Soccer Gallery Collection

hivi huyu mwamba alikujaga kuhusishwa na makundi ya kigaidi ..Ilikuwaje hadi sasa bado anacheza?
Hapana ameshatundika daluga huyu anaitwa Mohamed Mohamed Mohamed Aboutrika alizaliwa 1978 November 07 huko Giza kwa kina Mo Salah
 
[emoji460]Dazet Wilfried Armel Zaha anakipiga pale Crystal Palace 2010 aliingia rasmi kikosi cha kwanza akitokea kwenye academy yao kijana wa 92 tu huyu sijui kama ni kweli maana ngozi nyeusi hapo kwenye umri huwa tunadanganya sanaaaa [emoji460]
 
[emoji460] Alizaliwa December 23 1992 anatambulika na kila mtanzania anayependa mpira wa miguu Anaitwa Mbwana Ally Samatta kijana zao la Tanzania African Lyon mwaka 2008 hadi 2010 ambapo akajiunga na Simba amekipiga timu nyingi ambazo ni SSC ,TP Mazembe ,Genk ,Aston Villa ,fehrenbache na kwa sasa Antiwerp kwa mkopo ndiye mchezaji pekee kwa sasa wa Tanzania kucheza ligi kuu ya uingereza na kufanikiwa kufunga.

Japokuwa hakufanya vizur kama watanzania wengi tulivyokuwa tunatamani alipojiunga Aston Villa Instagram page yao ilipata wafuasi wengi sana ambao ni watanzania hata alipojiunga na fehrenbache watanzania wakahama naye na kuunfollow Aston Villa huku watanzania wengi sana wakiwa hawajafurahishwa na kuondoka kwake kutokana na namna alivyokuwa anachezeshwa na kukiwa na tetesi kuwa mchezaji mmoja hakuwa anataka kumpasia awe anashinda akiogopa umaarufu wake kupotea klabun hapo.

Binafsi Samatta namkumbuka zaidi na amecheza kwa mafanikio zaidi akiwa TP Mazembe alikuwa wa moto sana wakongo wanamjua lakini kubwa zaidi pale Genk ndipo alipojulikana zaid amefanya mambo makubwa sana pale na ameweka heshima kwenye ile klabu angedumu miaka mitano zaidi angeanza kama sio kuwa legend wa pale Genk akijukikana kama ""samagoal"" ni hatari sana kwenye mipira ya vichwa mafanikio yake klabu hapo ndiyo yakapelekea kupata deal la Premier league.

2015 alichukua tuzo ya mchezaji bora ya CAF na kufanikiwa kuwa mfungaji bora kwa huo mwaka.Yote haya team yake ya Taifa hajaitendea haki kama watanzania wengi walivyokuwa wanatamani kuwa angekuwa tegeneo kwa team yake na kuisaidia kwenye michuano ya kimataifa watanzania wengi wamekuwa na maoni tofauti juu ya kiwango chake akiwa team ya Taifa
View attachment 2157292View attachment 2157293
 
[emoji460] [emoji3064]so sad [emoji3064] [emoji460]
 
[emoji460]Enzi za Vuvuzela hizi [emoji460]
 
[emoji460]... Loading...[emoji460]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…