Someni taarifa ya Bernard Kamilius Membe

Ubabaishaji wa hali ya juu!Kwa nini usimuulize waziri mwenzako wa nchi ya Zanzibar? AG ametueleza ni nchi au siyo!Waziri wa uchukuzi na mawasiliano wa nchi hiyo amesema jambo kuhusu hilo.

Kuna laana gani imewapata. Watu waliopewa mamlaka makubwa ya kuamua mambo ya nchi yetu wamegeuka wababaishaji kiasi hiki?
Mmechokoza wakubwa kisha sasa mnaleta uswahili swahili, uyani yani,mtashughulikiwa.

Tuanawaomba wakubwa wajuwe kwamba watu hawa hatari ni ccm, magamba. Siyo Watanzania wa kawaida ila ni vibaka wa kitaifa ndiyo wanaoleta za kuletwa. Wawekeeni vikwazo vya kuja shopping ulaya na Mrekani.
 
Mkuu ina maana hata magazeti hasomi ?
"Majuto ni mjukuu"
Unafiki ni kitu kibaya sana.CCM hii na unafiki ni sehemu yao ya maisha.Madaktari wamegoma,wao wanatuonyesha bila aibu kwenye TV kwamba hakuna mgomo,Haya wameumbuliwa meli hizo,Membe anapinga wakati mwenzie wa ZNZ kakiri,Lissu kawaambia kuhusu ukweli wa Muungano leo hii hadi mwanasheria mkuu anaishia kumkejeli.haya ni mambo ya aibu sana.
Mficha maradhi kifo humuumbua.Hajui hao jamaa huwa hawakurupuki,wana kila evidence mpaka wanapofikia kuongea.wote tunakumbuka story ya Mapanki na silaha zilizokua zinakuja.
watz bado tutaona mengi na tutajuta kwa kuchezea kura zetu.Mie nasema "LIWALO NA LIWE"
 


  • [h=6]Bernard Kamilius Membe

    [/h][h=6]Serikali imepokea taarifa kuhusu tuhuma za meli za Iran kupeperusha bendera za Tanzania ili kukwepa vikwazo. Serikali ya Jamhuri ya Muungano na SMZ hazitaki kupuuza taarifa hizi. Serikali zote mbili zimeamua kufanya uchunguzi ili kuthibitisha. Tanzania imewaarifu nchi zilizolalamika marafiki kuwaomba kusaidiana nasi kufanya uchunguzi na kushirikiana kuthibitisha taarifa hii. Tumefanya hivyo kwa kuzingatia uwezo wetu wa kiutafiti na kutaka utafiti huu kuwa huru kwa kuwashirikisha wao wenye ujuzi mkubwa. Tunafanya hivyo kwa kuwa wakala wa ZMA anayefanya kazi za kusajili amekana kusajili meli za Iran, Balozi wa Iran nchini aliitwa akakanusha. Tutakapopata matokeo ya utafiti na ikithibitika kuwepo na ukweli hatua zitachukuliwa mara moja. Tukithibitisha tuhuma hizi tutafutilia mbali usajili wa meli hizo. Tunafanya hivyo kutimiza wajibu wetu kimataifa hususan Azimio 1920 la UN Security Council.Tanzani sio adui wa nchi yoyote duniani. Tunafurahia mahusiano yetu na nchi zote duniani. Hili ni jambo linalogusa maslahi ya Tanzania nje na maslahi ya Tanzania ya ndani (Muungano), tujihadhari na namna tunavyolizungumzia. Tusimame pamoja kama taifa. Nchi kwanza!
    [/h]



mmmm,membe bhana,,,,haya tumeshasoma
 
This time ccm and its government has bite something bigger than it can chew zanzibar wameshakubali na wairain mjini tuliwaona sasa mnachunguza nini mzungu hakurupuki wakuu hili wanalo na membe sijui kakanyaga mdudu gani mwaka huu huku m4c,huku lowasa na tume yake,huku mshiko wa gadafi sasa watu wazima usa,eu na wayahudi baba hutoki.
 


  • Bernard Kamilius Membe



    QUOTE]Serikali ya Jamhuri ya Muungano na SMZ hazitaki kupuuza taarifa hizi. Serikali zote mbili zimeamua kufanya uchunguzi ili kuthibitisha.
  • Tanzania imewaarifu nchi zilizolalamika marafiki kuwaomba kusaidiana nasi kufanya uchunguzi na kushirikiana kuthibitisha taarifa hii.[/QUOTE]
Mimi naona kweli kuna haja ya kuujadili huu muungani ili tujulishwe kuwa hivi ukoje. Membe anasema serikali ya Tanzania na serikali ya ZNZ. Baadae anasema serikali ya Tanzania. Hivi anamaanisha ni ipi anayoiongelea hapa?
 
Sasa anahitaji kufanya utafiti gani ili hali Zanzibar ilishakubali kwamba imesajili hizo meli? Hivi hawa watu huwa hawawezi kabisa kuwa straight katika kauli zao na kuomba radhi pale wanapokosea, isipokuwa kupindisha ukweli na kuleta blabla? Kwanini wasimtimue huyo waziri aliyehusika, waiombe radhi jumuia ya kimataifa na kufuta tu huo usajili badala ya kuanza longolongo?


Haya ni maajabu
 
Maskini Membe!!! Unachunguza nini?? Hebu muulize boss wako Kikwete aliongea nini na Makamu wa rais wa Iran (Mahammad Rahimi) alipoitembelea Tanzania tarehe 30/5/2012

542944290.jpg
 
kama serikali itafuta usajili wa meli hizi na kwa kuwa Zanzibar inapata mapato kwa kusajili meli hizi, na kwa kuwa vikwazo vilivyopo si vya Umoja wa mataifa ni vya USA na EU na ndio maana China bado inaendelea kukunua mafuta ya Irani, basi Zanzibar itabidi ilipwe fidia na aidha USA, EU au Serikali ya Muungano kwa kukosa mapato, na hili si ajabu kwa kwani USA imefanya hivyo kwa India ili isisnunue mafuta kutoka Iran ambayo walikuwa na mkataba nafuu ikilinganishwa na bei katika soko la duni. Kuwa masikini ni ghali kweli!
 
Sasa anahitaji kufanya utafiti gani ili hali Zanzibar ilishakubali kwamba imesajili hizo meli? Hivi hawa watu huwa hawawezi kabisa kuwa straight katika kauli zao na kuomba radhi pale wanapokosea, isipokuwa kupindisha ukweli na kuleta blabla? Kwanini wasimtimue huyo waziri aliyehusika, waiombe radhi jumuia ya kimataifa na kufuta tu huo usajili badala ya kuanza longolongo?
Membe wala JMT haina uwezo wa kumfukuza waziri liehusika, ni haki ya Wazanzibar kufanya hivyo. Kama tatizo bendera tutatoa tuweke ya Zanzibar. Aache kuongea pumba ''blaaa blaaaaaaaaa'',hajui wala hajielewi anasema nini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom