Soma ujifunze: Jinsi kijiwe changu kilivyosababisha mtu akalizwa 2M na tapeli leo

Sifa kubwa ya tapeli ni kukufanya umuamini

Ukishamuamini, umekwisha

Kuna jamaa mmoja from nowhere alifika kwenye mji/nyumbani kwa mtu na kilo ya steki ya nyama, akawaambia watoto (bahati mbaya na mke hakuwepo) kuwa ametumwa na baba "ile" redio kubwa ili aipeleke kwa fundi, baada ya kuona mboga watoto wakamuamini tapeli kuwa kweli ametumwa na mdingi wakampatia redio

Yule tapeli aliondoka na redio mpaka kesho hakurudi

Alinunua music system kubwa kwa kilo moja ya stake ya nyama

Kuna la kujifunza hapa
Nyama ni msala kudadeki!😁😁😁😁
Unataka dem akubali mpeleke akale nyama,
Unataka bodaboda ya bei chee unaaagiza nyama!🙌🙌🙌
 
Wakuu habarini za Mda Huu, Nina Kisa kimoja leo kama mnavyojua baada ya kumaliza Chuo Basi tunavyosubiri milioni Basi tunatafuta Buku.

Jana majira ya saa 4 Asubuhi nikiwa katika kijiwe changu cha kuchimba mchanga mgumu alitokea mteja mmoja aliyekua kavalia nadhifu sana akiwa ameshuka bodaboda kama abiria, kutokana na njaa niliyonayo ilibidi nimfate haraka nikijua labda Ni boss anaejenga apartment hapa mjini Basi amekuja kuchukua mchanga angalau trip 10.

Nikweli niliongeanae akasema anataka mchanga trip 4, na Bahati Nzuri kulikua na gari kubwa inamaliza kubeba mchanga trip ya mwisho Basi wakakubaliana na dereva ambebee mchanga wake Huku Mimi nikiongezewa dau toka 60000-70000 kwa trip.

Vijana walianza kupakia mchanga kwa kasi sana, Huku boss akiwa pembeni Kuna bucha akiagiza Nyama kg1 na baada ya hapo alimuomba pikipiki yule boda aliyekuja nae( ambae walionekana kuchangamkiana) Ili boss apeleke mboga nyumbani fasta sana Huku akidai atest isije ikawa kasahau kuendeshea.

Vijana wa kazi walimaliza kazi Huku tukimsubiri boss apande mbele Ili Twende location turudi kupakia tena, tulisubiri kwa Nusu saa Hakuna mtu, tukasema labda anasubr iive ale lakini mbaka sa 6 Hakuna mtu, tukamuuliza dereva boda kwani ulimtoa wapi huyo mtu, akadai walijuana Jana yake na alimtembeza Jana yake kutwa Huku akiwekewa mafuta ya 30,000.

Tulimuiliza unakujua kwake? Alijibu nilimpeleka sehem akanionyesha nyumba yake kwa mbali, tulimwambia aende lakini ALIPEWA JIBU kua hawamjui mtu huyo. Kijana alianza kuona mkojo unauma, kiungwana nilimuonesha choo.

ALISEMA amenunua pikipiki shilingi milioni 2 na Laki 3, wiki iliyopita, alionekana kuchanganyikiwa sana, Kuna mengi ya kujifunza. Kuhusu mchanga ilibidi tupeleke sehemu Yakwanza Huku bei ikishuka hadi 50,000.

Wanajf, usimuamini mtu KIZEMBE KIZEMBE. Bola Wali Nyama kuliko Walimwengu.
Karibuni kwa mchanga mgumu songea.

0738853634
Chai
 
Back
Top Bottom