>>>>>> somo la leo <<<<<<<

Mkubya

Member
Joined
Oct 2, 2013
Posts
53
Reaction score
24
MAma mmoja yeye huamka saa kumi na moja asubuhi, akoke moto,
akande unga na kisha atengeneze chapati za kuuza. Hii ni kazi yake ya kila siku. Anti huyu amekuwa akipika chapati kwa
miaka mitano sasa.Anaziuza hivyo hivyo kwa shida, maana
kinachofuatia hapo ni kusubiri wateja, chapati moja TSH 200/=. Bahati, hapo jirani yake akahamia mdada mmoja, akawa mteja wake,
anachukua chapati mbili kila siku anaenda nazo kazini. Mara yule mdada akaanza chukua nne, mara 8 mara 10, mara
akaweka oda ya chapati 100 kila siku. Mama akawa hana jasho la
kuuza tena, yaani dada wa watu akifika tu analamba chapati 100
anasepa. Kwa vile anachukua 100, mdada akaomba awe anauziwa
moja kwa 150/=, anti akaona inalipa, anti akakubali, mdada sasa
akawa anachukua chapati 200 kila siku. Mama wa watu akaanza fuatilia kisirisiri, mdada anapeleka wapi?
Kumbe yule dada anazichukua, anaenda nunua foil, anazifunga
kwenye foil anauza Ofisini kwao na ofisi ya shosti yake jirani.
Anauza moja Mia Tano. Mama kugundua, kaanza vimba, mara ananuna nuna, mara siku
nyingine atengeneze 40 tu, mara aseme leo nnaumwa, mara leo nna
oda kubwa dadaangu siwezi kukupa, basi akendelea hivyo ili mdada
ashindwe. Mdada akamwambia anti naona mie niache tu. Anti akafurahi. Kesho
yake anti akatengeneza 200 akamtuma mtoto wake wa kike akaziuze
ktk zile ofisi mbili, unajua nini, aliuza 10 tu. Yule mdada
alishaangaliaga plan B, anachukua kwa mama mwingine, tena
anazipata kwa mia mia, sasa ana ofisi ya 3 anasaplai chapati 300 kila
asbuhi. Kwa huyu mama mwingine jiko halikuwa zuri akampa jiko zuri na hotpots.
TUJIFUNZEE HAYA

1. Ukiuza Simu yako laki, aliyenunua akaenda uza milioni, piga kimya,haikuhusu!

2. Ukiona mwenzako kafanikiwa kwa kufanya kitu fulani, usidhanie
basi nawe unaweza kufanikiwa kwa kitu kilekile kama yeye hujui nini siri ya mafanikio

3.Jifunze kutokana na mafanikio ya mwenzako sio kukasirika na
kuweka bifu

4.Dada alishuhudia mwenzake akitumia foil kuweka chapati na kuuza
ofisini yaani inavutia kununua kutokana na vifaa vinavyotumika so
ilibidi nae abadilike na kuwa kidijitali zaidi..!

add me BBM pin 7B27A314]
 
Haya namimi ntaanza kuweka kwenye foil kumbe zitauzika eeh! Loh!!
 
Naam. ni somo zuri kwa kweli....
 
Pamojaa ndugu washawash lool kwanini ww hupenda comment wa logg off after every comment nikweli ww hulogg off maana kila unapocoment atii
 
Last edited by a moderator:
Beautiful somo kwa kweli..na siku yangu ianze vyema!
Cc: mwallu
 
Last edited by a moderator:
Pamojaa ndugu
washawash lool kwanini ww hupenda comment wa
logg off after every comment nikweli ww hulogg off maana kila
unapocoment atii

ni kweli kabisa kila ninapokoment huwa...
Nalog off
 
Last edited by a moderator:
Somo zuri aisee, mama mkaanga chapati alikuwa na kijiba cha roho
 
kwelii kila mtu anapata kwa njia tofauti kwa jinsi mungu alivyompangia
 
Watu hawapendi kuona mafanikio ya wenzao sababu wana choyo...ss itabidi tujifunze....
 
Ni somo zuri kwa kweli japo limewekwa katika jukwaa la Jokes.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…