Soma kama utaipenda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Soma kama utaipenda

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Viol, Jun 2, 2012.

 1. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Bado sijajua niiteje title yake.
  Ni ndefu kiasi,But nahitaji mawazo yenu na kunirekebisha kwa wale ambao hawataboreka kusoma.hii ni sehemu ndogo tu.(najaribu kuweka paragraphs ila zimegoma.  David alikuwa ameshakosa hamu ya maisha ya pale mtaani kwao,maisha yake yamebaki ya tabu na matatizo,familia ya kimasikini,kila siku kutatua matatizo,kwake shida zilikuwa kama za karne na mda wa furaha hauwezi kuzidi sekunde mbili,kila saa aliwaza amemkosea nini Mungu?tangu azaliwe hamfahamu baba yake ila alisikia tu kwamba anachimba madini Geita,kwahiyo yeye alikuwa anahusika kwa kila majukumu nyumbani,kulisha familia na kumsaidia mama kwa kila jambo na kusomesha wadogo zake wawili wanaosoma shule ya sekondari.Mtaani kwao kila kijana alikuwa na usafiri wake na amejenga nyumba yake,vijana wanabadilisha mavazi na ratiba za kubadili chakula.Akiwa njiani akitoka kwenye kibarua kuelekea nyumbani mawazo mengi yalimjia akilini,akili yake ilinaswa na fikra tofauti kwa wakati mmoja mithili ya nzi aliyejiingiza kwenye mtego wa buibui na kusubiri maamuzi ya hukumu kali kutoka kwa buibui,mawazo yake yalijikita jinsi ya kujikwamua na magumu ya maisha ili aingie kwenye ulimwengu ambao hauna bughda,ulimwengu wa kushika uma mkono wa kushoto na kisu mkono wa kulia kisha ukate kuku vipande vidogo vidogo na kupeleka mdomoni,ulimwengu ambao utafanya moyo wake uwe na paradiso yenye furaha na vigelegele vya furaha,ulimwengu ambao usafiri upo mbele ya hekalu lake iliyojengwa na vigae vya gharama,ulimwengu ambao wadogo zake wawili watakuwa wamevaa sare nadhifu na wanafundishwa na mwalimu aliyefuzu viwango vyote vya taaluma ya ualimu.Hayo ndo mawazo yaliyokuwa akilini mwake huku akielekea nyumbani,huku akikumbuka kisingizio alichosingiziwa kuwa aliiba kitabu cha Physics alipokuwa kidato cha tatu kisha sheria kali ya hiyo seminary ikayakata ndoto zake mithili ya msemeno ukatavyo mbao,alimua akifika nyumbani itabidi aende baa kwa mzee Urasa ili ayatulize mawazo kwa bia mbili,kabla mtitiririko wa mawazo haujakatika akajikuta ameshafika nyumbani,akahifadhi vifaa vya kazi,halafu akachukua maji na kuelekea bafuni ili apunguze jasho ambalo lilifanya shati lake jeupe lionekani kaki,akaoga kisha akabadili nguo na kuelekea kwa mzee kupata bia kwa mzee Urasa kama kikao cha akili yake ilivyopanga tangu akiwa njiani kuelekea nyumbani.
  Alipofika kwa mzee Urasa akaanza akaigiza safari,baada ya mda akaagiza tena safari ya pili.Kabla hajafungua bia akaingia kijana aliyeitwa Luis,huwa wanaonana tu ila hawakuwa na mazoea ya kuongea,Luis akaagiza bia na kukaa kwenye meza aliyokaa David,kisha akaanza kumsemesha David "Ee bhana mi na wewe huwa tunaonana ila huwa hatuzungumzi sijui inakwaje,haya majukumu yamezidi au?(huku akinywa bia taratibu),David "aisee shughuli zimezidi na haituingizii hata kipato,ila mda wenyewe ndo huu leo tumekaa chini".David akaona bia lake linaisha na mazungumzo yananoga,akajikagua mifuko yake ya suruali ila hakuambulia kitu akakuta amebakiwa na shilingi mia mbili tu mfukoni,Luis akaelewa kwamba David ameshaishiwa na hela,akamwambia aagize bia mpaka watakapoona wamelewa na atalipa kila kitu.Mda ukaenda na pale baa wakabakia wachache kila watu na meza yao wakiongea mambo yao,Luis akaanza kumshawishi David ""hela haitafutwi tu kuna njia zake,usione nina magari mawili na nyumba nzuri,kuna njia rahisi nakusaidia kama mtu wangu niliyesoma naye shule moja ya msingi,nitakupeleka kwa jamaa yangu flani,kwake Tanga ila kwa sasa tutamfuata Njiro kule Arusha maana yupo kule kikazi,upo tayari twende lini?David akaitikia kwa hamasa kubwa,twende hii jumamosi"basi wakaamua hiyo jumamosi kuanzia safari toka Manyoni Singida kuelekea Arusha.
  Ikafika jumamosi wakapanda basi kuelekea arusha,wakafika jioni nakuchukua text ya moja kwa moja mpaka kwa Njiro Amashi.
  Walipofika walikaribishwa na Mzee Amashi,Mzee Amashi alikuwa na walinzi wake wanne wamekaa sebuleni,akawaambia waondoke ili apate mda wa kuongea na wageni,walinzi wakatoka.Mzee Amashi akaanza kuongea kwa kujiamini"Kijana nadhani we ndo David na nimepata habari zako kutoka kwa Luis,nimesikitika sana kuona kijana mdogo kama wewe maisha yamekuchakaza mpaka unaonekana kama mzee,tatizo vijana wa siku hizi hamtafuti wazee wenu wanaojua maisha na jinsi ya kufanya maisha yapendeze,maisha yanapendeza,usione watu wana magorofa na magari,makampuni na uongozi wa ngazi za juu,walitufuata sisi na kutuheshimu,na ukitudharau utateketea kama kama nyasi kavu iliyomwagiwa petroli na kisha ikagusishwa kwa mwali wa moto,....Luis ebu tupishe niongee vizuri na kijana"Luis anatoka,mzee Amashi anaendelea kuongeana na David"Sikia kijana,masharti ni madogo tu,unakubali unataka uendelee kukaa kwenye lindi la uonevu wa umaskini au unataka nyota yako ing'are?upo tayari kwa masharti yangu marahisi?"david anaitikia kwa nguvu"nipo tayari kwa masharti.Mzee Amashi anaendelea,"haya piga magoti,shika huu mkaa,toa chochote ulichonacho mfukoni,ukibakiza utakuwa umeshaanza kuvunja masharti"David moyo unamdunda nakusema"mzee ila si nitabakiza nauli ya kurudi"nimesema usibakize kitu"Daudi anatoa kila kitu huku akiwaza labda atasaidiwa na Luis hela ya Nauli"mzee anaendelea "haya chukua hizo hela sakafuni uweke mwenyewe kwenye hii kofia langu"David anafanya kama alivyoagizwa.Mzee Amashi anaendelea "Haya toka kinyume nyume mpaka nje ya mlango,usiangalie nyuma,Nenda mpaka nje ya geti ukiona tu kuna kitu inakuja usitoke barabarani,usikwepe wala kukimbia,utakuwa umevunja masharti yangu, huo ndo usafiri utakurudisha mpaka nyumbani,ukifika nyumba ile unafika mlangoni utakachokutana nacho mlangoni ndo sadaka yangu halafu uniletee baada ya wiki mbili,bila kutii masharti yangu lazima ufe baada ya siku saba.
  Ile anatoka tu nje ya geti mara basi linakuja kwa kasi huku likipiga honi,akaanza kuwaza akwepe au ndo usafiri alioambiwa,hapo hapo anajiuliza je asipokwepa atapona?
  Akafumba macho huku basi linakuja kwa kasi likipiga honi,akavumilia agongwe,mara akashangaa alibebwa na upendo na ndani ya nusu saa akafika singida bila kufahamu Luis alimwacha wapi,ili tu anafika mlangoni akapokewa na mama yake,moyo ukamdunda kama tenesi,akakumbuka masharti aliyopewa kuwa chochote utakachokutana nacho mlangoni unapofika ndo sadaka na baada ya wiki mbili apeleke kwa mganga kafara itolewe.
  Wiki ya kwanza iliisha akiwa na huzuni kubwa,huku akiwa jinsi ya kumpeleka mama yake kwa huyo mganga.Akapanga namna ya kumdanganya mama yake ili aanze safari ya kumpeleka kwa mganga,siku moja asubuhi akaamka mapema na kufuata mama na kupeana salamu za asubuhi kisha akaanza "mama nilipokuwa arusha nilipata daktari wa kukutibia ugonjwa wako wa vidonda vya tumbo,ni daktari wa miti shamba na madawa ya asili,kwahiyo wiki ijayo tuanzee safari ya kuelekea Arusha maana mwezi ujao ataelekea Zambia kwahiyo tukichelewa ndo utakuwa umekosa matibabu"Mama alifurahi kweli na bila kusita akaanza kufanya maandalizi ya safari.
  Hatimaye wiki iliyofuata wakaanza safari,wakafika arusha usiku sana mana gari liliharibika njiani,ikabidi walale mjini,asubuhi wakapanda daladala kuelekea njiro.Kama kawaida walipofika walikaribishwa,wakaka sebuleni,Mzee Amashi akamwambia David atoke nje,David akatoka nje na kukaa kwenye kiti ambacho ilikuwa pale nje,mara akamwona mzee Amashi naye anatoka nje nakumwambia mlinzi"fanya haraka,fanya kama siku zote",kisha akafunga mlango na kurudi ndani,Mara mlizi akatoka kwenye chumba chake ndogo cha ulizi akiwa na panga lililonolewa na ina makali kisha akaelekea kule kwa mzee Amashi na Mama yake David,akafungua mlango na kuufunga kwa nguvu,baada ya dakika 10 David akiwa kwenye mawazo alisikia sauti ikisikika kwa nguvu ikisema " mwanangu unanifanyia nini mama yako,nimekusamehe"
   
 2. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,995
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda,coz inafundisha tabia flani hv,
  ila mbona naona kama dublebuble hapo mwishoni mwishoni?
   
 3. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,341
  Likes Received: 2,669
  Trophy Points: 280
  Stori nzuri lakini hujatupa mustakabali wa David, je alifanikiwa au?
   
 4. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Labda ni Part 1 halafu atakuja na part 11.

  Kichwa cha habari napendekeza kiwe hadithi hadithi, hadithi njoo uongo njoo utamu kolea Part 1.

  Ni stori nzuri sana ila umalizie jinsi ilivyokuwa.
   
 5. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,858
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  very interesting, ila nimefka katkat macho yananiwasha ntarudi baadae!
   
 6. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Mh hii inahitaji budget yake ya muda...ngoja niianze kusoma upya
   
 7. Good Guy

  Good Guy JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 4,511
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  mkuu kwenye fani ya uandishi umebobea (japo sehem chache zimekosewa ila hizo ni kaz za editor) big up saana 2nataka partII aisee ishanoga
   
 8. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,118
  Likes Received: 1,745
  Trophy Points: 280
  Ebana dah,kama muvi vile! Unaweza bana,ni makosa madogo tu ukirekebisha hayo,utatisha mbaya! Big up!
   
 9. CUTE

  CUTE JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 1,237
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  story nzur sana but hujamalizia juu ya devid
   
 10. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Asante kwa funzo, tusitamani vya watu, hatujui wamevipataje?
   
Loading...