Soko kuu la Urambo Mkoani Tabora linazidi kuteketea kwa moto muda huu,chanzo cha moto huo ni shoti ya umeme ambayo imetokea katika soko hili, mpaka sasa hakuna kikosi cha zima moto wala askari polisi aliyefika katika eneo la tukio, japo wananchi wanajaribu kuuzima moto pasipo na mafanikio.
Uchunguzi ufanyike mapema. Isijekuwa UKAWA wamelipiza kisasi.
Poleni sana waathirika.
Soko kuu la Urambo Mkoani Tabora linazidi kuteketea kwa moto muda huu,chanzo cha moto huo ni shoti ya umeme ambayo imetokea katika soko hili, mpaka sasa hakuna kikosi cha zima moto wala askari polisi aliyefika katika eneo la tukio, japo wananchi wanajaribu kuuzima moto pasipo na mafanikio.
nilikuwa eneo la tukio kunajamaa anaongea kwa hisia sana ila anasema hii ajari imepangwa kwani soko kuu la urambo halilipi ushuru halmashauri kwa mgongo wa sitta, hivyo limechomwa ili halimashauri ilijenge upya na lianze kulipa ushuru. Jamaa anaonesha ni km anauhakika na maneno yake kwani anasema hata TANESCO wamehusika kwani kabla ya moto umeme ulizima mjimzima na baada ya soko kuwaka umeme ulirudi km kawaida.
duu hii kali . hebu jaribu kumrekodi
Mmmmhh!!!...poleni saaana.