Slaa, Mbowe wamkaanga JK

Mkulu anakura rinchi tu! safari kila siku na anapokwenda ninavyofahamu huwa anaongozana na umati wa wapambe hapo ndipo pesa ya walala hoi inapoishia!
 
Eti Kikwete kaenda kusuluisha mgogoro wa Ivory coast? Hivi hana aibu huyu bwana? Yeye mwenyewe kajaa migogoro ya wizi wa kura kibao! Kaiba kura na kusema twende mahakamani. Sasa na yeye si awaachie waende mahakamani? anakwenda kusuruhisha nini? damn!
 
Hakuna chama Duniani ambacho kitamuruhusu kila anayetaka kugombea afanye hivyo bila kuchujwa. Kafulila unavyomuona ni mtu wa kuachiwa chama! Hata huyo Zitto! Na huwezi kusema waache eti demokrasia itawaondoa.

Unaweza kujikuta unakuwa na chama chenye m/kiti kama Kikwete na katibu mkuu kama Makamba. Bado CCM wanajiita chama kikongwe.

Hao ni watu ambao ukiwaonyesha cheki, wanahamisha mawazo ya chama kabla hata hawajafika benki.


he he he! ndiyo NEC nao wanavyosema you can't give country to Chadema, CUF, NCCR n.k au sio? democracy is not logic sometime....angalia Zuma south africa!!!
 
Safi sana Mkuu Webby.............

Hivi ilikuwaje wakati wa Mh Kafulila akiwa Chadema................ilikuwaje mpaka akatoka CDM?

Ogah acha uchokozi you know in and out, Kafulila aliitwa sisimizi, alikuwa sahihi kundoka, ila aliyoyasema baada ya kutoka CDM personally yalinikera sana na personally naona kama ni mjasiriamali tu! alitupa picha ya wapinzani wetu wengi
 
CHADEMA ni vigumu kuchukua nchi, kwa sababu hawana miongozo ya chama, hawana darubini wao sera zao zinategemea matukio ya viongozi ya leo. Ndio maana ni rahisi sana kuzi obsorb hoja zao. si mliona jinsi hoja ya katiba ilivyonyonywa , sasa wamehamia tukio la gongo la mboto,Teh teh teh teh wanachekesha sana.

Leo wanamshambulia Kikwete hafai sasa 2015 mgombea mpya naye sijui watamjengea hoja gani za kutofaa. CHADEMA ni walewale tu si unaona siku hizi wanajiita CDM.
 
Naona Chadema wameishiwa na sera, hawana kipya ila majungu, fitina na hoja zisizo na maana hata chembe.

Kuwepo au kutokuwepo nchini Rais si hoja ya msingi, kwani huko alikokwenda alienda kucheza?

Wanatubowa na vijineno neno vya ufataani na siasa za kuwabagua wananchi, halafu wanaongelea udini? Wamesahau kuwa kanisa liliwakataa waumini kwa kuwa wameipigia kura CCM? wamesahau Slaa alipoifananisha CCM na Taliban? Sasa hapo nani ni mdini?

CHAMAANA NI KIPI ALICHO FANYA? BAGBO ALIMWAMBIA KAMA WEWE HUJAIBA KURA ENDELEA KUNISHAURI NITOKE MADARAKANI IKABIDI KIKWETE ARUDI
TEh teh tehe teh ethe tehe!!!!!

Toa Boriti kwenye Jicho Lako ndipo utaona Kibanzi kwenye Jicho la Mwenzio!
jk ANA SIFA GANI ZA KUSULUHISHA MGOGORO WA WIZI WA MADARAKA WAKATI KWAKE MOTO UNAWAKA NA HAJAWEZA KUUZIMA?????????????
Usitupotoshe tena ukome!!!!!!!!!!!!!!!!
 
slaa, mbowe wamkaanga jk

• wamshangaa kwenda nje wakati wa matatizo

na mwandishi wetu

mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema), freeman mbowe na katibu mkuu wa chama hicho, dk. Willibrod slaa, wamemrushia kombora rais jakaya kikwete kuwa analea nyufa za udini, ukabila pamoja na kukataa kutoa fedha za kuharibu mabomu yaliyozua balaa kwa wakazi wa gongo la mboto.

viongozi hao walisema rais kikwete anashindwa kudhibiti nyufa za udini na ukabila kwa sababu ni mkakati wa chama cha mapinduzi (ccm) wa kuidhoofisha chadema ambayo hivi sasa imejizolea sifa na wanachama wengi, kwa sababu ya uimara wake wa kukiwajibisha chama tawala na serikali yake.

wakizungumza kwa wakati tofauti katika viwanja wa shule ya mkendo mjini musoma jana, viongozi hao walisema kwa hali ilivyo, rais kikwete, amekosa sifa za kuwa kiongozi imara.

mbowe alisema rais kikwete ameshindwa kudhibiti nyufa za udini na ukabila ambao umeonekana dhahiri kuanza kuota mizizi hapa nchini, hivyo zinahitajika juhudi za haraka na makusudi kuuwajibisha utawala wake ili kuinusuru nchi.

“taifa limeingia kwenye udini na ukabila ambao rais wa nchi ameshindwa kuudhibiti...sisi tunafahamu ajenda ya udini na ukabila ni mkakati wa ccm wa kutaka kuimaliza chadema, jambo ambalo kamwe hatulikubali,” alisema.

mbowe ambaye pia ni mbunge wa hai na waziri mkuu kivuli, aliwataka watanzania kuunganisha nguvu zao kwa pamoja katika kulikomboa taifa hasa katika kipindi hiki ambacho umasikini unazidi kushamiri siku hadi siku.

“tukiwaachia hawa ccm waendelee kututawala kama wanavyotaka kamwe umaskini hauwezi kutoweka miongoni mwetu, uwezo wa kubadilisha uongozi na hali zetu za kimaisha tunao, kwanini tunashindwa kuutumia?” alihoji.

kuhusu uundwaji wa katiba, mbowe aliionya serikali kuwa ni vema isifanye hila mara baada ya wananchi kutoa maoni yao, kwani mchezo wowote utakaofanywa kwa lengo la kupinga maamuzi ya umma hukumu yake itakuwa kubwa kama ile inayoonekana hivi sasa nchini libya au ile iliyotokea misri.

naye dk. Slaa, alisema kuwa amesikitishwa na milipuko ya mabomu iliyotokea gongo la mboto ambayo kwa kiasi kikubwa imesababishwa na uzembe wa serikali ambayo iligoma kutoa fedha kwa ajili ya kuyaharibu mabomu hayo.

alibainisha kuwa anazo taarifa kuwa rais kikwete alilinyima jeshi hilo fedha za kuharibu mabomu hayo ambayo yalionekana kwisha muda wake miaka miwili iyopita.

“ninayo taarifa kwamba serikali ya rais kikwete iliombwa fedha mara mbili za kuharibu mabomu lakini ilishindwa kufanya hivyo...hali hiyo ndiyo iliyosababisha vifo vya watanzania mbagala na sasa gongo la mboto,” alisema dk. Slaa.

aliongeza kuwa, kutokana na uzembe huo, anamtaka waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa, dk. Hussein mwinyi, pamoja na mkuu wa majeshi nchini, jenerali davis mwamnyange, kujiuzulu mara moja nyadhifa zao na iwapo watashindwa, basi rais kikwete awafukuze.

alisema watanzania hawawezi kuendelea kuvumilia viongozi kama hao wazembe wa kazi na kwamba ni vema waziri mwinyi akaiga mfano wa baba yake, ali hassan mwinyi, aliyeachia ngazi kutokana na mauaji yaliyotokea wakati akiwa waziri wa mambo ya ndani.

“tunamtaka waziri mwinyi ajiuzulu, na akishindwa basi rais kikwete amfukuze kazi huyu mtu pamoja na mkuu wa majeshi...wananchi wameshachoka kuona usanii wa uongozi,” alisema.

mbowe na slaa waliongeza kuwa wamemshangaa rais jakaya kikwete kwa kuacha msiba wa watanzania waliokufa kwa mabomu ya gongo la mboto, kisha kwenda nchini mauritania kusuluhisha mgogoro wa kisiasa wa ivory coast.

walisema ni aibu kwa kiongozi wa wananchi kuacha msiba mkubwa nchini kwake na kukimbilia nje ya nchi kwenda kusuluhisha mambo ya nchi nyingine.
“kwenda mauritania kwa rais kikwete ni kuwadhalilisha watanzania ...ni sawasawa na baba mwenye familia kuacha watoto wake wanakufa njaa, yeye anakwenda kutoa chakula nyumba ya jirani,” alisema katibu mkuu wa chama hicho, dk. Willibrod slaa.

katika hotuba yake, dk. Slaa alisema kamwe watanzania hawawezi kuvumilia kuona usaliti wa namna hiyo unafanywa na mtu mkubwa kama rais kikwete, ambaye ndiye amiri jeshi muu wa jeshi la wananchi wa tanzania (jwtz).
katika hatua nyingine, alimtaka rais kikwete na serikali yake kuitaifisha mitambo ya dowans, kwani mitambo hiyo imeingizwa nchini kwa njia za kitapeli na ujanja ujanja, kinyume cha sheria za nchi.


zote ni kelele za mlango ambazo hazimzii mwenye nyumba .........
 
[FONT=georgia, bookman old style, palatino linotype, book antiqua, palatino, trebuchet ms, helvetica, garamond, sans-serif, arial, verdana, avante garde, century gothic, comic sans ms, times, times new roman, serif]A chief is a man who assumes responsibility. He says "I was beaten," he does not say "My men were beaten." ~Antoine de Saint-Exupery[/FONT]
 
zote ni kelele za mlango ambazo hazimzii mwenye nyumba .........
[FONT=georgia, bookman old style, palatino linotype, book antiqua, palatino, trebuchet ms, helvetica, garamond, sans-serif, arial, verdana, avante garde, century gothic, comic sans ms, times, times new roman, serif]The kindest word in all the world is the unkind word, unsaid. ~Author Unknown[/FONT]
 
Ama kweli umefulia km chichiem yako, umesahau kuwa icho chama chenu kongwe kinatumai sera zetu? eboo! yan had aibu, we ngoja siku tukiingia madarakani ndo utaweza kuchambua mbivu za chadema na mbovu za kwenu coz sa iv nyie wenye vichwa vigumu ni ngumu kuitambua nia yetu ni nini kwa nchi hii.
 
Alitaka urais ili asafiri na kula raha sio kuumiza kichwa na matatizo ya wadanganyika!
Hapo umenena sawa sawa Lizzy, ila ngoja tuwasikie GeniusBrain na wenzake wataibua hoja zipi kutetea ?
 
Back
Top Bottom