nashukuru mzizimkavu kwa maelezo hayo mazuri kwakweli ila mimi nina maswali mengi sana ila ya muhimu sana ndio nitauliza, mimi mwenyewe miaka minne imepita nilinunua umeme wa sola kulikuwa kuna kampuni ya kutoka ujerumani walikuwa wanauza vifaa hivyo na mafundi wao nilitumia kama 1,200,000/= nikapewa na fundi nikaenda nae mkoani kijijini kabisa kunifungia umeme nikawa natumia bulb 11 za watt7 na vile vile switch socket za ukutani za kuchanrge phone na kusikiliza radio, radio ndogo tu lakini waliniambia umeme wangu ni wa watts 90 sasa lile kumpuni liliondoka sio siri kutoka moyoni sina imani kabisa na haya mashirika mengine yanayotoa huduma hapa maana nimeshasikia malalamiko mengi sana kutoka kwa watu nilijaribu kuangalia kwenye mtandao nikakutana na shirika hilo hilo germany nikawaomba kama wanaweza kunitumia vifaa maana nataka kuongeza watts nimeangalia gharama nitatumia pesa nyingi sana kwa kweli nimeshindwa lengo langu nataka kuwa na taa 14 badala ya 11 pia nataka kuwa naangalia tv kwa masaa mengi about four to six hours sasa naweza kutumia watts ngapi kitalaam zaidi now niko kwenye 90w na gharama naweza kufanyiwa estimation tu? na kweli hawa jamaa wana vifaa vya uhakika? maana kuna shirika moja ndugu yangu alienda kununua akaambiwa yaani ikileta shida uje ila ukweli vile vifaa vilikuwa sio original alipata hasara sana alivyorudi hata kumsikiliza hawakuweza, inauma sana watz wanafany biashara y kutudanganya sana once wakipata pesa hawaangalii wateja wao wanaendeleaje, mwisho wa siku watu wengine wakija na huduma nzuri ndio sisi tunaanza kulalamika kuwa wanatuzibia, ilingali walikuwa wanatusaidia sana kupata huduma inayostahili.