Soma then chukua hatua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Soma then chukua hatua

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mess, Sep 24, 2012.

 1. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mwanzoni mwa mwezi huu kuna jamaa alitoka kwenye mizunguko yake ya maisha (anakaa majohe kwa mkolemba) alipofika pale kwa mkolemba alikodi piki piki na yule dereva wa piki piki alimbeba na kumfikisha nyumbani kwake. Yule bwana kwa bahati mbaya hakuwa na change akamwambia mwendesha piki piki kuwa shemeji yako anaoga karibu ndani umsubiri tukulipe, yule bwana wa piki piki akaondoka na alipofika kijiweni akawaambia wenzake kuwa nilitaka kupolwa piki piki ila alieleza jinsi mkasa huo ulivyotokea.

  Hamadi yule bwana alikuwa na piki piki yake na akawa ameongea na mkewe kuwa twende pale kuna mtu wa piki piki aliyenileta sikumlipa tukamlipe ile kabla hajafika vizuri yule dogo akasema mwizi wa piki piki huyu hapa jamani ni kuwa yule mtu walimpiga kweli na sidhani kama alipona. Mimi nilifika baadae hapo nikawauliza watu wa piki piki nikaona kama kila mtu anakimbia kuongelea lile swala kama vile waliona kuwa walifanya kosa. Lakini mke wa yule bwana alitoa maelezo mazuri sana. Polisi walipokuja waliambiwa kuna mwizi wa piki piki kapigwa pale walifika wakachukua mwili bila kuhoji watu wa piki piki, kama waliwahoji basi itakuwa siku nyingine ambayo haikuwa ile.

  My take: Serikali iliangalie sana hili kundi la waendesha piki piki na wapewe mafunzo jinsi ya kutenda kazi yao, na polisi wakifika wawashike watu ambao wanaweza saidia upelelezi, mara nyingi tumeona polisi wakiambiwa mwizi huwa hawahangaiki kuchukua malelezo.
   
 2. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,736
  Likes Received: 1,448
  Trophy Points: 280
  Duh poleni sana. Ni mkasa wa kusikitisha sana! Jamaa tumwombee apone haraka andelee na mapambano ya maisha.

  Naunga mkono ushauri wako kuwa Polisi wafanye kazi waliyoundwa kuifanya sio mambo ya siasa mbuzi.
   
 3. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha, hivi vyama vya piki piki ni hatari sana. Vijana wanajifunza leo na leo wanabeba abiria ni mara nyingi wameponea mikononi mwangu kwa huruma tu wanapokuwa wana overtake maana ni kushoto na kulia kote wanapita
   
 4. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  kwa kweli inasikitisha sana, hawa wadudu ni hatari sana, inakuwa vigumu kuwadhibiti kwa kuwa wanatumika kisiasa pia.
   
 5. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  He wanatumikaje kisiasa ebu nijuze
   
 6. Mpigania Uhuru

  Mpigania Uhuru Member

  #6
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kuna kisa Kama hiki kimetokea takribani miezi 2 Bunju A eneo la Burumawe.
  Stori he yenyewe ni kuwa kuna mtu anamiliki eneo zaidi ya ekari moja maeneo hayo, kuna barabara kubwa ya Magari inapita katikati ya shamba lake. Waendesha pikipiki NA waenda Kwa miguu wakatengeneza njia nyingine ya short cut kwenye hilo shamba.
  Mama mwenye shamba kuona hivyo akamtuma ndugu yake NA watoto wawili waje waje wakazibe ile njia isiyo rasmi. Ilipfika jioni mwendesha pikipiki mmoja alijaribu kupita pale akakuta njia imezibwa Kwa kuchimba mtaro, NA jamaa yukon maeneo ya pale shambani, alichofanya ni kukimbia mbalimbali kidogo NA kuwapigia simu wenzake kuwa kuna wezi wa pikipiki kwenye lile shamba. Walichofanya walimvamia Yule bwana wakampiga NA lile jembe hadi wakamwua hapohapo, wakamtoboa NA macho .wale watoto aliokuwa nao walijeruhiwa vibaya sana NA bisibisi ingawa Kwa habari nilizokuwa nazo bado wanauguza majeraha. Waendesha pikipiki mpaka sasa hakuna aliechukuliwa hatua Kwa kisingizio mpelelezi wa kesi naye ni mgonjwa ameenda India Kwa matibabu!
   
 7. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Hii inasikitisha sijui ni nani atakuja kugeuza mwenendo wa Tanzania ilipofikia kurudi kwenye njia. Sasa imefikia mwenye haki ndiye anakatishwa maisha na mwenye makosa anazidi kutesa. Kwa kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa mara zote sasa imekuwa ndiyo njia ya wavunja amani kuendelea kujinufaisha.

  Hili siyo tu suala la serikali lakini pia jamii nzima inahitaji kuangalia sana mustakabli wa namna ya kusadia kutoa ukweli pale matatizo kama haya yanapotokea. Tatizo letu hata ushahidi nao tunaogopa kutoa sijui ni kwa sababu hizo hizo za kuhofia usalama au basi tu siyo hulka yetu kudai haki zetu.
   
 8. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Hapa Arusha pale Hospitali ya Mount Meru wana ward yao inaitwa TOYO WARD!
   
 9. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Elimu ndogo ya waendesha pikipiki ndio inapelekea mauaji yasiyo ya lazima.
   
 10. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  So sad! Ugua pole jombaa
   
Loading...