SLAA's WEBSITE: Are you serious?

Mwaka jana wakati wa kampeni niliandika sana hapa kuhusiana na website ya chadema, nikapigwa mawe kama nini. Kwa chama kama kile kinabid kiwe na site bora ambayo wanaweza kuitumia kuwaikia watu. Pia nimwulie mdau aliteleta hii mada, kwa nini ameweka mpaka details za watu waliocomment huko facebook?
 
Yaani kwa kuchakachua nimewakubali ccm, hii ni ya wapi halafu watu wanakimbilia kukoment negatively bila kuuliza, kweli watanganyika ni wagumu kujisomea na kutafuta, mbona nimeenda sikuona kitu kama hii? Msidanganywe kirahisi! Ni IT hackers wa mafisadi wamewadanganya wavivu wa kufanya utafiti na nyie mkakubali!

Mkuu umesema. Before you article JF na hata ujajadili na watanzania au mtu yeyote yule jitahidi kufanya utafiti wa hali ya juu. Things will cost you. Harakati za ccm kuchafua chama cha Chadema ndizo hizi na wakae wakijua rasmi kwamba "Hawata Fanikiwa Kamwe" Chadema si CUF au UDP. ccm mmekwisha sasa na mwende mkatafute kazi Libya.
 
Kwanza ninalaani yule aliyepachika tovuti ya Chedema iliyochakachuliwa.
Na hili limenifanya kuitafuta tovuti halisi ya Chadema. Mbali na ukurasa wa Dk. Slaa wa kampeni, nimeshindwa kuipata. Nilichogundua ni kurasa ambazo ama hazifunguki au kurasa za wapenzi wa Chadema. Pengine ni uelewa wangu mdogo wa ICT, au pengine haipo. Kama ni hivyo, ninawashauri watu wa ICT wa Chadema kujenga tovuti iliyo makini, inayokuwa "updated", tukikubali ukweli kuwa ICT ni nyenzo bora kwa nyakati tulizonazo kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Kuna yeyote anayo akatupa kiunganishi chake?

Hiyo ni tovuti hewa wala hai exit bila ata kuwa na ICT sio sababu ya kutokujua, hivi nani mpumbavu anayeweza kufanya utoto kama huo...? hii ndi tovuti halisi ya chadema mkuu, gonga hapa..Tovuti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
 
KUTOKUWA KWAO SERIOUS SI KOSA LANGU..... ukishikwa shikamana
 
Ni lini website iliwahi kuwa copied?
Are you serious?

Tukianzia hapo,hoja yako ni dhaifu kwa sababu hujui unachosema,you can't copy a website,but you can use a particular tempelate to create a website!
Kama ni tempelate walitumia,bado kosa lao sio kuweka ramani ya marekani,yawezekana walikuwa wana hamasisha watu walioko marekani!

Kosa lao ni hili,....
Website yao hiyo haiko updated,kwa sasa walipaswa kusema "Dr.Slaa kuelekea 2015" sa sijui kwanini wanasema for 2010!

Huo ni ugonjwa wa website nyingi za vyama,angalia thread yangu hii hapa chini:-

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/121317-vyama-vya-siasa-tanzania-na-website-zao.html

Mkuu html copying inawezekana kwa njia ya mirroring especially robots.txt ikiwa dhaifu. Kwenye Linux wanatumia wget command.
Hata hivyo hii website haijakopiwa na vile vile si ya Obama. Uko sahihi kwamba ishu templete, pengine hawakufanya hacking ya kutosha.

Template yenyewe waliyotumia ni ya best of joomla Hii hapa: Best Of Joomla!

Sina nia mbaya na wahusika ila nimependa tu kunyoosha hiyo technical issue.
 
nimeweka na comment za watu ili kuonyesha michango ya wengine nao ikoje ........... TO BE REALISTIC.......... !
 
Mkuu hiyo ramani ya marekani nahisi umeipandikiza bwana, mbona naona ina hang tu na jama imeziba website original!!??

Nina wasi wasi sivyo inavyoonekana bwana! Acha hizo
 
Mimi pia sikubaliani na hiyo web, maana atawadanganya wasiojua.

Ila cha msingi kwa ICT team ya Chadema ni kuwa up to date, maana kwa kweli lazima tuendane na wakati, website ya Chadema haiwi timely updated. na hilo sio tatizo la Chadema peke yake lakini Chadema inatakiwa kuongoza kwa kila kona, maana Chadema kwa sasa ndiyo inaongoza nchi hii. ndio mfano, ukiona kila kona unazungumzwa ujue wewe ni maarufu either kwa ubaya au kwa uzuri sasa Chadema kinazungumzwa kwa mazuri yake, na umakini wa viongozi wake sasa tujipange hata idara zote ziwe makini.
 
Jamani naona website hii imetoka hewani ila uki google bado unapata face yake, Nadhani Hakukuwa na haja ya kuitoa wale wasaidizi Wa dr Slaa Hebu tujuze pls
 
Back
Top Bottom