SMZ yakabidhiwa tani mia moja ya tende kwa ajili ya Ramadhani

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
792
1,144
Mfalme Salman Bin Abdul-azizi ametoa msaada wa tende tani mia 100 kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa ni sadaka kwaajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akikabidhi msaada huo Naibu Balozi kutoka Saudi Arabia Bandar Al-hadhani kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais katiba,sheria,utumishi wa umma na utawala bora amesema kila ifikapo mwezi kama huu Saudi arabia hutoa msaada katika sehemu mbalimbali ikiwemo Zanzibar ikiwa na lengo la kuwasaidia wananchi hasa wanyonge.

Kwaupande wake Waziri Haroun Ali Suleiman ameushukuru Ufalme Salaman kwa msaada huo ambao utasaidia waislamu wengi katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani.

Amesema Salman amekuwa mdau mkubwa kwa serikali yake kwa kuisaidia Zanzibar katika kipindi cha ramadhani nahata baada ya hijja hutoa msaada wa nyama.

Zanzibar24
 
tusaidien na elimu jaman mtatudumaza kiakili kula tyuu jmn tende tunazo nyng tyyu ifike mahali tuchague na misaada
 
Dodoma sehemu za mvumi,muungano,makulu n.k tende zinalimwa waje wawekeze wajenge kiwanda cha kusindika tende kama kweli wana nia nzuri
 
Back
Top Bottom