Somo kutoka ugiriki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Somo kutoka ugiriki

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Anfaal, Jun 21, 2011.

 1. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Uwezekano wa Ugiriki ku-default (kushindwa kulipa madeni yake) kwa hali ya sasa hivi unazidi kuwa mkubwa. Itakumbukwa kwamba wiki iliyopita S&P rating agent ili-dowgrade credit rating ya Ugiriki na kuifanya iwe least credit worthy country. Ugiriki ilikuwa downgraded from B to CCC. Pamoja na hatari inayoikumba Ugiriki, jumuia za kimataifa km IMF na EU zimefanya jitihada kubwa kuinusuru hali hiyo isitokee kwa masharti mbalimbali ambayo Ugiriki inatakiwa iyatimitize. Miongoni mwa mashartii hayo ni ubinafsishaji, kuongeza kodi na kupunguza matumizi ya serikali kwa hatua mbalimbali chungu zikiwemo kuzuia ongezeko la mishahara na hata kupunguza mishahara. Wananchi wa Ugiriki pamoja na vyama vya upinzani wamekuwa wakipinga hili kwa nguvu zote kwa wiki kadhaa sasa na hivyo kuifanya Jumuia ya Kimataifa kusimamisha mpango wake wa kuinusuru Ugiriki.
  Athari ipi inaweza kuletwa na Ugiriki kudefault
  Ni ukweli usiopingikia kuwa assets za ugiriki zimesambaa nchi mbalimbali kuanzia Marekani, Ulaya na hata Asia. Kwa ugiriki kushindwa kulipa deni lake kwa wakati wengine wanadhani athari yake huenda ikawa kubwa kuliko ile ya Lehman Br iliyotokea Marekani takribani miaka 3 iliyopita kwa hivyo kusababisha mtikisiko wa hali ya juu kwa sababu benki zitapata hasara kubwa na hivyo zitalazimika kujipanga upya kujiokoa na hali hiyo. Sio hivyo tu, nchi kama Hispania, Ureno na Ufaransa nazo gharama ya kukopa zitaongezeka na hivyo kufanya hali hiyo kuwa mbaya zaidi huko Ulaya.
  Options zipi zipo mezani kwa Ugiriki
  Mapendekezo yaliyopo mezani ni mawili;
  1. Aidha ugiriki ijitoe kutumia sarafu ya Euro na irejee mpango wake wa zamani wa currency yake.
  Hii inamaana nchi itakuwa na autonomy zaidi kwenye financial issues na control za investment na mambo mengine.
  2. Ni |Euro kuikoa nchi hiyo hata kama Ugiriki watashindwa kutimiza baadhi ya masharti.
  Hii itaongeza credibility ya Euro na hivyo kufanya hata zile nchi zenye hali tete kuweza kukopeshwa by virtual of European Union.
  Lakini tofauti na hivyo kuiacha Ugiriki i-default na huku ikiendelea kutumia Euro ni kusababisha contagion risk ambayo madhara yake yatakuwa makubwa zaidi.
  Kwa EAC
  Kelele za common currency zinaongezeka kila kukicha. Lakini nidhamu ya matumizi, ukwepaji kodi na udhaifu wa Taasisi wetu ni wa hali ya juu. Ni ukweli usiopingika kwamba hata swala la transparency (uwazi) kwenye mataifa haya ni wa kutilia mashaka. Kwahiyo, ukitazama mifumo yetu ya kisiasa, kiuchumi na hata kifedha, haraka ya kukimbilia kwenye common currency na hizi weak institutions hauna maana. Tunaweza kushirikiana kwa muda katika mengine wakati jitihada za kuimarisha taasisi zetu zikifanyika. Mfano rahisi; Leo hii tukisema tunaingia kwenye common currency reserves yetu ya local currency haieleweki kutokana na mfumo mbovu. Km nchi ambazo toka 1950's zimehangaika kutengeneza mfumo huu na mpaka miaka 1990's ulipoanza rasmi kutumika, zinachechemea kwa kiasi kikubwa, je sisi wenye mifumo mibovu tutafika? Mfano mwingine; Nchi zinakopa hovyohovyo mara bila kufuatwa kwa bajeti hali hii itakuwaje mbeleni?
  Kwa mtazamo wangu, tutengeneze msingi imara kwanza hasa kwenye economic na monetary policy, ndio tujiunge na mfumo wa fedha moja.
   
Loading...