Socrates: Mwanafalsafa aliyekataa kutoroshwa,na kukubali kuawa kwa Sumu kuliko Kuishi Uhamishoni

Guru Master

JF-Expert Member
Jan 14, 2017
226
594
SOCRATES

Wengi tumemsikia au kumsoma Socates kwenye elimu,falsafa,kwenye saikolojia ,siasa na fasihi lakini ni wachache ambao waliamua kwenda ndani Zaidi kumwangalia huyu Socrates ni nani. Huyu ni mmoja ya wana falsafa mahiri kabisa waliopata kutokea katika dunia hii. Ukienda karbia kila Nyanja utamkuta kama ni kwenye elimu utakuta misingi yake, kama utazungumzia falsafa utamkuta kama utakuja kwenye saikolojia utamkuta na pia siasa na fasihi yupo. Ni mmoja ya watu waliokuwa na akili au upeo mkubwa sana na kutokana na wao tumeweza kujua na kujifunza mengi sana kwa kukubaliana nae au kumkosoa baada ya kupitia maandiko yake.

KUZALIWA KWA SOCRATES

Socrates alizaliwa mwaka 470 Kabla ya Kristu. Nasisitiza Kabla ya Kristu. Huko Athens ugiriki. Habari zake nyingi tunazipata kupitia wanafunzi wake Plato and Xenophon. Namna yake ya ku reason ndiyo iliyosaidia kutengeneza msingi kwa watu wa magharibi kutengeneza logic na falsafa. Upepo wa kisiasa ulipobadilika huko ugiriki Socrates ikamliwa auawe kwa sumu aina ya hemlock mwaka 399 Kabla ya Kristu. Kumbuka miaka ya nyuma walikuwa wanahesabu miaka kwa kurudi nyuma yaani kuanzia juu kuja chini. Na ndo maana unaweza shangaa ilikuaje alizaliwa mwaka 470 na akauawa 399.

MAISHA YA SOCRATES

Kama ambavyo nimesema alizaliwa mwaka 470 huko Athens ugiriki maisha yake Socrates yameelewa kwa vyanzo vichache sana. Sana sana mazungumzo yake na Plato and Xenophon na michezo ya kuigiza ya Aristophanes. kwa sababu ya maandiko yake mengi yalikuwa si maalum kwa ajili yakuzungumzia maisha yake. Yaani lengo lilikuwa Zaidi kuzungumzia mafundisho yake hivyo ikasababisha yasipatikane mengi kuhusiana na maisha yake binafsi.

Socrates alikuwa mwana wa Sophroniscus huyu mwa athen ambaye alikuwa ni mhunzi na mchongaji nadhan mhunzi ni mtu anayeshughulika na uchongaji na ujenzi wa kutumia mawe kwa lugha ya malkia tungesema ni stone mason. Na mamaye alikuwa akitwa Phaenarete huyu alikuwa mama mkunga. Na kwa kuwa hakuwa katika familia ya daraja la kwanza zile family zinaitwa noble family inawezekana alipata elimu ya msingi tu ya kigiriki na kujifunza shughuli za uhunzi za baba yake toka akiwa mdogo. Inaaminika Socrates alifanya kazi kama mhunzi kwa miaka mingi sana kabla hajayatoa maisha yake kwenye falsafa.

Kuna mkanganyiko kiasi katika mambo kadhaa kuhusiana na kazi aliyokuwa akifanya badaye ya ualimu kama alikuwa akilipwa ama laah. Xenophon na aristophanes wao wanasema alikuwa akilipwa kwa mafundisho yake lakin Plato anasema katika maandishi yake kuwa Socrates hakuwa akipokea malipo yoyote.akinukuu shairi lake pia kama uthibitisho.

Socrates alimuoa Xanthippe bint mdogo ambaye alikuja kumzalia watoto 3 lampcocles,sophroniscus na Menexenus. Inasemekana mkewe hakuwa akifurahia kazi ya pili ya mumewe yaani kuishi kifalsafa na kufundisha falsafa kwa kuwa ilikuwa hamlipi sana na hivyo akawa hawezi kuitunza vizuri familia yake akiwa kama mwanafalsafa. Kwa maneno yake mwenyewe Socrates anakiri kuwa hakuwa akijihusisha sana na malezi ya watoto wake zaid Zaidi alikuw alijihusisha na makuzi ya vijana wote wa Athen.

AKIWA MWANAJESHI NA USHUJAA WAKE

Sharia za Athen zilikuwa zinataka kila mtu mwenye uwezo kuanzia miaka 18 mpaka miaka 60 kujiunga na jeshi. Kulingana na plato alichoandika anasema Socrates aliwah fanya kazi kama mwanajeshi aliyekuwa akibeba ngao na mkuki mrefu na kuvaa kinyago usoni. Na alishawah kupigana mara tatu kwenye vita vya Peloponnesian na delum pamoja na amphipolis na potidea huko alifanikiwa kuokoa maisha ya Alcibiades ambaye alikuwa ni general wa jeshi. Socrates alikuwa akifahamika sana kwa uwezo wake wa kupabana pasipo woga kwenye mapambano na akikataa kabisa kurudi nyuma tabia ambayo alibaki nayo maisha yake yote.

Alikuwa akifananisha tabia hiyo na jambo la mwanajeshi kukataa ku surrender hata napokutana na kifo.

Plato anamzungumzia Socrates alivyokuwa ameumbika.kuwa alikuwa mfupi na mnene kiasi akiwa na pua fupi na macho makubwa. Wakati wote alionekana kama mtu aliyekuwa akikodoa macho. Lakini plato anasema kwenye macho ya wanafunzi wake alikuwa akionekana kuwa na mvuto flan kutokana na akili aliyokuwa nayo hasa kwenye majadiliano na kuwa na mawazo yenye kufikilisha sana.

Wakati wa maisha ya Socrates athen ilikuwa inapitia katika kipindi cha mpito toka kwenye jamii ya kale yenye umiliki na ukuu kuwa taifa lililofadhaishwa baada ya kupokea kipigo toka kwa Sparta katika vita vya Peloponneas. Waathen waliingia katika kipindi chenye mashaka kuhusu utambulisho wao na sehemu yao ya kuishi hapa duniani na matokeo yake wakaingia katika kipindi kigumu sana katika maisha yao. Ili kubaki na utukufu wakijikuta wanang’ang’ania utukufu waliokuwa nao hapo nyuma. Wakati huo huo waathen wengi wakawa wakifurahia jinsi ambavyo Socrates alikuwa akichallenge hekima ya kigiriki tena kwa namna ambayo iliwafanya wengi wacheke hivyo hivyo pia kukawa kuna watu ambao walikuwa wakichukizwa na kitendo hicho na kuona alikuwa akitishia utamaduni na maisha yao kwa ujumla.

ANAHUKUMIWA KIFO.

Mambo hayo yalifanya Socrates achukiwe na baadaye akaundiwa mashtaka ambayo yalimsababishia kifo. Kilichotokea ni kuwa aliposhtakiwa kwa kuonekana akifundisha mafundisho ya yenye kukinzana na wakubwa majaji wakaamua kupiga kura ambapo katika hilo majaji 280 walimhukumu na 221 walisema hana hatia. Taratibu zilikuwa kama mtu amehukumiwa basi pia alipaswa apewe nafasi ya kujitetea na kuchagua adhabu katika zile ambazo zilikuwa zimependekezwa likiwepo suala la kuwa alipaswa afukuzwe athen. Spcrates aliamua kuwa ilipaswa apewe zawadi kwa kuwa alikuwa amewafungua vijana wengi wa athen ambao walikuwa kama makondoo hapo mwanzo na sasa wana mwanga wa kuhoji na kutafakari.hivyo alipaswa apewe enzi na pesa kwa hilo.majaji walikasirishwa sana na namna alivyokuwa akiongea kwa majidai na kuwasanifu na hivyo kupelekea ahukumiwe kunyweshwa kinywaji chenye mchanganyiko na sumu ya hemlock

Harakati za kumwokoa na kifo.

Kabla ya kuuawa kwa sumu rafiki zake walifanikiwa kumwokoa baada ya kumhonga pesa mlinzi na kumwokoa ili akimbilie nchi nyingine. Alikataa na kusema kuwa hakuwa akiogopa kifo na kuwa asingekuwa na wakati mzuri akiwa uhamishon maana yeye alikuwa ni mwananchi mwaminifu wa athen.alisema alikuwa tayari kuifuata sharia kama ilivyo hata ile inayomhukumu kifo.plato anaelezea kifo cha Socrates kuwa kilikuwa cha kishujaa na ilishangaza wengi jinsi ambavyo alikunywa ile sumu bila hata kusita na taratibu akawa akipigwa ganzi kuanzia moyoni hadi mwili wake mzima. Kabla ya kifo chake Socrates alielezea kuwa ilikuwa ni kuitoa nafsi au roho toka kwenye mwili wake kuiacha hai iwe huru.
 
Asante sana mkuu.. Bt katika maelezo yako hatujaona historia yake ya kielimu. Yaani aliipata wapi hii elimu. Inasemekana kuwa alisoma Misri kwa miaka kadhaa na ndiko alikopata hii elimu bt kama kuna anaejua zaidi anaweza kutuelimisha.
 
Wayunani walimuheshimu mwanafalsafa

Wajerumani walimuheshimu mtu mwenye ubavu.

Wayahudi walimuhusudu mtu wa miujiza.

Waafrika sasa!!!
Hasa watanzania bora nisisitaje.
 
Back
Top Bottom