Watu mnang'ang'ana kuyatafuta makansa na magonjwa ya kisukari kwa nguvu sana kwa kuyakumbatia hayo masoda yenye misumu.
Angejitokeza mzalendo mmoja bilionea na kufanya uwekezaji kwenye kinywaji kipya cha barid(juisi za matunda) kije kuwa mbadara wa hizo takataka ziitwazo soda.
Namaanisha si kwamba majuis yaliyopo sasa hayapendwi, bali ujio wa kinywaji kipya chenye ujazo mzuri na bei nzuri ambacho kitakuja kureplace uwepo wa hizo soda.
Yaan kwa jero tu unajipatia chupa ya juis yenye ujazo wa ML350-500, tena zenye radha tofauti tofauti ili kuwavuta vzur wateja
Tujarbu kuwa kama Mo, yaan ujio wa hayo madude yake ya mo-extra kumepunguza sana unywaji wa vinywaji vingine, ushahid waweza upata hapo mtaani kwako kwa kutizama makopo yanayozagaa, ktk Kopo5 basi 3 za mo na 2 za maji ya kilimanjaro&uhai.
Tuweni wabunifu ili kujikinga na madhara yasiyokuwa ya lazima