Napendekeza kwa mazingira mengine Polisi wafanye kazi kwa kuzingatia muktadha tukio kuliko kufuata protokali

Candela

JF-Expert Member
Aug 12, 2021
748
1,937
Linapotokea tukio mtu kauwawa mara nyingi tunaita polisi wachukue mwili, lakini pia inapotokea mtu kajiua tunawaita polisi. Kuna ile mtu kajiua kwa sumu au kujinyonga ndani kwake, nitolee mfano tukio lililotokea mtaani.

Polisi walijulishwa kuwa kuna mtu kanywa sumu, wakafika eneo la tukio na kusimama nje kuzuia watu wasisogee bila hata kuingia ndani ya ile nyumba. Wakakaa pale wakisema wanasubiri utaratibu wabebe mwili.

Mpaka alipofika swaiba wa mhanga akauliza kama wamemuona jamaa wakasema asubiri jamaa akafosi kungia ndani kukuta mhanga hajakata roho ndio yupo tulii lakini hajafa bado.

Ndio kutoka kuwaambia polisi jamaa anapumua wakamkimbiza hospitali na polisi walifika pale takribani dakika 45 kabla ya jamaa. Kwa hiyo kama jamaa asingefika mhanga angekufa.

Chanzo cha yule bwana kunywa sumu ni kuwa alikopa pesa bank akaenda nazo home akamwonesha mkewe, takribani milion 35. Asubuhi akiwa kazini akapigiwa simu na jirani mtoto analia ndani mda mrefu na geti limefungwa, ikabidi arudi akakuta mkewe hayupo kasepa na hela zote.

Jamaa alipona na sasa anaishi na mkewe baada ya kufatiliwa walimpata akiwa ameshatumia milioni 5 ndani ya wiki 1.

KALULU THE HARE
 
Duh mke huyo huyo Jambazi?

Hlf unakopaje Hela unakomba yote kwenye akaunti na kwenda nazo nyumbani kwako?
 
Mbona naona kama ni uzembe mkubwa wa karne? Yaani polisi walipofika eneo la tukio wakasimama nje bila kuangalia hali ya aliyekunywa sumu? Walikuwa wanasubiri nini? Naona kama kawaida ya wabongo, watu wamekimbilia kujadili ni kwa nini kanywa sumu badala ya kujadili jinsi polisi walizembea.
 
Aliyeanza uzembe ni aliyeenda kutoa taarifa polisi binafsi najua alianza kumuona muhanga kwanza Kisha ndio akaenda polisi,je alisemaje kule maana kama ni interval ya dk 45 mpaka jamaa aje basi polisi waliitwa mapema zaidi na yule mjumbe aliingia mapema zaidi na kuona jamaa kanywa Sumu kwa Nini hakupendekeza waende hospital ye akawaza police!?
Vituko mtaani
 
Wabongo maisha yetu tunaishi kimungumungu na kubahatishabahatisha. Kila kitu tunafanya na kuchukulia kimzaha. Hatujali katiba ya nchi, sheria za nchi, utaratabi. Hata kunya tu hatunyi ipasavyo.
 
Imejini unakunya choo cha shimo na umeziba pua...je yataisha au utakatisha😂😂
 
Polisi hawatakagi shida ya kuandika majalada , hata mkiwaitia mwizi wanachelewa ili mumuue kabisa.
Hapo ukute walikuwa wanavuta muda jamaa afe wachukue mzoga.
 
Aliyeanza uzembe ni aliyeenda kutoa taarifa polisi binafsi najua alianza kumuona muhanga kwanza Kisha ndio akaenda polisi,je alisemaje kule maana kama ni interval ya dk 45 mpaka jamaa aje basi polisi waliitwa mapema zaidi na yule mjumbe aliingia mapema zaidi na kuona jamaa kanywa Sumu kwa Nini hakupendekeza waende hospital ye akawaza police!?
Vituko mtaani
Haya tuchukulie walifanya makosa! Je, inahalalisha jeshi la polisi lenye utaalam wa ku deal na mambo kama hayo kufanya ujinga waliofanya? najua kazi ya jeshi la polisi wewe? Vituko kwenye JF!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom