So called Presidential Fund-raising Dinner...

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Tupo hapa mlimani city conference centre, kuna fund raising dinner ya udsm. si mtaalamu wa uchumi lakini naona gharama ni kubwa kuliko matarajio. kiingilio kilikuwa laki mbili, ila naona nafasi za bure ni nyingi sana achilia mbali gharama za vinywaji, chakula na ulinzi ambavyo vyote ni executive. more updates to come wakuu!
 
nalazimishwa kusimama hapa kwa ajili ya ******! roho inaniuma kwa kweli...
 
Maalim seif, ahmed salim, jaji sinde warioba, rpc wa dsm wote ndani. sijui ni kwa gharama ya nani?
 
Prof. rwekaza s. mukandala ameongea, ametoa hotuba nzuri na kueleza uhitaji wa students centre!
 
Jaji joseph warioba anasema, naona porojo nyingi kwenye hotuba yake. anaonesha walimu wake wa kitambo hapa, wote ni wazungu!
 
Anawaomba wahitimu wa udsm kuungana katika kutekeleza mradi huu, anamtolea mfano yoweri museveni aliyefanya tafrija iliyochangia ush. 500 milioni.
 
shukuru kawambwa ashaongea, ni zamu ya mkw.ere sasa, anaongea pumba, ati amevaa kitenge wakati wageni wamependeza. pumba!
 
Anatoa stori ya nyani na wanawe... mkw.ere bwana?
 
Anasema kuhusu historia ya wazee wa tanu kukabidhi jengo la sukita liwe kianzio cha udsm. nyc story! mwaka 64 wakahamia mlimani...
 
kama kawaida, mvuto wa hotuba zake upo katika matumizi ya lugha, sio maudhui, porojo ni nyingi sana!
 
Yale yale ya mechi ya simba na yanga kuchangia maafa Gongo la mboto wakapata mapato milioni kumi, matumizi yakawa milioni nane wakapeleka milioni moja na ushee hivi na bado ikawa mbinde kupeleka!
 
Hata mi nashangaa, mbona ni kama sherehe na si harambee! Maana kila kitu humu ndani kimegharimu mapesa kibao!
 
k, chaji ilikwisha simuni wakuu. ila mpaka naondoka pale saa 6 kasoro, mkw.ere ndio alikuwa mc wa mnada, na porojo za ki-mc, for he fits for the job! mhe. john mnyika, mbunge, alichangija mil. 2 kama sikosei. crdb bank plc walinunua picha ya nyerere kwa mil. 35, vingine sikumbuki kwa kuwa nilikuwa nimelewa mvinyo wa bure!
 
Back
Top Bottom