Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,114
- 34,956
Ni muhimu kuelewa sola ni nini na jinsi ina fanya kazi. Mwongozo zifuatazo zitamsaidia mtu ambaye anataka kununua vifaa vya sola kwa maarifa wa kuelewa masuala ya sola haraka. Na pia itakusaidia kuchagua ukubwa wa mfumo wa sola itayofaa mahitaji yako nakukupa wazo la gharama ya wastani.
Nishati ya Jua
Jua linatoa kiasi kikubwa cha nishati katika mionzi yake ambayo inaweza kutumika umeme. Teknolojia inayotumika kuzalisha umeme kutoka mionzi ya jua hutumia chombo kinaitwa sola au moduli ya jua. PV inasimama badala ya maneno mawili: Photo (P) na Voltaic (V).
Sola inafanya kazi kwa mwanga wa jua (Photo) kubadilishwa kuwa mkondo wa umeme (Voltaic). Jua huwaka kwa masaa mengi kwa siku. Katika muda huo umeme unaweza kuzalishwa na kuhifadhiwa kwenye betri. Usiku unaweza ktumia umeme uliohifadhiwa kwenye betri kwa matumizi mbalimbali. Kiasi cha umeme kinachoweza kuzalishwa hutegemea uwezo wa moduli na jinsi jua linavyowaka kwa siku. Umeme mdogo huzalishwa siku yenye mawingu au wakati wa msimu wa mvua.