Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,036
- 828,829
Angalia kwa makini picha hii
Chatu kamkaba mfalme cobra huku mfalme cobra akimng'ata chatu..Nyoka wote wawili walikufa, mmoja kutokana na kukosa hewa na mwingine kutokana na sumu.
Na hivi ndivyo watu wanavyoangamizana. Urafiki huisha
uhusiano huisha
Familia huishia kuharibikiwa kwa sababu kila mmoja anataka kuwa bora kuliko mwingine.
Baadhi ya watu "hujaribu" kwa ubinafsi wao na kujiona wao ni bora kuliko wengine!.. wengine huishia kueneza sumu za ubaya na mafarakano kwa porojo, umbea,husuda, wivu, kijicho na udanganyifu hadi kuangamizana.
Chagua upendo, huruma, uaminifu, ukweli na msamaha .. Utaona faida yake kwenye maisha yako kupitia, ndugu, familia, jamaa na hata marafiki
Unaweza kuwa na kiburi na kujiamini kama nyegere lakini fanya hayo pale unapotaka kupigania heshima na ustawi wa familia, ukoo ama jamii yako