki.

Maalim Seif alisema kua, licha ya utaratibu kuweka wazi kua, documents zote za uteuzi wa nafasi hizo zinapaswa kua na saini ya Katibu Mkuu, documents zilizopelekwa na Prof. Lipumba hazikua na saini ya Katibu Mkuu lakini Bunge liliwapitisha wagombea wao.

Akiendelea kuonyesha namna ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyopandikiza migogoro hiyo, awali Maalim Seif alisema kua, baada ya Viongozi wa Bunge kuona kwamba, Chama cha Wananchi CUF kina mgogoro wa Uongozi, Viongozi hao waliamua kusitisha Uchaguzi wa Chama hicho mapaka pale mgogoro huo utakapomalizika, lakini gafla Viongozi hao walipigiwa simu kutoka ikulu ikiwataka waendelee na Uchaguzi hivyo hivyo na Wateule hao hao (wa Prof. Lipumba). Kutokana na hali hiyo, Maalim Seif alisema kua, hata raisi Magufuli anahusika katika kupandikiza mgogoro wa Chama chake na Prof. Lipumba.

Kwa upande mwengine, mmoja wa waliofatilia mahojiano hayo kupitia social media (Facebook account) alimtaka Maalim Seif kufafanua juu ya ahadi yake aliyowaahidi Wazanzibari kua, haki ya Wazanzibari ingepatikana ndani ya miezi mitatu huku sasa ikiwa ni takribani mwaka mmoja umepita hakuna kilichotokea na kumtaka Maalim Seif kueleza iwapo bado hajakata tamaa juu ya jambo hilo.

Maalim Seif alisema kwamba, ni kweli alisema mnamo mwezi August 2016 kua, haki ya Wazanzibari ingepatikana ndani ya miezi mitatu na kuongeza kua, alisema vile kwasababu ya namna ya mchakato wa kuutaftia ufumbuzi mgogoro wa kuporwa kwa haki hiyo ulivyokua unakwenda.

Kwa mujibu wa Maalim Seif, mcahakato wa kulitaftia ufumbuzi swala hilo kwa kipindi kile ulikua unakwenda vizuri na kulikua na kila dalili kua, haki hiyo ingerudi ndani ya miezi mitatu lakini CCM waligeuka.

Maalim Seif alisema kua, kama ilivyo kwa CCM kwamba, kuna baadhi ya Viongozi Wakubwa ambao hawana nia ya kuona Wazanzibari wanakua wamoja na wanahitaji kila siku wakae wao tu madarakani ndio sababu ya swala hilo kushindikana kwa kipindi chote hicho.

Hata hivyo, Maalim Seif alisema kua, bado anaamini kwamba, haki hiyo itapatikana na atakua raisi wa Zanzibar huku akisistiza kua, yeye sio mtu wa kukata tamaa na kuongeza kwamba, Serikali ya Dr. Shein haiwezi kufika 2020.

Akijibu juu ya kile alichokiita maneno ya mitaani kuhusu yeye kukutana na kufanya vikao na Dr. Shein na Jumuiya mbali mbali za Kimataifa ambapo Maalim Seif alitakiwa kueleza mafanikio ya Vikao hivyo, Maalim Seif alisema kua, hayo ni maneno ya mitaani (rumours) ambayo hayana ukweli wowote na kuongeza kwamba, hajawahi kukutana na Dr. Shein.

Maalim Seif alisema kwa kuhoji kua, ikiwa aliukataa mkono wa Dr. Shein, atawezaje kukaa na kuzungumza na kiongozi huyo?

Maalim Seif alisema kua, hakuna sababu ya yeye kukutana na Dr. Shein kwasababu yeye si lolote si chochote na hawezi kufanya chochote kwani funguo za mambo yote zimo mikononi mwa raisi Magufuli.

Maalim Seif alisema kwamba, anaeweza kuzungumza nae ni raisi Magufuli na sio Dr. Shein, kwasababu Dr. Shein ni kibaraka tu aliekwa, hana uwezo wa kuamua chochote.

Kwa mujibu wa Maalim Seif ni kwamba, licha ya kua raisi Magufuli ndie mtu pekee anaeweza kulimaliza swala la Zanzibar, raisi huyo (Magufuli) mpaka sasa hataki kufanya mazungumzo na Maalim Seif juu ya kulimaliza swala hilo. Maalim Seif alisema kua, licha ya kumuandikia barua kadhaa raisi Magufuli, mpaka sasa raisi Magufuli hajajibu barua hizo.

Hata hivyo, Maalim Seif alisema anaskia kwamba, mkakati wa Chama cha Mapinduzi (CCM) juu ya kulimaliza swala hilo kupitia njia ya mazungumzo ni pale itakapofikia 2019 ambapo kwa mujibu wa Maalim Seif, CCM wamepanga hadi itakapofika muda huo ndipo watakapokubali mazungumzo na Katibu Mkuu huyo wa Chama cha Wananchi CUF.

Mkakati huo ambao Maalim Seif aliukataa kwa kusema kua, wao CUF hawatokubali mazungumzo ya mwaka huo na kusema kua, CCM wasidhani kwamba, Viongozi wa CUF ni watoto wadogo na wataweza kuwadanganya, unaonyesha nia mbaya ya Viongozi wa CCM dhidi mustakbali wa kile anachokiamini Maalim Seif kua ndio suluhisho pekee la tatizo la Zanzibar ambacho si chengine bali ni kupewa haki yake aliyoporwa na hatimae kuviongoza Visiwa vya Zanzibar akiwa raisi.

Maalim Seif akiwa mmoja wa Viongozi mashuhuri nchini Tanzania na duniani, kutokana na mazingira hayo na namna Sheria mbali mbali za Uchaguzi zilivyobadilishwa, amesema kua, haoni kama kutakua na Uchaguzi 2020 endapo hali itaendelea kua hivi hivi hadi 2020 pasi na swala la Zanzibar kupatiwa ufumbuzi. Hivyo, Maalim Seif ametoa fursa kwa raisi Magufuli kuona haja ya kuonana na kulitaftia ufumbuzi swala la Zanzibar.

Akizungumza kuhusu namna anavyoziunga mkono jitihada za raisi Magufuli na uumini wake kuhusu Muungano, Maalim Seif alisema kua, awali alipendezwa na sera za raisi Magufuli za kupambana na rushwa na kurejesha nidhamu kazini, lakini kila siku zinavyokwenda mbele anakatishwa tamaa na raisi huyo hasa baada ya kukosa mipango na kufanya vitu tofauti na alivyoahidi.

Kwa upande wa Muungano, Maalim Seif alisema kua, yeye ni muumini wa Muungano lakini Muungano ambao kila upande utamuheshimu mwenzake na kutoa fursa sawa.

Akifafanua kauli hiyo, Maalim Seif alisema kua, tatizo kubwa la Muungano uliopo sasa ni kua, Tanganyika imejivisha koti la Muungano na kujifanya ndio Tanzania na hivyo kupelekea kuisemea Zanzibar hata katika mambo yasiyo ya Muungano.

Akitolea mfano wa swala hilo, Maalim Seif alisema kua, Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Wanachama wa Jumuiya hiyo wamekubaliana kuungana katika mambo 13.

Kwa mujibu wa Maalim Seif, licha ya kua katika mambo 13 hayo ni mambo matatu tu ndio mambo yaliyomo katika orodha ya mambo ya Muungano na 10 yaliyobakia hayamo katika orodha ya mambo ya Muungano, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Tanganyika) imekua ikiyasimamia na kuyasemea mambo hayo jambo ambalo linaifanya Zanzibar kua haina sauti.

Hivyo, Maalim Seif alisistiza umuhimu wa kuheshimiwa maoni ya Wananchi yaliyokusanywa kupitia Tume ya Jaji Warioba na kusisitiza kua, laiti maoni hayo yangesimamiwa na kuheshimiwa, Tanzania isingekua na matatizo haya yanayoikabili sasa.

Abdalla Dadi.
[25/05 09:50] Mmm: Dondoo za aliyoyasema Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad katika mazungumzo yake na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (Union of Press Clubs of Tanzania) wenye makao makuu Mwanza, leo tarehe 24 Mei, 2018

● Serikali iheshimu mawazo ya wananchi, waachwe huru kutoa mawazo yao.

● Katika maandamano ya mwaka 2001 wananchi wengi sana waliuawa na vyombo vya dola tofauti na idadi ya watu 45 waliotangazwa na tume iliyochunguza.

● Maridhiano ya mwaka 2010 hayakuwa ya Maalim Seif na Karume, yalikuwa ya Wazanzibari wote na ndiyo maana yalithibitishwa na Baraza la Wawakilishi na Wananchi wote kupitia kura ya maoni.

● Wapo viongozi wa CCM wenye nia mbaya ambao hawataki maridhiano, wanaona maridhiano yanazuia mipango yao binafsi ya uongozi, hao ndiyo wanatukwamisha.

● Zanzibar itajengwa na vijana waliofundishwa upendo na siyo chuki, wapo viongozi wanawaaminisha vijana wa vyama vyao kuwa hawa wakiingia madarakani watawaleta masultani, watapinga mapinduzi, watapinga maendeleo. Vijana hao wanapotoshwa.

● Uchaguzi wa Oktoba 2015 ulikuwa huru na wa haki na waangalizi wote wa ndani na nje ya nchi walithibitisha kwamba Zanzibar ilikuwa imefanya uchaguzi wa kwanza huru na wa haki.

● CUF ilishinda uchaguzi wa Oktoba 2015 kwa uwazi na bila ubishi, tulikuwa na matokeo kutoka kwenye kila kituo "polling station". Tulipojumuisha yote tukakuta nimemshinda Dk. Shein kwa kura zaidi ya 20,000.

● Wenzetu walipoona CUF tumeshinda, wakamwamrisha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC) afute matokeo, ndugu waandishi, Mwenyekiti huyo wa ZEC hana mamlaka ya kikatiba wala ya kisheria ya kufuta uchaguzi.

● Mimi ni mtu nisiyependa kabisa vurugu, baada ya hatua ile ya ZEC nikamwandikia barua Dk. Shein kumuomba tukutane, akanijibu tukutane na wajumbe wengine, nikakubali, tukakutana.

● Wakati tumeanza kukutana ili kujadiliana, wenzetu wakatuzunguka wakajitangazia uchaguzi mwingine mpya bila kujali kuwa Katiba ya Zanzibar haina kipengele kinachoruhusu kurudiwa kwa uchaguzi.

● Kama CUF ingeshiriki kwenye uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi 2016 ulioitishwa kinyume cha katiba ingekuwa inashiriki kuvunja katiba na sheria za nchi.

● Pia, chama chetu kilitoa wito kwa Wazanzibari wote wasiende kupiga kura, ndiyo maana kati ya wapiga kura wote 350,000 walioenda kupiga kura hawafiki 25,000.

● Baada ya kuwa nje ya serikali chama chetu kimezidi kuimarika, jambo msilolijua ni kuwa uamuzi wowote wa CUF huwa unaenda na wanachama na wafuasi wake, hata uamuzi wa kukataa kushiriki uchaguzi haramu umeungwa mkono na wanachama wetu wote.

● Hatujutii kabisa kuwa nje ya serikali, hatukuwa tunamtafutia cheo Maalim Seif, tulikuwa tunataka kuifanya Zanzibar iwe na maendeleo, iwe Singapore ya Afrika. Tulichokitaka ni kuongoza serikali siyo kuwa na Makamu wa Rais, tulikuwa na malengo makubwa sana.

● Wito wangu kwa Rais Magufuli tukae na tujadiliane kuhusu masuala muhimu ya Zanzibar.
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
28,474
2,000
Maalim anajiona mwenye chongo kwenye kundi la vipofu... tehteehhh
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
28,474
2,000
Seif aliiga kunya kwa tembo, ona sasa hadi amepasuka msamba na kujisaidia tele.... tehteehhh
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom