Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 676
kidogo kidogo tutafika, hatutochoka kudai haki yetu kwenye muungano hadi mambo yawe sawa.
hongereni wawakilishi na nnakuhusieni acheni siasa za kubaguana na kuweka uzanzibari kwanza kisha utanzania na uccm au ucuf
SMZ yataka marekebisho sera ya ushirikiano
na Mwandishi Wetu
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar, imetaka kutazamwa upya kwa sera ya ushirikiano wa kimataifa ili kuepusha usumbufu kwa viongozi wa kitaifa.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Tafana Kassim Mzee, wakati wa semina ya kujadili sera mpya ya Mambo ya Nje iliyoandiliwa kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Waziri huyo, alisema hatua za lazima zichukuliwe kutokana na tukio alilolishuhudia akiwa nchini Uingereza katika ziara ya Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Sheni.
ALieleza kushangazwa na kitendo cha kutaka kufanyiwa upekuzi, Dk. Shein wakati ni kiongozi wa kitaifa na kwamba jambo hilo halileti picha nzuri katika ushirikiano wa kimataifa.
Hata hivyo, waziri huyo alipongeza msimamo wa maofisa wa Makamu wa Rais kukataa kubaguliwa na kusema kuwa huo ni ujasiri katika masuala ya uhusiano wa kimataifa.
Hivi jamani Waziri Mkuu wao wa Uingereza anaweza kufanyiwa kitu kama hicho (akimaanisha kupekuliwa akiwa uwanja wa ndege), alisema Waziri Tafana.
Naibu waziri huyo, alitaka kujua faida za Zanzibar katika Jumuiya ya Madola kwa vile katika siku za nyuma ilinyimwa misaada na nchi wanachama wa jumuiya hiyo.Tafana, alisema ili kufanikisha sera hiyo ipo haja ya kutizama suala la watendaji na mabalozi likaangaliwa pia kutokana na ukweli kuwa watendaji wengi katika ofisi za ubalozi hivi sasa wanatoka upande wa Tanzania Bara.
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, alisema Tanzania imepiga hatua katika kuzingatia itifaki kwa viongozi wanapokuwa ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo alikiri kuwapo kwa matatizo yatokanayo na katiba, ingawa hakuwa wazi kubainisha vipengele vyenye utata.
http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/12/2/habari4.php