SMS hizi zinaelimisha,zinakosoa, zinatia faraja, zinajenga ujasiri, zinaburudisha na kuonya

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,305
12,969
Kuna SMS mbali mbali za busara ambazo watu hutumiana kwenye simu za mikononi zikiwa na jumbe mbali mbali za kuelemisha, kufariji, kutia moyo, kukosoa, kukejeli, kuasa, utani na vichekesho ambapo huelimisha na kuburudisha. Zipo za milengo tofauti kama ya kidini na ya matukio ya kawaida. Ninabahati ya kutumiwa nyingi na kuziforward. Hapa nina toa tatu na ninaomba kila mwenye nayo/nazo nyingine atupie hapa kwani huwa ni elimu na burudani tosha.

1. "Sikiliza ushuhuda huu; mtu mmoja alikuwa na ng'ombe wake. Alikuwa akimfuga nyumbani kwake. Siku moja yule ng'ombe alitumbukia katika shimo refu na mwenye ng'ombe alijaribu kumtoa asiweze. Akaamua aende kazini. Huku nyuma majirani wakajaribu kumfukia kadiri wawezavyo. Kumbe hawakupenda mwenzao awe na ng'ombe. Wakawa wanajitahidi kumfukia ng'ombe. Kumbe kadiri walivyojitahidi, yule ng'ombe alikuwa akijikung'uta na kukanyaga ule mchanga ukamsaidia kupanda juu. Hatimaye akafika juu na kutoka salama shimoni! WAKATI MWINGINE MUNGU HUWAFANYA MAADUI ZAKO KUWA DARAJA LA MAFANIKIO YAKO. MUNGU AKUBARIKI SANA!"

2. MTOTO: Baba kuna tofauti gani kati ya kilichopo katikati ya mapaja ya mama na mapaja yako?
BABA: Kwa mama yako kuna geti la kuingilia PARADISO. Na kwangu kuna ufunguo wa kufungulia hilo geti..
MTOTO: Ulimpa mtu yeyote ufunguo?
BABA: Hapana! Kwanini?
MTOTO: Badili kufuli, yule jirani yetu atakuwa amechongesha ufunguo. Ukiondoka huwa anakuja kufungua. Akifungua
mama anapiga kelele sana. Itakuwa funguo yake kubwa sana. Ataharibu kufuli!

3. "Yule punda aliye mbeba YESU baada ya kuona wamemtandikia nguo, huku wakimshangilia, akajionea fahari kubwa. Hakujua ni kwasababu amembeba YESU ... Siku moja akaamua kwenda Yerusalem peke yake. Akashangaa mbona watu hawamshangilii kama mwanzo?.. Alipofika hekaluni alikimbizwa kwa viboko ile mbaya... Ndugu yangu fahari yako ni kwakuwa umembeba YESU. Usimtue kwani itakuwa mwanzo wa fedheha, aibu na kukataliwa kwako. Usithubutu kumwacha YESU kamwe!"

Umeipenda ipi? Na wewe tupia yako/zako!
 
Wahaya kwa mbwembwe ni nomaaa,! Jamaa ni mhudumu wa mochwari, sasa anavyojitambulisha kwenye harusi, my name is rwechungura mgisha rweyemamu am working with Muhimbili National Hospital, infact profesionally nawahudumia watu ambao madaktari bingwa, wame shindwa kunusuru uhai wao! Watu haaaa rudiaaa tenaa! Chezea wahaya weye hatariii.
 
Mhh, hiyo ya ufunguo na kufuli huo ushauri wa dogo baba akiufuata, dogo ajiandae kwa hekaheka ya mama mpya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom