mkalamo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 324
- 347
Katika Kuimarisha Ushirikiano wao wa Kijeshi,Majeshi ya India na Ugiriki Jumamosi, Septemba 16,2023 walifanya mazoezi ya Pamoja
Mpango huo wa Mazoezi ya Pamoja umelenga kustawisha ushirikiano wao wa Kijeshi kati ya Jeshi la Ugirik (Hellenic Armed Forces) ikiwa ni sehemu ya mpango wake unaohusisha mazoezi ya Pamoja (PASSEX)
Mazoezi hayo yamefanyika kwa kutumia Melivita ya jeshi la wanamaji la Ugiriki na Meli za kivita za Sumedha ya jeshi la wanamaji la India,kwenyeb ukanda wa bahari Kusini mwa mji wa Crete.
Mazoezi ya Pamoja yamezua maswali kuhusu mawasiliano, na mazoezi ya kimedani ya ndege vita ambayo yamefanyika, miongoni mwa maswali hayo ni je huo ni muendelezo wa shughuli za Pamoja za ushirikiano kati ya Ugiriki na India wanazofanya Pamoja ama kuna jambo jengine.
Hata hivyo Ushiriki wa vikosi vya anga vya India kwa mara ya kwanza vilionekana katika mazoezi ya Kimataifa ya “INHIOHOS 23” ambapo ndegevita aina ya SU-30 ilionekana kuthibitisha ukaribu wa vyombo vya Ulinzi vya mataifa hayo mawili.
Shughuli hizo za kijeshi ni muendelezo wa jitihada za kuongeza ulinzi na utayari katika makabiliano Pamoja na kuhuisha ushirikiano na maelewano kati ya washirika hao wawili kwenye eneo la mahusiano ya kijeshi kati ya Ugiriki na India.
Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app