Zanzibar siyo nchi. Haitambuliki kimataifa.
Jasusi, hawaelewi kuwa pale UN New York ipo bendera ya Tanzania na hakuna ya Zanzibar. Ni kwa muktadha huo Marekani waliona meli zenye bendera ya Tanzania na wametoa malalamiko kwa Tanzania.
Wale wanaosema kuna sheria gani imevunjwa nadhani wanapaswa kuelewa kitu kinachoitwa diplomasia.
Kuna sheria, kanuni, mikataba na maazimio. Kwahiyo kushikilia sheria gani imevunjwa ni kuangalia jambo katika mtizamo finyu sana.
Kidiplomasia waziri wa Zanzibar kulitolea kauli jambo hili ni utaratibu wa kawaida wa Wazanzibar kukurupuka bila kufahamu wanasema au wanatetea nini. Kuna waziri mmoja wa mambo ya nje wa Tanzania na hayo ya baraza la wawakilishi yanabaki kuwa mambo ya barazani kama vile tunavyojadili Simba na Yanga. Hata hivyo timu hizo pia zina bendera lakini hazina kiti wala waziri wa mambo ya nje.
Kama kuna ujinga ni pale nitakaposikia kuwa suala hili ni sehemu ya kero za muungano. Ni ujinga kwasababu kwa kutumia Tanzania Zanzibar inachangia 0% na inapata 7%. Hiyo ni pamoja na misaada na madeni.
Kwa deni la nje la nchi Zanzibar inalipa ''0'' na wala haijawahi kulalamika kuwa inakosa fursa za muungano za kulipa deni la nchi.
Lakini pia kama ni kero za muungano mbona Zanzibar haijawahi kujitokeza na kudai kuwa Gaidi la kimataifa M. Ghailani ni raia wa nchi yao? Iweje leo wasimame na kusema meli za mafuta ni za nchi yao! Kwanini Ghailan asiwe kero kwa Tanzania kama kero za meli kwa upande wao!
Na mwisho, wanaposafiri wanabeba passport za Tanzania, kwanini hilo lisiwe kero kama basi bendera na nembo ya Tanzania hawazitambui?