Slaa, Mbowe wamkaanga JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa, Mbowe wamkaanga JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 27, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,947
  Trophy Points: 280
  Slaa, Mbowe wamkaanga JK

  • Wamshangaa kwenda nje wakati wa matatizo

  na Mwandishi wetu

  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, wamemrushia kombora Rais Jakaya Kikwete kuwa analea nyufa za udini, ukabila pamoja na kukataa kutoa fedha za kuharibu mabomu yaliyozua balaa kwa wakazi wa Gongo la Mboto.

  Viongozi hao walisema Rais Kikwete anashindwa kudhibiti nyufa za udini na ukabila kwa sababu ni mkakati wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kuidhoofisha CHADEMA ambayo hivi sasa imejizolea sifa na wanachama wengi, kwa sababu ya uimara wake wa kukiwajibisha chama tawala na serikali yake.

  Wakizungumza kwa wakati tofauti katika viwanja wa Shule ya Mkendo mjini Musoma jana, viongozi hao walisema kwa hali ilivyo, Rais Kikwete, amekosa sifa za kuwa kiongozi imara.

  Mbowe alisema Rais Kikwete ameshindwa kudhibiti nyufa za udini na ukabila ambao umeonekana dhahiri kuanza kuota mizizi hapa nchini, hivyo zinahitajika juhudi za haraka na makusudi kuuwajibisha utawala wake ili kuinusuru nchi.

  “Taifa limeingia kwenye udini na ukabila ambao rais wa nchi ameshindwa kuudhibiti...sisi tunafahamu ajenda ya udini na ukabila ni mkakati wa CCM wa kutaka kuimaliza CHADEMA, jambo ambalo kamwe hatulikubali,” alisema.

  Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Waziri Mkuu Kivuli, aliwataka Watanzania kuunganisha nguvu zao kwa pamoja katika kulikomboa taifa hasa katika kipindi hiki ambacho umasikini unazidi kushamiri siku hadi siku.

  “Tukiwaachia hawa CCM waendelee kututawala kama wanavyotaka kamwe umaskini hauwezi kutoweka miongoni mwetu, uwezo wa kubadilisha uongozi na hali zetu za kimaisha tunao, kwanini tunashindwa kuutumia?” alihoji.

  Kuhusu uundwaji wa Katiba, Mbowe aliionya serikali kuwa ni vema isifanye hila mara baada ya wananchi kutoa maoni yao, kwani mchezo wowote utakaofanywa kwa lengo la kupinga maamuzi ya umma hukumu yake itakuwa kubwa kama ile inayoonekana hivi sasa nchini Libya au ile iliyotokea Misri.

  Naye Dk. Slaa, alisema kuwa amesikitishwa na milipuko ya mabomu iliyotokea Gongo la Mboto ambayo kwa kiasi kikubwa imesababishwa na uzembe wa serikali ambayo iligoma kutoa fedha kwa ajili ya kuyaharibu mabomu hayo.

  Alibainisha kuwa anazo taarifa kuwa Rais Kikwete alilinyima jeshi hilo fedha za kuharibu mabomu hayo ambayo yalionekana kwisha muda wake miaka miwili iyopita.

  “Ninayo taarifa kwamba serikali ya Rais Kikwete iliombwa fedha mara mbili za kuharibu mabomu lakini ilishindwa kufanya hivyo...hali hiyo ndiyo iliyosababisha vifo vya Watanzania Mbagala na sasa Gongo la Mboto,” alisema Dk. Slaa.

  Aliongeza kuwa, kutokana na uzembe huo, anamtaka Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, pamoja na Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Davis Mwamnyange, kujiuzulu mara moja nyadhifa zao na iwapo watashindwa, basi Rais Kikwete awafukuze.

  Alisema Watanzania hawawezi kuendelea kuvumilia viongozi kama hao wazembe wa kazi na kwamba ni vema Waziri Mwinyi akaiga mfano wa baba yake, Ali Hassan Mwinyi, aliyeachia ngazi kutokana na mauaji yaliyotokea wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

  “Tunamtaka Waziri Mwinyi ajiuzulu, na akishindwa basi Rais Kikwete amfukuze kazi huyu mtu pamoja na Mkuu wa Majeshi...wananchi wameshachoka kuona usanii wa uongozi,” alisema.

  Mbowe na Slaa waliongeza kuwa wamemshangaa Rais Jakaya Kikwete kwa kuacha msiba wa Watanzania waliokufa kwa mabomu ya Gongo la Mboto, kisha kwenda nchini Mauritania kusuluhisha mgogoro wa kisiasa wa Ivory Coast.

  Walisema ni aibu kwa kiongozi wa wananchi kuacha msiba mkubwa nchini kwake na kukimbilia nje ya nchi kwenda kusuluhisha mambo ya nchi nyingine.
  “Kwenda Mauritania kwa Rais kikwete ni kuwadhalilisha Watanzania ...ni sawasawa na baba mwenye familia kuacha watoto wake wanakufa njaa, yeye anakwenda kutoa chakula nyumba ya jirani,” alisema Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.

  Katika hotuba yake, Dk. Slaa alisema kamwe Watanzania hawawezi kuvumilia kuona usaliti wa namna hiyo unafanywa na mtu mkubwa kama Rais Kikwete, ambaye ndiye Amiri Jeshi Muu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
  Katika hatua nyingine, alimtaka Rais Kikwete na serikali yake kuitaifisha mitambo ya Dowans, kwani mitambo hiyo imeingizwa nchini kwa njia za kitapeli na ujanja ujanja, kinyume cha sheria za nchi.
   
 2. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  mapambano yanaendelea
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,947
  Trophy Points: 280
  Nchi yako imejaa matatizo chungu nzima wewe huyooooo Kiguu na njia! Angeweza kudelegate na kumuachia Membe afanye safari hiyo kwa niaba yake

  [​IMG]
  CONFLICT RESOLUTION: PRESIDENT Jakaya Kikwete is welcomed by his host, Ivorian President Laurent Gbagbo (right) on his arrival at Felix Houphouet-Boigny International Airport, Ivory Coast, where he is taking part in resolution of a conflict between President Gbagbo and his opponent, Mr Allasane Ouatarra. President Kikwete is a member of the high level AU Panel working for the solution of the post-election crisis in the West African country. (Photo by Freddy Maro)
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Alitaka urais ili asafiri na kula raha sio kuumiza kichwa na matatizo ya wadanganyika!
   
 5. s

  sentimental Member

  #5
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 3
  This is so true. Hata mimi nilijiuliza hivi hayo mabomu yalivyotokea ina maana hakuweza kutuma ujumbe halafu yeye akae nyumbani...Ina maana huo mkutano usingeweza kuwa mkutano bila yeye? I'm new to this site and I really like it so far....
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,947
  Trophy Points: 280
  Tumeshamstukia atuachie nchi yetu ili tupate kiongozi mwenye sifa ya kuiongoza na siyo huyu ambaye hana sifa hata ya kuwa mjumbe wa nyumba kumi kumi. Nchi inazidi kwenda mrama kutokana na uongozi wake finyu na usio na maadili.

 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mwana JF Babu Atakakusema, jaribu kuhariri habari unapoileta hapa ili iwe na mfumo wenye mtiririko mzuri. Hakuna umuhimu wa kukopi kila kitu hata matangazo ya sayari. Bila kusahau source ya habari kama umeikopi kutoka chanzo kingine cha habari. Angalia mfano huu hapo chini.

  Slaa, Mbowe wamkaanga JK
  - Wamshangaa kwenda nje wakati wa matatizo

  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, wamemrushia kombora Rais Jakaya Kikwete kuwa analea nyufa za udini, ukabila pamoja na kukataa kutoa fedha za kuharibu mabomu yaliyozua balaa kwa wakazi wa Gongo la Mboto.

  Viongozi hao walisema Rais Kikwete anashindwa kudhibiti nyufa za udini na ukabila kwa sababu ni mkakati wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kuidhoofisha CHADEMA ambayo hivi sasa imejizolea sifa na wanachama wengi, kwa sababu ya uimara wake wa kukiwajibisha chama tawala na serikali yake.

  Wakizungumza kwa wakati tofauti katika viwanja wa Shule ya Mkendo mjini Musoma jana, viongozi hao walisema kwa hali ilivyo, Rais Kikwete, amekosa sifa za kuwa kiongozi imara.

  Mbowe alisema Rais Kikwete ameshindwa kudhibiti nyufa za udini na ukabila ambao umeonekana dhahiri kuanza kuota mizizi hapa nchini, hivyo zinahitajika juhudi za haraka na makusudi kuuwajibisha utawala wake ili kuinusuru nchi.

  “Taifa limeingia kwenye udini na ukabila ambao rais wa nchi ameshindwa kuudhibiti...sisi tunafahamu ajenda ya udini na ukabila ni mkakati wa CCM wa kutaka kuimaliza CHADEMA, jambo ambalo kamwe hatulikubali,” alisema.

  Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Waziri Mkuu Kivuli, aliwataka Watanzania kuunganisha nguvu zao kwa pamoja katika kulikomboa taifa hasa katika kipindi hiki ambacho umasikini unazidi kushamiri siku hadi siku.

  “Tukiwaachia hawa CCM waendelee kututawala kama wanavyotaka kamwe umaskini hauwezi kutoweka miongoni mwetu, uwezo wa kubadilisha uongozi na hali zetu za kimaisha tunao, kwanini tunashindwa kuutumia?” alihoji.

  Kuhusu uundwaji wa Katiba, Mbowe aliionya serikali kuwa ni vema isifanye hila mara baada ya wananchi kutoa maoni yao, kwani mchezo wowote utakaofanywa kwa lengo la kupinga maamuzi ya umma hukumu yake itakuwa kubwa kama ile inayoonekana hivi sasa nchini Libya au ile iliyotokea Misri.

  Naye Dk. Slaa, alisema kuwa amesikitishwa na milipuko ya mabomu iliyotokea Gongo la Mboto ambayo kwa kiasi kikubwa imesababishwa na uzembe wa serikali ambayo iligoma kutoa fedha kwa ajili ya kuyaharibu mabomu hayo.

  Alibainisha kuwa anazo taarifa kuwa Rais Kikwete alilinyima jeshi hilo fedha za kuharibu mabomu hayo ambayo yalionekana kwisha muda wake miaka miwili iyopita.

  “Ninayo taarifa kwamba serikali ya Rais Kikwete iliombwa fedha mara mbili za kuharibu mabomu lakini ilishindwa kufanya hivyo...hali hiyo ndiyo iliyosababisha vifo vya Watanzania Mbagala na sasa Gongo la Mboto,” alisema Dk. Slaa.

  Aliongeza kuwa, kutokana na uzembe huo, anamtaka Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, pamoja na Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Davis Mwamnyange, kujiuzulu mara moja nyadhifa zao na iwapo watashindwa, basi Rais Kikwete awafukuze.

  Alisema Watanzania hawawezi kuendelea kuvumilia viongozi kama hao wazembe wa kazi na kwamba ni vema Waziri Mwinyi akaiga mfano wa baba yake, Ali Hassan Mwinyi, aliyeachia ngazi kutokana na mauaji yaliyotokea wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

  “Tunamtaka Waziri Mwinyi ajiuzulu, na akishindwa basi Rais Kikwete amfukuze kazi huyu mtu pamoja na Mkuu wa Majeshi...wananchi wameshachoka kuona usanii wa uongozi,” alisema.

  Mbowe na Slaa waliongeza kuwa wamemshangaa Rais Jakaya Kikwete kwa kuacha msiba wa Watanzania waliokufa kwa mabomu ya Gongo la Mboto, kisha kwenda nchini Mauritania kusuluhisha mgogoro wa kisiasa wa Ivory Coast.

  Walisema ni aibu kwa kiongozi wa wananchi kuacha msiba mkubwa nchini kwake na kukimbilia nje ya nchi kwenda kusuluhisha mambo ya nchi nyingine.
  “Kwenda Mauritania kwa Rais kikwete ni kuwadhalilisha Watanzania ...ni sawasawa na baba mwenye familia kuacha watoto wake wanakufa njaa, yeye anakwenda kutoa chakula nyumba ya jirani,” alisema Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.

  Katika hotuba yake, Dk. Slaa alisema kamwe Watanzania hawawezi kuvumilia kuona usaliti wa namna hiyo unafanywa na mtu mkubwa kama Rais Kikwete, ambaye ndiye Amiri Jeshi Muu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
  Katika hatua nyingine, alimtaka Rais Kikwete na serikali yake kuitaifisha mitambo ya Dowans, kwani mitambo hiyo imeingizwa nchini kwa njia za kitapeli na ujanja ujanja, kinyume cha sheria za nchi.

  Source: Tanzania daima
   
 8. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Naona Chadema wameishiwa na sera, hawana kipya ila majungu, fitina na hoja zisizo na maana hata chembe.

  Kuwepo au kutokuwepo nchini Rais si hoja ya msingi, kwani huko alikokwenda alienda kucheza?

  Wanatubowa na vijineno neno vya ufataani na siasa za kuwabagua wananchi, halafu wanaongelea udini? Wamesahau kuwa kanisa liliwakataa waumini kwa kuwa wameipigia kura CCM? wamesahau Slaa alipoifananisha CCM na Taliban? Sasa hapo nani ni mdini?
   
 9. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  SI MUUZA SURA,,HALAFU KIINGEREZA CHENYEWE HAJUI
  bora akae hapa asome english school kwanza
   
 10. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  kwani taliban ni dini gani?
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Gonjwa baya kabisa ambalo hurudisha nyuma maendelea barani Afrika ni lile linalolinganishwa na ukoma au donda ndugu ambalo ni hali ile ya kushabikia bila kupima kiakili mambo ya msingi katika mfumo wa uongozi na nini wananchi wananufaika na mfumo uliopo.
  Kwa sasa wengi barani Afrika wanaofunguka akili na kudai haki idadi inaongezeka, na wamebaki wachache wenye mtazamo hasi dhidi ya mtazamo chanya wa wenye kutaka uongozi unaofuata misingi ya haki kuushinikiza uongozi unaotumia mfumo wa utawala wa kisanii usioibua maendeleo kwa taifa kwa miongo kadhaa.
  Afrika Katikati ya karne iliyopita tulikuwa tunapigania kudai uhuru kutoka kwa mkoloni, na badala yake afrika ikashikwa na wakoloni wazawa ambao kizazi cha sasa kina mwamko wa mfumo wa maendeleo na utawala wa utandawazi wanye kutaka kujua nini kinafanyika na kwa namna gani kwa kuwanufaisha wananchi na taifa ili kuibua ushindani wa kimaendeleo.
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,317
  Likes Received: 19,478
  Trophy Points: 280
  huyu dr na mboye nakubali mambo wanayoongea, ila wasije tu wakawa wanasumbua mahakama na hukumu iko palepale. Wao kama wanataka watoe tamko , na watu wanaingia street
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,947
  Trophy Points: 280
  Mhhhhhh! eti ya CHADEMA ni "majungu, fitina na hoja zisizo na maana hata chembe" makubwa haya! Kwako wewe yasemwayo na CCM ndiyo yenye maana! Dah! Kazi kweli kweli!
   
 14. k

  kajembe JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  songeni mbele chadema sisi tunawaunga mkono msikatishwe tamaa na watu kama hawa walioshiba matumbo yao na ubia na wanaotuibia na wala hamtuboi kabisa wewe ndiyo unatuboa huna hata aibu jamani wananchi wanateseka vijijini wewe unashangilia Mungu atakulipa tu siku moja.
   
 15. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  we ndo mpumbavu kweli sasa kama hakwenda kucheza alienda kufanya nini?kwanza akili zenyewe anazo za kuelewa vitu na kuongea kiingereza wakamuelewa? usiwe unakurupuka tu ..Ni upuuzi rais wa nchi unaacha matatizo nchiuni mwako kwa ajili ya kwenda kusuluhisha matatizo ya majirani..by the way hata asingekwenda kusingekuwa na effect yoyote kwa kuwa nina uhakika hakuna anachojua na kuongea kikaleta mantiki zaidi ya kuchekacheka tu
   
 16. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  OK ni muhimu kujua kuwa CCM wako humu na hata UWT
   
 17. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2011
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kamanda elewa kuwa CCM ni chama cha hovyo. Kipindi tunapata msiba wa kuzama meli ya MV bukoba waziri mkuu alikuwa Frederic Sumaye akiwa yuko mkutanoni kule S. Africa. Alitatakiwa aachane na mikutano aje haraka sana kuwa -GRIEF wananchi na siyo kuendelea kukaa hotelini.

  Today is likely to be the same issue JK kapanda ndege badala ya Kuwa-grief victims. Raisi Obama alikuwa aende Australia mwaka jana mwezi wa June alighairi safari ili aipigie debe health policy kwenye Congress na pia alisema sitaweza kwenda kwa sababu ya financial crisis iliyotokea kwa hiyo akabaki kugrief na wananchi namna ya kutatua matatizo.

  Huyu JK mtalii....
   
 18. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Sucker!

 19. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #19
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Hivi ndio kikubwa kinachoongelewa huko? JK ameoza na hafai hata kuongelewa , kuacha misiba si mara ya kwanza, CDM waste time kupata wanachama wapya, kuuza sera zenu na kuwapa hope watanzania! jengeni ubalozi wa nyumba tano tano, tumieni style za Halima mdee kipindi cha uchaguzi, tumieni style ya mihadhara ya waislamu au mikutano ya injili....... SPREAD GOSPEL OF REVOLUTIN AND CHANGE kumsema Kikwete is wastage of time..
   
 20. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Kamuulize Silaa, Dokta wa Kanoni.
   
Loading...