Slaa tishio CCM Uchaguzi 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa tishio CCM Uchaguzi 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 7, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sunday, 07 August 2011 | Mwandishi wetu

  MGAWANYIKO wa makundi ya kisiasa ndani ya CCM na utendaji wa Serikali yake unaotia shaka vimechangia kwa kiasi kikubwa kumpandisha chati Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, hadi kuwa tishio kwa nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

  Matokeo ya utafiti uliofanywa hivi karibuni na Taasisi ya Utafiti ya Synovate ni ishara tosha kwamba, kama hali itaendelea hivi ilivyo ndani ya CCM, utawala utaenda kambi ya upinzani na Dk Slaa atakuwa tishio kwa wagombea wote wa urais katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015 kama atagombea.

  Wachambuzi wa mambo ya siasa na wasomi nchini, wanayaona matokeo ya utafiti huo kuwa yanamfanya Dk Slaa, ambaye alikuwa mgombea wa urais katika Uchaguzi Mkuu uliopita kuwa mwiba mkali kwa CCM katika uchaguzi mkuu ujao, kama chama hicho tawala hakuyapatia ufumbuzi mambo yanayokifanya kipoteze mvuto kwa wananchi.

  Matokeo ya utafiti huo si tu kwamba yamweka juu Dk Slaa bali yanaifanya CCM iamke na kuweka mikakati dhabiti kukabiliana na changamoto inazohatarisha nafasi ya chama hicho kuendelea kuongoza nchi.

  Ni dhahiri kuwa Dk Slaa amepata ushindi huo kutokana mambo makubwa matatu ambayo ni, kwa sasa ukimwondoa Rais Kikwete, CCM haina mgombea tishio.
  Pili, utafiti huu unafanyika wakati kuna mgawanyiko mkubwa ndani ya CCM unaochochewa na makundi hasimu ya wanasiasa yanayoviziana na kumalizana, tofauti na miaka iliyopita.

  Tatu, hivi sasa CCM inakabiliwa na changamoto nyingi zinazoifanya ipoteze mvuto. Baadhi ya changamoto hizo ni ugumu wa maisha unaotokana na mfumuko wa bei na kuanguka kwa uchumi, matatizo ya umeme, mgogoro wa bei ya mafuta, kashfa mbalimbali za kifisadi zilizoibuka na zinazoendelea kuibuka na utendaji mbovu wa Serikali uliojionyesha dhahiri katika bajeti ya mwaka huu.

  Nape Mnauye
  Alipoulizwa jana na gazeti hili kuhusu mtazamo wake juu ya matokeo ya utafiti huo kwa uchaguzi wa 2015, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye, alisema hawezi kutoa maoni yake kwa kuwa bado hajasoma ripoti ya utafiti huo.

  Kwa mujibu wa Nape, utafiti unahusisha mambo mengi, ikiwa ni pamoja na namna ulivyofanywa, watu walioulizwa, walipatikana vipi na ulilenga watu wa kada gani.

  "Mimi sijapata ripoti hiyo na nimeagiza ofisi yangu waitafute ripoti hiyo, kwa sasa siwezi kutoa maoni yeyote," alisema Nape.

  Mtazamo wa utafiti
  Utafiti uliofanywa na Synovate kuhusu nafasi ya urais na ripoti kutolewa Oktoba 10, mwaka jana kabla ya uchaguzi mkuu, ulionyesha kuwa mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipata asilimia 61 ya kura zote, akifuatiwa na Dk Slaa wa Chadema ambaye alipata asilimia 16 na nafasi ya tatu ikashikwa na Ibrahim Lipumba wa CUF aliyepata asilimia tano.


  Matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita Rais Kikwete aliibuka mshindi kwa kupata asilimia 61 huku, Dk Slaa akiwa wa pili kwa kupata asilimia 26.

  Lakini katika utafiti huu wa sasa wa taasisi hiyo unaonyesha kuwa kama Rais Kikwete angeamua kujiweka kando na ukaitishwa uchaguzi mkuu sasa, Dk Slaa angeibuka mshindi wa nafasi hiyo.

  Nafasi ya wapinzani
  Ripoti ya Synovate iliyotolewa jijini Dar es Salaam wiki hii inabainisha kuwa, kwa ujumla CCM katika uchaguzi huo ingeanguka na nafasi yake hiyo kuchukuliwa na wapinzani wakiongozwa na Chadema.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo inawapa wapinzani fursa ya ushindi kwa mara ya kwanza, wagombea kutoka vyama vya upinzani wana uwezo wa kupata ushindi wa jumla wa asilimia 67 iwapo uchaguzi ungefanyika sasa.

  Dk Slaa anaongoza katika kundi la wapinzani kwa kupata asilimia 42, akifuatiwa na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, asilimia 14 huku Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe akipata asilimia tisa.

  Kutokana na utafiti huo ni wazi kuwa hali kama itaendelea kama ilivyo hivi sasa ni Dk Slaa anazidi kupanda chati huku wapinzani wake wakizidi kushuka katika medani ya siasa nchini.

  Dk Mkumbo
  Akichambua matokeo ya utafiti huo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Kada wa Chadema, Dk Kitila Mkumbo, alisema utafiti huo ni ishara njema kwa Dk Slaa na onyo kwa CCM kwani haijawahi kutokea kiongozi wa upinzani kuongoza kura za maoni.

  Hata hivyo, alisema licha ya utafiti huo kutoa picha nzuri kwa Chadema, bado una upungufu mwingi.

  Dk Mkumbo alisema kufanya utafiti kama huo wakati watu wametoka kwenye uchaguzi na kuacha mambo ya msingi kama utendaji wa Serikali na kukubalika kwa vyama ni sawa na kuhamisha hisa za watu na kuzima ajenda za maana.

  Kwa mujibu wa Dk Mkumbo, Synovate wangepaswa kufanya utafiti unaohusu utendaji wa Rais Jakaya Kikwete hadi sasa na kukubalika kwa vyama vya upinzani, si kutafiti nani atakuwa rais ikiwa rais aliyepo madarakani angekaa kando.

  "Mimi kama mwanataaluma nadhani utafiti huu una upungufu wa msingi. Huwezi kufanya utafiti wa kutaka maoni kwa kumtoa mtu ambaye alishinda katika uchaguzi na unamuacha aliyemfuatia kwa mbali akipambana na wengine ambao ni dhaifu," alisema Dk Mkumbo.

  Mchungaji Mwamalenga
  Naye Mchungaji William Mwamalanga wa Kanisa la Kipentekoste, alipinga matokeo hayo akisema utafiti huo umekuja haraka sana.

  Aliongeza kuwa muda ulitumika kufanya utafiti huo ni mfupi sana, na yeye kama mtaalamu wa masuala ya utafiti, mambo nyeti kama Siasa na Uchumi si ya kufanyiwa utafiti kwa muda mfupi.

  Mchungaji Mwamalanga pia alikosoa utafiti huo kwa kusema kuwa umekuja wakati nchi ikiwa kwenye matatizo mengi ya kiuchumi na hasa suala la mgao wa umeme, bei ya mafuta na ongezeko la ugumu wa maisha.

  Kuhusu wana CCM walioshiriki katika utafiti huo na kusema kuwa Dk Slaa anafaa kuwa rais kama uchaguzi utafanyika hivi sasa, Mchungaji huyo alisema kuwa wana CCM hao ni ndumila kuwili.

  Mallya wa TGNP
  Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Usu Mallya, alisema ni vema tafiti zinazofanywa hivi sasa zikalenga fursa zilizopo kwa maslahi ya taifa.

  Akifafanua Mallya alisema wakati huu kuna mambo kama mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya ambayo yangepaswa kutiliwa mkazo na si masuala ya uchaguzi kwani nchi ndio kwanza imetoka kwenye uchaguzi.

  "Mimi nadhani hata nyie mnaweza kujiuliza kwa nini utafiti huo uje waka huu? Kuna mambo ya msingi ambayo tukitumia fursa hii yanaweza kuwa na manufaa kwa nchi yetu," alisema na kuongeza:

  "Ni vema kama mtu anafanya utafiti akaelezea mambo ya msingi, kwani kuja na mambo ambayo si ya msingi sana hivi sasa, kutafanya nafasi zilizopo hivi sasa kupotea na hivyo kuja kujuta baadaye."

  Katika kupata maoni juu ya mtu ambaye wangependa awe rais waliuliza: "Mbali na Rais Kiwete, ni mtu gani ungeweza kumchagua kuwa rais iwapo atakuwa miongoni mwa wagombea?"

  Kutoka CCM, kiongozi anayeonekana kukubalika zaidi ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amepata asilimia 12, akiwa nyuma ya Dk Slaa na Profesa Lipumba.
  Hali hiyo inathibitisha kwamba iwapo uchaguzi ungefanyika hivi sasa, Pinda angeambulia nafasi ya tatu.

  Katika utafiti wake huo uliofanywa kati ya Mei 2 hadi 19, mwaka huu, jumla ya watu 1,994 walihojiwa.

  Mbali na Dk Slaa, utafiti huo unatoa pia nafasi kubwa kwa wanasiasa wengine wa upinzani kung'ara katika uchaguzi mkuu ujao, akiwamo Profesa Lipumba na Zitto.

  Wanasiasa wengine wanne wanaofuatia kwa umaarufu na asilimia walizopata kwenye mabano ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli (4), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samweli Sitta (2) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (2).

  Kada wa CCM ambaye hakupenda kutajwa jina lake alisema kilichowaponza baadhi ya vigogo wao, akiwamo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta (2), Naibu Waziri wa Ujenzi,Dk Harrison Mwakyembe (1), Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya (1) na Spika wa Bunge Anne Makinda (1) ni kushiriki katika siasa za makundi.

  Alitoa mfano wa Waziri Mkuu Pinda na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, walipata kura nyingi kunaonyesha kuwa hawajajiingiza katika siasa za makundi ndani ya chama hicho kikongwe nchini.
   
 2. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hata uchaguzi mkuu mwaka jana 2010 Dr. Slaa alishinda hivyo hivyo na alimshinda JK ila walichakachua kama kawaida yao magamba!
   
 3. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Matokeo ya tafiti ya Synovate yanaonesha Dr. wa Ukweli 42%, Prof. Lipumba 14%, Kabwe Zitto 9%. Ukichukua mara mbili ya kura za Prof unapata 28%, mara tatu unapata 42%-hivyo Dr. Slaa ni mara tatu ya Prof. Kwa upande wa Zitto, mara mbili ni 18%, mara tatu ni 27%, mara nne 36%, mara tano ni 45%.

  Hivyo Zitto afyate mkia kwa Dr. aache mbwe mbwe na kukivuruga chama, hawezi kumfikia, aishie kwenda Sudan Kusini na rais wa magamba. Kuhusu Dr. amekuwa akipanda kwa kasi sana. Oct. 10, 2010, kabla ya uchaguzi Synovate walisema Dr. 16%, Kiwete 61%, matokeo ya uchaguzi 31 Oct. Dr. 26%, Kiwete 61%-alisizi wakati Dr. 10% ziliongezeka.  Matokeo ya juzi Kiwete angepata 0% km angehusika. Dr. 46%, ongezeko 20% toka 26% matokeo ya uchaguzi. Nawaasa Prof. na Zitto wanyoshe mikono juu, wapige 'salute' kwa Dr. CCM ndo kabisa, wameshuka daraja, hata wakisajiri upya hawawezi kunyakua kombe 2015, hata ligi ndogo ya Igunga wasitegemee ushindi. Refa wao NEC na washika vibendela- Shimbo, polisi na Intelligensia feki- wajiandae kwenda CELLO.

  Mnasemaje wana JF?
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mawazo ya chooni.
  Labda kama unaongelea kule uchagani na kule karatu
   
 5. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hata leo hii wakiitisha uchaguzi slaa hatashinda. Hebu akajaribu ubunge kule igunga kama atapa. hizo ni ndoto za mchana kweupe.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu ukipenda chongo.......
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu nawaeleza watu ukweli tu. unajua wengi hatuipendi ccm lakini mwelekeo wa chadema hauko sawa. thats why mtu anaona bora hata hii ccm mara 100 kuliko chadema. chadema wanainfluence baadhi ya maeneo tu ya nchi na vyombo vya habari vinawasaport sana. tunajua vingi ni vya wachaga au vina mikono ya wachaga, na chadema huwezi itenganisha na hawa watu. lakini ungejua ukija maeneo haya ya kwetu na yanayofanania chadema inanuka .
   
 8. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Cdm chama makini na ni chama safi.dr endelea kuelimisha watanzania.
   
 9. p

  plawala JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda kama wewe ndiye utakayekuwa unahesabu kura
   
 10. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  siaende akajaribu kugombea igunga? au igunga si sehemu ya TZ? kwa nini tunaandikia mate?
   
 11. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Iguga atamwakilisha nani? Ni vizuri ukajifunza na kuelewa tofauti ya uwakilishi na kuafuta "ajira"!
   
 12. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Dr kazana kuelimisha watu nchi hii itakuja mikononi mwako muda si mrefu,tuombe uzima na Mungu azidi kutubariki, wee need freedom
   
 13. M

  Magarinza Senior Member

  #13
  Aug 7, 2011
  Joined: May 9, 2008
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />
  kwenu wapi we kiazi, isijekuwa unaishi uganda.
   
 14. nachid

  nachid JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
   
 15. Lamtongi

  Lamtongi Member

  #15
  Aug 7, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Aug 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Ukiondoa uwezekano wa ccm kutuburuza chaguzi ijayo na katiba hii iliyokithiri kwa viraka au kutengeneza ya kwao waonayo itawanufaisha wao na hivyo kuiba kura kwa mara nyingine tena..........................uwezekano wa Dr. Slaa na chadema kutwa dola sasa siyo hadithi tena ila ni ukweli usio na ubishi...........................uonapo kwenye kura za maoni ccm haina mgombea mtarajiwa mwenye mvuto kwa wapigakura................hapo ni wazi kuwa ccm's game is up for grabs.............................labda TISS na NEC watafute karatasi nyingine za kupigia kura ambazo zinafutikafutika ili kujenga mazingira ya dhuluma dhidi ya wapigakura ambao tumechoshwa na utawala wa ccm usio na mwelekeo zaidi ya uporaji wa mali za taifa na kumilikisha wageni...................................

  soma habari hii kwa ufafanuzi zaidi Slaa tishio CCM Uchaguzi 2015
   
 17. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #17
  Dec 9, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Kwa muda sasa imeoneka kuwepo kwa jitihada za nguvu toka kwa wana CCM kumjadili na kujaribu kumchafua Kamanda wetu mkuu, Dr. Slaa kwa kila hali. Hii inatokana na jinsi gani ambavyo amekuwa mwiba mkali na kuwanyima usingizi hawa magamba wakiongozwa na mwimbaji wa BONGO FLAVA mashuhuri, kijana Nape Nnauye.

  Labda kwa kuwasaidia inafaa kuelewa kuwa matokeo ya mafanikio yote haya ya chama chetu cha cdm, hayatokani na Dr. Slaa pekee yake! Bali ni mikakati madhubuti iliyotengenezwa na mfumo mzima wa uongozi wa chama, hivyo kwenu ninyi wote mnaofikiri kuwa kumshambulia Dr. Slaa kwa ndoto za kuua nguvu ya chama, hapo bado mnanawa mikono kwa kujipuliza na midomo.

  Kumbukeni Dr. Slaa na wengine wengi watapita lakini chama kitabaki imara.

  Tafakalini upya.
   
 18. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #18
  Dec 9, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Mkuu Dr.Slaa ni mti wenye matunda so ni halali yake upigwe mawe, pia jiulize why daily Dr.slaa? And why not Shibuda?

  Shardcole.
   
 19. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #19
  Dec 9, 2012
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 44,523
  Likes Received: 25,351
  Trophy Points: 280
  Kwa Nape hana lingine analoweza , magamba yamemshinda amebakisha matusi tu , bali ana ' akili nyingi ' ametambua kwamba ili akubalike kwa mwenyekiti lazima ashambulie Dr slaa , fuatilia bajeti ya waziri kivuli wa fedha , pamoja na matusi yake ndugu Mwigulu mchemba kasifiwa na Mwenyekiti na kupandishwa cheo ! Shortly ni kwamba Kikwete anamuogopa Dr slaa kuliko kitu chochote , kwa hiyo wanaomtukana anawaona lulu , mtazame Shibuda , kwa Kikwete kageuka lulu .
   
 20. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #20
  Dec 9, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,095
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nape haliwezi game la siasa,ni KELELE TU NA AJUE KUWA KELELE ZA CHURA HAZIMZUII NG'OMBE KUNYWA MAJI TENA KW RAHA ZAKE!
   
Loading...