Socialist party of Tanzania

Tupo pamoja katika hilo, nitakuwa mwanachama namba mbili baada ya wewe, lakini iwapo Azimio La Arusha litafanyiwa marekebisho kidogo/machache sana. Tunahitaji chama cha namna hiyo.

Mkuu ujamaa ni sawasawa na ubepari i.e. ujamaa=ubepari

Wakati ujamaa wanaomiliki mali ni serikali (theoritcally) lakini in fact wanaomiliki ni viongozi wa chama au walio na madaraka

Ubepari wanaomiliki mali ni kampuni binafsi (watu wachache) in fact lazima wawe na uhusiano mzuri na wenye madaraka

Ujamaa ni siasa za kale ambazo hazina tija kwa nchi na watu wake; muhimu tuangalie something between those "extreme opposite sides"
 
utaoperate vipi ujamaa ndani ya multiparty system?QUOTE]

Kwenye Chaguzi kwenye multi party system kila chama kinakuwa na itikadi yake kingine ubepari,kingine ujamama n.k anayeshinda huyo ndiye atatekeleza itikadi yake.Akishinda mjamaa bepari anafungishwa virago na sera na mipango ya kijamaa inaingia kazini.Ina maana kunaweza kuwa na kubadilika badilika kutoka ujamaa baadaye ubepari na mara ingine toka ubepari kwenda ujamaa kutegemea nani anashinda uchaguzi.

Lakini nadhani kuna tatizo kwenye multi party system hii tuliyodandia sisi ambayo wachina wameiona na wakaigomea kwa sababu ya kuogopa mikanganyiko ya kiitikadi ya nchi kubadilibadilika kiitikadi na mipango uchumi kunapokuwa na mabadiliko ya vyama shika madaraka.

Watanzania hawajawahi piga kura mfumo gani wa siasa wanautaka kama wanautaka ujamaa au ubepari tumeachia vyama vituburuze vitupeleke vitakavyo.Nadhani ilikuwa vizuri kwa nchi yetu serikali ipeleke mswada kwa wananchi waamue kwa kuupigia kura ni mfumo gani watanzania wanautaka utumike kuendesha nchi kama ni ujamaa,ubepari au upi.Wakishauchagua vyama vyote vilivyopo na vitakavyoundwa vilazimike kufuata itikadi hiyo ila vitofautiane tu kwenye mikakati ya namna ya kutekeleza hiyo itikadi.Iko haja pia wananchi wapewe nafasi ya kuchagua mfumo vinginevyo huwezi jua hata vyama vingine mfano CHADEMA,CUF,TLP,NCCR ikishika nchi itaiendesha nchi kwa mfumo gani ujamaa,ubepari au holela.No body knows.Hilo litapelekea taifa kutokuwa na dira eleweka bali kuishia kuwa taifa lenye dira holela ambalo kila ashikaye atajijua mwenyewe ataliendesheje taifa.Hii inaweza pelekea taifa kuwa kichwa cha mwendawazimu ambacho kila chama kinajifunzia kunyoa kikishika madaraka.
 
Style ya utawala wa China sio .. full kunyongana matajiri wa kichina wamekimbia inchi wengi waishi Canada .... Sidhani kama watu flani flani watakubali
 
Mimi na wengi tu akiwemo Raisi Kikwete,Edward Lowasa.Mizengo Pinda,Anna Makinda,Wilbroad Slaa,Anna makinda,Augustino lyatonga MREMA,freeman MBOWE na wengi tu tullisoma bure na kupata huduma bure kuanzia shuleni,kulala bure mabwenini,kula bure boarding kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu wengine wazazi walikuwa na uwezo mkubwa wa kusomesha watoto hata ulaya lakini walisoma bure na kutibiwa bure chini ya ujamaa.Wewe ndio nakushangaa kama umesoma hivyo vitabu ulivyosema hapo juu na hujui mwisho wa ideology iliyomo humo huwa ni kwa benefit ya masses na siyo minority.Ukisema ujamaa hautoi huduma bure naiachia hadhira ya jamii fforum iammue nani mbumbumbu wa kutupwa kati ya wewe na mimi .Ujamaa wengine tumeuishi hatukusoma kwenye vitabu na kukariri tupasi mitihani kama wewe sisi tunajua reality ya ujamaa kwa kuuishi siyo kuuona kwenye mashelf ya maktaba za vitabu.Na bahati nzuri tumeishi mifumo yote miwili ule wa ujamaa na huu wa kibepari sasa tunaweza kusema kwa kujidai kabisa tunadhani upi ni bora zaidi.Kwangu mimi nikilinganisha mifumo hii miwili ambayo yote nimeishi nimeiona nasema hivi UJAMAA HOYEE na UBEPARI ZII na naomba tuchague turudi kwenye ujamaa.

labda hujui tu, kilichofanya uhisi umesoma bure ni equal distribution of resources. umewahi kujiuliza hizo pesa mlizokuwa mnapewa kama nauli, chakula na mavazi, malazi na matibabu zilikuwa zinatoka wapi? acha umbumbumbu open ur mind elewa ujamaa na sio kulewa ujamaa
 
labda hujui tu, kilichofanya uhisi umesoma bure ni equal distribution of resources. umewahi kujiuliza hizo pesa mlizokuwa mnapewa kama nauli, chakula na mavazi, malazi na matibabu zilikuwa zinatoka wapi? acha umbumbumbu open ur mind elewa ujamaa na sio kulewa ujamaa

Source za hizo pesa zilikuwa
1.Kodi za mapato.Tanzania ilikuwa iko kati ya nchi zenye viwango vya juu sana vya kodi ili kuhakikisha mwenye nacho anachangia sana tu kikodi kumsaidia asiyer nacho kwa njia ya kodi ili wote wainuke.Hicho cha juu kilipelekwa kumsaidia maskini asome bure
2.Mgao wa faida toka mashirika ya umma yaliyokua yamezagaa nchi nzima na kila sekta
3.Mikopo ambayo serikali ilikuwa inahangaika kukopa na kukopa sana tu siyo ili wafisadi bali wawajengee uwezo wananchi wake wasikokuwa na uwezo kwa kuwasomesha bure
4.Misaada toka kwa wahisani ilipoletwa ilikuwa ikitumiwa vizuri mno hasa kwenye sekta ya elimu.Nyerere alikuwa akienda huko na huko kuomba asomeshe wanawe watanzania na wengi ziliwafikia wakafaidi hadi wale waliozaliwa maporini kwenye mangedere na umaskini wa kutupwa wakasomeshwa hadi kuwa maprofesa na watu wa kuaminiwa duniani.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom