funaku
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 39,119
- 31,639
Kama kweli CHADEMA iko serious kutaka kuingia ikulu ni lazima ikapanga wagombea wake kama nilivyopendekeza yaani mgombea urais awe ni Dr slaa na mgombea mwenza awe ni Zitto. Mchanganyiko wa timu hii kwa order ya Slaa-Zitto ni mchanganyiko wenye uwezo wa kuzoa kura nyingi.
CHADEMA kama mnanisikia zingatieni hili hamtajuta. Malizeni tofauti za watu hawa kama zipo na muanze maandalizi ya kuwauza kwa wananchi kama timu!
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
- Timu hii ina uwezo wa kuvuta vijana hasa ukizingatia wote Slaa na Zitto ni maswahiba wakubwa wa vijana.
- Timu hii yaweza kuvuta wazee kwa kutumia uzee na busara za Dr Slaa na busara za zitto.
- Timu hii yaweza kuvuta wakristu kwa waislamu
- Timu hii yaweza kuvuta watu wa mikoa mbalimbali hasa ile ya kanda za magharibi ambapo M4C imesuasua.hapa kwa wale wa kaskazini(especially wachaga) wasilete wivu na minongo'ono bali wajue hii ni timu ya kuwapa kiti cha urais kama wanataka mamlaka watayapata kupitia uwaziri n.k lakini for the sake ya ushindi ni muhimu kuisupport timu hii.
- kwa upande wa wanawake inaweza kuwa tatizo lakini hii sio shida kwani wanawake wengi wa 2015 wataangukia kwenye kundi la vijana
CHADEMA kama mnanisikia zingatieni hili hamtajuta. Malizeni tofauti za watu hawa kama zipo na muanze maandalizi ya kuwauza kwa wananchi kama timu!
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA