mimi binafsi Slaa alinivutia pale alipolalamika kuwa wabunge wanalipwa pesa nyingi lakini duuh hili halikupata kuungwa mkono na mbunge yeyote yule wa chama chake, upinzani wala sisiemu sijui kwasasa wakati kuna dalili kadhaa kwamba watz tunaweza kumpa ridhaa atuongoze sijui atathubutu kuliendeleza hili?
Dirty POLITICS!Dr. W.Slaa ana sifa nyingi sana za uongozi,, lakini mojawapo ya sifa za kiongozi ni kutoa kauli zenye uhakika hasa unapokuwa kiongozi mkuu. Slaa anatarajiwa kuwa Rais,, sifa hii ya umakini wa kauli anapungukiwa sana hasa ukizingatia kauli kadha ambazo amewahi kuzitoa katika kipindi kifupi cha nyumba.
Mathalani kuhusu kontena la kura, kifo cha RC shinyanga na nyingine nyingi. Hizi ni kauli nzito ambazo kiongozi makini asingeweza kuzitoa hadharani kabla hajapata uhakika..
Nashauri ikiwa atakuwa Rais basi ajifunze kuwa na subira, ukisikia jambo usifanye pupa na kuropoka hadharani kuuvuruga muamana.
Bado naendelea na uchunguzi kujua kama kweli Mbowe na SLAA ni waadilifu. Isije kuwa ni usanii tu.
Nitarudi
Usisahau pia yeye analipwa na Chama chake sh. milioni 13 kila mwezi kwa mkataba waliokubaliana kabla ya uchaguzi hivyo angeanza kwanza na kupunguza mshahara wake ndipo ageukie wa Wabunge!!!
sasa mkuu kama wanaolipwa ni waajiriwa tuu ambao kimsingi ni wachache sana sasa haya mamilioni ya SABODO na mabilioni kutoka nje ya nchi wanayopewa CDM yanatumika kwenye nini? maana ofisi za kuhesabu,tungesema wanalipia pango,umeme maji nk! pesa zinaenda wapi? tunaomba tupewe mchanguo la sivyo kuna ufisadi hapoUna uhakika na unachokisema , CDM, wanaolipwa ni waajiriwa tu , david kafulila alikuwa analipwa pamoaja na waajiriwa wenzake, lakini viongozi wa juu including Zitto kabwe wanafanya kazi za kujitolea mkuu,
mishahara hiyo CDM haipo labda Utuambie tambwe Hizza analipwa shillingi ngapi tena ana cheo ambacho hata kwenye katiba ya CCM hakipo
acha KUKURUPUKA tu from no where unasema upupu,
crap
Tell me about it!1 Nakwambia hawa wote ni power struggle tu ndiyo inawasumbua. Leo hii na anyoshe mkono mbunge wa CDM au chama kingene chochite aliyekataa Mil 90 za gari? Yu wapi mwenye uchungu wa kweli wa nchi Tanzania? Nani aliyemuunga mkono Slaa juu ya mshahara wa wabunge? Wenzetu wanakula bata sisi huku ndiyo tunatukanana. Ndiyo maana niliacha ushabiki hata wa mpira,, timu ifungwe eti na chakula ususe? Kocha na hata wachezaji hawakujui na wanakula pesa yao kama kawaida!! Acha nikanunulie dagaa wanangu hapa tunadanganyana tu hakuna CHADEMA wala nini,, wote walaji tu.Usisahau pia yeye analipwa na Chama chake sh. milioni 13 kila mwezi kwa mkataba waliokubaliana kabla ya uchaguzi hivyo angeanza kwanza na kupunguza mshahara wake ndipo ageukie wa Wabunge!!!
Kweli Dr. kiboko bado tu na kampeni zenu kumhusu.watu hawana naji safi,mfumuko wa bei juu,barabara mbovu,shule ni magofu.Embu badilikeni wakumbukeni wananchi maskini waliowapa kura..wanataabika
Dr. W.Slaa ana sifa nyingi sana za uongozi,, lakini mojawapo ya sifa za kiongozi ni kutoa kauli zenye uhakika hasa unapokuwa kiongozi mkuu. Slaa anatarajiwa kuwa Rais,, sifa hii ya umakini wa kauli anapungukiwa sana hasa ukizingatia kauli kadha ambazo amewahi kuzitoa katika kipindi kifupi cha nyumba.
Mathalani kuhusu kontena la kura, kifo cha RC shinyanga na nyingine nyingi. Hizi ni kauli nzito ambazo kiongozi makini asingeweza kuzitoa hadharani kabla hajapata uhakika.
Nashauri ikiwa atakuwa Rais basi ajifunze kuwa na subira,, ukisikia jambo usifanye pupa na kuropoka hadharani kuuvuruga muamana.
Bado naendelea na uchunguzi kujua kama kweli Mbowe na SLAA ni waadilifu. Isije kuwa ni usanii tu. Nakaribisha matusi.
Nitarudi
Mpuuzi kweli wewe,we slaa si alisha kujibu upuuzi wako huo kwenye thread ya liberia?
Bahati yako hamna mods wakatili kama mimi,ungekuwa ukirudia thread moja mara nyingi nakufungia kuanzisha thread
Salimia,
Salamu toka Monrovia. Kama sikosei nilikwisha kufanya posting kwenye Jamvi hili kutoka hapa Monrovia tulipokuwa tu tumewasili hapa tarehe 9 Machi, 2011. Nilieleza kuwa tuko hapa na Mheshimiwa Mwenyekiti wa Taifa kuhudhuria Mkutano wa Mwaka wa Democratic Union of Africa, (DUA) ambayo wengi wenu watakumbuka hadi 2009 Chadema ilikuwa Secretariat, na NPP ya Ghana ilikuwa mwenyekiti.
DUA ni Chapter ya Africa ya vyama vya mrengo wa "Centre Centre Parties" katika mfumo wa vyama vya siasa Duniani na wote tunaunganika katika International Democratic Union kwa Dunia nzuri. Wanachama ni pamoja na vyama tawala katika nchi zao na au vyama vya upinzani ikikumbukwa kuwa kutawala au kutokutawala kwa wanaoelewa demokrasia ni swala la kupokezana vijiti. Hivyo kinachotuunganisha ni "values" au mambo tunayosimamia katika jamii.
Kama nilivyosema huu ni mkutano wa Mwaka yaani Annual General meeting, na wajumbe ni wenyeviti na Makatibu wakuu. Si kosa lako inawezekana umechangia bila kufahamu Katiba ya umoja huo. Mkutano una sehemu kubwa mbili, Deliberative Session, ambayo theme yake ni "Re-bilding the blocks of Democracy in Africa". Mhe. Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinani Bungeni alitoa Mada kuhusu "Consolidating Democracy -Tanzania Election and Aftermath".
Mkutano pia umejadili Trends zinaziojitokeza katika Demokrasia Afrika mifano ya Afrika Kaskazini, Ivory Cost,Kenya na Zimbabwe. Hakuna siri katika Democrasia na kesho Mkutanpo utatoa Tamko rasmi kutokana na mambo yaliyojitokeza katika deliberative Session. Sehemu ya pili na maswala zaidi ya uongozi wa umoja wenyewe Dua. Nadhani ulinganisho na upande mwingine ungelikuwa na maana iwapo "wakubwa" hao wangelikuwa wanahudhuria tu semina ambayo hata mtu mwingine angeliweza kuhudhuria.
Mzushi tu hana lolote na hafai kupewa nchi sababu yeye na wasaidizi wake hawako makini katika kupokea na kutoa habari