Socialist party of Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Socialist party of Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kingadvisor, Jan 7, 2012.

 1. kingadvisor

  kingadvisor Senior Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kutokana na vyama vyote kukosa dira inayoeleweka ya kuongoza Taifa.Naomba wale wapenda ujamaa ambao naamini bado wako wengi waanzishe chama cha kijamaa cha Tanzania (socialist party of Tanzania) chenye lengo la kufuata ujamaa kamili na kuweka raslimali zote mikononi mwa umma badala ya mafisadi wachache wa ndani na nje.

  Ubepari kwa Tanzania dalili zinaonyesha hauna uwezekano wa kufanikiwa Tanzania zaidi ya kuleta mitafaruku,vita na migongano kati ya wenye nacho na wasio nacho,kati ya wawekezaji na wananchi wazawa n.k Hali hii yaweza ingiza nchi vitani baadaye.Watanzania walio wengi inaonyesha hawajawa tayari kuupokea mfumo wa ubepari bado wanatamani tiba za bure,shule na vyuo vya bure,ajira za umma bwerere kila kona,Migodi na raslimali zingine kuwa chini ya umma badala ya wawekezaji wa nje,n.k

  Wengine wanaweza sema ujamaa umeshindwa nchi nyingine ninachoweza sema sio umeshindwa ubepari ndio umeshindwa kwenye nchi hizo.Kwa mfano chukulia Urusi.Wakati wa ujamaa Urusi lilikuwa taifa moja lenye nguvu kubwa duniani ubepari ulipoingia umeshindwa kulifanya liwe taifa liendelee kuwa moja limesambaratika nchi nyingi kibao.Na nchi nyingine vivyo hivyo zilizokuwa za kijamaa.Umoja huu tulio nao ni sababu ujamaa bado upo kwa mbali japo unapumulia kwenye mashine hospitali.

  Ni vizuri wawezao kuanzisha chama hicho cha kijamaa waanzishe na kijitambulishe hivyo kabisa na wadhamirie kulirudisha taifa kwenye ujamaa nina hakika watatoa upinzani wa nguvu uchaguzi ujao na wanaweza ingiza wabunge kibao bungeni.

  Watanzania walio wengi siyo siri bado wanaota Nyerere na ujamaa wake na hata waliozaliwa baadaye bado wanaota serikali iwasomeshe vyuoni bure,wale bure, walale bure ajira ziwe kibao serikalini.Turudi tu kwenye ujamaa na azimio la Arusha letu tuokoe nchi yetu isisambaratike na kuwa na migongano ya kijamii (class struggle) isiyoisha.

  Mimi nitakuwa mmojawapo wa wanachama.Ila sijui taratibu za kuanzisha wanasheria mtusaidie au wajuzi anzisheni sisi tuje tujiunge.
   
 2. G

  Godwine JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  yaani umesikia Hamad Rashid anataka kuanzisha chama cha kijamaa nawewe unatoa wazo...nadhani wewe ni mmoja wao ...wewe ni mfuasi wa hamad rashid
   
 3. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja! Zitto,Nape,Mnyika,Kafulila chukueni wazo hili mlijadili kwa kina zaidi nina imani kitakua chama chenye nguvu!
   
 4. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja! Zitto,Nape,Mnyika,Kafulila chukueni wazo hili mlijadili kwa kina zaidi nina imani kitakua chama chenye nguvu!
   
 5. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  nadhani mtoa mada bado ni mbumbumbu kuhusiana na sera za ujamaa, umefanya utafiti na ukajua kwamba kweli watanzania wanapenda vya bure? eti kusomeshwa bure, kulala bure, acha kuwatukana bana. watanzania wanachadai ni mgawanyo wa rasilimali ambao unaweza ukafanyika katika mfumo wpwote ule na bado maisha yakaenda, na siyo rasilimali zao zitumike kuwanufaisha wazungu na watanzania wachache. haiwezekani leo, umhamishe mtu kwenye ardhi yake yenye rutuba kupisha uchimbaji, unampeleka sehemu ambayo hawezi hata kulima viazi then anabaki kula vumbi tu na kelele toka mgodini halafu unamwambia hata maji anunue, kwa kipato kipi wakati alichotegemea( ardhi) umechukua? tusaidie kuwakomboa watanzania. atleast hata wakiwa shareholders kwenye migodi inaweza kusaidia sio kuwatukana kiasi hiki. aliyekwambia ujamaa unatoa huduma bure ni nani? soma Das capital, Greman ideology za Karl marx, selected essays za Mao Tse Tung, soma sociolist party ya lenin, then njoo utoe argument ukiwa una kitu kichwani sio kusikia watu wanasoma kwenye magazeti unakimbilia kupost
   
 6. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,042
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mimi ni mjamaa!
   
 7. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ujamaa wako upo wapi
   
 8. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  unaweza ukanipa principle walau tano za ujamaa then niambie ipi unaifuata
   
 9. kingadvisor

  kingadvisor Senior Member

  #9
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi na wengi tu akiwemo Raisi Kikwete,Edward Lowasa.Mizengo Pinda,Anna Makinda,Wilbroad Slaa,Anna makinda,Augustino lyatonga MREMA,freeman MBOWE na wengi tu tullisoma bure na kupata huduma bure kuanzia shuleni,kulala bure mabwenini,kula bure boarding kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu wengine wazazi walikuwa na uwezo mkubwa wa kusomesha watoto hata ulaya lakini walisoma bure na kutibiwa bure chini ya ujamaa.Wewe ndio nakushangaa kama umesoma hivyo vitabu ulivyosema hapo juu na hujui mwisho wa ideology iliyomo humo huwa ni kwa benefit ya masses na siyo minority.Ukisema ujamaa hautoi huduma bure naiachia hadhira ya jamii fforum iammue nani mbumbumbu wa kutupwa kati ya wewe na mimi .Ujamaa wengine tumeuishi hatukusoma kwenye vitabu na kukariri tupasi mitihani kama wewe sisi tunajua reality ya ujamaa kwa kuuishi siyo kuuona kwenye mashelf ya maktaba za vitabu.Na bahati nzuri tumeishi mifumo yote miwili ule wa ujamaa na huu wa kibepari sasa tunaweza kusema kwa kujidai kabisa tunadhani upi ni bora zaidi.Kwangu mimi nikilinganisha mifumo hii miwili ambayo yote nimeishi nimeiona nasema hivi UJAMAA HOYEE na UBEPARI ZII na naomba tuchague turudi kwenye ujamaa.
   
 10. L

  Luiz JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2012
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante
   
 11. Mwanyasi

  Mwanyasi JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 5,761
  Likes Received: 1,894
  Trophy Points: 280
  Eti ni great thinker!
   
 12. C

  Cassian Lucas Member

  #12
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwambie
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Hoja inaungwa Mkono 100%
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  He/she is not just a Great Thinker, he/she is more than a great thinker!
   
 15. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Pamoja
   
 16. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  KWA HIYO UNATAKA TUANZE TENA KUIMBA KWAYA MAKUKWANI NA KUMSIFIA RAISI SIFA ZA BURE WAKATI WATU WANaTEMBEA UCHI MIKOANI? unajua ujamaa ni siasa za utumwa? unataka tena kuwanyima watu raha ya kuona TV na kukalia kusikiliza redioni taarifa zote muhimu duniani? unataka kuwanyima wanamuziki hati miliki na kubakia kufa masikini kama ahmedi kipande balisidya, na marijani shabani?

  ujamaa ni unyama na una sera za kishetani, hivyo sisi tumejionea wenyewe madhala yake ambayo ni kunyang'anya sifa za mungu katika jamii na kumtukuza kiongozi aliyekuwa madarakani kama mungu mtu.maneno yake , hugeuzwa na makada kama injiri na kuhutubiwa vijijini kwa wajinga walio wengi ili wayaabudu!

  shetani alitaka kuitawala duniania kwa kupitia sera za kinyama kama hizo, ndio maana mungu akautokomeza kabisaa. unataka mambo ya chama chashika hatamu, ambapo kila kiongozi akiuugua lazima akatibiwe ulaya? kila akiugua karibia ya kufa , lazima akafie ulaya , halafu maiti huletwa kwa gharama kubwa?
   
 17. GIUSEPPE

  GIUSEPPE JF-Expert Member

  #17
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 4,473
  Likes Received: 4,481
  Trophy Points: 280
  huyu marijani Shabani alikuwa nani enzo hizo, nimepekuwa katika majina ya wanamuziki wa kale lakini jina hilo sikuliona au unamaana mzee Marijani Rajabu?
   
 18. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #18
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,448
  Likes Received: 781
  Trophy Points: 280
  Ujamaa sio kwamba ulisoma bure ila mfumo wake walichangia watu wengi na huyo marekani bepari alichangia katika mfuko wa elimu.Siasa ya ujamaa ni ngumu kuitekeleza inataka malaika vinginevyo hutumika mabavu ndio ifanikiwe,lakini demokrasia halisi itakuwa imekufa kifo cha mende. Kwani ndio ilitufikisha hapa tulipo.Unajua kisa cha sigeuki jiwe na pesa za madafu ? Kwanini Mwl Nyerere alistaafu 1985 wakati ndio ukombozi wa nchi za afrika kusini ulikua umefika peak? Pammoja na umahili wake wa kueleza na kuwafundisha waandamizi na makada wa TANU na CCM kwa vitendo kwa miaka 20 ambao hao viongozi tulionao ni wanafunzi wa Mwalimu lakini hawakufaulu.Tusiwe wepesi kusahau historia yetu kwa muda mfupi.Kuanzisha chama kwa jina la kijamaa sio suruhisho, Korea Kaskazini na Kongo ya Kabila zinatumia majina ya Demokrosia lakini demokrasia ni kiduchu.
   
 19. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Tupo pamoja katika hilo, nitakuwa mwanachama namba mbili baada ya wewe, lakini iwapo Azimio La Arusha litafanyiwa marekebisho kidogo/machache sana. Tunahitaji chama cha namna hiyo.
   
 20. Mnyamwezi wa Urambo

  Mnyamwezi wa Urambo JF-Expert Member

  #20
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwa hapa tulipofikia Ujamaa hauwezi kutekelezeka,kwa misingi ya ujamaa kila nyanja ya uchumi iwe mikononi mwa serikali utawafanya vipi wale matajiri waliopo ambao wanamchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yako?utaoperate vipi ujamaa ndani ya multiparty system?Na-imani kwa sera ya kila kitu bure unaweza ukapata wafuasi lakini lazima utakwama katika utekelezaji na hapo ndiyo unaweza ukaleta vita kubwa zaidi na machafuko kuliko yale uliyodhani utayaepuka kwa misingi ya ujamaa.CHINA ujamaa kwasasa upo kwenye hati hati maana classes katika jamii yao kati ya walionacho na wasionacho.Utekelezaji wa misingi ya kijamaa ni mgumu sana katika ulimwengu wa sasa hasa kwa taifa masikini kama Tanzania ambalo bado halina technolojia na nguvu kazi ya kiufundi katika kutumia rasilimali zake kunyanyua uchumi!Nadhani labda upatikane mfumo mwingine ambao upo kati ya ubepari na ujamaa ambao nyanja nyingi za uchumi ziwe chini ya serikali lakini na sekta binafsi ziwepo,huo mfumo ndiyo ninao uona CHINA ya sasa ni wa namna hiyo,sasa hivi kuna mamilionea wakumwaga,this is a sign of failure of communism!!
   
Loading...