Soda zote kwa ujumla ni sumu!

maji yanaozesha chuma hata kiwe chuma kigumu kwa kiasi gani kikikutana na maji kinaoza
ila bado tunakunywa hivi unajua fanta ikipita kooni utamu wake ni balaa
Au mirinda nyeusi daah shidaaa
 
Cokakola ukimwaga chooni husaidia kuondoa uchafu. Niliambiwa sijatafiti. Ni kweli? Kumbuka (no research no right to speak)

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilisikia watu wakijibizana nauliza aliyeandika kuhusu hatari ya soda. Kama alishafanya utafiti anijibu. Kwa maneno mengine inaondoa madoa

Unatakiwa kujua kuwa, hamna chakula chochote kilicho salama kwa asilimia mia moja. Kwa mfano, caffein inapatikana katika vyakula na vinywaji vingine vingi tu kama coffee. Kwa nini u-single out soda tu? Two, sababu ya unene wa kupita kiasi huchangiwa na vitu vingi sana, kikubwa kikiwa ni aina ya maisha unayoishi. Mtu anayeishi mazingira ya kutokuwa active sana ana nafasi kubwa ya kuwa mnene kuliko aliyeactive hata kama wanakula chakula cha aina moja. Pia kuna swala la Genetics yaani maubile ya mtu. Kuna watu ambao ni prone kuwa wanene kwa kiwango kile kile cha chakula ambacho kwa wengine hakiwapi shida. So, bottom line ni kuwa fuata utaratibu wa kuwa na kiasi katika chochote unachofanya. Kitaalam kuna kitu kinaitwa Acceptale daily intake, yako kiwango kinachokubalika kuliwa kwa siku bila kumsababishia mlaji madhara. Pia, ikumbukwe kuwa kuna kitu kinaitwa threshold. Hata sumu ukinywa chini ya threshold ya kuweza kuua, huwezi kufa. So, everything is dangerous and or safe depending on how much you take.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
usipokufa kwa kunywa soda,utakufa kwa ukimwi,usipokufa kwa ukimwi,utakufa kwa kugongwa na gari,usipokufa kwa kugongwa na gari utakufa kwa kurogwa,usipokufa kwa kurogwa basi utakufa kwa maralia,kama usipokufa kwa maralia basi utakufa kwa mapenzi ya mungu,mwisho kufa hakuna sababu na wala hakukwepeki ndio maana kuna mtoto anazaliwa leo na anakufa kesho bila hata sababu ya msingi,mwisho ni kwamba never doubt the death,once u were born no way you must die,
soda oyeee!
Aisee! Huo ni upotoshaji mkuu,.. Kwakua watu tunalazimika kufa, basi tusijali afya zetu, kweli!?
 
Siiiiikamatiiiiki, nikionja msisimmnko, aaaha..cocacola acha kabisa.

Haihitaji utafiti kujua kwamba soda zina madhara kiafya. Nnachojiuliza, kama wanapiga marufuku Bangi na gongo, kwanini wanashindwa kwenye sigara na soda ilihali zina madhara makubwa?
 
Soda ndio burudani pekee ya watu wengi wasio na makuu. Sasa na yenyewe wakianza kuitilia fitina itakuaje? Vipi kuhusu juice na energy drinks zilizosambaa mtaani huku zikiinekana kabisa kuwa na kiwango duni?

Maisha yetu Mungu tu anayalinda, siku ikifika utapelekwa India, Ulaya, Asia ila nafsi itarudi tu.
Kunywa maji mkuu, hayana mashaka
 
Sawa kabisa Mbona vyakula vyote tunavyokula ni full poison hamsemi?! Unga una chembechembe za vyuma, mboga mboga, hadi hewa tunayovuta, tuishi maisha marefu sie kobe? Ukipiga hata 40yrs inatoisha watoto wako watendeleza ulipoishia.

Sent using Jamii Forums mobile app
unavunja mbavu zangu mkuu,.. hahahahaaaah... Nimecheka sanaaa
 
yaani ununue kokakola usafishie choo
utakuwa upo hovyo kichwani
comments za hii thread ni kicheko tu,... Kwanini watu wanaitetea sumu inayoweza kuwaletea kifo!?
 
Coke zero ndo best product kwa watu wanaozingatia diet,.ina 0 calories,0 fat, 0 sugar,.wanatumia sweeteners kama aspartame,ambayo sio sukar ila ina ladha ya sukar,..mi natumia hii soda,ni nzur sana,ulaya na marekan ndio imekua mbadala,watu wanakunywa zero tuu
 
Hayo ya dawasco yakishachemshwa tu, yako salama sana

Kwa maana wengine tumekulia vijijini ndanindani huko mkienda kutafuta kuni msituni ukikuta maji unapiga goti unakunywa haujali kama fisi au nyani alipita. Hauwezi kuamini nimekuja kusikia taifodi mjini..
 
Back
Top Bottom