Somalia yapata ATM ya kwanza ya kutolea pesa

Somalia yapata ATM ya kwanza ya kutolea pesa

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,345
Reaction score
15,850
10701981_502838356520298_3969694005569073594_n.jpg

Watu katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu wameanza kutumia mtambo wa kwanza kuwahi kutumika wa kutoa pesa mjini humo.

Mtambo huo wa benki ya Salaam Somali Bank, umewekwa katika hoteli moja na tayari umeanza kutumika na kuwaruhusu wateja kutoa dola za kimarekani.

Mtambo wenyewe uko karibu na hoteli ya kifahari ya Jazeera ambayo ina ulinzi mkali sana.

Watu wengi wameshangazwa na mashine hiyo kwa kuwa hawajawahi kuiona na hata kuitumia.
Sekta ya benki nchini Somalia, bado sio thabiti huku wafanyabiashara wengi na familia zao wakitumia vijisanduku vya siri kuweka akiba zao.
Banki hiyo imesema inajiandaa kuweka mitambo mingine ya pesa mjini humo.

Wadadisi wanasema hii ni ishara kwamba mji wa Mashambulizi ya mara kwa m ara yaliyokuwa yakifanyika mjini Mogadishu yamepungua huku angalau hali ya utulivu ikianza kushuhudiwa.

Chanzo:BBC
 
niliona kipindi kimoja cha makwaiya yule wa chanel ten huko somaliland watu wakiende kubadili hela zikiwa zimejazwa kwenye toroli kama mananasi
 
kumbe awachekani na watu mbeya
Mbeya gani? ya TZ au kuna mbeya ningine. Mbeya ni sehemu za mwanzo kabisa kuwa na ATM baada ya Dar. Somalia huwezi kuilinganisha hata na Tabora sembuse mbeya?
 
SIPATI PICHA hiyo ATM ingekuwa inatoa Somalia Shillings...,

1113.jpg

20110625_MAP506.jpg

somalia-171.jpg

2.jpg

Hizo hela lazima unanunua kitu kwa kuzipima kilo sio kuhesabu. Haitawezekana!
Mfano mkate utakua labda kilo 2 ya elfu elfu, nanasi kilo 2 na nusu n.k.
Kuzihesabu kila ukinunua kitu haitawezekana. Maana kitu kama gari itakua ni figure ambayo haiko hata kwenye vocabulary ya namba!
 
Haaaahhh haaaa..!! Zimbabwe ni mashahidi wa huo mkasa
 
idoyo vipi!
Mbona unaniijia kinjenje hapa!
Au hio idoyo yako ina matatizo?

Naona umefuraahi! Dah...!

ATM yenyewe inatoa USD, haitoi pesa chafu za kisomali zisizokuwa na hadhi. Somali First ATM. sharia tupilia mbali, wameukaribisha umagharibi. haha!! yani mkipata shida makafir na teknolojia zao ndo wanawaokoa. how does that sound? inakereketa eh?
 
hii ndo faida ya kujitambua!!1
 
Mahakama ya Kadhi imeridhia hiyo makitu? au kwasababu inatoa Dollar za Marekani? Kimei hachelewi kujisogeza apeleke ATM za kutoa TSHS kuwapunguzia urasimu wasomali maana Tunao hadi kina
 
Mbeya gani? ya TZ au kuna mbeya ningine. Mbeya ni sehemu za mwanzo kabisa kuwa na ATM baada ya Dar. Somalia huwezi kuilinganisha hata na Tabora sembuse mbeya?

Tatizo majuha wengi JF wanaropoka tu bila hata kuijua wala kufika mbeya....wanafikiri mbeya sawa na Long'ido...?eti Mbeya hakuna ATM wala lift......karibuni mbeya city
 
duh watakuja ingoaaa hiyo atm qe ngojeni mtaskiaaaa
 
Mahakama ya Kadhi imeridhia hiyo makitu? au kwasababu inatoa Dollar za Marekani? Kimei hachelewi kujisogeza apeleke ATM za kutoa TSHS kuwapunguzia urasimu wasomali maana Tunao hadi kina

maliziaaa mkuu pugilia msumari hadi mwisho
 
Back
Top Bottom