Leo kwa masikitiko makubwa nimeona jinsi sukari inayozalishwa kutoka viwanda vyetu vya ndani ilivyokosa soko huku sukari kutoka nje ikiuzwa kwa bei ya chini. Leo pia imetangazwa kuwa tani moja ya miwa imeteremka kutoka Tshs.1,200,000 mpaka Tshs.800,000. Binafsi sijaamini kama kweli Serikali inataka kuwaondolea wananchi umaskini kuona mambo haya yakiendelea bila kuchukua hatua. Yafuatayo ni athari zinazojitokeza:-
Suala hili amekwishaelezwa Mhe. Waziri wa Kilimo na hakuna hatua iliyochukuliwa na mambo bado yako palepale. kama Waziri anaelezwa na hachukui hatua kuna nini kimejificha nyuma ya pazia. Binafsi namwomba Mhe. Rais aingilie kati suala hili ili jambo hili lipate ufumbuzi. Mhe. Rais wewe ni Baba yetu. Watoto wako wanapokuwa wana matatizo, wanaposononeka, hawana amani ni budi tukukimbilie. Inasikitisha kuona maghala yamejaa sukari eti hakuna wanunuzi.TUSAIDIE MHE. RAIS.
- Ukosefu wa sera ya kulinda viwanda vyetu ili vizalishe ajira.
- Ukosefu wa mapato ya Serikali kwa waagizaji toka nje kutolipa kodi stahiki.
- Ukosefu wa ajira kwa wananchi wetu. Hii ni kupelekea viwanda kupunguza wafanyakazi.
- Kuendeleza umaskini kwa wananchi. Mfano kama tani moja ya sukari ilikuwa inauzwa Tshs.1,200,000 na sasa inauzwa Tshs.800,000.
- Wananchi kuchukia Serikali yao.