Solo Thang: Nakupenda ila hujatulia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Solo Thang: Nakupenda ila hujatulia

Discussion in 'Entertainment' started by Obi, Jun 15, 2011.

 1. Obi

  Obi JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 376
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Kweli huyu jamaa anafikiria sana. Anajua anachokifanya. Kwenye wimbo huu anamsifia Miss Tanzania (Nchi ya Tanzania). Anasema kuwa anampenda sana Miss Tanzania ila Miss mwenyewe hajatulia. Ameacha viungo vyake wazi (Rasilimali za Nchi) vinashikwa na kila mtu (Mafisadi).
  Jamaa amejitahidi sana. Keep up Man
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hakuna S bila O L bila O! hata mimi namkubali sana tokea ile single yake aliyoimba na Afande Sele '' Ni MATAZAMO"
  [​IMG]
   
 3. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Dah jamaa yuko juu sana,message ya maana.
   
 4. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa ni noma,anaimba vizuri sana.Hivi kwa sasa SOLO THANG yopo wapi.Aliimba vizuri sana single ya mtazamo.
   
 5. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kabla ya single ya mtazamo alikuwa ameimba nyimbo nyingi kama vile Homaya dunia,kipaji changu e.t.c.
   
 6. Obi

  Obi JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 376
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nafikiri yupo Dublin kama sijakosea.
   
 7. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Solo Thang - Miss Tanzania - Hulk Share - Music Distribution Platform

  MISS TANZANIA
  verse 1

  BABA YAKE ALIKUA MKOLONI KIPINDI HUYU MISS MWALI
  MCHONGA ALIKATA UTEPE LAKINI HAKUVINJARI
  SABABU ALIKUA BUSY KUMLINDA NA GETI KALI
  KUMBE WENZAKE WANABINJUKA KUSHTUKA AKAKAA MBALI
  DEMU ALIKUA NA HESHIMA KABLA HAIJATANGWAZWA RUKHSA
  CHUKUA CHAKO MAPEMA UKIMKONYEZA TU UMEGUSA
  ANA KIFUA KIMEBETUKA SIO MAZIWA NI MADINI
  KAYAACHA WAZI WATU WANASHIKA HAPO NDIO ANAPONIUDHI MIMI
  WATU WANAGONGA TU IKULU TENA KWA MITINDO HURU
  KAVU KAVU BILA KINGA HAJALI VINAVYODHURU
  KAWA SHANGINGI NA AMEDATA HANA UWOGA WA KUNGURU
  ANAPENDA SANA CHAPAA HAIMTOSHI KODI NA USHURU
  ANA KIJUNGU MATATA LAINI KAMA NYANYA MASALO
  ANATINGISHA AFRIKA NZIMA NA MZIGO KILIMANJARO
  USIMCHEZEE KWA VIDANI SIO PETE SIO HERENI
  ANAMILIKI TANZANITE KAMA ARDHI YA MERERANI
  SURA DHAHABU INAITA KAMA AMEZALIWA GEITA
  TATIZO NDIO KICHECHE KILA MWANAUME NDIO AMEPITA
  HATA BENJA HAKUTOKA KAPA HUYU DEMU HAJATULIA
  KAMA RUSHWA NDIO KIKWAPA ANANUKA NA KUNUKIA

  CHORUS

  MISS TANZANIAAAA
  Nakupenda ila hujatuliaa
  Vitendo vyako sitojivunia
  Sifa yako kubwa umefulia
  MISS TANZANIA
  VERSE 2
  BORA ANGEBAKI KUWA MODO KAMA FLAVIAN MATATA
  ILA DEMU AMEJIACHIA KISA ANAENDEKEZA BATA
  SITACHOKA KUWAKILISHA JINSI ANAVYONIACHA HOI
  JUZI JUZI KAOPOLEWA NA HANDSOME BOY
  KABLA HAPO SHOGA ZAKE WOTE KASHAWAONA MABWEGE
  SABABU HAWANA DIRA NA YEYE AMESHAHONGWA NDEGE
  ANAFAA KUA MISS DUNIA MAANDALIZI LONGOLONGO
  TATIZO ANAKULA SANA AKIJAMBA NI SONGOSONGO
  MARA GHAFLA KANENEPA KUMBE MIMBA B.O.T
  KUMBE DEMU ALIGAWA EPA WATU WAMEPIGA HAFU JII
  ALIZUGWA NA AKAUNT HEWA KUWADI BWANA BILAL
  MARA MDOMO NAE KAZIMWA BILA HATA PICHA YA KABURI
  KINACHOMPONZA HUYU SHAWTY UTULIVU SIFURI
  ILA HAKUNA ANAEPINGA KWAMBA HUYU DEMU NI MZURI
  MIXER SIASA NA BIASHARA DEMU AMESHAKUA CHOTARA
  MISHE ZA DAR AKIMALIZA MJENGONI ANAKWENDA LALA
  KADRI MIAKA INAVYOKWENDA DEMU ANAZIDI FULIA
  KUMBE WEUPE NI MKOROGO ONA MWILI SASA UMEFIFIA
  DEMU KAZIDI UMALAYA WACHA MABWANA WAMTEME
  HAOGOPI KULIWA MTUNGO KISA NAGAWA UMEME


  VERSE 3

  WADAKU WALISHAMFUMA ANAKULA DENDA NA RICHMOND
  DOWANS AKAZIDI KETE AKAMVISHA PETE YA DIAMOND
  BINTI MASKINI AKANASA BWANA MSHENGA NDIO LOWASA
  SHEMEJI HATAKI HATA PICHA NDIO TABIA GANI SASA
  NDOA ILIFUNGWA KWA VIFIJO VIGOGO WAKALA PIZA
  KEKI NZIMA WALE WAO SHARE YETU SI NI GIZA
  SIO HAYO DEMU ANA MENGI YA KUCHUKIZA
  MALI GHAFI ASHAZINADI FORSALE ANAJIUZA
  MTAANI ILIVUMA RUMOR DEMU KAWA MAMA HURUMA
  UCHUMI UMEFUNGWA DRIP MAEMDELEO NDIO KALI HOMA
  MALI ASILI NDIO KITASA KILA UFUNGO NDIO UNAPITA
  TOKA ALIPOVUNJA UNGO NUSU KARNE IMESHAPITA
  MAPENZI KAFANYA MRADI ANAMEGWA NA MAFISADI
  AMANI KWA TIME BOMB BINTI AMEKUMBATIA RADI
  VITENDO VYAKE VIBAYA VINAFANYA ADHARAULIKE
  TABIA KATIBA SIO MSAHAFU NDIO USEME ISIBADILIKE
  MIKOSI INAYOMKUTA NDIO KWANZA ANATABASAM
  HAJALI WALIOMZUNGUKA KAMA NAO BINAADAM
  MBAGALA WALIMBAKA MPAKA AKAMWAGA DAMU
  NA JUZI GONGO LA MBOTO KAANZA KUJAMBA MABOMU

  Kwa hisani ya : SOLO THANG "I AM TRAVELLAH": MISS TANZANIA LYRICS!!!!
   
 8. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  JF inakupenda ila haujatulia
   
 9. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Solo Thang ametoa bonge la song linaloielezea Tanzania!!!
  Huu ni wimbo wa kisiasa na umekaa kisiasa ndo maana nimeuweka hapa japo katumia lugha ya picha!!!!

  tazama hii video
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  niice....
   
 11. Fred Katulanda

  Fred Katulanda Verified User

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Angalia Video ya Wimbo huu usikie mabeti yake haya

  http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=plDLceKKPco


  Ila kwa wale wasioweza kufungua video kwa simu....mashairi yake haya hapa:

  "[Ubeti wa Kwanza]
  Baba yake alikuwa mkoloni kipindi huyu Miss mwali
  Mchonga alikata utepe lakini hakuvinjari
  Sababu alikua busy kumlinda na geti kali
  Kumbe wenzake wanabinjuka, kushtuka akakaa mbali
  Demu alikua na heshima kabla haijatangazwa Rukhsa
  Chukua Chako Mapema ukimkonyeza tu umegusa
  Ana kifua kimebetuka sio maziwa ni madini
  Kayaacha wazi, watu wanashika hapo ndio anaponiudhi mimi
  Watu wanagonga tu Ikulu tena kwa mitindo huru
  Kavu kavu bila kinga hajali vinavyodhuru
  Kawa shangingi na amedata hana uwoga wa kunguru
  Anapenda sana chapaa haimtoshi kodi na ushuru
  Ana kijungu matata laini kama nyanya masalo
  Anatingisha Afrika nzima na mzigo Kilimanjaro
  Usimchezee kwa vidani sio pete sio hereni
  Anamiliki tanzanite kama ardhi ya Mererani
  Sura dhahabu inaita kama amezaliwa Geita
  Tatizo ndio kicheche kila mwanaume ndio amepita
  Hata Benja hakutoka Kapa huyu demu hajatulia
  Kama rushwa ndio kikwapa ananuka na kunukia
  [Kiitikio]
  Miss Tanzania
  Nakupenda ila hujatuliaa
  Vitendo vyako sitojivunia
  Sifa yako kubwa umefulia
  Miss Tanzania
  [Ubeti wa Pili]
  Bora angebaki kuwa modo kama Flavian Matata
  Ila demu amejiachia kisa anaendekeza bata
  Sitachoka kuwakilisha jinsi anavyoniacha hoi
  Juzi juzi kaopolewa na Handsome Boy
  Kabla hapo shoga zake wote kashawaona mabwege
  Sababu hawana dira na yeye ameshahongwa ndege
  Anafaa kuwa Miss Dunia maandalizi longolongo
  Tatizo anakula sana akijamba ni Songosongo
  Mara ghafla kanenepa kumbe mimba B.O.T.
  Kumbe demu aligawa EPA watu wamepiga hafu jii
  Alizugwa na akaunti hewa kuwadi Bwana Bilal
  Mara mdomo naye kazimwa bila hata picha ya kaburi
  Kinachomponza huyu shawty utulivu sifuri
  Ila hakuna anayepinga kwamba huyu demu ni mzuri
  Mixer siasa na biashara demu ameshakuwa chotara
  Mishe za Dar akimaliza Mjengoni anakwenda lala
  Kadri miaka inavyokwenda demu anazidi fulia
  Kumbe weupe ni mkorogo ona mwili sasa umefifia
  Demu kazidi umalaya wacha mabwana wamteme
  Haogopi kuliwa mtungo kisa anagawa umeme
  [Kiitikio]
  [Ubeti wa Tatu]
  Wadaku walishamfuma anakula denda na Richmond
  Dowans akazidi kete akamvisha pete ya diamond
  Binti masikini akanasa bwana mshenga ndio Lowasa
  Shemeji hataki hata picha ndio tabia gani sasa
  Ndoa ilifungwa kwa vifijo vigogo wakala pizza
  Keki nzima wale wao share yetu si ni giza
  Sio hayo demu ana mengi ya kuchukiza
  Malighafi ashazinadi for sale anajiuza
  Mtaani ilivuma rumor demu kawa mama huruma
  Uchumi umefungwa drip maendeleo ndio kali homa
  Mali asili ndio kitasa kila ufunguo ndio unapita
  Toka alipovunja ungo nusu karne imeshapita
  Mapenzi kafanya mradi anamegwa na mafisadi
  Amani kwa time bomb binti amekumbatia radi
  Vitendo vyake vibaya vinafanya adharaulike
  Tabia Katiba sio Msahafu ndio useme isibadilike
  Mikosi inayomkuta ndio kwanza anatabasamu
  Hajali waliomzunguka kama nao binaadamu
  Mbagala walimbaka mpaka akamwaga damu
  Na juzi Gongo la Mboto kaanza kujamba mabomu
  [Kiitikio]"

  Source: Solo Thang – Miss Tanzania
   
 12. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Solo hapa kweli kafanya Sanaa!! Hapa si jukwaa lake japo jamaa katika wimbo kaweka siasa... Kamsema sana BOSS wa nchi yetu(I GUESS)
   
 13. J

  JF2050 JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 2,086
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama anaimba mtu fulani mkubwa! Nisije nikapigwa ban bure.
   
 14. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hapana Go between lines,
  anaongelea milestones ya Tanzania tangu ilipopata uhuru,
  chini ya Nyerere,
  Mwinyi,
  Mkapa
  na sasa Kikwete
   
 15. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ukiiona haraka haraka ni ndefu hutasoma.
  Ukisoma mistari miwili hutaacha hadi umalize
   
 16. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hapa msanii kafanya sanaa. Big up Solo Thang! Wenzio wanaimba mapenzi wakati nchi inateketea!
   
 17. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ndo jukwaa lake haswaaa.
  Wimbo mzima ni siasa.
   
 18. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nilitaka kuponda kuwa kachoka kabla sijasoma mistari,
  Nimeipitia na kurudia,
  Solo Thang kudos!
   
 19. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #19
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,528
  Trophy Points: 280
  Nimeisikia jaman jamaa anawezwa kuwekwa kizuizini kachana mbayaaaaaa
   
 20. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #20
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,528
  Trophy Points: 280
  Jamaaa wakisikia utasikia marufuku kupigwa nchini
   
Loading...