So funny

Ginner

JF-Expert Member
May 8, 2011
1,307
1,030
Shekhe
mmoja wa makamu na heshima zake alikuwa
anatembea njiani siku moja... Mara akamuona mtoto
wa kama miaka 5 akijaribu sana kubonyeza kengere ya
nje ya mlangoni wa nyumba fulani bila mafanikio
kutokana na ufupi wake na kengele kuwa juu sana...
Basi Shekhe baada ya kumuangalia sana kwa hekima
yule dogo akiangaika bila mafanikio ndipo akaamua
kwenda karibu kumsaidia kwa huruma...
Akasogea kwa ustaarabu mpaka nyuma ya dogo,
akainama na kumuomba amsaidie kubonyeza ile
kengele ya mlangoni... Dogo kwa furaha zote akakubali
tena kwa tabasamu kubwa.. Baada ya yule Shekhe
kumsaidia kubonyeza ile kengele mara 2 ndipo
akamuuliza dogo kama kuna kingine...
Yule dogo kwa tabasamu kubwa akamjibu huku
akianza toka nduki...
"Hakuna kingine zaidi ya kukimbia tukajifiche kabla
mwenyewe hajatoka...."
 

Bushbaby

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,590
434
inabidi usubiri wenyewe wakitoka unawauliza kama wamemwona mbuzi wako kwao.....
 

malaika2

Member
Dec 16, 2011
38
3
Dogo ananikumbusha miaka ya 1994 wakati nipo shule ya msingi. Zilikua ndio zetu hizo na marafiki zangu. Tukitoka shule tunapita kila nyumba yenye kengele. Tunagonga kengele halafu wenyewe wakija tunakimbia.
 

mzawahalisi

JF-Expert Member
Jan 11, 2010
752
234
Wenyewe wakifungua unawaambia tafadhalini jamani, tummbo limenivuruga naomba mnisaidie mahala pa kwenda msala. Ukiona hiyo soo, omba maji ya Kunywa.
 

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,483
1,358
Itabidi siku nyingine asimsaidie mtu kabla ya kumuuliza anafanya hivyo kwa 7bu gani. Otherwise imenifurahisha sana
 

TUMY

JF-Expert Member
Apr 22, 2009
705
92
Hujakosea watoto wa uswahilini hawachelewi kukuletea balaa, wanamizinguo kinoma
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Top Bottom