Kwamba wafanyabiashara wa nchi ulizozitaja wao China hawapafahamu??
Hapa sio serikali kuiua Kariakoo. Kariakoo ni soko la bidhaa kutoka kokote duniani ingawa asilimia kubwa ya bidhaa ni za ChinaSerikali ikiua Kariakoo itakuwa kosa kubwa la kihistoria la kiuchumi kuwahi kufanywa Tanzania!
Ndio hivyo, viongozi wanawachukulia wabongo wapumbavu. Wanachukua ma mikopo makubwa, wananchi wakilalamika wanaambiwa wahamie Burundi. Maisha magumu wakiambiwa wanaambiwa wenyewe ni wachumi hawakusomea uganga wa kienyeji, kuna siku watu watachoka watakapoona utwana ndani ya nchi yao. Wawalete tu wachina, hao ccm na serikali yao wanadhani wabongo watakua wajinga milele iko siku kitawaka tu. Nchi zilizoendelea hali imekua ngumu pia lakini zinakua zinasaidia watu wa matabaka ya chini . Uvumilivu una mwisho haswa binadamu anapokosa chakula huku wengine wakiwa nacho na wako kwa V8s.Kuna bomu litakuja kulipuka mbeleni tuwe wapole tu, muda ni mwalimu. Gap la walionacho na wasionacho ni kubwa sana, hatari sana
Asilimia 90 ya bidhaa za hardware K/koo ni za ChinaSerikali tupo makini na tumefanya upembuzi yakinifu kuhusu ili jambo. Halitaleta madhara yoyote, lengo tunataka zaidi Kariakoo yabakie maduka ya hardware.
Nadhani wamelegwa zaidi nchi za jirani waje huku kwetu.Wageni walitakiwa kufungua viwanda Tanzania, na sio kufanya Tanzania sehemu ya kuleta mizigo yao.
Ubungo panajengwa soko la jumla la Wachina. Hili soko litakuwa lauza bidhaa za kutoka China kwa bei ya jumla, maana yake watashindana na maduka ya kawaida.
Je, serikali imewafikiria Watanzania na yatayotokea huko mbeleni?
Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Safi sana sisi tuakikishe wafanya biashara wa nje na majirani zetu wanakuja kwa wingi hapo ilitukusane kodi za kutosha.Ukiwa China hizi exhibition platform centers ni vitu vya kawaida sana.
Kila jiji la China wanazo ili kuzitangaza bidhaa zao pia zinawasaidia wafanyabiashara wanaoenda China kuona bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa China
Sasa hivi Mchina kaamua awafuate wateja hukohuko wanapotoka na kufungua hizi centers za maonyesho ya bidhaa za China ili wafanyabiashara wajionee bidhaa na wafanye kuagiza wakiwa nchi zao bila kwenda China
Mojawapo ni hii itakayofunguliwa Ubungo
Hii ndo point zingine ni lawama tuHiyo si sawa maana wataua kabisa viwanda vya ndani.
Wao walipaswa waje kujenga viwanda ili wananchi wapate ajira, na sio kuleta ready made items
Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Hizi Stori za Vijiweni mkuu, mwendazake Aliongeza Income inequalities, MO hakuwa Billionea, ila ndani ya miaka 5 ya huyo jamaa utajiri ukafika hadi 1.5B usd.Hii nchi uko inakokwenda inatengeneza vita vya wenyewe kwa wenyewe maana gap la walionacho na wasio nacho linazidi kuongezeka kwa kasi sana.
Mwendazake alijaribu kulipunguza lakini huyu Hangaya kaja na yake. Anyway time will tell.
ANGALIZO: Mimi sio mmoja wa wasio nacho, ni wa walionacho, ila ninawaza tu kwa kuangalia jicho la tatu.
Naona Mchina ameona bandari ya Dar au akija kula shavu ile ya Bagamoyo ni potential ni lango la kusafirisha bidhaa zao kwenda Congo, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, UgandaSafi sana sisi tuakikishe wafanya biashara wa nje na majirani zetu wanakuja kwa wingi hapo ilitukusane kodi za kutosha.
Asante Mzee wa Kupambanua mambo!Hapa sio serikali kuiua Kariakoo. Kariakoo ni soko la bidhaa kutoka kokote duniani ingawa asilimia kubwa ya bidhaa ni za China
Hapo Ubungo Mchina anawekeza anaanzisha exhibition trading platform, cros-border E-commerce platform, commodity procurement platform kwa Made in China goods only
Hata huyo mfanyabiashara wa K/koo badala ya kwenda China anaweza kwenda Ubungo akajionea bidhaa anazopenda then akaenda kwa watu wa procure watakaokuwa na ofisi zao hapo hapo akafanya malipo akaagiza mzigo kutoka China. Ubungo itakuwa ni one stop wholesale center
Hakutakuwa na biashara za rejareja Ubungo
Kajifunze kichina uwe makalimani hapo sokoniWageni walitakiwa kufungua viwanda Tanzania, na sio kufanya Tanzania sehemu ya kuleta mizigo yao.
Ubungo panajengwa soko la jumla la Wachina. Hili soko litakuwa lauza bidhaa za kutoka China kwa bei ya jumla, maana yake watashindana na maduka ya kawaida.
Je, serikali imewafikiria Watanzania na yatayotokea huko mbeleni?
Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Maafisa usafirishaji na maafisa ubashiri ndiyo ajira mpya Tz.Sisi Watanzania tutaendesha bodaboda wala hamna shida
Sijui ni vya nnNi viwanda vya consumer goods au capital goods?
Tunahitaji viwanda vya capital goods hizo consumer goods hata wasipowekeza sio mbaya sana