Solo Thang: Tuzidi kumuombea Chid Benz

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,823
2,000
Rapa Solo Thang ameposti video akiwa na Rapa Chid Benz ambaye walikutana usiku na kuongea baadhi ya mambo, lakini kutokana na hali aliyokuwa nayo Chid Benz Solo Thang alisema hawezi kumuhukumu bali anastahili kuombewa tu.
Chid%20Benz%20.jpg

Rapa Chid Benz

Katika ujumbe ambao Solo Thang aliandika kwenye mtandao wake wa Instgram alisema hawezi kuhukumu na hata iweje bado Chid Benz ataendelea kuwa mdogo wake, rafiki yake na mtu wake wa karibu.

"Met with my Young brother Chid Benz last night almost cried, I dont judge, no matter what still my hommie, tumeongea sana, tuzidi kumuombea Mola" aliandika Solo Thang

Tazama video hii ikimuonyesha Rapa Chid Benz akiwa na Solo Thang
 

Guasa Amboni

JF-Expert Member
Aug 13, 2015
8,494
2,000
Kusema aombewe tu bila huyo anaesema tumuombee angeonyesha njia kwanza kwa kumpeleka sehemu husika kisha ndio atoe ombi hilo vinginevyo haileti maana . Kifupi inaumiza watu sababu CHID ni maarufu lakini kuna malaki mangapi kama CHID ila wenyewe hawana ujulikano kitaifa ambao wametumbukia penye janga hili ?
 

Mr.Wenger

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
1,905
2,000
Dah nakumbuka Chidi wakati anatoka ghafla tu akapewa tuzo ya Mwanahiphop bora huku akiwa na ngoma mbili tu moja kamshirikisha matonya mpenzi usinipe lawama na nyingine Chidi soo akiwa na Klyn wabongo walinung'unika sana Chid kupewa ile tuzo maana wengi walikuwa hawamfahamu. Ikabidi Chidi awajibu kwa kurelease bonge la ngoma "MMENISOMA"
 

Guasa Amboni

JF-Expert Member
Aug 13, 2015
8,494
2,000
Dah nakumbuka Chidi wakati anatoka ghafla tu akapewa tuzo ya Mwanahiphop bora huku akiwa na ngoma mbili tu moja kamshirikisha matonya mpenzi usinipe lawama na nyingine Chidi soo akiwa na Klyn wabongo walinung'unika sana Chid kupewa ile tuzo maana wengi walikuwa hawamfahamu. Ikabidi Chidi awajibu kwa kurelease bonge la ngoma "MMENISOMA"
Yaah ! kweli TUMEMSOMA
 

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,710
2,000
Aiseee yani huyu wamebaki kumzika tuu ana hali mabaya sana na wanao weza kumsaidia kwa sasa ni ndugu zake tuu,....
 

thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,526
2,000
Watafuta kiki wakina babu tale wameamua kumuacha jamaa. Walimtoa rehab baada ya mwezi huku msimamizi wa kituo alisema mwezi mmoja hautoshi walau akae hata miezi 6. Pole sana chidi benz, mkono mfururu yaani pahpahpah wamekaa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom