Wafanyabiashara katika soko la Tandika watabidi watafute makazi mengine baada ya mfanyabiashara ambaye jina lake halikutajwa kuuziwa soko hilo na atatumia shilingi milioni 200 kujenga maduka na kuyapangisha kwa wafanyabiashara atakaowatafuta yeye mwenyewe.
Wafanyabiashara katika soko la Tandika jijini Dar es Salaam, wako katika wakati mgumu baada ya mfanyabiashara mmoja ambaye hakupatikana jina lake wala kampuni yake kulilinunua soko hilo.
Barua iliyotoka Halimashauri ya manispaa ya Temeke, ofisi ya afisa Mtendaji kata ya Tandika iliyoandikwa Februari2,2009. yenye kumbukumbu namba TMK/TNK/127/02/09.ikiwa na kichwa cha habari Kisemacho
YAH. KUMTAMBULISHA MWEKEZAJI M/S TECHNICAL DEVOLEPERS.
Barua hiyo ilikuwa ikitoa maelekezo kwa uongozi wa soko kuwa tayari mtajwa hapo juu ameshinda zabuni ya kujenga maduka katika soko hilo na atajenga kwa miezi 6 na kutafuta wapangaji kwa miezi 6 na kutokana na kutoa pesa zake itachukua muda wa miaka 8 kabla ya mkataba wake kuisha.
Hata hivyo soko hilo ambalo lilijengwa na Mwalimu Nyerere miaka ya 1974 wakazi wa eneo hilo kwa muda wote huo walikuwa wakinufaika na soko hilo kabla ya kukodishwa kwa mfanyabiashara huyo mwaka huu.
Kutokana na kukodishwa kwa soko hilo jumla ya wafanyabiashara ya maduka 150 na wafanyabiashara ya meza 700 watapoteza nafasi zao kwani mkandarasi huyo amepanga kujenga maduka hayo na kutafuta wapangaji wake mwenyewe.
Wafanyabiashara hao wameapa kuwa hawatakuwa tayari kufukuzwa katika soko hilo ambalo ni mali yao hasa kuzingatia wao pia ni wazawa wa hapa nchini.
Kumekuwana vitisho kutoka kwa viongozi wakuu hasa mkuu wa kituo cha Polisi cha Chang'ombe kwa kuwambia wafanyabiashara hao kuwa kila mmoja atakamatwa na kufunguliwa shitaka lake kinyume na sheria.
Mfanyabiashara mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake akiongea na Nifahamishe alisema "Kumekuwa na uonevu mwingi sana hasa anapotokea mtu mmoja mwenye fedha zake kiasi cha kuhonga viongozi na kutusahau sisi wanyonge ambao tupo wengi ". Mfanyabiashara mwingine alisema
Katika bajeti ya serikali ya mwaka 2009/10, serikali ilianisha sehemu zitakazopewa kipaumbele kuwa nikuboresha sehemu za wafanyabishara ikiwemo soko la Tandika ambalo lilipangiwa kujengwa jengo la ghorofa lenye uwezo wa kutoa nafasi kwa watu 2,000 likiwa limewekewa bajeti ya shilingi 2,500,000.00 sasa iweje huyo tajiri aende kinyume na bajeti sisi wafanyabiasha hatutakubali mtu yeyeto kujenga hapa pasipo maelezo ya kutosha".
Msukuma mkokoteni katika soko hilo akisoma kibao kilichowekwa na wafanyabishara katika soko hilo chenye ujumbe usemao kuwa hili ni eneo la wafanyabiashara sokoni Tandika, eneo hili haliuzwi na haliruhusiwi kujengwa.
Last edited by a moderator: